Je, CHADEMA inaweza kushinda 2020? Is it serious, credible & mature enough opposition?

Tatizo la CHADEMA ni Mbowe

Kile chama kimekuwa kikubwa sana kuliko uwezo wake

Yes..Amefanya mengi..lakini uwezo wake umefika mwisho...Hawezi kufanya kingine kipya ambacho hajawahi kufanya...Tatizo kubwa zaidi ni yeye anaamua kila kitu

Huwezi kufanya jambo lile lile kila siku...kwa namna ile ile na kutegemea majibu tofauti...

CHADEMA ikitaka kutokufa ikubali kufanya mabadiliko ya ndani ya msingi kabisa na kukihuisha chama .

Chama kikijenge katika msingi imara na thabiti ya kitaasisi.....waweke mifumo inayowawezesha kuweka sera imara...tested policies...na mwisho watengeneze demokrasia ya kweli ndani ya chama.

Tatizo la CHADEMA ni CCM ya Magufuli!
Mbowe hawezi na hatakuja kuwa tatizo la CHADEMA!
Kama kuna kitu kinawanyima CCM na Magufuli wao usingizi basi ujue ni CHADEMA chini ya uongozi imara na mahiri wa Mwenyekiti Mbowe! Hii siyo siri na hata Magufuli analijua hilo!
 
Uchaguzi wa kesho wa Mwenyekiti wa Chadema ni very instrumental kwenye mustakabali wa 2020, kama mtajichagulia tuu kwa ule ule utaratibu wenu wa mazoea ya as usual, matokeo ya uendeshaji wa Chadema pia utakuwa as usual, lakini kama mtaamua kufanya changes, then things will change hata Uchanguzi Mkuu wa 2020 mnaweza angalao kuambulia ambulia.

P

P,
Kabla ya Uchaguzi wa CHADEMA wewe ulikuwa ni mmoja wa walokuwa wana chagiza Cecil Mwambe achaguliwe badala ya Mhe. Mbowe!
Wana CHADEMA sio wajinga kama ww na puppets wenzako wa CCM! Walikaa wakatafakari na kuchagua kilicho bora: Mhe. Freeman Aikael Mbowe.
Kusema kuwa CHADEMA wataambulia ambulia 2020 ni matusi kwa Wanachadema! Hiv mara hii wewe na puppets wenzako mmesahau kuwa CHADEMA walipata KURA MILIONI 6+ (pamoja na juhudi kubwa za wizi na Uchakachuaji) ili kuibeba CCM kwene Uchaguzi Mkuu~2015? Hizi kura kwa akili yako unafikri ni zakuambulia ambulia kweli ?
 
Uchaguzi wa kesho wa Mwenyekiti wa Chadema ni very instrumental kwenye mustakabali wa 2020, kama mtajichagulia tuu kwa ule ule utaratibu wenu wa mazoea ya as usual, matokeo ya uendeshaji wa Chadema pia utakuwa as usual, lakini kama mtaamua kufanya changes, then things will change hata Uchanguzi Mkuu wa 2020 mnaweza angalao kuambulia ambulia.

P
Washauri wenzako waruhusu tume huru ya uchaguzi,uchaguzi sio lazima chama kishinde uchaguzi ni haki ya kila chama kishiriki na haki itendeke
Kama ccm watashinda kwa haki Kuna tatizo gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawawezi kushinda hawajajiandaa kushinda ,hawana sera safi , siasa safi kazi yao kupinga tu na kukosoa kila uchwao lakin hawahubiri kwa habari ya maisha mazuri kwa wananchi wapo wapo tu

sent from toyota Allex
 
Weka uwanja wa siasa sawa then uwapime washindani wote kwa kutumia same sampling....

Sijawahi kuona tunafanya uchaguzi nchi ulio huru na haki bali huwa ni justification tu....anayekwenda kutawala anakuwa kishachaguliwa tayari na watu wasiozidi watatu.

Kuna safari ndefu mno kufikia ile demokrasia ya kweli...kwamba mawazo ama maamuzi ya wengi ndiyo yapite...kwa nchi za kiafrica bado saana.
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali la tathmini kuhusu upinzani kuweza kuchukua nchi uchaguzi wa 2020. Kwa upande wa huku Tanzania Bara, ulizungumzia upinzani ni unazungumzia Chadema, hivyo hili bandiko kuihusu Chadema, as a representative wa upinzani kwa huku Tanzania Bara, vipi kuhusu Chadema, seriousness yake, its abilities and the capabilities kuelekea uchaguzi wa 2020. Hivi CHADEMA, hii, hivi ilivyo, inawezo wa kushinda uchaguzi wa 2020?, na hata ikatokea ikashinda kwa muujiza tuu kama wa Kenya, Zambia na Malawi, jee inaweza kuendesha nchi?. Is it a Serious Party?, is it Capable, is it Credible?. Is it Organized?, does it have Succession Plan?. Is it Mature Enough Opposition, Kuweza Kukabidhiwa Nchi yetu 2020?!.

Maswali haya ni kufuatia tathmini yangu jinsi Chadema inavyo deal na baadhi ya issues mbalimbali na ndogo ndogo tuu ikiwemo the current one ya uteuzi wa wawakilishi wake kwenye Bunge la EALA. Chadema kuna wakati ina behave childish na ikikwama kwa kutofuata sheria, taratibu na kanuni, ina pandisha na kupaza loud noises za baby cry kuwa inaonewa!.

Kutawala nchi sio jambo dogo au jambo la mchezo mchezo. Ikulu yetu haipaswi kugaiwa kwa majaribio bali kwa uhakika, tutakaye mkabidhi ikulu yetu ni lazima kwanza atuthibitishie amekomaa, na anawezo, mature enough with the abilities and capabilities, na sio tuu kumpa mtu ikulu yetu kwa kumjaribishia simply kwa sababu tuu CCM imeshindwa hili na lile na baadhi ya watu wameichoka sana CCM mpaka basi!.

CCM inaendelea kushinda na kuchaguliwa mwaka hadi mwaka, na itaendelea kuchaguliwa sio kwa sababu CCM is the best party, au CCM imeweza au inauwezo kivile!, no!. CCM has failed this nation, since then, CCM imeshindwa na ilishindwa siku nyingi na inaendelea kushindwa, kwa kufanya madudu mengi tuu ya ajabu ajabu, lakini bado imekuwa ikiendelea kushinda kwa kuchaguliwa mwaka hadi mwaka kwa mazoea tuu kwa sababu, Tanzania bado hatuna mbadala muafaka wa kuiondoa CCM!.

Yaani Tanzania bado hatuna any serious, capable and a credible opposition party ya kuwapa wapiga kura wa Tanzania a choice to choose from, hivyo CCM kujikuta ikiendelea kuchaguliwa na kushinda kwa ku sail through na upepo wa mazoea, kwa sababu ndio the only one iliyopo!, we have no any serious, capable na credible choice to choose from, hivyo we have no choice. Matokeo yake ni CCM inashinda kwa an easy ride ya mazoea na itaendelea kushinda na kushinda tena na tena mpaka tutakapo pata a credible opposition such that we'll have a choice to choose from!.

Kwa Zanzibar hakuna ubishi kuhusu uwezo wa CUF as a credible opposition kuweza kutawala Zanzibar, lakini kwa upande wa huku Tanzania Bara, bado kabisa hatuna any serious, capable and a credible opposition ya kuiondoa CCM na kuikabidhi Ikulu yetu.

CHADEMA ndio angalau angalau wameonyesha nia na dalili za kuweza kuaminiwa, na kiukweli wakiamua, wanaweza kabisa, ila natatizwa na haya madudu yao madogo madogo yanayo onyesha all signs za immaturity kwa upande wa Chadema, such that bado ni chama ambacho hakijaonyesha ukomavu wa kutosha enough to convince Tanzanians kuikabidhi ikulu yetu comes 2020, waipige chini CCM na kuikabidhi Chadema Ikulu yetu ya Magogoni.

Jee kwa maoni yako, unaiona Chadema as a credible,capable na serious opposition, iliyokomaa na kuwa mature enough with the ability, capability and credibility ya kukabidhiwa ikulu yetu 2020?.

Kwa upande wangu, honestly, I don't think, ila kabla sijasema why I don't think and what should we do, naomba kupata mawazo yako, assuming uchaguzi wa Tanzania utaendeshwa kwa uhuru na haki, na chama kitakacho shinda kimeshinda kwa haki, Jee Chadema hata kikishinda, kinauwezo?. Kimeonyesha uwezo wa utayari wa kutawala nchi endapo kitashinda uchaguzi 2020?. Ila kabla hata hakijashinda huo uchaguzi wa 2020, kwa Chadema hii tunayoiona sasa, jee inao huo uwezo wa kushinda?.

Na hata tukiachana na udhaifu wa upinzani imara, everything has it's limits, suppose CCM imewafikisha Watanzania at their limits wakaamua sasa imetosha, they've had enough of CCM and now they are fed up hivyo kuamua liwalo na liwe, wakaipiga chini CCM kwenye sanduku la kura na kuichagua Chadema, jee CCM itakubali kuachia?. Can you just imagine mtu aliyepo Ikulu kukabidhi madaraka sijui kwa nani hiyo 2020, is it possible?.
Kuna mtu yoyote ameishawahi kusikia maandalizi yoyote ya succession plan ya changing arms kwa vyombo vya serikali, na vyombo vyetu vya dola na vyombo vya ulinzi na usalama, kujiandaa kukitumikia chama kingine chochote nje ya CCM?.

Kwanza tuu hata ikatokea Watanzania wengi zaidi wakaichoka CCM na kuipiga chini kwenye sanduku la kura, jee huyo mshindi halali atatangazwa?!, na Tume hii hii?!, Au inawezekana zoezi zima la uchaguzi wa vyama vingi ni kwenye ubunge tuu na udiwani, lakini kwenye urais, licha ya the playing field kutokuwa level, inawezekana uchaguzi wa rais ni igizo tuu la uchaguzi?!.

Nawatakia Furahi Dai Njema.
Paskali.
Rejea.
CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga! - jamiiforums.com

CHADEMA: Tujadili Utayari wa Kutawala Nchi 2015 | Page 7 ...

Kuelekea 2020: CHADEMA Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If ...

Kuelekea 2020: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM ...

CHADEMA Ikipewa Nchi, October 2020, Hakuna Hatari Kugeuka Utawala ...

Mtazamo: Kanda ya Kaskazini, CCM imechokwa mpaka basi ...

Kuichagua tena CCM, Je ni kielelezo cha kufanya informed decision ...

Ikitokea CCM ishinde, Je ushindi huo ni kutokana kuwekeza kwenye ...

Watanzania ni ignorants au tumelogwa?

CHADEMA Hamkujipanga, hamjajipanga, hamjipangi na hamtajipanga ...

Wenye Matumaini na Upinzani Kushika Dola!, Sahauni! CCM Inajiandaa Kuua Kabisa na Kuuzika Jumla

Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana, kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!. Apunguze...

Lizarazu
Ili kukiondoa chama tawala lazima tujiulize Maswali kama haya Je CCM amabacho ni chama tawala kimeshindwa kuleta matokeo chanya kwa wananchi? Kama kujenga miundo mbinu, kutoa huduma za afya na kuhakikisha nchi na rasilimali zake zinalindwa . Usalama wa mali na raia unalindwa? Kwa ujumla Chama tawala lazima kiwe kimeshindwa kuongoza nchi.Pia lazima tujiulize huyo anayekuja kutawala ataweza kuyatekeleza haya? Mimi binafsi naona Chama tawala kinatekeleza vizuri katika kuongoza nchi. Maana ufisadi umezibwa, miundo mbinu imejengwa na mengine yanatekelezwa vizuri tu. Hasa katika suala la kuhakikisha rasilimali za nchi zinalindwa. Sasa Chadema kama chama cha upinzani wana hoja gani ya kuweza kusema wanaweka mgombea ili kukiondoa chama Tawala. Pia Tangu Dk wilbroad slaa ashuhudie choo kinapakuliwa na kuwekwa sebuleni na akambonyeza Prof safari unayaona hayooo! Chadema wananchi hawana imani nayo sana kimekuwa kama chama cha wazee wa dili tu.
N.B mimi si mwanachama wa chama chochote.
 
Aiseee CCM wacha iitwe CHUKUA CHAKO MAPEMA.

Ila chadema kamweeeeeee madarakan never.

UKANDA DAIMA UTAWATAFUNA.

MFIA CHADEMA RUKSA KUBOBOKA.

Wapinzani halisi waja lipo tumaini na hawatatoka CCM kama ticha alivyowaaminisha Zama zake.
 
Labda washinde njaa!

Kwa hizi rough zilizoonekana Local government na by elections na reaction yao ni dhahiri hata hiyo November watakuwa frustrated kwa figisu ili wasuse halafu ngoma inatambaa.

Wataanza maigizo ya UN na The Heague zile balozi viherehere vitatoa tamko then Who cares?

Bado safari ni ndefu sana! Decades!!
 
Ingekuwa Hivi Alivyondika Pascal Mayala Basi Mama Zetu Nina Hakika Wasingetuzaa Yaani Mama Akizaa Mtoto Mwenye Matatizo Huwa Siyo Mwisho Wa Uzazi

Sasa Mature Unaypitaka Wewe Ni Ipi?
Duniani Kote Vyama Mbalimbali Vinaongaza Nchi Zao Bila Hilo Neno Mature
Watanzia Wengi Wanataka Kuona Ccm Siku Moja Inapisha Tena Kwa Amani Sana

Tuendelee Na Ccm Hata Kama Itashindwa Uchaguzi Ndicho Ulichoandika Wewe
Huyu jamaa hoja yake ni dhaifu sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ili kukiondoa chama tawala lazima tujiulize Maswali kama haya Je CCM amabacho ni chama tawalakimeshindwa kuleta matokeo chanya kwa wananchi? Kama kujenga miundo mbinu, kutoa huduma za afya na kuhakikisha nchi na rasilimali zake zinalindwa . Usalama wa mali na raia unalindwa? Kwa ujumla Chama tawala lazima kiwe kimeshindwa kuongoza nchi.Pia lazima tujiulize huyo anayekuja kutawala ataweza kuyatekeleza haya? Mimi binafsi naona Chama tawala kinatekeleza vizuri katika kuongoza nchi. Maana ufisadi umezibwa, miundo mbinu imejengwa na mengine yanatekelezwa vizuri tu. Hasa katika suala la kuhakikisha rasilimali za nchi zinalindwa. Sasa Chadema kama chama cha upinzani wana hoja gani ya kuweza kusema wanaweka mgombea ili kukiondoa chama Tawala. Pia Tangu Dk wilbroad slaa ashuhudie choo kinapakuliwa na kuwekwa sebuleni na akambonyeza Prof safari unayaona hayooo! Chadema wananchi hawana imani nayo sana kimekuwa kama chama cha wazee wa dili tu.
N.B mimi si mwanachama wa chama chochote

Non~sense!
Kwa kauli zako tu,ww ni CCM Damu hata kama huna kadi ya chama!
 
Mawazo yako yamefika mwisho sawa tu na mtoa mada.
Sio sahihi kusema fulani ni mrefu bila kulingabishwa na mwingine; huenda ni mfupi kuliko tunavyodhani.
Hata rangi ( nyekundu, kwa mfano) hazifanani. Swali hiyo nyekundu unayoisifia; unajuaje hakuna ya kuizidi? Kipimo kipi watumia kuhoji?
Ni sawa na kufikiri ya kwamba ili uendeshe Roli unapaswa uwe na mwili mkubwa ama misuli ama na nguvu nyingi. La, kinachosukuma gari ni injini na vikolokolo vingine.
Sawia nchi haiongozwi eti na Maturity na mambo kama hayo, (ingawa upo usahihi) lkn siosahihi kabisa. Moyo na Nia na Hekima ya Mungu na Hofu ya Mungu ikiambatana na Sera nzuri vinasukuma nchi.
Ili kukiondoa chama tawala lazima tujiulize Maswali kama haya Je CCM amabacho ni chama tawala kimeshindwa kuleta matokeo chanya kwa wananchi? Kama kujenga miundo mbinu, kutoa huduma za afya na kuhakikisha nchi na rasilimali zake zinalindwa . Usalama wa mali na raia unalindwa? Kwa ujumla Chama tawala lazima kiwe kimeshindwa kuongoza nchi.Pia lazima tujiulize huyo anayekuja kutawala ataweza kuyatekeleza haya? Mimi binafsi naona Chama tawala kinatekeleza vizuri katika kuongoza nchi. Maana ufisadi umezibwa, miundo mbinu imejengwa na mengine yanatekelezwa vizuri tu. Hasa katika suala la kuhakikisha rasilimali za nchi zinalindwa. Sasa Chadema kama chama cha upinzani wana hoja gani ya kuweza kusema wanaweka mgombea ili kukiondoa chama Tawala. Pia Tangu Dk wilbroad slaa ashuhudie choo kinapakuliwa na kuwekwa sebuleni na akambonyeza Prof safari unayaona hayooo! Chadema wananchi hawana imani nayo sana kimekuwa kama chama cha wazee wa dili tu.
N.B mimi si mwanachama wa chama chochote.

SAJILI KAMPUNI; LTD, JINA LA KAMPUNI, PARTNERSHIP, HESABU ZA KAMPUNI, PROFORMA INVOICES ETC 0652411402 -0684205039
 
Mawazo yako yamefika mwisho sawa tu na mtoa mada.
Sio sahihi kusema fulani ni mrefu bila kulingabishwa na mwingine; huenda ni mfupi kuliko tunavyodhani.
Hata rangi ( nyekundu, kwa mfano) hazifanani. Swali hiyo nyekundu unayoisifia; unajuaje hakuna ya kuizidi? Kipimo kipi watumia kuhoji?

SAJILI KAMPUNI; LTD, JINA LA KAMPUNI, PARTNERSHIP, HESABU ZA KAMPUNI, PROFORMA INVOICES ETC 0652411402 -0684205039
Mawazo yako yamefika mwisho sawa tu na mtoa mada.
Sio sahihi kusema fulani ni mrefu bila kulingabishwa na mwingine; huenda ni mfupi kuliko tunavyodhani.
Hata rangi ( nyekundu, kwa mfano) hazifanani. Swali hiyo nyekundu unayoisifia; unajuaje hakuna ya kuizidi? Kipimo kipi watumia kuhoji?

SAJILI KAMPUNI; LTD, JINA LA KAMPUNI, PARTNERSHIP, HESyaaABU ZA KAMPUNI, PROFORMA INVOICES ETC 0652411402 -0684205039
Sijakuelewa chochote hata!
Mawazo yako yamefika mwisho sawa tu na mtoa mada.
Sio sahihi kusema fulani ni mrefu bila kulingabishwa na mwingine; huenda ni mfupi kuliko tunavyodhani.
Hata rangi ( nyekundu, kwa mfano) hazifanani. Swali hiyo nyekundu unayoisifia; unajuaje hakuna ya kuizidi? Kipimo kipi watumia kuhoji?

SAJILI KAMPUNI; LTD, JINA LA KAMPUNI, PARTNERSHIP, HESABU ZA KAMPUNI, PROFORMA INVOICES ETC 0652411402 -0684205039
Kipimo kipi kinatumika kuhoji kama chama tawala kinaleta maendeleo na kinatekeleza vipi kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya n.k( kinatekeleza vipi ilani yake ya uchaguzi) we hujui hicho kipimo !
Au umeleta Tangazo la biashara tu.
 
Unadhihirisha kiwango cha ufahamu & uelewa wako boss. kama hukuelewa suala dogo km hilo; sina la kukusaidia. Sidhani km inahitajika elimu kubwa kunielewa.
Ila nashukuru pia kunipa ripoti kua tangazo linasomeka

SAJILI KAMPUNI; LTD, JINA LA KAMPUNI, PARTNERSHIP, HESABU ZA KAMPUNI, PROFORMA INVOICES ETC 0652411402 -0684205039
 
Back
Top Bottom