Wanabodi,
Hili ni bandiko la swali la tathmini kuihusu Chadema, seriousness yake, its abilities and the capabilities. Hivi CHADEMA, inawezo wa kushinda uchaguzi wa 2020?, na hata ikatokea ikashinda, jee inaweza kuendesha nchi?. Is it a Serious Party?, is it Credible?. Is it Organized?, does it have Succession Plan?. Is it Mature Enough Opposition, Kuweza Kukabidhiwa Nchi yetu 2020?!.
Maswali haya ni kufuatia tathmini yangu jinsi Chadema inadeal na baadhi ya issues mbalimbali ikiwemo the current one ya uteuzi wa wawakilishi wake kwenye Bunge la EALA.
Kutawala nchi sio jambo dogo au jambo la mchezo mchezo. Ikulu yetu haipaswi kugaiwa kwa majaribio bali kwa uhakika, tutakaye mkabidhi ikulu yetu ni lazima kwanza atuthibitishie amekomaa, na anawezo, mature enough with the abilities and capabilities, na sio tuu kumpa mtu ikulu yetu kwa kumjaribishia simply kwa sababu tuu CCM imeshindwa hili na lile na baadhi ya watu wameichoka sana CCM!.
CCM inaendelea kuchaguliwa mwaka hadi mwaka, na itaendelea kuchaguliwa sio kwa sababu CCM is the best, au CCM imeweza au inauwezo kivile!, no!. CCM imeshindwa na ilishindwa siku nyingi na inaendelea kushindwa, kwa kufanya madudu mengi tuu lakini bado imekuwa ikiendelea kushinda kwa kuchaguliwa mwaka hadi mwaka kwa mazoea tuu kwa sababu, Tanzania bado hatuna mbadala muafaka wa kuiondoa CCM!.
Yaani Tanzania bado hatuna any serious and a credible opposition party ya kuwapa wapiga kura wa Tanzania a choice to choose from, hivyo CCM kujikuta ikiendelea kuchaguliwa na kushinda kwa ku sail through na upepo wa mazoea, kwa sababu ndio the only one iliyopo!, we have no any serious credible choice to choose from, hivyo we have no choice. Matokeo yake ni CCM inashinda kwa easy ride ya mazoea na itaendelea kushinda na kushinda tena na tena mpaka tutakapo pata a credible opposition such that we'll have a choice to choose from!.
Kwa Zanzibar hakuna ubishi kuhusu uwezo wa CUF as a credible opposition kuweza kutawala Zanzibar, lakini kwa upande wa huku Tanzania Bara, bado kabisa hatuna any serious and a credible opposition ya kuiondoa CCM na kuikabidhi Ikulu yetu.
CHADEMA ndio angalau angalau wameonyesha nia, na kiukweli wakiamua, wanaweza kabisa, ila natatizwa na haya madudu madogo madogo yanayo onyesha all signs za immaturity kwa upande wa Chadema, such that bado ni chama ambacho hakijaonyesha ukomavu wa kutosha enough to convince Tatanzanians kuikabidhi ikulu yetu comes 2020, waipige chini CCM na kuikabidhi Chadema Ikulu yetu ya Magogoni.
Jee kwa maoni yako, unaiona Chadema as a credible, serious opposition, iliyokomaa na kuwa mature enough with the ability and credibility ya kukabidhiwa ikulu yetu 2020?.
Kwa upande wangu, honestly, I don't think, ila kabla sijasema why I don't think and what should we do, naomba kupata mawazo yako, assuming uchaguzi wa Tanzania utaendeshwa kwa uhuru na haki, na chama kitakacho shinda kimeshinda kwa haki, Jee Chadema hata kikishinda, kinauwezo?. Kimeonyesha uwezo wa utayari wa kutawala nchi endapo kitashinda uchaguzi 2020?. Ila kabla hata hakijashinda huo uchaguzi wa 2020, kwa Chadema hii tunayoiona sasa, jee inao huo uwezo wa kushinda?.
Na hata tukiachana na udhaifu wa upinzani imara, everything has it's limits, suppose CCM imewafikisha Watanzania at their limits wakaamua sasa imetosha, they've had enough of CCM and now they are fed up hivyo kuamua liwalo na liwe, wakaipiga chini CCM kwenye sanduku la kura na kuichagua Chadema, jee CCM itakubali kuachia?. Can you just imagine mtu aliyepo Ikulu kukabidhi madaraka sijui kwa nani hiyo 2020, is it possible?.
Kuna mtu yoyote ameishawahi maandalizi yoyote ya succession plan ya serikali, vyombo vyetu vya dola na vyombo vya ulinzi na usalama kukitumikia chama kingine chochote nje ya CCM?.
Kwanza tuu hata ikatokea Watanzania wengi zaidi wakaichoka CCM na kuipiga chini kwenye sanduku la kura, jee huyo mshindi halali atatangazwa?!. Au inawezekana zoezi zima la uchaguzi wa vyama vingi ni kwenye ubunge tuu na udiwani, lakini kwenye urais, licha ya the playing field kutokuwa level, inawezekana uchaguzi wa rais ni igizo tuu la uchaguzi?!.
Nawatakia Furahi Dai Njema.
Paskali.
Rejea.
CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga! - jamiiforums.com
CHADEMA: Tujadili Utayari wa Kutawala Nchi 2015 | Page 7 ...
Kuelekea 2020: CHADEMA Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If ...
Kuelekea 2020: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM ...
CHADEMA Ikipewa Nchi, October 2020, Hakuna Hatari Kugeuka Utawala ...
Mtazamo: Kanda ya Kaskazini, CCM imechokwa mpaka basi ...
Kuichagua tena CCM, Je ni kielelezo cha kufanya informed decision ...
Ikitokea CCM ishinde, Je ushindi huo ni kutokana kuwekeza kwenye ...
Watanzania ni ignorants au tumelogwa?
CHADEMA Hamkujipanga, hamjajipanga, hamjipangi na hamtajipanga ...
Wenye Matumaini na Upinzani Kushika Dola!, Sahauni! CCM Inajiandaa Kuua Kabisa na Kuuzika Jumla
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?
Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana, kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!. Apunguze...