CHADEMA Hamkujipanga, hamjajipanga, hamjipangi na hamtajipanga!-2015 ni CCM tena!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,428
113,425
Wanabodi,

Haya ninayoyaandika hapa, yanatoka ndani kabisa ya moyo wangu na ninaandika kwa uchungu!, kwa mtu yoyote ambaye alikuwa na matumaini ya labda 2015, tunaweza kupata mabadiliko, akiangalia hii trend ya Chadema inayokwenda nayo sasa, atakubaliana na mimi, kuwa the trend is not good at all!, 2015 is just around the corner!, I'm afraid, by the time Chadema ita realize imefanya nini, ilipaswa kufanya nini, sasa inafanya nini, na 2015 itafanya nini!, it will be too little too late!, huu ni ukweli mchungu sana kumeza, kuwa Chadema Haikujipanga (jana), Chadema Haijajipanga (leo), Chadema Haijipangi (kesho), na amini nawaambieni!, Chadema Haitajipanga (2015), hivyo huu ni ukweli mchungu kweli kweli kumeza kuwa 2015, ni CCM Tena!.

Tangu 2010, Chadema Hamkujipanga!.
Mara Baada ya kumalizika uchaguzi mkuu wa 2010, uliofufua kwa kiwango kikubwa matumaini ya uwezekano wa Chadema kuchukua nchi, 2015, mimi ni miongoni mwa wana jf wa mwanzo kutinga viwanja vya Bunge Dodoma, kuwapongeza baadhi ya makamanda waliokata vigogo wa CCM!, nikatoa tathimini yangu kuwa kwenye baadhi ya maeneo, Chadema imeshinda uchaguzi, sio kwa sababu ilijipanga vizuri!, no!, nikasema Chadema imeshinda uchaguzi katika baadhi ya maeneo kwa sababu tuu CCM Imechokwa; CHADEMA Haijajipanga!. hapa Chadema niliwaambia hivi
Hakuna ubishi, Chadema imenyanyuka, toka wabunge 5 mpaka 22 wa kuchaguliwa tena majimbo ya haja, huku sio kukua bali ni kupaa, tatizo kubwa la Chadema, bado hawajipanga.

Kichama, wanachadema mkubali msikubali, chama chenu japo kipo juu, lakini bado hamjajipanga kwa sura ya kitaifa au mkao wa kutawala nchi.
Kwa vile CCM imekaa mkao wa kifo, hii ndio opportunity yenu kujipanga muwe na sura ya kitaifa, kuonyesha ukomavu na utayari wa kutawala, Watanzania wawamini wawakabidhi nchi mwaka 2015.

Hakuna ubishi kuhusu kitakachompata yoyote atakayeteta ukosoaji wa Chadema humu jukwaani, na mimi ndicho kilichonikuta, na miongoni mwa walionijibu uzi wangu huo, ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dr. Wibrod Silaa, alinijibu hivi
PASCO,

Mwanajamvi nimefurahi sana kujitambulisha kama Political analyst. Ningelifurahi sana kusaidia Taifa lako kama analist kama ungelitusaidia yafuatayo:

i) Utafuti unaonyesha nini duniani kuhusu Leader of the Opposition katika mifumo ya mabunge yaliyoko Duniani. Kwa mtu yeyote anayefanya analysis angelitegemea kuona American Model na WestMinster Model zinaeleza nini. Analysis yako ime base kwa personalities badala ya Model na analysis ya aina hii kwa maoni yangu ni ya hatari sana kwa kuwa inakosa misingi ya kisayansi. Politics is science and should never be reduced to anything less than empirical analysis to be scientific.

ii) Analysis yako imetoa Conclusions kabla ya kujenga plausible major and minor. Scientific and logical conclusion can only be based on a well founded "major and minor". Ili tunaofuatilia tuweze kunufaika na analysis yako ningelitegemea a properly constitued logical arugement inayofuata clasical logical construction ambayo ndio msingi wa analysis yoyote ambayo ni credible.

Natanguliza shukrani za dhati, na ninategemea kupata objective political analysis ya mapendekezo yako.

Mungu Ibariki Tanzania.
Kiukweli baada ya jibu hili, mimi nikaishia kuwa mdogo tuu kama piriton, ukijumlisha na comments wa wengine, kwa kweli nilikuwa kama sisimizi!.

Hii maana yake ni nini, Chadema wakiambiwa ukweli, badala ya kusikiliza hoja na kuzifanyia kazi, wao ndio kwanza wana react na hawasikii!, kwenye uzi huo, hoja kuu nilisema Chadema isiendelee kutegemea kutwaa majimbo kwa sababu tuu CCM imechokwa!, ili Chadema ishinde kihalali very good clear and sweet victory, ni pale wananchi wanapokuwa wamehamasika na kufanya informed decision kuwa tunaichagua Chadema kwa sababu hizi, hizi na hizi, hivyo Chadema lazima ije na mkakati, itafanya nini tofauti na kinachofanywa na serikali ya CCM, ili wanaoichagua, wajione wanachagua chama mbadala.

CCM Imechokwa:
Kwenye uzi huo nilisema CCM imechokwa lakini imekuwa ikishinda chaguzi mbalimbali sio kwa sababu inapendwa sana!, no way, nilisema CCM imekuwa ikishinda chaguzi nyingi kutokana na mazoea, huku iki take advantage ya ignorance ya Watanzania, hawana choice to choose from kwa kushindanisha sera, kutokana na ujinga, na umasikini uliotopea, wengi wa wapiga kura, hawanauwezo wa kushindanisha sera, wala kujua wanachagua kwa sababu gani, bali wanachagua kwa "shibe" ya leo!, yeyote atakayekushibisha leo, huyo ndie!, hata kama atakulaza tena njaa miaka mitano ijayo, na ikifika, kama kawaida atarudi tena na T-shirt na kofia na ile shibe ya siku moja!, tutaichagua tena!, kama sio ignorance ni nini?!.

Kwenye uzi huo nilipendekeza dawa ya kuitibu CCM iliyochokwa kama ifuatavyo
Dawa pekee ya kuitibu CCM, ni kuirevamp CCM completely, task nambari moja ni Makamba should go first with his old guards team. Msisubiri mpaka uchaguzi mkuu wa chama chenu, miaka miwili ijayo (2012), itakuwa too late. If you are to do anything, doi it now and fast!. Leteni fresh blood kina January type, Kippi, Nape type and the like ambao wanaweza siasa za kisasa za dot com type.

Hakuna mwana CCM yoyote aliyekanusha kuchokwa kwa CCM, lakini haukupita muda, hiyo dose niliyoipendekeza ilidungwa CCM!, wala sijitambi kuwa CCM inafuatilia jf, au ndio chanzo cha mabadiliko hayo chanya, ukiona mbeba pakacha linavunja, ukamshtua mbebaji kuwa pakacha linavuja, akasimama kivulini na kuliziba kisha akaendelea na safari yake!, wewe unaweza kujiaminisha kuwa nimemsaidia yule mbeba paka kumtaarifu kuvuja kwa pakacha lake!, kumbe ukweli ni kuwa mbemba pakacha ulijua pakacha linavuja lakini akapanga ngoja afike kivulini ndipo alitue kuliziba na kupumzika kidogo!, hivyo useme usisema mabadiliko yangekuja!.

Kufuatia mabadiliko ya sasa ya CCM, 2015, Chadema isitegemee majimbo ya ubwete wa CCM chovu, na tena isipokuwa makini na baadhi ya wabunge wake haswa wale "vichaa!", CCM inaweza kuwapokonya, only save kwa baadhi ya maeneo ambayo machalii wa kipande hiyo, vichaa ndio huwa machaguo yao,hivyo kwa kadri unavyozidi kuwa kichaa ndivyo unavyozidi kupendwa na kukubalika!.

Uso kwa Uso na Dr. Slaa!.
Niliwahi kwenda ofisini kwa Dr. Slaa for official visit, wakati huo nikiwa utumwani kwenye utumwa fulani, hivyo unapokuwa mtumwa, ukitumwa mahali, unawakilisha kile ulichotumwa na bwana wako aliyekutuma, hivyo sijihesabu kama mimi nilionana na Dr. Slaa!.

Siku tulionana rasmi na kwa nafasi, ni pale tulipokutana tuu mahali, sote tukiwa safarini, tukatokea kujipumzisha mahali na kupata mlo, hivyo kukutana kwa bahati!.

Kwa vile mimi ni mwandishi, kwanza nilimkabili, na kuamsalimia huku nikitanguliza kuomba radhi, maana mahali hapo ni privacy ya mtu, na watu wako na watu wao, hivyo mwandishi kupenyeza penyeza pua its uncalled for!, ila nikakaribishwa!.

Nakumbuka vuzuri nilimweleza resevations zangu kwa "Chadema kutokujipanga" na haswa kuhusu utaratibu wake wa kupata viongozi wake na wagombea!.
Nilisema nimenote wengi wa wagombea wao, ni wagombea sadakalawe!, baada ya kukosa kwenye ile sadalawe ya kule, then hukimbilia huku na ndivyo Dr. alivyoingia Chadema. Nikasema huwezi kushinda uchaguzi na kushika dola kama hauna able people behind!. Nikashauri, kama kweli Chadema kina nia ya dhati ya kushika dola 2015, lazima kitayarishe watu, by investing in people, hakiwezi kushika dola kwa kuwategemea wagombea wanaopatikana kwa game of chance!. Lazima Chadema ifanye "head hunting" ya able people na ikikosa "able people", ifanye hata spotting na grooming from grassroot, ili ijenge kada yake ya viongozi iliyowalea na kuwakuza kichadema, ambao hawa watakuwa ni waaminifu na tegemeo lake, na sio kusubiria "makapi" ya CCM!.

Kusema ukweli, Dr. Slaa alinieleza a very fine na promising strategies, zikiwemo succession plan, pia alinieleza msimamo wake binafsi kuhusu kugombea tena urais 2015!, hivyo mimi ni mmoja wa watu wachache sana wanaujua msimamo wa Dr. Slaa kwenye kugombea urais 2015 from the horses mouth!. (Naomba nisiutaje humu kwa sababu mazungumzo yetu yalikuwa informal hivyo ni off the record).

Chadema Haijajipanga!.
Matokeo mabaya Chadema katika baadhi ya chaguzi ndogo za ubunge na udiwani, ni uthibitisho kuwa Chadema bado haijajipanga!. Hata ushindi wa Chadema Arumeru kwa kijana Nasari, umechangiwa na support ya vita vya wenyewe kwa wenyewe CCM ndani kwa ndani kulikomoa chaguo la yule "jamaa yangu". Kama wengi mtakuwa na maswali, Chadema ijipange kwenye nini, mnaweza kunitembelea hapa nimeeleza kila kitu!. Kuelekea 2015: CHADEMA Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If ...

Chadema Hamjipangi!.
Hata baada ya kipigo kitakatifu cha Kalenga, kuna kitu nimewashauri Chadema kuhusu uchaguzi wa Jimbo la Chalinze!, ili Chadema kujionyesha chenyewe ni kidume, au kuvunjika kwa koleo sio mwisho wa uhunzi, bado itang'ang'ana na kuendelea kutumbukiza pua Chalinze!, angalau kwa Kalenga picha ilikuwa haisomeki sana!, Chalinze ndio maeneo ya strong hold ya wale vibonde niliowazungumzia kule ambao ndio mtaji wa CCM!. Uchaguzi Mdogo Jimbo la Chalinze: CHADEMA Muungeni mkono mgombea ...

Uchaguzi kama vita!, ukijijua huwezi kushinda, ule msemo wa "no retreat, no surrender" wa "kupigana hadi risasi ya mwisho na tone la mwisho la damu limwagike!" huo ndio huo unaitwa "ushujaa!" alikufa vitani akiipigania nchi yeke!, mkiisha malizika wote, adui atapata walk over victory kuitwaa nchi yenu yote na nyinyi nyote kugeuka mateka!. Wapiganaji makini ni wale wakishajipima na kujiona hawawezi, hurudisha majeshi nyuma (retreat) na kujipanga upya!.
Chadema wakikubali ku retreat na kujipanga upya, wata boost kidogo morali ya wapiganaji wake, kiliko kuendelea kupeleka vikosi vyake vitani na kuishia kuwa wiped!.

Na Kwa 2015!, Chadema Haitajipanga!.
Kwa maoni yangu, Bunge hili Maalum, likifuatiwa na kikao cha Bunge, then kura ya maoni, then uchaguzi wa serikali za mitaa!, then uchaguzi wa ndani wa Chadema (uongozi uliopo madarakani kwa mujibu wa katiba ya Chadema, umalizika mwaka huu baada ya kuuongezea mwaka mmoja!, katiba ya Chadema haikutoa any possibility ya extra extension, japo uongozi wa Chadema unaweza kumuandikia Msajili na kulitaja Bunge Maalum ni "force majeure" hivyo kutofanya uchaguzi wake wa ndani kihalali kabisa!". Ndipo ufuate uchaguzi mkuu, huku kuna ile pending case!!. Kikweli kabisa, my honest opinion, kwa time iliyobakia kabla ya uchaguzi mkuu wa 2015, mambo yaliyopo mbele ya Chadema ni too much! kwa Chadema kujipanga and the time is too little too late!, hivyo naiona wazi kabisa CCM ikirudi kujichukulia nchi kiurahisi kama imeokota!.

Hitimisho: Chadema na "Karma!"
Namalizia kwa kusisitiza, Chadema katika kupanga mambo yenu, zingatieni sana hii kitu inaitwa "Karma", msiidharau kabisa!, karma is real!.
Do the right thing or else!.

Poleni kwa ya Kalenga!.

Jipangeni

Paskali

NB. Paskali, ni mwanachama wa chama cha siasa na mtazamaji mzuri tuu wa hii game la siasa kazi yake ikiwa kutazama tuu!, na kueleza, na kutoa ushauri wa bure!.
 
Unampigia zitto kurudi?

Sasa kulikuwa na ulazima gani ku-quote habari nzima ya Pasco ili kuandika sentensi ya mstari mmoja!?

Mijitu mingine sijui ni mishamba ya wapi. Hii tabia inakera sana.

Jifunzeni kutoa maoni yenu tu na sio lazima ku-quote habari nzima. Hicho kitufe kimewekwa kwa wale wenye kutaka kutoa ufafanuzi/usahihi wa kina kwenye hoja ya mleta mada.
 
strategies za chadema ni zero. badala ya kujenga chama ngazi za chini kabisa wenyewe wanaruka na chopa tu kama machizi

Hili niliwahi kuliongelea sehem...CDM.. haina mashina mitaani...hata matawi yenyewe sio imara na machache....ccm wao wana wajumbe Wa Nyumba kumi kumi karibu Tanzania nzima ktk mitaa yote ..na hawa wajumbe wanawajua watu wao....wana rekodi za wapiga kura...tena sehemu zingine wanajua hadi Nyumba zenye kura zao....
Leo hii ukiniambia ni mitaa ipi ina Mjumbe Wa shina Wa cdm cjui km wapo.

Cdm inatakiwa kufanya hivi...iwe na mashina toka mitaani...

Ccm baadhi ya maeneo wameanza kujipanga kwa ajiri ya uchaguzi Wa serikali za mitaa..kwa kuwaambia wajumbe wahakiki watu wao..( wapiga kura)..

Mimi sio mtu Wa siasa ila napenda mabadiliko..namuelewa mtoa hoja@Pasco
 
Sidhani kama tatizo ni CHADEMA kutojipanga. Mi nadhani CCM na Rais hawako tayari kuachia madaraka kwa amani na ndiyo maana Rais akatoa amri kwa Green guards na tumeona ikitekelezwa Kalenga.
http://m.youtube.com/watch?v=xQi0PAy...e_gdata_player

Katika mazingira kama haya CHADEMA inabidi wajipange KUFA NA KUPONA? -Nilipoiangalia hii video nikajua umuhimu wa katiba itakayoruhusu Rais kushitakiwa kwa makosa ya makusudi aliyoyafanya akiwa Rais.
 
Sidhani kama tatizo ni CHADEMA kutojipanga. Mi nadhani CCM na Rais hawako tayari kuachia madaraka kwa amani na ndiyo maana Rais akatoa amri kwa Green guards na tumeona ikitekelezwa Kalenga.
http://m.youtube.com/watch?v=xQi0PAy...e_gdata_player

Katika mazingira kama haya CHADEMA inabidi wajipange KUFA NA KUPONA? -Nilipoiangalia hii video nikajua umuhimu wa katiba itakayoruhusu Rais kushitakiwa kwa makosa ya makusudi aliyoyafanya akiwa Rais.

Vipi kuhusu kauli ya Dr Slaa iliyosema "damu lazima imwagike"?

Kumbuka mhe rais Kikwete alitoa hiyo kauli kama mwenyekiti wa CCM, na Dr Slaa alitoa hiyo kauli yake kama katibu mkuu wa CHADEMA. Haya nambie unasemaje kuhusu kauli ya babu?
 
Wanachama wa Chadema msipuuze huu uzi wa Pasco hata ikiwezekana muwafikishia Viongozi wenu ni kichaa tena yule aliekimbia Mirembe ndio anaweza sema kilichoandikwa humu hakuna kitu.
 
Nakuunga mkono Mia kwa Mia mkuu Pasco, huwezi kushindwa mfululizo na kujiona bado una nguvu.

Tuliwahi kuwashauri hawa jamaa kuwa wajitahidi kuwa na ofisi ngazi ya wilaya na kuajiri makatibu wa wilaya watakaokuwa wanalipwa mshahara na chama badala ya kuwa na viongozi wa kujitolea ambao ukifika wakati wa uchaguzi CCM inawanunua, au wengine wanaficha fomu za wagombea CCM inapita bila kupingwa. At least CHADEMA ingeanzia hata ngazi ya mkoa kuwa na makatibu wa kuajiriwa, wenye JOB SECURITY kwenye kazi ya chama, ambao wanatumwa kokote, watafanya kazi za chama kama Pasco anavyofanya kazi za PPR. Kutegemea watu wanaojitolea ni udhaifu ambao CCM wanautumia toka 1995 kwa kuweka watu wao ndani ya vyama vya siasa. Mwisho mnabakia kuwaita wasaliti huku mnasahau kuwa njaa ndio iliwatuma.

Mwisho nasema kutegemea kurusha helikopta katika sehemu ambazo haukuwa na matawi kama kalenga ni TOP DOWN APPROACH, hakuna chama kimefanikiwa duniani kwa hii approach. Grassroot system ndio njia pekee, weka matawi ngazi za chini, wape mamlaka wajiongoze. Kusubiri Slaa na Mbowe waje kwenye operation Sangara ni siasa za kizamani, acheni matawi yafanye operation dagaa ili sangara akija akute kuna samaki wengine pia.
 
Vipi kuhusu kauli ya Dr Slaa iliyosema "damu lazima imwagike"?

Kumbuka mhe rais Kikwete alitoa hiyo kauli kama mwenyekiti wa CCM, na Dr Slaa alitoa hiyo kauli yake kama katibu mkuu wa CHADEMA. Haya nambie unasemaje kuhusu kauli ya babu?

Dr Slaa alisema dhuluma, wizi, ufisadi na kuminya haki za raia mnakofanya maCCM kuna siku damu lazima itamwagika. Hakusema IMWAGIKE kama ma spin doctors mnavyotwist. Na damu imemwagika kweli, Yuko wapi Ally Zona, yuko wapi Mwangosi, wako wapi wahanga wa January 5, wako wapi wahanga wa Soweto na Olasiti. Kote huko Savimbi Nchemba amapoteza damu za watu kwa vile Kikwete alipuuza ushauri wa Dr Slaa ambao ungezuia damu kumwagika
 
Chadema kuingia Ikulu ni ndoto ya mchana kweupe peee.... Kwakifupi bado sana tena sana.
 
Ndugu Pasco nakupa salute kwa ushauri wa hekima kwa wapenda mageuzi. Chadema huwa hawataki kukiri kwa wapenzi wao kuwa hata maeneo wanayobahatika kushinda na sababu ya kura za maruhani za wapenzi wa CCM, Mf. Ubungo, Iringa mjini, na hata Mwanza na juzi udiwani Njombe mjini. Kosa jingine ni kuwavimbisha vichwa watu wa maeneo fulani tu ndio wanaweza kusimamia mageuzi mf. kupeleka vijana toka maeneo mengine Kalenga kulinda kura, vijana kama hawa kisaikolojia hujiona bila wao Chama ni hoi wanafanya na mengine ya kupitiliza na kuwadhibiti ni kazi, waulizeni Simba na Yanga na tabu wanayopata kuwadhibiti 'Baunsa' wao. Chadema gari inayodaiwa kutekwa siku ya uchaguzi watu wale walitoroka Iringa saa kumi jioni ilikuwa Ruaha mbuyuni ina yeya na bendera zake kurudi Dar baada ya kukwepa msala.
 
Pasco naona unatafuta ugali kwa kila njia. Uko tayari uwe kituko kama sasa kwenye huu uzi lakini kwakuwa watoto watapishana maliwatoni, wewe hujali
 
Last edited by a moderator:
Samaki mkunje akiwa angali mbichi!. Siasa za kilaghai haziwezi kupambana na uharisia wa kisiasa nchini.

Pasco acha "kupotosha" wanaJf. CHADEMA ni chama makini na kimejiandaa kuchukua nchi 2015, come rain or shine!.

CHADEMA haliwezi kuwa ni sikio la kufa bali ni sikio ambalo limeisha kufa muda mrefu na kilichobaki ni maziko.

Soma maelezo hapa chini ya Katibu Mkuu wa CHADEMA akiwaambia washabiki, wapenzi na wanachama wa CHADEMA.

Appriciator na Watanzania,

Nimefuatilia mjadala kwa ujumla. Kwa manufaa ya wengi naomba nitoe taarifa ifuatayo:
1. Awali narudia kauli niliyotoa na imetolewa Mara nyingi na viongozi wa Chadema kuwa ndani ya Chadema hakuna mwenye hati miliki ya Chama, na hivyo maamuzi ya Chadema, kwa mambo yanayohusu chama au nje ya Chama hufanywa kufuata Katiba ya Chama, Kanuni ya Chama na au maazimio ya vikao vya maamuzi yaani Kamati Kuu, Baraza Kuu na Mkutano Mkuu.

2. Tumekwishasema kutangaza Mara kadhaa kwenye Press Conference mbalimbali baada ya vikao hivyo, kuwa Chadema imeamua kutekeleza sera yake ya Kanda/Majimbo ndani ya Chama wakati inajiandaa kutekeleza sera hiyo katika muundo wa utawala wa Taifa letu wakati utakapofika. kanda 8 za Bara zimekwisha kuundwa, na Kanda 2 za Zanzibar zinasubiri kuundwa baada ya kujua mwelekeo wa Katiba Mpya. chaguzi za viongozi wa Kanda zilikamilika mwezi Augusti, 2013. Uundwaji huo wa Kanda ambao ulisimamiwa katika Kanda zote na Mhe. Freeman Mbowe ulisimamiwa na Freeman Mbowe(MP), Mwenyekiti wa Chama na uchaguzi wa Viongozi wa kisiasa umefanyika katika ngazi zote. Hatua inayoendelea kukamilika sasa ni uteuzi wa viongozi watendaji yaani Mratibu wa Kanda na Afisa wa Kanda na viongozi wasaidizi. Nafasi hizo zote zimetangazwa kwenye vyombo vya habari na kwenye maeneo yote ya Kanda husika. Ofisi ya Katibu Mkuu imekwisha kuletewa mapendekezo mbalimbali kwa uteuzi wa mwisho, na kazi hii inategemewa kukamilika kufuatana na speed ya kila kanda kukamilisha taratibu zilizo chini ya mamlaka yake.

3. Nilikwisha kutangaza Mara kadhaa, lakini nafafanua ten a kwa manufaa ya watanzania wengi wanaoweza kukwazwa na upotoshwaji unaoendelea.

a) Tulipanga kutoa mafunzo ya kina kuanzia ngazi ya Taifa, Kanda, majimbo na Kata kwa viongozi wetu wapatao 36,000 watakaokuwa injini ya kujenga na kuimarisha mtandao wa chama kwa nchi nzima. Nilitoa Taarifa kuwa kaxini ya wakufunzi hao ni kuunda timu za kufungua misingi ya Chadema ( kwa ccm ni Mashina) ipatayo 250,000 nchi nzima yaani kuwa na msingi wa Chadema kwa kila shina la ccm. Aidha baada ya kutoka kwenye misingi watafanya kazi hiyo pia kuunda na au kuimarisha pale ambapo tayari kuna matawi. Lengo ni kuwa na matawi 18,000 kwa nchi nzima. Yaani kuwa na tawi kila palipo na tawi la ccm, ili tubanane huko huko vijijini. Kazi ya mafunzo ikifanyika kwa ufanisi, na sasa kazi iliyoko ni kufungua misingi na matawi, kaki ambayo kwa formation iliyoko inategemewa kukamilika mwezi wa October. Ni kweli kazi hii imechelewa kwa mwezi mmoja kutokana na mwingiliano wa shughuli mathalan uchaguzi mdogo wa madiwani, zoezi la ukusanyaji wa maoni ya Katiba, mambo ambayo chadema hatuna mamlaka ya ratiba yake.

C) Baada ya kuunda misingi na matawi uundaji na uchaguzi katika ngazi ya kata, majimbo wilaya hadi Taifa itafuata, na ngazi hizo hazina kazi kubwa Kama ngazi ya msingi na matawi kwa vile zina idadi kubwa, lakini pia indigo walk wanachama. Ngazi ya kata kwenda juu ni ngazi za uongozi tu, na wanaohusika kwenye ngazi hizo ni viongozi hivyo kaki inakuwa rahisi zaidi.

Hivyo, watanzania muelewe kuwa Chadema ni chama makini, inafanya kaki zake kisayansi siyo kwa propaganda. Huwezi kuzungumzia uchaguzi bila kufanya kazi ya kujenga chama. Wengi hawajui uzito wa kazi hiyo, kumbukeni Mwl. Nyerere Aliwahi kujiuzulu ili avenge mtandao wa Tanu. Ndipo baada ya kukamilisha kaki hiyo akarudi kuwa Raisi wa kwanza wa Jamhuri ya Tanganyika. Uchaguzi unafanyika baada ya kuwa na chama imara. Ndiyo kazi inayofanyika, na ninawapongeza wale makamanda wote wanaofanya kaki hiyo katika mazingira magumu sana. Nina hakika wote hao wataingia katika historia ya ukombozi wa pili wa Taifa letu.

Ni Imani yangu kuwa baada ya ufafanuzi huu watakaopenda kubishana na kufanya propaganda ni juu Yao. Mwenye kutaka kupokea elimu hii naomba aeleze na kwa wengine pia ili kuwasaidia. Mungu Ibariki Tanzania Mungu Ibariki Chadema.

Unaweza kusoma hii thread kupitia hapa,
 
Hiki chama ni sawa na kundi la misukule hawajui walipo,hawelewi walipotoka wala hawajitambui wanakokwenda, kushabikia chadema lazima uwe na akili za kobe.
 
Back
Top Bottom