Je, CHADEMA inaweza kushinda 2020? Is it serious, credible & mature enough opposition?

kama mtu wa darasa la saba anaweza kuongoza jimbo nini chadema kuongoza nchi?ambapo kuna wasomi kibao

Jambo hili la elimu Bajaj lipo kikatiba lakini limepitwa na wakati na ndio maana watu wanaomba katiba ibadilishwe kupitia kwa haohao akina Bajaj lakini nao wamegoma kumwaga kitumbua chao wakiwa wanaangalia na ukichunguza huko kwao ndio kumejaa watu wa type hiyo ya vibajaj?
 
Kwa nini wasibezwe wakati wanalisababishia taifa hasara ya mamilioni? Nenda kawaambie watu wa Ukerewe ambao wamepoteza ndugu zao simply kwa kuwa waokoaji walikosa taa za kuokolea usiku kwamba hawa watu wasibezwe. Watoto wengi hawana madawati, wakinama wanajifungulia kwenye sakafu halafu huyu mla rushwa anataka turudi uchaguzi...
 
Tangu siasa za vyama vingi zianze sijawahi sikia uchaguzi usiokuwa na figisu wala malalamiko.
Lakini, upinzani wamekuwa wakishinda na kuendelea kujikusanyia majimbo mengi uchaguzi hadi uchaguzi.

Hivi sasa kinachoendelea ni dalili za upinzani kushindwa kuhimili vishindo. Inaonekana hatari ya kupoteza majimbo ya upinzani 2020 ni kubwa saaaana.
Sasa tunajiuliza kulikoni? Sababu za figisu kuwepo hilo sio jipya..swala la tume hilo sio jipya...ni nini kipya awamu hii?

Na kuhusu 'tume huru' na kuhoji matokeo mahakamani nakupa mfano wa nchi ya kenya. Wanayo katiba mpya (waliyoisifu sana), kisha wakaunda 'tume huru' (waliyoitaka wao) na kisha wanaouwezo wa kupinga matokeo mahakamani.
Uchaguzi wa 2017 umetoa funzo kubwa. Wamelia tume si huru...wapinzani wameipinga sana na mishipa ikawasimama, wanasema wazi kupinga matokeo ya urais mahakamani ni upuuzi (kindumbwendumbwe cha Mzee Maraga kimewarudi) na mapengo ya katiba yamechomoza wazi na sasa kampeni za refferendum ya kurekebisha katiba imeanza.

Swali tunalojiuliza hivi sasa ni kulikoni?
Kulikoni hatari ya kufutika hivi sasa katika majimbo ya upinzani ni kubwa sana ilhali changamoto ni zilezile?
 
Kinachosababisha hasara ya kurudia uchaguzi sio wahamaji bali ni sheria mbovu ya uchaguzi. Mbunge huchaguliwa na watu, aliopaswa kuwa huru kuhama na ubunge wake kama Kenya.
Rushwa ya ahadi kwenye sheria zetu sio kosa.
Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law!, Kuendelea Kuitumia ni Ujinga?, Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!. - JamiiForums
P
 
Kutokuwa na sheria kama Kenya hakuhalalishi hawa watu kufanya huu ujinga. Tanzania ni nchi maskini tuna matatizo mengi ya msingi yanayohitaji kila senti tunayoyapata. Haingii akilini kutumia mamilioni ya shilingi kufanya uchaguzi wakati watoto wetu wanasoma kwenye mazingira magumu.
 
Zanzibar hakuna ubishi kuhusu uwezo wa CUF as a credible opposition kuweza kutawala Zanzibar, lakini kwa upande wa huku Tanzania Bara, bado kabisa hatuna any serious, capable and a credible opposition ya kuiondoa CCM na kuikabidhi Ikulu yetu.
Hapa naona umeshatupa mwelekeo (clue) kwamba chama chochote cha upinzani hakitopkabidhiwa madaraka hata kama kitashinda, na ndivyo ilivyo!! Sasa hili swali wala halikuhiotajika, yaani jawabu tayari unalo mkuu. sisi twende tu.
 
Is CCM credible anyway? It has a succession plan anyway but CCM itself isn't confident apart from it being older than opposition parties.
 
Mkuu Nguruvi3, asante kwa hii. Hii ni dalili ya Chadema angalau kuanza kuonyesha maturity, japo not for 2020, its too little too late.

P
 
Kwa hyo we una akili kumzidi msajili wa vyama vya siasa ambae amekisajili na anaamini kinaweza kuongoza nchi?maswali yako kamuulize msajili wa vyama.hata goliati alikuwa na dharau sana kwa kijana daudi.
 
Huu ndio ukweli wenyewe. Hebu tuchangie bila povu wajameni.

Mkuu Magonjwa Mtambuka, asante sana kwa hii kitu. Huyu ni mmoja wa ma Prof wa ukweli ninao waaminia, hivyo naunga mkono hoja ya Prof. Safari.

Tulisema humu akina sisi,

Kuna kitu hapa kilisemwa na Masha

Kikapuuzwa, sasa leo kusema Prof. Safari, haya sasa manazi wa Chadema, njooni mumponde kama kawaida yenu.

Mkiambiwa
Mnakasirika

P.
 
Uchaguzi wa kesho wa Mwenyekiti wa Chadema ni very instrumental kwenye mustakabali wa 2020, kama mtajichagulia tuu kwa ule ule utaratibu wenu wa mazoea ya as usual, matokeo ya uendeshaji wa Chadema pia utakuwa as usual, lakini kama mtaamua kufanya changes, then things will change hata Uchanguzi Mkuu wa 2020 mnaweza angalao kuambulia ambulia.

P
 

Hakuna Chama kinaweza kushinda kwasababu mmoja kubwa uchaguzi Tanzania kwenye level ya Uraisi sio wa haki. Angalia mfano mdogo Zanzibar uchaguzi ulivyokuwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…