Je, Hamas wanasaidiwa katika hii vita dhidi ya Israel?

Doctor Ngariba

JF-Expert Member
Jan 28, 2020
480
765
Wakuu naamini muko buheri wa afya, pole kwa ambao wanapitia changamoto ya afya na Mungu awaponye.
Naombeni wanajukwaa munijibu swali langu kuhusu vita kati ya Hamas na jeshi la Serikali ya Israel. Nitashukuru iwapo jibu/majibu yataepuka yale maneno na misamiati ya "Wazee wa Makobazi", "migalatia" na mengine yenye kuashiria kuegemea upande flani ili kuweza kujifunza.

Japo nina imani yangu, lakini nauliza hili nikiwa neutral na dhamira kuu ni kupata maarifa kwa watu wenye utaalamu wa maswala ya kivita pamoja na siasa za kimataifa kwa hiyo naomba pia wenye kujibu wawe neutral.

Niende kwenye mada kama ilivyo kwenye kichwa cha habari hapo juu.
Hamas kwa uchache wao (kwa kuzingatia eneo la Kijiographia) sidhani kama wangekuwa bado wanapambana na jeshi la IDF takribani kwa miezi miwili bila kupata msaada wowote wa kijeshi iwe silaha,milltary personnel au hata upelelezi dhidi ya jeshi linaloaminika kuwa bora na lenye kupata back up kutoka kwa Marekani na washirika wake (kama wapo)

Kama wanasaidiwa, swali linakuja na nani na hiyo misaada inaingiaje kwenye eneo dogo na ambalo kwa kiasi kikubwa limezingirwa na linashambuliwa kwa makombora mazito ya kila siku na jeshi la Israel?

Kwa kuzingatia eneo dogo la ukanda wa Gaza na kuwa Palestina ni nchi (japo haina sovereignty) ambayo almost inazungukwa kila upande na Israel, nadhani siyo rahisi kuingiza silaha kutoka nje hasa kipindi hiki cha vita bila kufahamika na jeshi la IDF(niko tayari kurekebishwa kama nitakuwa nimekosea)
Rejea hapa 👇
"With around 2 million Palestinians on approximately 365 km2 (141 sq mi) of land, Gaza has one of the world's highest population densities. The Strip contains eight refugee camps."(WIKIPEDIA)

Na kama hawana msaada (hususani wa kijeshi ndani ya eneo la kivita) nguvu hii ya kupambana hadi leo wanaitoa wapi na silaha zao mfano wa manati dhidi ya vifaru na ndege vita bora kuwahi kutokea. Au kwamba walidunduliza kwa kipindi kirefu kabla ya vita?

Mwisho kwa ajili ya kujifunza, nini hatma ya vita hii iwapo Israel itafanikiwa kuwaondosha Hamas katika ukanda wa Gaza? Je, eneo hili litakuwa mali halali ya Israel au wataachiwa Wapalestina wenyewe chini ya uangalizi wa Serikali Jerusalem?

Nawasilisha na naomba kujifunza kutoka kwenu.
 
Rejea hapa

CC: HIMARS ,Proved ,T14 Armata
 
Hamas hawana msaada wowote ujasiri wao na umoja wao ndiyo sifa yao kubwa.
Hamas wangepata msaada japo wa nchi moja Misri, Jordan, Lebanon, Iran saizi tungeongea mengine.

Makombora wanayotumia ni kienyeji yametengenezwa Tabata ya Gaza, gharama yake ni dola 200 tu inashangaza inaripua kifaru cha gharama ya dola laki 3 na nusu linakata mpaka chein.

Gaza hawaruhisiwi kuingiza silaha yeyote kila mzigo wa meli ukingia Gaza lazima Israel wakague.

Hivi tunavyongea hali tete huko Israel.

Somaa hii.

Gazeti la Israel la Haaretz kuhusu idadi halisi ya wanajeshi wa Israel waliojeruhiwa:

Kuhusu takwimu za uongo za msemaji wa jeshi linalokalia kwa mabavu kuhusu idadi ya watu waliojeruhiwa katika hospitali za Israel tangu kuanza kwa vita dhidi ya Gaza.

Takwimu za msemaji wa jeshi hadi sasa juu ya wanajeshi 1,593 waliojeruhiwa tangu kuanza kwa operesheni:

Gazeti hilo lilifichua yafuatayo:

  • Hospitali ya Barzelazi (Beersheba) ilitibu wanajeshi 1,490
  • Hospitali ya Assuta iliwatibu wanajeshi 178
Hospitali ya Ichilov huko Tel Aviv ilitibu wanajeshi 148
  • Hospitali ya Rambam huko Haifa iliwatibu wanajeshi 188
  • Hospitali ya Hadassah mjini Jerusalem ilitibu wanajeshi 209
-Hospitali ya Shaare Zedek huko Jerusalem ilitibu wanajeshi 139
-Hospitali ya Soroka kusini iliwatibu wanajeshi 1,000
-Hospitali ya Sheba kusini iliwatibu wanajeshi 500

Jumla ya wanajeshi 3,852 waliojeruhiwa, kulingana na data ya hospitali ya Israeli, pamoja na kujeruhiwa kidogo katika hospitali za rununu za jeshi, Ambayo inaweza kusababisha zaidi ya 7000 kwa urahisi.
 
Ngoja ningojee wajuvi waje watie maneno zao hem
Ila kwa hapa kwa hamas kama wataondolewa nadhani hilo eneo litakua mali ya israel sidhanii kama itakua kinyume ya hv
Hii mada imesimama sana mzee kongole ila kuna watu watakuja kuiharibu
 
Kama utakumbuka gogoro la Uikrane/Urusi mwanzoni mwa SMO, Putin alisema yeyote atakayeingilia atakiona Cha moto.Hili utathibitisha Hali ilivyo nchi za ulaya kiuchumi na nyinginezo.

Ukumbuke Urusi na Israel wanamahusiano mazuri,hasa Urusi iliwasaidia Waisrael Toka mikononi mwa Hitler,kosa watakalojutia ni kupeleka siraha kimya kimya Uikrane huku wakimwambia Putin tupo pamoja,Wala usijali.

Wagner walipotokomea nchini Belarus Toka Urusi,wapiganaji wapatao 20,000 WA Wagner hawajulikani walipo humo nchini Belarus,UK ililalamikia hili suala.Uk ikaenda mbali zaidi na kusisitiza kuwa hao wapiganaji juu ardhi hawapo labda chini ya ardhi.Wiki mbili hazijapita kikawaka Israel.Mkong'oto aloupata Israel hatosahau na hatokubali Hali kama hiyo kujirudia.

Wafatiliaji wa masuala ya kivita wanapoangalia aina ya upiganaji WA Hamas hauna tofauti na Urusi.

20231008_214225.jpg
20231007_211819.jpg
Screenshot_20231014-231529.png
 
Mkuu hapo awali Hamas walikuwa na ushirikiano wa kijeshi na Iran na Syiria kwa miaka mingi lakini ushirikiano wao uliingia mushikeli mwaka2011 baada yakulipuka vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria , mushikeli hiyo ilitokea baada ya Hamas kugoma kumuunga mkono Asad kwenye vita yake na waasi hivyo kundi hilo likazikasirisha serikali ya Syria na Iran hali iliyo pelekea mataifa hayo kusitisha msaada wa kijeshi kwa kundi hilo.

Baada ya vita kati ya kundi hilo na Israel mwaka 2014 Iran ilirudisha msaada kwa kundi hilo, lakini msaada wa kijeshi ahuusishi kupewa silaha za moja kwa moja kutoka Iran na ndio maana mpaka sasa hakuna silaha yeyote inayo tengenezwa nchini Iran ambayo imesha onekana ikitumiwa na Hamas kwenye uwanja wa vita,bali Iran ulipa fedha tu na jukumu la wapi watanunua hizo silaha ni la kwao ina maana silaha karibia zote anazo nunua hamas huwa anazinunua kwenye brack market kupitia Misri.
Pia kundi hilo lina miliki biashara mbali mbali duniani hivyo fedha nyingine ya kudhamini shughuli zao za kijeshi wanazipata kutoka kwenye biashara zao wenyewe , kwahiyo ukiona viongozi wa Hamas wako nchi mbali mbali duniani usidhani wapo kwa ajili ya kujificha ili wasiuawe na Israel bali wapo kwa ajili ya kusimamia biashara za chama hicho.

Hata hivyo pesa hizo ni ndogo hazitoshi kununua silaha za kisasa na za kutosha badala yake wanarazimika kununua silaha chache na hafifu ambazo hasa sio rais kwao kuweza kutengeneza mfano kama bunduki.
Na fedha zinazo baki wana zitumia kununua source mbali mbali kwa ajili ya kujitengenezea silaha zao wenyewe ili wawe na silaha za kutosha kwa sababu kutengeneza ni gharama ndogo kuliko kununua.
Kwa hiyo silaha nyingi wanazo zitumia ni silaha walizo jitengenezea wao wenyewe mfano Ant_tank,mabomu ya mikono , mabomu ya kurusha kwa mota,maroketa ,drone na risasi hata hivyo ni silaha zilizo tengeneza kwa teknolojia dhahifu sana kutokana na uchache wa fedha na vizuizi vikali sana vya Israel.

Pia hamas ina uhusiano wa kisiasa na mataifa mengi tu ikiwemo S.africa na Algeria,Qtar, Urusi, Uturuki, malasia,Oman,Chile, Venezuela, Nikaragua,Cuba,Syiria na Lebanon , Bolivia,Colombia na Tunisia, unapo sema uhusiano wa kisiasa ina maana mataifa hayo yanaliunga mkono kisiasa na kulitambua kama chama cha ukombozi hivyo kuruhusu kundi hilo kufungua ofisi za uwakilishi ndani ya nchi hizo lakini hazitoi msaada wowote wa kifedha au wa kijeshi.

Bali Uturuki na Qtaar wanalisaidia fedha kwa ajili ya kuhudumia raia wa gaza hasa kulipa wafanyakazi wa huduma muhimu kama madaktari,walimu, zima moto, na ujenzi wa miundo mbinu lakini fenda hizo ni razima zipitie kwenye mabenki ya Israel kuhakikiwa ili zisitumike kwa malengo ya kijeshi.

Kwa hiyo hamas kijeshi anawezeshwa na Iran tu japo ni kwa uchache sana.
 
Kwaza operation hapo Gaza sio baina ya taifa na taifa, hivyo sio kipimo sahihi cha uwezo wote wa kivita wa nchi. Ni kipimo cha kipengele kidogo cha uwezo wa kijeshi kufanya counter terrorism na missions within civilian populated areas controlled by your enemy. Hamas ni kundi la Wapalestina, sio Wapalestina wote ni wanachama wa Hamas ila ni almost Wapalestina wote hawaipingi Hamas (kuna wasioikubali kadhaa, nao sio hawaikubali totally bali njia zake zinazosababisha majibu kutoka Israel ndizo hawakubaliani nazo).
Kupigana na kundi lenye ideology ya kidini sio rahisi na haitumii muda mfupi.

Kinachoilinda Hamas ni kupigana na professional military inayojaribu kuzingatia sheria za kimataifa za kuendesha vita. Kama ingekuwa wote ni vichaa hapo Gaza pangekuwa pamejaa mashimo na watu laki kadhaa wamefariki. Na Hamas wanajichanganya na raia, hawana sare, hawana kambi, hawana ofisi. Wao kila kitu wanatumia cha raia wa kawaida kasoro silaha. Hivyo ukiwashambulia unazingatia kulinda wasio na hatia, raia waliokufa wote hao ni collateral damage ni bahati mbaya, ingekuwa Israel wanapiga tu vyovyote wakiona gaidi moja la kawaida limeingia sokoni kuna watu elfu moja hapo linadondoshwa bomu basi watu wengi wangekwishafariki.

Israel imejipa mwaka kumaliza hii operation na hadi sasa ina performance nzuri. Pale Syria walikuwepo waasi wakapigana na jeshi la Syria tangu 2011, Iran ikaingia 2013 au 2014 hivi, na jeshi la Urusi likaingia 2015 ila mpaka sasa Syria haijatawaliwa nzima na serikali. Ina maana Urusi, Iran na Syria nchi tatu zote kwa pamoja zina majeshi dhaifu dhidi ya waasi?
Mfano serikali ya Syria ilitumia mabomu ya sumu kwenye miji dhidi ya waasi yale mabomu yakaleta athari hadi kwa raia, wakimbizi walikimbilia Uturuki ila baadae wakajifungua walemavu sababu ya ile sumu
Mwishowe Assad akalaumiwa na jumuiya ya kimataifa kuwa mkatiri, wakati waasi na magaidi hawana masharti, wakiamua kuchoma moto mji wanachoma, wakiamua kukata watu koromeo wanafanya, wakiamua kulipua mifumo ya umeme na madaraja na ofisi mradi watie hasara serikali wanafanya. Ila professional military haiwezi fanya hivyo.

Uturuki ina magaidi, India ina magaidi, Pakistan, Misri vilevile, Morocco ina waasi na zote hizo zimeshindwa kumaliza waasi na magaidi kwa miaka nyingine hata 50 ila zote hizo pia zina uwezo wa kuipiga nchi fulani ya Afrika Mashariki. Ila hiyo nchi haina waasi wala magaidi.
Wakati India haikutumia mwaka kuipiga Pakistan mara mbili tofauti, Israel ilipigana na Waarabu vita mbili moja ilitumia siku 6 nyingine ikatumia kama mwezi ila hizo nchi zinapata shida kupigana na magaidi sababu ni suala la ideology.

Hamas haipati msaada kwa sasa sababu supplies zote zinazoingia Gaza kupitia Rafar closing zinakaguliwa na IDF, ni silaha chache sana zinaweza penya. Wao walikuwa na stockpile miaka yote kumbuka muda wote wanatamani kuitoa Israel hapo, lifestyle yao ni kuwaza kushambulia. Silaha, mafunzo, ujuzi na ufundi wanapita

Narudi.....
 
Wakuu naamini muko buheri wa afya, pole kwa ambao wanapitia changamoto ya afya na Mungu awaponye.
Naombeni wanajukwaa munijibu swali langu kuhusu vita kati ya Hamas na jeshi la Serikali ya Israel. Nitashukuru iwapo jibu/majibu yataepuka yale maneno na misamiati ya "Wazee wa Makobazi", "migalatia" na mengine yenye kuashiria kuegemea upande flani ili kuweza kujifunza.

Japo nina imani yangu, lakini nauliza hili nikiwa neutral na dhamira kuu ni kupata maarifa kwa watu wenye utaalamu wa maswala ya kivita pamoja na siasa za kimataifa kwa hiyo naomba pia wenye kujibu wawe neutral.

Niende kwenye mada kama ilivyo kwenye kichwa cha habari hapo juu.
Hamas kwa uchache wao (kwa kuzingatia eneo la Kijiographia) sidhani kama wangekuwa bado wanapambana na jeshi la IDF takribani kwa miezi miwili bila kupata msaada wowote wa kijeshi iwe silaha,milltary personnel au hata upelelezi dhidi ya jeshi linaloaminika kuwa bora na lenye kupata back up kutoka kwa Marekani na washirika wake (kama wapo)

Kama wanasaidiwa, swali linakuja na nani na hiyo misaada inaingiaje kwenye eneo dogo na ambalo kwa kiasi kikubwa limezingirwa na linashambuliwa kwa makombora mazito ya kila siku na jeshi la Israel?

Kwa kuzingatia eneo dogo la ukanda wa Gaza na kuwa Palestina ni nchi (japo haina sovereignty) ambayo almost inazungukwa kila upande na Israel, nadhani siyo rahisi kuingiza silaha kutoka nje hasa kipindi hiki cha vita bila kufahamika na jeshi la IDF(niko tayari kurekebishwa kama nitakuwa nimekosea)
Rejea hapa
"With around 2 million Palestinians on approximately 365 km2 (141 sq mi) of land, Gaza has one of the world's highest population densities. The Strip contains eight refugee camps."(WIKIPEDIA)

Na kama hawana msaada (hususani wa kijeshi ndani ya eneo la kivita) nguvu hii ya kupambana hadi leo wanaitoa wapi na silaha zao mfano wa manati dhidi ya vifaru na ndege vita bora kuwahi kutokea. Au kwamba walidunduliza kwa kipindi kirefu kabla ya vita?

Mwisho kwa ajili ya kujifunza, nini hatma ya vita hii iwapo Israel itafanikiwa kuwaondosha Hamas katika ukanda wa Gaza? Je, eneo hili litakuwa mali halali ya Israel au wataachiwa Wapalestina wenyewe chini ya uangalizi wa Serikali Jerusalem?

Nawasilisha na naomba kujifunza kutoka kwenu.
Hii vita Israel kapihana kwa ustaarabu mkubwa sana. Karibia mwezi mzima hakuingiza keshi, ila ilikuwa mashambulizi ya angani tu kulenga popote Hamas na mali zao zilipo.
Hamas walitumia muda mrefu kujenga mahandaki ya chini tena karibu na miundombinu ya kiraia kama shule, hospital na nyumba za ibada. Lakini pia wapiganaji wa Hamas wengi hawana sare ila wamevaa kiraia hata ukiwaua unaambiwa umeua raia.
Hivyo Israel amekuwa akipigana na watu wanajificha kwenye mahandaki na katikati ya raia. Hii siyo conventional war ila operation ya kusafisha mji.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Kwaza operation hapo Gaza sio baina ya taifa na taifa, hivyo sio kipimo sahihi cha uwezo wote wa kivita wa nchi. Ni kipimo cha kipengele kidogo cha uwezo wa kijeshi kufanya counter terrorism na missions within civilian populated areas controlled by your enemy. Hamas ni kundi la Wapalestina, sio Wapalestina wote ni wanachama wa Hamas ila ni almost Wapalestina wote hawaipingi Hamas (kuna wasioikubali kadhaa, nao sio hawaikubali totally bali njia zake zinazosababisha majibu kutoka Israel ndizo hawakubaliani nazo).
Kupigana na kundi lenye ideology ya kidini sio rahisi na haitumii muda mfupi.

Kinachoilinda Hamas ni kupigana na professional military inayojaribu kuzingatia sheria za kimataifa za kuendesha vita. Kama ingekuwa wote ni vichaa hapo Gaza pangekuwa pamejaa mashimo na watu laki kadhaa wamefariki. Na Hamas wanajichanganya na raia, hawana sare, hawana kambi, hawana ofisi. Wao kila kitu wanatumia cha raia wa kawaida kasoro silaha. Hivyo ukiwashambulia unazingatia kulinda wasio na hatia, raia waliokufa wote hao ni collateral damage ni bahati mbaya, ingekuwa Israel wanapiga tu vyovyote wakiona gaidi moja la kawaida limeingia sokoni kuna watu elfu moja hapo linadondoshwa bomu basi watu wengi wangekwishafariki.

Israel imejipa mwaka kumaliza hii operation na hadi sasa ina performance nzuri. Pale Syria walikuwepo waasi wakapigana na jeshi la Syria tangu 2011, Iran ikaingia 2013 au 2014 hivi, na jeshi la Urusi likaingia 2015 ila mpaka sasa Syria haijatawaliwa nzima na serikali. Ina maana Urusi, Iran na Syria nchi tatu zote kwa pamoja zina majeshi dhaifu dhidi ya waasi?
Mfano serikali ya Syria ilitumia mabomu ya sumu kwenye miji dhidi ya waasi yale mabomu yakaleta athari hadi kwa raia, wakimbizi walikimbilia Uturuki ila baadae wakajifungua walemavu sababu ya ile sumu
Mwishowe Assad akalaumiwa na jumuiya ya kimataifa kuwa mkatiri, wakati waasi na magaidi hawana masharti, wakiamua kuchoma moto mji wanachoma, wakiamua kukata watu koromeo wanafanya, wakiamua kulipua mifumo ya umeme na madaraja na ofisi mradi watie hasara serikali wanafanya. Ila professional military haiwezi fanya hivyo.

Uturuki ina magaidi, India ina magaidi, Pakistan, Misri vilevile, Morocco ina waasi na zote hizo zimeshindwa kumaliza waasi na magaidi kwa miaka nyingine hata 50 ila zote hizo pia zina uwezo wa kuipiga nchi fulani ya Afrika Mashariki. Ila hiyo nchi haina waasi wala magaidi.
Wakati India haikutumia mwaka kuipiga Pakistan mara mbili tofauti, Israel ilipigana na Waarabu vita mbili moja ilitumia siku 6 nyingine ikatumia kama mwezi ila hizo nchi zinapata shida kupigana na magaidi sababu ni suala la ideology.

Hamas haipati msaada kwa sasa sababu supplies zote zinazoingia Gaza kupitia Rafar closing zinakaguliwa na IDF, ni silaha chache sana zinaweza penya. Wao walikuwa na stockpile miaka yote kumbuka muda wote wanatamani kuitoa Israel hapo, lifestyle yao ni kuwaza kushambulia. Silaha, mafunzo, ujuzi na ufundi wanapita

Narudi.....
Tatizo lako uchambuzi wako siku hizi ulisha kaa kipropaganda zaidi.

Hoja yako ya Israel kuepusha mauaji ya raia ni mufisirisi kabisa kwa sababu Israel amesha vuka mipaka yote ya sheria za kimataifa hivyo hicho kisingizio hakina uzito.
Israel ingekuwa inazingatia maisha ya watu na sheria za kimataifa isinge kuwa inashambulia shule, hospital,kambi za wakimbizi magari ya wagonjwa ambazo anajua kabisa kuna maelfu ya watu wamejihifadhi kwa ajili ya kutafuta usalama.Ni leo tu waziri wa Ulinzi wa Marekani mdhamini mkuu wa Israel ameitadharisha Israel kuwa haifanyi vya kutosha kuepusha mauaji ya raia.
Jana Ujerumani ameimbia Israel kuwa ni razima ijitathimi kwa sababu mauaji ya raia hayaendani na uhalisia wa vita bali kinacho onekana ni mauaji ya kiholela.
Wiki chache zilizo pita raisi wa Ufaransa aliikosoa Israel na kuiambia kuwa inatakiwa ifuate kilicho wapeleka Gaza na sio kuuwa watoto na wanawake, leo tena rais wa kamisheni ya umoja wa Ulaya amesema uharibifu huko gaza ni zaidi ya ule uliotokea Ujerumani kwenye vita ya dunia maana yake ni kuwa uharibifu wa Israel huko gaza umevuka mipaka. Kwahiyo inataka kuniambia kuwa ww una uwelewa wa kijeshi kuliko viongozi hao.

Nimeamua nikuwekee nikuu za viongozi ambao mataifa yao ni waungaji mkono wa Israel maana ninge kuwekea za rais wa Iran au Uturuki ungesema kuwa wanafanya propaganda kwa sababu Israel ni mshindani wao.
Ina maana mpaka washirika wake wanashangazwa na mauaji na uharibifu wa kiholela unao fanywa na huyo mshirika wao walio amini kuwa ana weledi

Ww kama una hoja nyingine uiweke ila hiyo haiuziki kabisa.

Kuhusu waasi nchini Syria sehemu ambayo mpaka sasa haidhibitiwi na serikali ni jimbo la Idrib ambapo lina dhibitiwa na waasi wanao ungwa mkono na Uturuki na pia kule kuna wanajeshi wa Uturuki na Urusi ndo iliyo izuia serikali ya Syria kulishambulia eneo hilo kutokana na makubaliano na Uturuki, eneo lingine ni jombo la Raqaa ambalo linadhibitiwa na wakrudi wanao ungwa mkono na Marekani na pia kuna wanajeshi wa Marekani hivyo Syria haiwezi kulishambulia kwa kujizuia kuingia moja kwa moja kwenye mzozo na Marekani na pia wapiganaji wa kikurdi hawana uhasama wowote na Asad na wala hawajawahi kushiriki vita ya kumtoa Asad Madarakani.
 
Nashkuru kwakumuekea hizo nukuu nilitaka kumjibu pia ila umeniwahi
Israhell kaishakiuka sheria zote zakimataifa hapo
Yaani dunia nzima wanaona kama israhell anakiuka sheria za zinazoitwa umoja wa mataifa ila bwana huyu yeye anasema israhell inajizuia
Kama ntakua sawa israhell imemnyima viza yakuingia kwao mpaka Michelle basheler kamishna wa haki za binaadam wa umoja wamataifa kisa tu aliwaambia kwamba israhell wanakiuka sheria za vita za UN
 
Hii vita Israel kapihana kwa ustaarabu mkubwa sana. Karibia mwezi mzima hakuingiza keshi, ila ilikuwa mashambulizi ya angani tu kulenga popote Hamas na mali zao zilipo.
Hamas walitumia muda mrefu kujenga mahandaki ya chini tena karibu na miundombinu ya kiraia kama shule, hospital na nyumba za ibada. Lakini pia wapiganaji wa Hamas wengi hawana sare ila wamevaa kiraia hata ukiwaua unaambiwa umeua raia.
Hivyo Israel amekuwa akipigana na watu wanajificha kwenye mahandaki na katikati ya raia. Hii siyo conventional war ila operation ya kusafisha mji.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
Israel kupigana kistaarabu ndani ya miezi miwili ameuwa raia elfu 18000? Wewe ukapimwe akili hauko sawa kichwani.
 
Waarabu wote na iran wanaisaidia Hamas, we jua hilo.
Warabu wote wana msaidia Israel isipo kuwa Yemen, Oman, Algeria, Syria peke ndio Hawamsaidi Israel.

Hamasi hasaidiwi na mtu wanajitegemea, Wenyewe hata Iran anamsaidia sababu Iran anawasaidia Jihad Al Islam ndio Hamasi nayeye anachukua hapo baadhi ya silaha.

Ukweli 85% silaha za Hamasi wao wanatengeneza na zingine wanzitoa Israel, wanawapa bangi wanajeshi wa Israel na unga afu wanapewa silaha 😄
 
Kama utakumbuka gogoro la Uikrane/Urusi mwanzoni mwa SMO, Putin alisema yeyote atakayeingilia atakiona Cha moto.Hili utathibitisha Hali ilivyo nchi za ulaya kiuchumi na nyinginezo.

Ukumbuke Urusi na Israel wanamahusiano mazuri,hasa Urusi iliwasaidia Waisrael Toka mikononi mwa Hitler,kosa watakalojutia ni kupeleka siraha kimya kimya Uikrane huku wakimwambia Putin tupo pamoja,Wala usijali.

Wagner walipotokomea nchini Belarus Toka Urusi,wapiganaji wapatao 20,000 WA Wagner hawajulikani walipo humo nchini Belarus,UK ililalamikia hili suala.Uk ikaenda mbali zaidi na kusisitiza kuwa hao wapiganaji juu ardhi hawapo labda chini ya ardhi.Wiki mbili hazijapita kikawaka Israel.Mkong'oto aloupata Israel hatosahau na hatokubali Hali kama hiyo kujirudia.

Wafatiliaji wa masuala ya kivita wanapoangalia aina ya upiganaji WA Hamas hauna tofauti na Urusi.

View attachment 2840725View attachment 2840727View attachment 2840728
Hapa umeeleweka vizur sana kiongoz
 
Back
Top Bottom