Je, Captain Tesha ni nani?

Je, Captain Tesha ni nani?

Wewe jichanganye tarehe 29/ 10 ndiyo utaijuwa nembo halisi ya JWTZ
Sioni tofauti kati yake na wewe kwa kila mtu upande wake. Hapo ulipo sasa huna hakika na hiyo tarehe 29 Oktoba!

Tofauti kubwa iliyopo, wewe na Samia sasa hivi hamna amani kabisa ndani ya mioyo yenu.
 
sare za jeshi si ata ukimaliza form 6 unapewa aisee kijana
Hahaha.. nacheka kwa dharau nikiona machawa mnavyotapa tapa manina zenu...

Hebu tuambie ni sheria ipi hiyo inayoelekeza mtu akimaliza form six akapita JKT anazawadiwa nguo za Jeshi?

Kwa hiyo unataka kutuambia yawezekana Captain Tesha ni muhitimu wa form six aliyezawadiwa nguo za jeshi tena zenye badge ya nyota tatu au?

Wajinga nyie mwisho wenu ndio umefika. Wewe jiandae kurudisha pesa zote za uma mlizopora kwa hii miaka minne.
 
Hahaha.. nacheka kwa dharau nikiona machawa mnavyotapa tapa manina zenu...

Hebu tuambie ni sheria ipi hiyo inayoelekeza mtu akimaliza form six akapita JKT anazawadiwa nguo za Jeshi?

Kwa hiyo unataka kutuambia yawezekana Captain Tesha ni muhitimu wa form six aliyezawadiwa nguo za jeshi tena zenye badge ya nyota tatu au?

Wajinga nyie mwisho wenu ndio umefika. Wewe jiandae kurudisha pesa zote za uma mlizopora kwa hii miaka minne.
acha ushamba umesahau mpaka wakaanza kutafuta watu wanaovaa sare za jeshi mtaani?
 
sare za jeshi si ata ukimaliza form 6 unapewa aisee kijana
Wee jamaaa acha ufala ,,,utatiwa mwiko nyuma ,,,,,,.etii hata ukimaliza form six unapewa?.. na mashaka hata kama hiyo form six umefika !... Tuliza kipwinto
 
Wee jamaaa acha ufala ,,,utatiwa mwiko nyuma ,,,,,,.etii hata ukimaliza form six unapewa?.. na mashaka hata kama hiyo form six umefika !... Tuliza kipwinto
tulia dogo huezi elewa chochote saahv
 
Tunaongea lugha moja kuna watu wamesema atakuwa detained nimewajibu wako nyuma ya muda ukishika huyo nyuma yake wapo wangapi na watakuja kwa mtindo upi hapo ndio kinabaki kitendawili.

Mimi tangu mwanzo nilisema ulikuwepo muda mrefu sana wa kufanya marejeo na kujikosoa tulipofika ukipita katika mitandao unaona chuki kubwa ya watu dhidi ya serikali.

Huyu ni mwanajeshi mmoja tu kaongea naambiwa YouTube imekuwa blocked huku 95% ya comments wanamuunga mkono je kwa mtindo huu adui akitokea watu watasimama na serikali au adui sababu ya chuki kubwa?

Ni busara kujua mtu anayesema bora tukae mezani tujenge na kupata mabadiliko au yule anayesema twende hivyo hivyo nani hapo yuko katika nafasi kubwa ya kuleta machafuko.?
Huwa nakubali sana michango yako kaka, halafu huwa inatokea coincidence tu tunakuwa tunafanana kimawazo..

Siku chache nyuma hata mimi kuna uzi nilicomment humu kwamba kwa hatua tuliyofikia kuna haja ya Samia kuacha kiburi cha dola na kisha kuliaddress taifa tena kwa speech isiyopungua masaa mawili, ambapo ataongelea kwa kina sana matatizo yooote yanayowafanya wanainchi wanung'unike na kutoa wayfoward atayatatua vipi mambo hayo, hili watu watulize hasira zao na hata kurejesha imani kwa serikali yao... na zaidi ya hilo huu uchaguzi ausogeze mbele ufanyike hata december.

Lakini badala yake Samia ameendelea kuweka pamba maskioni na kutoa kauli za vitisho tu kwa wanainchi.. sasa hivi kwenye kila mkutano lazima arudie hii kauli ya "vyombo vyetu vya dola viko imara"... "vyombo vyetu vya dola viko imara"

Yaan yeye amejianda kutumia mabavu kukabiliana na tatizo ambalo kama akiliwahi mapema wala hata halitakuwa na gharama zozote.

Nadhani akiona jinsi machawa wanavyomsifia anaamini bado anapendwa na watanzania wengi.

Na asichokijua ni kwamba endapo kama ikitokea hiyo tarehe 29 akapita salama, atakuwa ndio amezidisha chuki sana kwa wanainchi kiasi kwamba yeye mwenyewe atakuwa halali usingizi, maana mpaka hapo adui yake namba moja atakuwa ni mwanainchi wa kawaida..

Sijajua wanamtandao wanamshauri nini Samia, ila duniani hapa hakuna raisi ambaye aliyeweza kutawala kwa amani ilihali idadi kubwa ya wanainchi wanamchukia, unless labda aamue sasa na yeye awe Museven tu, kila anapoenda anaenda na jeshi na walinzi binafsi wasiopungua 500.
 
Tarehe 29 Capt C.J Traore Tesh apewe nchi kuongoza kipindi cha mpito.
 
1759599422918.jpeg
 
Huwa nakubali sana michango yako kaka, halafu huwa inatokea coincidence tu tunakuwa tunafanana kimawazo..

Siku chache nyuma hata mimi kuna uzi nilicomment humu kwamba kwa hatua tuliyofikia kuna haja ya Samia kuacha kiburi cha dola na kisha kuliaddress taifa tena kwa speech isiyopungua masaa mawili, ambapo ataongelea kwa kina sana matatizo yooote yanayowafanya wanainchi wanung'unike na kutoa wayfoward atayatatua vipi mambo hayo, hili watu watulize hasira zao na hata kurejesha imani kwa serikali yao... na zaidi ya hilo huu uchaguzi ausogeze mbele ufanyike hata december.
Shukran sana mkuu, na huu ndio ukweli taifa liko vipande vipande chawa na wapambe wanamdanganya Samia hali ni shwari sababu wanapata handouts kama ujira , kinachoshangaza ni Samia kuwahi kukiri pia anaingia mitandaoni yeye kama yeye je hayaoni haya?

Leo ukipita mitandaoni aina ya uungwaji mkono wa Cpt Tesha ambaye pengine mimi na wewe ndio leo mara ya kwanza tunamuona na kumsikia inatoa alarm kuwa hali tuliyopo ni mbaya.
Lakini badala yake Samia ameendelea kuweka pamba maskioni na kutoa kauli za vitisho tu kwa wanainchi.. sasa hivi kwenye kila mkutano lazima arudie hii kauli ya "vyombo vyetu vya dola viko imara"... "vyombo vyetu vya dola viko imara"
Hili la vyombo kuwa imara kila nchi lazima iseme ni aina fulani tu ya hadhi na sifa ila kwa kusema ukweli vyombo vyote vya ulinzi duniani ni imara ila sio kwa wananchi wake waliogadhabishwa , mfano mingi ipo tu na wala haina shaka tumeona watawala wakiachwa kwenye mataa na walinzi wao huku wakishughulikiwa na wananchi wenye hasira kali.
Yaan yeye amejianda kutumia mabavu kukabiliana na tatizo ambalo kama akiliwahi mapema wala hata halitakuwa na gharama zozote.
Na bahati mbaya nguvu hii ya mabavu kwa hatua aliyofika haitasaidia leo umeonekana mpasuko wa wazi je tutajuaje kama hakuna polisi naye atajitokeza kuitisha press yake kutoa ya moyoni?

Je wale wazee na wanaccm wengine wangapi hawaungi mkono sasa wakijitokeza wazi wazi .?
Nadhani akiona jinsi machawa wanavyomsifia anaamini bado anapendwa na watanzania wengi.

Na asichokijua ni kwamba endapo kama ikitokea hiyo tarehe 29 akapita salama, atakuwa ndio amezidisha chuki sana kwa wanainchi kiasi kwamba yeye mwenyewe atakuwa halali usingizi, maana mpaka hapo adui yake namba moja atakuwa ni mwanainchi wa kawaida..
Uchawa inabidi tuuongeze kama maadui wa taifa.
Sijajua wanamtandao wanamshauri nini Samia, ila duniani hapa hakuna raisi ambaye aliyeweza kutawala kwa amani ilihali idadi kubwa ya wanainchi wanamchukia, unless labda aamue sasa na yeye awe Museven tu, kila anapoenda anaenda na jeshi na walinzi binafsi wasiopungua 500.
Hawa ndio wanampotosha kwa maslahi yao ila watashangaa sana kuwa nchi ni kubwa kuliko mtu mmoja au kikundi cha watu.

Wamechelewa sana kujua wako nyuma ya wakati na watanzania wa sasa sio wa 1960-1970.
 
huyo sio mwanajeshi na pia ccm haiwezi toka madarakani leo wala kesho, infact ccm ndo chama kikuu afrika
Haaha.. endelea kutoa kauli za kishujaaa wakati huo hapo ulipo tumbo joto.

Eti ccm haiwezi kutoka madarakan leo wala kesho, kwa hiyo nyie licha ya kuingia kwenye uchaguzi ila hamjajiandaa kushindwa sio?

Kwa maana nyingine unatwambia mko tayari kumwaga damu za mamilioni ya watu, hili tu msitoke madarakani?

Sasa kauli kama hizi ndio zimemuibua Captain Tesha, maana ameona nyie wahuni mmeamua kujimilikisha nchi na kuibagaza mnavyotaka
 
upigaji ni hulka ya binadam sio swala la ccm, na sio kitu cha kukufanya wewe ushindwe kuendelea, huezi sema umekua maskini kwa sababu ya upigaji
Mseng..e kweli wewe, unajua kuna miradi mingapi imeshindwa kukamilika ndani ya awamu hii hii ya samia kwa sababu ya upigaji?

Na unajua kutokamilika kwake kumeathiri vipi maisha ya watu?

Hapo hospitali ya General dodoma, kuna siku tulimpeleka dogo alipata ajali ya piki piki, tukaambiwa CT scanner ya mid range ambayo ingeweza kubaini kama amevunjika uti wa mgongo haipo twende sehemu nyingine, na bei ya hiyo scanner ni $700,000 tu... sasa hebu ona Hospitali kubwa ya serikali kama General inakosa kifaa muhimu chenye thamani ya tsh 1.8b tu wakati huo Abdul amejaza magari ya 20B uwani kwake ambayo kihalisia ameyanunua kwa pesa alizofisadi taifa hili...

Mpaka hapo hujaona kuwa upigaji unaathiri maisha ya watanzania kwa ujumla?

Yaani nyie mafisadi sijui huwa mnatumia nini kufikiri... ni kwamba mkishakula manyama choma kwa hela za ufisadi mlizogawana, basi mkija huku ni kuandika utumbo tu kama hamna vichwa.
 
Amejifukuzisha kazi leoleo ,wanamshabikia wamemponza

USSR
Ona hii kenge..

Kwani yeye anajali hilo la kufukuzwa kazi?

Unafikiri kula mtu anaangalia tumbo lake tu kama nyie machawa?

Ulifikiri kila mwanajeshi atavumilia tu kuona nchi ikichezewa na wahuni, kisa analinda kibarua chake!?

Kuna watu bado wanalipenda taifa hili na wako tayari kufa na njaa kuliko kufumbia macho uovu.
 
acha ushamba umesahau mpaka wakaanza kutafuta watu wanaovaa sare za jeshi mtaani?
Kubwa jinga wewe, haujui hata unachokiandika... wewe umesema huwa wanapewa sare za jeshi wakishahitimu program ya JKT.... sasa na mimi nakuuliza wanapewa sare za jeshi kwa misingi kwa misingi ipi?

Naona ulishaanza kutapa tapa, maana zile hela chafu ulizozoea kuzivuna bila jasho zinaelekea kufika tamati, hapo sasa hivi unawaza vile vijumba vyako ambavyo sasa hivi viko kwenye renta kule chanika, hautakuwa na hela tena ya kuvimalizia.. manina, mafisadi kwisha habari yenu
 
Kubwa jinga wewe, haujui hata unachokiandika... wewe umesema huwa wanapewa sare za jeshi wakishahitimu program ya JKT.... sasa na mimi nakuuliza wanapewa sare za jeshi kwa misingi kwa misingi ipi?

Naona ulishaanza kutapa tapa, maana zile hela chafu ulizozoea kuzivuna bila jasho zinaelekea kufika tamati, hapo sasa hivi unawaza vile vijumba vyako ambavyo sasa hivi viko kwenye renta kule chanika, hautakuwa na hela tena ya kuvimalizia.. manina, mafisadi kwisha habari yenu
umemeza dawaa zaako?
 
ha
Mazingira na visababishi vya fukuto ndani ya jeshi ni kama ilivyokuwa mwaka 1985.

Hii 2025 kuna mazingira na visababishi kutaka mabadiliko turejee historia :


TOKA MAKTABA: KESI YA UHAINI

Kapteni Mstaafu Rodrick Roberts : Sitasahau nilipohukumiwa maisha jela

View attachment 3483274
Kapteni mstaafu Rodrick Roberts

Rubani wa ndege aliyeonja kifo kwa ajali ya ndege na kifungo cha maisha, Rubani huyu ni Kapteni Mstaafu Rodrick Roberts (69). Picha na Maktaba

Na Lauden Mwambona, Mwananchi

Posted Alhamisi, Novemba 28 2013 saa 13:0 PM

KWA UFUPI

Rubani huyu ni Kapteni Mstaafu Rodrick Roberts (69) mrefu, mweupe ambaye si mnene na wala si mwembamba akiwa na nywele laini zinazoashiria wazi kwamba mmoja wa wazazi wake alikuwa mtu wa nje ya Bara la Afrika.
Nje kidogo ya Mji wa Songea, kipo kijiji kinachoitwa Mateka. Bila shaka jina la kijiji hicho lina historia yake, lakini kubwa ni kwamba ndiko anakoishi rubani wa ndege aliyeonja kifo kwa ajali ya ndege na kifungo cha maisha.

Rubani huyu ni Kapteni Mstaafu Rodrick Robert (69) mrefu, mweupe ambaye si mnene na wala si mwembamba akiwa na nywele laini zinazoashiria wazi kwamba mmoja wa wazazi wake alikuwa mtu wa nje ya Bara la Afrika.

Ni mara ya kwanza kumwona alipokuwa akifungua mlango, lakini anatoka na tabasamu baada ya kuona wageni nje wakiwa na mkewe aitwaye May Daud Robert aliyeniongoza kufika hapo mara ya pili baada ya kumwomba aachie kidogo kazi yake mjini Songea na kunipeleka nyumbani kwake nikaonane na mumewe.

Kwa kweli ilikuwa mara ya pili kwangu kufika pale saa 11.00 jioni baada ya mara ya kwanza ya saa 4.00 asubuhi ya siku hiyo kuwakosa nilipopelekwa na msamaria kwa pikipiki mbili.

Robert anatukaribisha ndani huku akisema alipata taarifa za kuwapo kwa wageni wanaomtafuta tangu asubuhi. Tunaingia ndani na kufika kwenye sebule ikiwa na makochi ya kawaida na hatimaye Robert, mkewe na mimi tunaketi.

Akiwa anamwangalia mkewe aliyeketi upande wa kushoto kwake, Rubani Robert ananikaribisha.

Anasimulia kidogo historia yake.

Rubani: Nilizaliwa Mtaa wa Mtini mjini Songea mwaka 1944 na baba yangu alikuwa mhandisi wa kujenga barabara na nyumba za Serikali na alishiriki kujenga Uwanja wa Ndege za Jeshi Dar es Salaam.

Nilisoma chekechea mjini Songea, Shule ya Msingi Songea na Peramiho baadaye Sekondari ya Wavulana Songea kabla ya kujiunga St Michael ya Iringa ambayo baadaye ikawa Mkwawa Sekondari na sasa ni chuo.

Baada ya kumaliza Mkwawa nilingia Chuo Kikuu cha Dar e Salaam kuchukua Sayansi ya Jamii, lakini nilisoma mwaka mmoja nikaacha.

Mwandishi:Ni sababu zipi zilikuachisha chuo?

Rubani: Sikumbuki.

Mwandishi:Baada ya kuacha chuo kikuu ulikuwa unafanya nini?

Rubani:Nilikuwa nyumbani nikijishughulisha na uandishi na pia kuchora jambo ambalo lilinifanya niitwe kwenye mafunzo ya siku sita kuhusu uandishi Chuo Kikuu cha Makerere ambako nikawa mmoja wa watu wa kwanza tulioandika jarida la kwanza la chuo hicho. Niliporudi nchini nilipata kazi kwenye Shirika la British America Tobacco Company (BAT) ambako nilifanya kazi karibu mwaka mmoja na baadaye niliacha.

Mwandishi: Ni kwa nini uliacha?

Rubani: Sikumbuki.

Mwandishi: Baada ya hapo ulikwenda wapi?

Rubani: Nakumbuka mwaka 1970 nikiwa nyumbani Songea, alikuja Jenerali Luis ambaye alikuwa mwenyeji wa Mkoa wa Rukwa na kuniambia kwamba walikuwa wakihitaji vijana waliosoma ili wawe marubani wa jeshi. Hoja hiyo niliipenda na nikakubali, hivyo aliniandikisha na kunitaka niende kwenye mafunzo ya kijeshi (TMA) Dar es Salaam kwa ajili ya uofisa.

Nilimaza mafunzo kwenye kikosi cha anga Dar es Salaam na baada ya hapo pamoja na wenzangu karibu 14 tuliendelea na mafunzo ya kuendesha ndege kwa chini (Ground School) kwa mwaka mmoja na baada ya hapo tulianza mafunzo ya awali ya kurusha ndege.

Mwandishi: Tangu mafunzo hadi kuanza kazi, je uliwahi kupata ajali?

Rubani: Ndiyo, nilipata ajali mwaka 1978 nikiwasafrisha askari 26 kutoka Dar es Salaam kwenda Beira Nover Freesco Msumbiji ingawa sikujua askari wale walikuwa wakienda nchi gani. Sijui walikuwa wa Zimbabwe au Angola sijui. Injini ya kushoto ilizimika ghafla na baadaye injini ya kulia ikazima hivyo nililazimika kutua kwenye shamba dogo porini na askari wote tulitoka salama isipokuwa mmoja alipata michubuko kutokana na bawa la ndege kugonga kichuguu. Kipande hiki (anainuka kuchukua na kukionyesha kichuma cha bawa la ndege) nilipewa kama kumbukumbu.

Baada ya ajali hiyo, mwishoni mwa mwaka 1978 nilikwenda Uingereza kusoma utaalamu wa ndege aina ya Hauca Cidre748.

Mwandishi:Je, vita dhidi ya Idd Amin Dada ulishiriki?

Ruban: Tangu mwanzo hadi mwisho mimi nilikuwa mmoja wa walioshiriki mchana na usiku hadi vilipoisha.

Mwandishi: Unakumbuka nini kwenye vita hivyo?

Rubani: Nakumbuka siku moja nilikuwa off (napumzika kidogo), nikaamua kunywa bia. Na ratiba ilikuwa ikionyesha nitakuwa kazini kesho yake. Lakini ghafla kiongozi wangu alinijia na kunitaka nirushe ndege. Mimi nilikataa katakata kwa sababu nilikuwa nimekunywa pombe. Niliwahi kumwendesha Nyerere.

Mwandishi: Je, ni kweli ulimwendesha Nyerere? Na kazi ya jeshi iliendelea hadi lini?

Rubani: Ni kweli baada ya vita vya Amini niliendelea kurusha ndege za jeshi na pia kufanya kazi ya kuendesha ndege ya Rais Nyerere. Mwaka 1983 Januari 7, nilikamatwa na wanajeshi wengine wengi kwa tuhuma za uhaini. Tulidaiwa tulitaka kumuua Rais Julius Nyerere. Nilikamatwa nikiwa eneo la Airwing Dar es Salaam. Tulikaa kizuizini hadi Julai mwaka 1983 Mahakama ilipotangaza kwamba hatukuwa na kesi ya kujibu. Lakini cha kushangaza mwaka 1984 watu tisa kati ya wale walioshikiliwa mara ya kwanza, tulikamatwa tena na kufikishwa mahakamani kwa kosa la kutaka kumuua Rais Nyerere.

Mwandishi: Je, kiukweli mpango huo ulikuwapo?

Rubani. Aaa...ulikuwapo haukuwapo, it was planned by high official (ulipangwa na baadhi ya maofisa za ngazi za juu), unajua baada ya vita vya Uganda nchi ilikuwa imefilisika. Haikuwa na unga, sabuni, sukari na hata nguo, karibu kila kitu hakikuwapo. Hivyo Watanzania wengi walikuwa wamechanganyikiwa na hali ile.

Mwandishi: Kwa maana hiyo mpango huo ungefanikiwa je bidhaa hizo zingeonekana?

Rubani: Rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi aliiokoa nchi baada ya kuruhusu kila kitu kiingie nchini hata bila ya kutoza kodi. Mwinyi aliituliza nchi. Pia Serikali iligundua kwamba waliokamatwa walitaka mfumo wa vyama vingi vya siasa ili kuishtua CCM ambayo ilikuwa imejisahau na hivyo kuanzishwa kwa vyama vingi jambo ambalo lilitekelezwa baadaye.

Mwandishi: Matatizo yaliyokuwapo enzi hizo na sasa unatofautishaje?

Rubani:Kama nilivyosema, enzi za Nyerere nchi ilifilisika, Mzee Mwinyi aliiokoa nchi, Rais Mkapa akaweka msingi wa kukusanya kodi, hivi sasa sijui kinachoendelea kwa kuwa sisomi sana magazeti kwani sina fedha za kununua.

Mwandishi: Mama Robert ulifanikishaje safari yako kurudi Songea. ?

Mkewe: Mimi niliposikia anafungwa maisha nilipigwa na butwaa na simanzi kubwa. Hivyo sikuwa na nguvu, lakini cha ajabu, baada ya saa 12 kupita, mkuu wa kikosi aliniita na kunitaka niondoke kwenye nyumba ndani ya saa 24. Kumbuka wakati ule mimi nilikuwa nafundisha Chuo Cha Utumishi Magogoni Dar es Salaam, hivyo nilihitaji kupata nafasi ya kuomba uhamisho na kufunga mizigo. Lakini mambo ya jeshi ni amri na nilitolewa mizigo ili nisafirishwe kwa ndege ya Jeshi ambayo nayo iliharibika. Lakini kwa bahati ilipona kabla ya saa 12 kumalizika, nikatakiwa nitaje niende wapi.

Suala hilo lilinifanya nitaje Songea kwa vile nilikuwa na watoto sita na Robert na watoto walikuwa wakiwafahamu ndugu wa Songea.

Hivyo mizigo na watoto walisafiri kwa ndege mimi nikabaki Dar es Salaam nikiomba uhamisho wa kwenda kufundisha Shule ya Sekondari ya Songea Wasichana.

Kwa kweli ilikuwa fedheha kubwa. Serikali inampenda mfanyakazi mzuri, lakini huyohuyo akiteleza kidogo ni takataka. Ipo haja ya kubadilisha msimamo huo.

Mwandishi: Kwako rubani, je unalo neno kwa Serikali?

Rubani:Aaaa , tangu nifike huku sijapata na wala sina senti ya Serikali. Wapo wenzangu waliosema eti Serikali inafikiria kutupatia chochote, lakini mpaka sasa sijasikia lolote.

Mwandishi: Kwa sasa afya yako ikoje na unajishughulisha na nini?

Rubani. Afya yangu nashukuru Mungu naendelea vyema, mambo mengine Mungu anasaidia.

Kapteni Mstaafu Rodrick Robert anasema ni suala la msingi kwa watu kuwa na moyo wa kulitumikia taifa kwani ndio msingi wa kuhakikisha tunakuwa na taifa lenye maendeleo makubwa.

Jambo la msingi ambalo napenda kusisitiza ni moja tu kwamba kwa kila kitu ambacho mtu anafanya, anapaswa kuweka mbele maslahi ya taifa kwanza, anasisitiza akiwaasa Watanzania kujenga tabia ya kuheshimu mila na tamaduni za taifa, pia kujali maadili ya uongozi.

Aidha anawashauri vijana kufanya kazi kwa bidii ili kuharakisha maendeleo nchini, kwani vijana ndio tegemeo kubwa kwa taifa na ulimwengu kwa ujumla kwa vile wana nguvu za kutosha.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi
Hapo kwanini aliacha chuo akajibu Sikumbuki
Jibu ni kwamba ali disco chuo hukatizi kama unavyosoma primary na secondary mradi ufike
 
Back
Top Bottom