Je, CHADEMA inaweza kushinda 2020? Is it serious, credible & mature enough opposition?

NDIO MAANA NIMEKUULIZA KWA WAKATI ULIOPO.....je hao au sisi wananchi tuingie barabarani kwa ajili ya chama GANI PINZANI???????.....tutaingia barabarani siku tukiwa na UPINZANI UNAOJITAMBUA....si hawa wapuuzi.....
Hahahhhahahahaha hakuna sababu? Ssa mlizuia UKUTA wa nni??? Kwani Tanzania hayajawahi tokea maandamano na mkaua watu umesahau Arusha, pemba, mbeya je 2012??? Na huko kote mliua watu ssa kipi kinashindikana!!!!

Ndio maana nasema mko madarakani kwa kuwa watanzania sio agressive kma wakenya/au wahutu wa burundi!!! Ila sio kwa sababu ya SYSTEM sijui watanzania hawatuelewi no MCHAWI wetu wa kuingia ikulu ni upole wa watanzania na pia upole wa viongozi wa upinzani ila naamini siku tukipata kiongozi wa upinzani "gaidi" kma SAVIMBI au ODINGA ndipo siku tutaingia ikulu

Ila tume ya uchaguzi sijui sera sijui chama kujirekebisha vyote hivo havina maana kma MATOKEO ya uchaguzi yanachezewa na watawala

Hivyo nashauri wapinzani hasa chadema tuhakikishe tunachagua mwenyekiti "gaidi" ili aweze kupress watawala wasituchezee ila tukiendekeza viongozi wandiplomasia kma lowasa sijui mashinji au mbowe tutaendelea kuonekana sisi ndio wakupuuzwa
 
Mkuu...nadhani wewe hiyo kulala selo na kupigwa mabomu ni dogo kuliko la Mawazo aliyeuawa kinyama...

Hoja hapa ni chama chenu CHADEMA kinafanya nini katika hayo

Kwani nani hajui kuwa hakuna urari katika uwanja wa kisiasa nchini? Ninyi mnafanya nini katika kuupigania huo urari?

Ninyi mmeendelea kushiriki chaguzi zote katika mazingira yaleyale ya kikatiba na tume na mkishindwa mnaanza kulia lia ooh..sijui tume and whatsover.....

Sasa hivi uchaguzi umepita badala ya ku strategize jinsi gani tume huru inapatikana mnahangaika na Makonda....Seriously?

Kabla ya 2015..Wananchi walikuwa wanaielewa CHADEMA kiasi...lakini tangu 2015 hadi sasa hamueleweki..Wananchi hawaoni hata faida ya kuchagua watu wa CHADEMA majimboni kwao...kwa sababu you guys are worse off kuliko hata ma CCM....

Nikupe somo mdogo wangu....System inashawishiwa kwa kuwa na watu imara wenye mipango thabiti na wanaoaminika...Niamini mimi siku ambapo chama cha upinzani kitakuwa na mifumo imara...watu imara...mipango madhubuti...trustworthiness....kitaweza kushawishi system kuwa wapewe dola.

Mkuu, pamoja na mapungufu ya CHADEMA, wewe kweli bado unaaminini kuwa kuna namna sauti ya wananchi inasikika kupitia chaguzi zetu kiasi cha kusema hawaoni faida ya kuichagua CHADEMA majimboni? You have to believe in some semblance of credibility in our elections to conclude that way. Na ni kivipi CHADEMA iwe worse off kuliko CCM? Halafu hiyo system unayoizungumzia hapa ni ipi hasa?

Nakubaliana nawe kwamba ni ujinga kwa CHADEMA kuendelea kushiriki katika chaguzi na shughuli za kisiasa katika mfumo uliopinda kiasi hiki halafu kuishia kulalamika kuonewa tangu 1995. Ukiwauliza baadhi yao watakwambia: si busara kumuachia fisi bucha. Lakini ni wazi kabisa kuwa wasitarajie kuwa na fursa yoyote ya kushika dola na hata kuwa na wabunge wengi ilhali CCM inazidi kuongeza udhibiti kupitia vyombo vya dola.

Lakini ni hasara kwa nani hasa? Kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA pekee? No. Ni kwetu wananchi wote tunaoruhusu kuongozwa na mfumo usiotoa fursa ya mawazo mbadala kufanya kazi nchini. A totalitarian system. Hivyo kuwakasirikia CHADEMA na kuwaona wako ovyo kuliko CCM haisaidii sana. Kwangu mimi hata kama CHADEMA wangefanikiwa kushika dola bado ningebakia na swali kama kweli tumeshaachana na ujinga wa kuendekeza totalitarian systems. Isiwe ni suala la kubadili vyama tu. Hapo ndipo lilipo tatizo kubwa la nchii hii ambalo naona hatuwezi kutegemea chama cha siasa kama CHADEMA pekee walitatue - pengine hata hawana lengo hilo.
 
NDIO MAANA NIMEKUULIZA KWA WAKATI ULIOPO.....je hao au sisi wananchi tuingie barabarani kwa ajili ya chama GANI PINZANI???????.....tutaingia barabarani siku tukiwa na UPINZANI UNAOJITAMBUA....si hawa wapuuzi.....
What a joke! Mtu uliyeridhika na utawala bora na thabiti wa CCM una mawazo ya kuingia barabarani? What for?
 
Pascal umetoa mada nzuri sana, hata mimi niliamini sana CHADEMA kuwa ni chama makini kabla ya 2015. Na ndio maana nikawa mfuasi wao. Baada kumpokea Edo na kumpandisha kupeperusha bendera ya CHADEMA, nilitafakari kwa kina mno kwa kujiuliza hivi kwa miaka 20 ya upinzani kweli CHADEMA wamekosa mtu wa kumweka mpaka kumpokea mtu ambae sisi wenyewe tunamwimba fisadi kwa miaka zaidi ya nane, nikaona viongozi wakuwa hawana maono na dhamira za dhati au kuna kitu sio cha kawaida ambacho kiliwanufaisha wachache nikaachana nao. Hivyo kiujumla upinzani Tanzania bado sana, hivi vyama vya siasa ni kama SACCOS za watu. Ukiangalia hata uchanguzi wa juzi unawaleta wagombea kwa majaribio walipochaguliwa wanalalamika eti dhaifu hii inachekesha sana.
Nani alilalamika ni dhaifu sana??? Jamiiforums ndio ofisi za chadema?? Au hawa wanaotumia ID feki ndio wanaongea kwa niaba ya chama???? Mambo ya jf yatofautishwe na misimamo ua vyama vyetu!!! Hilo moja

Pili mkuu inabidi urudi ujifunze kuhusu siasa kafanye case study ya mwai kibaki au mahathir mohammed ...... ngoja niongee kineutral leo!!!!!

watu wakiwa na lengo moja watashirikiana kummaliza adui mmoja ssa kma lowassa hajawahi kuwa implicated na chombo chochote kuwa ni fisadi unataka chadema waendelee kuimba wimbo huo huo miaka yote even if it was proven otherwise?? Je unajua kabla ya chadema kumpokea hawakujua kuwa wanapokea FISADI?? je hawakujua kma ni fisadi anaweza fungwa muda wowote na wakakosa mgombea urais?? Je Tundu lisu hakusema walijadili suala hili kabla ya kumpokea??? Ni vema mkuu ujifunze flexibility lasihivyo hutaelewa maana ya uongozi au siasa..... cuf waliitwa CCM B so was mbatia too ila leo hii chadema hawakupewa makam wa rais na ccm B?? Kwanni walikubali???

Mkuu nikiwa neutral tu ni kwamba magufulo wa very strong 2015, angewekwa membe hta slaa angempiga knockout sema alipowekwa magufuli mwenye rekodi safi ya utendaji at least kuliko ccm wenzake hta slaa alijua kushinda hawezi ndio maana akaongea na lowassa aingie chadema kuongeza nguvu ssa mmi kma mwanachama loyal nina imani viongozi wetu walifanya tathmini na walijua impact positve na negative za kumchukua lowasa na kma it became a success na watanzania walituamini na kutupa kura za rekodi lawama hizi zinatoka wapi tena especially kma unadai wwe ni chadema???
 
d2a23e681230940e72aeb27040b3f3a3.jpg
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali la tathmini kuihusu Chadema, seriousness yake, its abilities and the capabilities. Hivi CHADEMA, inawezo wa kushinda uchaguzi wa 2020?, na hata ikatokea ikashinda, jee inaweza kuendesha nchi?. Is it a Serious Party?, is it Credible?. Is it Organized?, does it have Succession Plan?. Is it Mature Enough Opposition, Kuweza Kukabidhiwa Nchi yetu 2020?!.

Maswali haya ni kufuatia tathmini yangu jinsi Chadema inadeal na baadhi ya issues mbalimbali ikiwemo the current one ya uteuzi wa wawakilishi wake kwenye Bunge la EALA.

Kutawala nchi sio jambo dogo au jambo la mchezo mchezo. Ikulu yetu haipaswi kugaiwa kwa majaribio bali kwa uhakika, tutakaye mkabidhi ikulu yetu ni lazima kwanza atuthibitishie amekomaa, na anawezo, mature enough with the abilities and capabilities, na sio tuu kumpa mtu ikulu yetu kwa kumjaribishia simply kwa sababu tuu CCM imeshindwa hili na lile na baadhi ya watu wameichoka sana CCM!.

CCM inaendelea kuchaguliwa mwaka hadi mwaka, na itaendelea kuchaguliwa sio kwa sababu CCM is the best, au CCM imeweza au inauwezo kivile!, no!. CCM imeshindwa na ilishindwa siku nyingi na inaendelea kushindwa, kwa kufanya madudu mengi tuu lakini bado imekuwa ikiendelea kushinda kwa kuchaguliwa mwaka hadi mwaka kwa mazoea tuu kwa sababu, Tanzania bado hatuna mbadala muafaka wa kuiondoa CCM!.

Yaani Tanzania bado hatuna any serious and a credible opposition party ya kuwapa wapiga kura wa Tanzania a choice to choose from, hivyo CCM kujikuta ikiendelea kuchaguliwa na kushinda kwa ku sail through na upepo wa mazoea, kwa sababu ndio the only one iliyopo!, we have no any serious credible choice to choose from, hivyo we have no choice. Matokeo yake ni CCM inashinda kwa easy ride ya mazoea na itaendelea kushinda na kushinda tena na tena mpaka tutakapo pata a credible opposition such that we'll have a choice to choose from!.

Kwa Zanzibar hakuna ubishi kuhusu uwezo wa CUF as a credible opposition kuweza kutawala Zanzibar, lakini kwa upande wa huku Tanzania Bara, bado kabisa hatuna any serious and a credible opposition ya kuiondoa CCM na kuikabidhi Ikulu yetu.

CHADEMA ndio angalau angalau wameonyesha nia, na kiukweli wakiamua, wanaweza kabisa, ila natatizwa na haya madudu madogo madogo yanayo onyesha all signs za immaturity kwa upande wa Chadema, such that bado ni chama ambacho hakijaonyesha ukomavu wa kutosha enough to convince Tatanzanians kuikabidhi ikulu yetu comes 2020, waipige chini CCM na kuikabidhi Chadema Ikulu yetu ya Magogoni.

Jee kwa maoni yako, unaiona Chadema as a credible, serious opposition, iliyokomaa na kuwa mature enough with the ability and credibility ya kukabidhiwa ikulu yetu 2020?.

Kwa upande wangu, honestly, I don't think, ila kabla sijasema why I don't think and what should we do, naomba kupata mawazo yako, assuming uchaguzi wa Tanzania utaendeshwa kwa uhuru na haki, na chama kitakacho shinda kimeshinda kwa haki, Jee Chadema hata kikishinda, kinauwezo?. Kimeonyesha uwezo wa utayari wa kutawala nchi endapo kitashinda uchaguzi 2020?. Ila kabla hata hakijashinda huo uchaguzi wa 2020, kwa Chadema hii tunayoiona sasa, jee inao huo uwezo wa kushinda?.

Na hata tukiachana na udhaifu wa upinzani imara, everything has it's limits, suppose CCM imewafikisha Watanzania at their limits wakaamua sasa imetosha, they've had enough of CCM and now they are fed up hivyo kuamua liwalo na liwe, wakaipiga chini CCM kwenye sanduku la kura na kuichagua Chadema, jee CCM itakubali kuachia?. Can you just imagine mtu aliyepo Ikulu kukabidhi madaraka sijui kwa nani hiyo 2020, is it possible?.
Kuna mtu yoyote ameishawahi maandalizi yoyote ya succession plan ya serikali, vyombo vyetu vya dola na vyombo vya ulinzi na usalama kukitumikia chama kingine chochote nje ya CCM?.

Kwanza tuu hata ikatokea Watanzania wengi zaidi wakaichoka CCM na kuipiga chini kwenye sanduku la kura, jee huyo mshindi halali atatangazwa?!. Au inawezekana zoezi zima la uchaguzi wa vyama vingi ni kwenye ubunge tuu na udiwani, lakini kwenye urais ni igizo tuu la uchaguzi?!.

Nawatakia Furahi Dai Njema.
Paskali.
Rejea.
CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga! - jamiiforums.com
CHADEMA: Tujadili Utayari wa Kutawala Nchi 2015 | Page 7 ...
Kuelekea 2020: CHADEMA Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If ...
Kuelekea 2020: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM ...
CHADEMA Ikipewa Nchi, October 2020, Hakuna Hatari Kugeuka Utawala ...
Mtazamo: Kanda ya Kaskazini, CCM imechokwa mpaka basi ...
Kuichagua tena CCM, Je ni kielelezo cha kufanya informed decision ...
Ikitokea CCM ishinde, Je ushindi huo ni kutokana kuwekeza kwenye ...
Watanzania ni ignorants au tumelogwa?
Wenye Matumaini na Upinzani Kushika Dola!, Sahauni! CCM Inajiandaa Kuua Kabisa na Kuuzika Jumla !.

Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana, kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!. Apunguze...
Asante kwa mada nzuri na ya kufikirisha. Nina swali maswali machache:

Moja- Unaposema kwamba upande wa Zanzibar upinzani (CUF) ni imara na una uwezo wa kuongoza nchi lakini kwa upande wa Tanganyika (ukipenda Tanzania Bara au Jamhuri ya Muungano wa Tanzania), umetumia vigezo gani kufikia hitimisho hilo?

Pili - Kwa mtazamo wako, CCM has a succession plan in place. Je unaweza demonstrate succession plan ya CCM, especially kutoka awamu ya nne kuingia awamu ya Tano?

Hoja yako inaonyesha your t belief kwamba ili Chama cha siasa kiweze kuongoza Taifa, ni lazima kiwe na manpower yenye haiba ya kisiasa zaidi kwa maana ya wanasiasa wengi/makada wenye sifa za kujaza nafasi za uwaziri na manaibu mawaziri, nafasi za wakuu wa mikoa na wilaya, lakini pia nafasi za civil service ambapo chama kitachounda serikali mpya kitatarajiwa kufanya replacement katika mfumo wote kwa kuweka watu wapya. Maswali yanayofuatia:

-Kwa mtazamo wako, kwa nchi yenye population ya 50m, tunahitaji kuwa na mawaziri na manaibu wangapi?

Je tukifuta nafasi zote za wakuu wa mikoa na wilaya tutapungukiwa nini/nchi haitaendesheka?

Je ni nafasi gani muhimu na ngapi ambazo unadhania Chadema/Ukawa wanahitaji kuzijaza kutokana na makada miongoni mwao?

Any modern state huendeshwa na taasisi, na hizi hubakia intact regardless ni Chama gani kimeshinda uchaguzi, na ikibidi kubadili uongozi wa taasisi husika, wateule huwa sio wanachama au makada wa vyama vya siasa.

Ukawa wakifanikiwa kuingia ikulu (maana kushinda sio suala la mjadala sana kwa sasa), watachohitaji ni kuteua watu kwa nafasi zifuatazo na hawa wote hawatokani na ukada na wengi wanaweza kupatikana kwenye mfuko uliopo sasa:

1. Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
2. Jaji Mkuu
3. Katibu Mkuu Kiongozi
4. Makatibu wakuu
5. Wakurugenzi wa idara mbalimbali
6. Wakurugenzi wa miji, majiji na halmashauri.
7. IGP na wengine ngazi za chini.
8. TISS na wengine ngazi za chini.
9. Regulatory authorities
10. Mabalozi

Nk nk nk.

Ukawa haihitaji mawaziri na manaibu hamsini. Isitoshe, sio lazima kuteua mawaziri kutoka miongoni mwa wabunge. Nchi inaweza endeshwa na makatibu wakuu hata kwa mwaka huku sheria mpya ikipitishwa bungeni kuzuia mawaziri kutokana na wabunge Kisha kuteua waziri wazuri tu kutoka miongoni mwa watanzania wazalendo na wenye sifa husika waliopo ndani na nje ya nchi.

Bunge linaweza pitisha sheria ya kufuta nafasi za wakuu wa mikoa na wilaya na kazi zao zikaendeshwa na Nchi Wakurugenzi wa majiji, miji, halmashauri.

Mwisho wa siku utakuta kwamba kumbe ili kuongoza nchi, ukawa/chadema itahitaji wanasiasa au Viongozi wenye sifa za kisiasa wasiozidi Kumi ikijumuisha Rais, makamu wake na Waziri mkuu (iwapo nae atalazimika kuwepo au kuwa mwanasiasa).

Tatizo ni kwamba CCM imetengeneza mfumo wa mazoea ambao wengi kwa kutokufikiria vizuri tunadhania kwamba it's an ideal system of rule. Lakini ni hao hao ambao tumekuwa mbele kujadili kwamba mfumo uliopo ni mbovu na umechangia maendeleo duni nchini na kwa wananchi kisiasa, kiuchumi na kijamii.
 
Tatizo la CHADEMA ni Mbowe

Kile chama kimekuwa kikubwa sana kuliko uwezo wake

Yes..Amefanya mengi..lakini uwezo wake umefika mwisho...Hawezi kufanya kingine kipya ambacho hajawahi kufanya...Tatizo kubwa zaidi ni yeye anaamua kila kitu

Huwezi kufanya jambo lile lile kila siku...kwa namna ile ile na kutegemea majibu tofauti...

CHADEMA ikitaka kutokufa ikubali kufanya mabadiliko ya ndani ya msingi kabisa na kukihuisha chama .

Chama kikijenge katika msingi imara na thabiti ya kitaasisi.....waweke mifumo inayowawezesha kuweka sera imara...tested policies...na mwisho watengeneze demokrasia ya kweli ndani ya chama.

Tatizo la vyama vya Tanzania havibadilishi viongozi wanatakiwa kujifunza kutoka nchi zilizoendelea. Mfano nchi zilizoendelea chama cha upinzani kikishindwa uchaguzi ina maana viongozi wake wame-failed. Kawaida kiongozi wa chama huwa anajiuzuru mwenyewe hata kabla hajatolewa na wanachama. Na hili linafanyika kwa makusudi ili kukijenga chama, kwa maana anachaguliwa kiongozi mpya mwenye mawazo na idea mpya. Mifano ni hii hapa chini.

  • CUF - Zanzibar, Maalim Seif ameshiriki chaguzi kadhaa 1995 alishindwa kwa kura 3000! Mwaka 2015 watu wote tunajua kadhurumiwa urais bila aibu kimabavu. With no justification to annulled the election results. Lakini Maalim Seif ni competetive hivyo anastahili kuendelea kuongoza CUF Zanzibar
  • CUF - Bara, Prof. Lipumba kashindwa kuongoza chama na sasa ndiyo kabisa anakiua kwa kutumiwa na CCM. uchaguzi wa mwaka 1995 Lipumba alipata asilimia ndogo sana 6.43%, mwaka 2000 kapata 16.26%, 2005 kapata 11.18% mwaka 2010 kawa wa tatu baada ya Dr. Slaa, alipata 8.3%. Slaa kapata kura nyingi kuliko Lipumba. Na perfomance ya CUF bara ilikuwa mbaya chini yake hivyo alitakiwa atolewe zamani sana. Sababu hakuwa na idea mpya. CUF -Bara imesaidiwa na UKAWA mwaka 2015 kupata wabunge wengi. Wakati Lipumba alikuwa kajiengua.
  • CHADEMA - Mbowe hana idea mpya hafai kuwa kiongozi sababu hana jipya. Inatakiwa mtu mpya mwenye mawazo mapya atayoyanadi kwa wananchi. CHADEMA imefeli kuchukua madaraka chini yake hivyo anakiwa kuchukua kiongozi mwingine. Kosa lingine kashindwa kuleta katibu mkuu mwenye uwezo kama wa Dr. Slaa au zaidi yake. Katibu mkuu wa CHADEMA wa sasa Dkt. Mashinji does not have charisma. Hana mvuto wa kuwashawishi watu kifupi kama mwanasiasa.
  • NCCR-Mageuzi - James Mbatia ameshakuwa mwenyekiti wa hiki chama kwa miaka mingapi? Hiki chama kifupi kimekufa na James Mbatia alitakiwa awe ameshaondolewa madarakani kwenye hichi chama siku nyingi sababu hakina mafanikio yeyote.
 
Asante kwa mada nzuri na ya kufikirisha. Nina swali maswali machache:

Moja- Unaposema kwamba upande wa Zanzibar upinzani (CUF) ni imara na una uwezo wa kuongoza nchi lakini kwa upande wa Tanganyika (ukipenda Tanzania Bara au Jamhuri ya Muungano wa Tanzania), umetumia vigezo gani kufikia hitimisho hilo?

Pili - Kwa mtazamo wako, CCM has a succession plan in place. Je unaweza demonstrate succession plan ya CCM, especially kutoka awamu ya nne kuingia awamu ya Tano?

Hoja yako inaonyesha your t belief kwamba ili Chama cha siasa kiweze kuongoza Taifa, ni lazima kiwe na manpower yenye haiba ya kisiasa zaidi kwa maana ya wanasiasa wengi/makada wenye sifa za kujaza nafasi za uwaziri na manaibu mawaziri, nafasi za wakuu wa mikoa na wilaya, lakini pia nafasi za civil service ambapo chama kitachounda serikali mpya kitatarajiwa kufanya replacement katika mfumo wote kwa kuweka watu wapya. Maswali yanayofuatia:

-Kwa mtazamo wako, kwa nchi yenye population ya 50m, tunahitaji kuwa na mawaziri na manaibu wangapi?

Je tukifuta nafasi zote za wakuu wa mikoa na wilaya tutapungukiwa nini/nchi haitaendesheka?

Je ni nafasi gani muhimu na ngapi ambazo unadhania Chadema/Ukawa wanahitaji kuzijaza kutokana na makada miongoni mwao?

Any modern state huendeshwa na taasisi, na hizi hubakia intact regardless ni Chama gani kimeshinda uchaguzi, na ikibidi kubadili uongozi wa taasisi husika, wateule huwa sio wanachama au makada wa vyama vya siasa.

Ukawa wakifanikiwa kuingia ikulu (maana kushinda sio suala la mjadala sana kwa sasa), watachohitaji ni kuteua watu kwa nafasi zifuatazo na hawa wote hawatokani na ukada na wengi wanaweza kupatikana kwenye mfuko uliopo sasa:

1. Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
2. Jaji Mkuu
3. Katibu Mkuu Kiongozi
4. Makatibu wakuu
5. Wakurugenzi wa idara mbalimbali
6. Wakurugenzi wa miji, majiji na halmashauri.
7. IGP na wengine ngazi za chini.
8. TISS na wengine ngazi za chini.
9. Regulatory authorities
10. Mabalozi

Nk nk nk.

Ukawa haihitaji mawaziri na manaibu hamsini. Isitoshe, sio lazima kuteua mawaziri kutoka miongoni mwa wabunge. Nchi inaweza endeshwa na makatibu wakuu hata kwa mwaka huku sheria mpya ikipitishwa bungeni kuzuia mawaziri kutokana na wabunge Kisha kuteua waziri wazuri tu kutoka miongoni mwa watanzania wazalendo na wenye sifa husika waliopo ndani na nje ya nchi.

Bunge linaweza pitisha sheria ya kufuta nafasi za wakuu wa mikoa na wilaya na kazi zao zikaendeshwa na Nchi Wakurugenzi wa majiji, miji, halmashauri.

Mwisho wa siku utakuta kwamba kumbe ili kuongoza nchi, ukawa/chadema itahitaji wanasiasa au Viongozi wenye sifa za kisiasa wasiozidi Kumi ikijumuisha Rais, makamu wake na Waziri mkuu (iwapo nae atalazimika kuwepo au kuwa mwanasiasa).

Tatizo ni kwamba CCM imetengeneza mfumo wa mazoea ambao wengi kwa kutokufikiria vizuri tunadhania kwamba it's an ideal system of rule. Lakini ni hao hao ambao tumekuwa mbele kujadili kwamba mfumo uliopo ni mbovu na umechangia maendeleo duni nchini na kwa wananchi kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Vyombo/watu hao wanahitaji usimamizi na mwongozo kutoka kwa cabinet ya watu makini.
Tatizo la vyama vya Tanzania havibadilishi viongozi wanatakiwa kujifunza kutoka nchi zilizoendelea. Mfano nchi zilizoendelea chama cha upinzani kikishindwa uchaguzi ina maana viongozi wake wame-failed. Kawaida kiongozi wa chama huwa anajiuzuru mwenyewe hata kabla hajatolewa na wanachama. Na hili linafanyika kwa makusudi ili kukijenga chama, kwa maana anachaguliwa kiongozi mpya mwenye mawazo na idea mpya. Mifano ni hii hapa chini.

  • CUF - Zanzibar, Maalim Seif ameshiriki chaguzi kadhaa 1995 alishindwa kwa kura 3000! Mwaka 2015 watu wote tunajua kadhurumiwa urais bila aibu kimabavu. With no justification to annulled the election results. Lakini Maalim Seif ni competetive hivyo anastahili kuendelea kuongoza CUF Zanzibar
  • CUF - Bara, Prof. Lipumba kashindwa kuongoza chama na sasa ndiyo kabisa anakiua kwa kutumiwa na CCM. uchaguzi wa mwaka 1995 Lipumba alipata asilimia ndogo sana 6.43%, mwaka 2000 kapata 16.26%, 2005 kapata 11.18% mwaka 2010 kawa wa tatu baada ya Dr. Slaa, alipata 8.3%. Slaa kapata kura nyingi kuliko Lipumba. Na perfomance ya CUF bara ilikuwa mbaya chini yake hivyo alitakiwa atolewe zamani sana. Sababu hakuwa na idea mpya. CUF -Bara imesaidiwa na UKAWA mwaka 2015 kupata wabunge wengi. Wakati Lipumba alikuwa kajiengua.
  • CHADEMA - Mbowe hana idea mpya hafai kuwa kiongozi sababu hana jipya. Inatakiwa mtu mpya mwenye mawazo mapya atayoyanadi kwa wananchi. CHADEMA imefeli kuchukua madaraka chini yake hivyo anakiwa kuchukua kiongozi mwingine. Kosa lingine kashindwa kuleta katibu mkuu mwenye uwezo kama wa Dr. Slaa au zaidi yake. Katibu mkuu wa CHADEMA wa sasa Dkt. Mashinji does not have charisma. Hana mvuto wa kuwashawishi watu kifupi kama mwanasiasa.
  • NCCR-Mageuzi - James Mbatia ameshakuwa mwenyekiti wa hiki chama kwa miaka mingapi? Hiki chama kifupi kimekufa na James Mbatia alitakiwa awe ameshaondolewa madarakani kwenye hichi chama siku nyingi sababu hakina mafanikio yeyote.
 
Vyombo/watu hao wanahitaji usimamizi na mwongozo kutoka kwa cabinet ya watu makini.
Kwa mtazamo wako, watu hao makini ni lazima wapatikane kupitia mchakato wa kisiasa kama vile wawakilishi wa wananchi majimboni au wanaweza kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi ili mradi wawe na integrity, management experience, uzalendo, among other things.

Sent from my 5023F using JamiiForums mobile app
 
Bila kujibu hoja nyingine ni kuwa watanzania huwa hawachagui kwa kufuata political maturity wala manifesto! Chaguzi nyingi za Africa zinakuwa determined na mambo matatu, rushwa, wizi wa kura na vyombo vya ulinzi na usalama. Kigezo cha political maturity kwa Africa kina matumizi madogo sana katika kuamua matokeo ya uchaguzi
 
Nmesoma vzur umeeleweka vyema. Nmejibu hoja flan hapo juu khs katibu mkuu wa cdm. Ukweli ni kua cdm kwa sasa haina hoja zenye mashiko na maovu yanayo kemewa wao wanaunga mkonon ili ionekane wananch wanaonewa. Mm cna chama na stegemei kujiunga na chama chochote cha siasa ila natoa ushauri. Mfn, nmemskia kiongozi wa juu wa cdm akisema wenye vyeti fake cdm ikiingia madarakan itawaludsha makazn huo ndo msimamo wa chama. Siungi mkono mtu kufukuzwa kazi bali kwann adanganye then cdm mnaona kaonewa? Mlfanya kosa kubadl gia angani na mmebak kumuabud Mbowe hata kwa mambo msiyo yataka. Sina chuki na Mbowe nila uongozi wake niwa kifalme na chama ni mali yake bnafs wengne wanabuluzwa tu. Bora tubaki majipu yaliuopo ambayo yamepata mtumbuaji kuliko kuleta uozo. Walituaminisha nchi nzma na nje ya nchi kua Lowassa ni fusadi tukawaamin na hata wakati anaenda Dodoma kuchukua fomu kugombea urais ndan ya chama, Mbowe alipaza sn saut kua ccm inapeleka mafisad Ikulu ila alipokuhamia cdm akawa mtakatifu na akastahl kuingia Ikulu si fisad tena. Kwann mnacheza na akl zetu kwa manufaa yenu kisiasa?
Yaan mkuu 2015 japokuwa nilikuwa na kadi ya kijani, kichwani nilijua kura yangu napigia CDM. Lakini baada ya kumpokea ENL na kumbatiza kisha wakampa utakatifu, nilitamani niwe na ka-certificate ka sheria, nitafute magazeti ya mwanahalisi niliyokuwa nanunua kila wiki miaka ya 2007 nikiwa form 5, nimshitaki huyu mbunge wa Ubungo kwa kuniaminisha uongo, nidai hela yangu na thamani ya muda niliotumia kusoma magazeti yake.
Sio siri wanaoshabikia chadema nawaona ni waswagwaji.
 
Paskali: Kwani uwezo wa kutawala unaoongelea ni upi? Kwa mfano, ile nchi maskini kabisa kiuchumi duniani (Sikumbuki hata jina lake tena) inaongozwa na Serikali au Chama au kikundi cha watu fulani . Je unafikiri Serikali au watu hao hiyo wana uwezo wa kutawala?????
 
Hapo ndipo na mimi napata ukakasi zaidi in short ni kwamba chadema hawajajipanga it looks like kuna matukio tu wanayasubiri ili,kuyatumia kama kiki but yasipokuwapo chadema wanazizima kabsa......hawana road map ya namna yakufika ikulu.....hawabadiliki kimkakati sambamba na srkali inayotawala yani approach zao za awamu ya nne ndizo hzo wazitumiazo awamu ya5. Serikali imeshawajua kwamba hawa tuki wa miss treat tu wataishia kusema
"Tunalaani vikali"
"Tutakwenda mahakamani"
"Tunasikitika sana" nk
Kwa kauli kama hzo watasubiri sanaa but inatakiwa wajue kuwa wana mtaji mkubwa sana wa wapiga kura na mashabik so wanaweza kutoa tamko tu litakaloashilia mgawanyiko katika jamii as a plan B yakuifanya serikali(CCM) iogope kurudia uonez dhidi yao mfano kule zanzibar ambavyo ishu yakubaguana kivyama iliwashtua sana serikali pale ambapo hawakuzkana msktn walibaguana na masokoni na katka vyombo vya usafiri.....ki strategic inafaa sana coz watatumwa askari wangap kuwa harass wawabaguao wenzao
Ishu nyngne nikuwatumia wapga kura haohao kuto kutoa ushirikiano kwa serikali mpaka pale itakapo acha uonevu kwa opposition hilo nalo ni strategy pia......but the problem is nani yuko tiari kutamka hayo bila woga katka uongoz wa chadema?....in short watanzania c waoga wala hatujalala but we need an initiater wa jambo au kauli just like Julius malema wa south Africa kwa upande wa viongoz wa opposition au yule kjana wa Tunisia aliejichoma moto kwa upande wa raia
 
Back
Top Bottom