Hamas ina mpango kabambe wa kujihami katika vita na Israel

Malaria 2

JF-Expert Member
Oct 17, 2023
2,646
3,936

Dec 06, 2023 12:21 UTC

Afisa wa ngazi ya juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu (muqawama) ya Palestina, Hamas, amesema harakati hiyo ya kupigania ukombozi wa Palestina yenye makao yake Gaza imeandaa mpango mkubwa wa kujihami katika kukabiliana na mashambulizi ya Israel, na kusisitiza kwamba umoja kati ya makundi ya muqawama wakati wa Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa uliwashangaza makamanda wa kijeshi wa Israel.

Ali Baraka, mkuu wa Uhusiano wa Kitaifa wa Hamas Nje ya Nchi, ameiambia tovuti ya habari ya al-Ahed ya Lebanon kwamba: "Tuna uhakika kwamba tutaibuka washindi katika vita hivi. Tunawahakikishia wenzetu wa Palestina kwamba mapambano yana nguvu zinazohitajika kuwaachilia wafungwa wote wa Kipalestina."
Ameongeza kuwa jeshi la Israel limeshindwa kupata mafanikio yoyote katika vita vya nchi kavu dhidi ya Ukanda wa Gaza.

Baraka amebainisha kuwa utawala ghasibu wa Israel ulianzisha mashambulizi ya nchi kavu huko Gaza baada ya idara zake za usalama kushtukizwa katika Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa. Amesema hadi sasa Israel haijaweza kufikia malengo yoyote iliyotangaza ambayo yalikuwa ni pamoja na kuangamiza Hamas, kuachiliwa wafungwa wake wote na kutimuliwa Wapalestina kutoka Gaza.

Kwingineko afisa wa ngazi ya juu wa Hamas amesema utawala haramu wa Israel "unazidi kuzama ndani na zaidi katika kinamasi cha Gaza", akisisitiza kuwa utawala huo ghasibu umeshindwa kupata ushindi hata mmoja baada ya siku 60 za vita katika eneo hilo linalozingirwa.

Osama Hamdan, mwakilishi mkuu wa Hamas nchini Lebanon, aliyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari katika mji mkuu Beirut siku ya Jumanne, na kubainisha kuwa kundi la Hamas "limejiandaa vyema" kupigana bila kujali ni muda gani vita vya Israel vitaendelea.

Hamdan pia amewapongeza wapiganaji wa Brigedi ya al-Qassam, tawi la kijeshi la Hamas, ambao wanatetea haki za watu wa Palestina na ardhi yao, akisema "kila wakati wanamfanya adui kupata majeraha na hasara na kuifanya Gaza kuwa makaburi ya wavamizi.”
 
Mbali na kujificha nyuma ya Wanawake na watoto hawana mpango mwingine wowote huo ndio ukweli
 
Wazayuni waliingia Gaza wakiwa na matokeo yao mfukoni..........walizani itakuwa kama ile 6 days war
 
Wazayuni waliingia Gaza wakiwa na matokeo yao mfukoni..........walizani itakuwa kama ile 6 days war
Six day war ilikua ni myths tu hakuna ukweli wowote ule
Haiwezekani muyashinde mataifa zaidi ya matano kwa siku sita ila mukishindwe kikundi cha wapiganaji af saba kwa miezi miwili
Six day war na ile suala la entebe kule uganda yote ni myths tu
Hamas wakamatie hapo hapo wazayuni wataikimbia tu ghaza nisuala la muda tu kwakweli
 
kweli usionee mtu huruma, dunia nzima inawaonea huruma ila ndo kwanza mnatamba hivi.... ubaya ni kwamba habari hzi kutaziona aljazeera, kule utaona picha za watotot na wanawake na majumba yaliyobomoka, utadhan gaza wanaonewa kumbe wao ndo wanakiri kuwachakaza israel vibaya sana.
nadhan kitu pekee wanachokosea hamas ni kujificha katikati ya makazi ya watu , kushambulia na kurudi shimoni, hicho kinawafanya raia wake wauawe maana moto unaelekezwa sehemu moto umetokea.
hamas wawatoe wananchi maeneo yao, wabaki wajeda kwa wajeda watwangane.
nami naungana na putin kuwa kama wanaume wameamua kupigana basi wapigane mpaka mmoja akubali, ila wasihusishe watoto au wanawake kwa manufaa yao au ulinzi wao.
kwahyo namimi leo nafuta huruma kwa yanayoendelea huko mashariki ya kati, nasema zipigweeee mpaka mshindi apatikane,.. anayehisi yeye sio mwanajeshi akimbie eneo la vita tusilaumianee
 
Six day war ilikua ni myths tu hakuna ukweli wowote ule
Haiwezekani muyashinde mataifa zaidi ya matano kwa siku sita ila mukishindwe kikundi cha wapiganaji af saba kwa miezi miwili
Six day war na ile suala la entebe kule uganda yote ni myths tu
Hamas wakamatie hapo hapo wazayuni wataikimbia tu ghaza nisuala la muda tu kwakweli
muhimu kusiwe na vilio wala lawama, kichagua vita yajue madhara ya vita, waandae na watu wako kisaiolojia... nami nasema hamas piga haoooo.... na idf piga haooo zipigwe tu watu waheshimiane maana hakuna namna nyingine
 
muhimu kusiwe na vilio wala lawama, kichagua vita yajue madhara ya vita, waandae na watu wako kisaiolojia... nami nasema hamas piga haoooo.... na idf piga haooo zipigwe tu watu waheshimiane maana hakuna namna nyingine
Acha hamas waendelee kujitetea nia wanayo sababu wanazo na haki pia wanazo
 
Back
Top Bottom