Je, Captain Tesha ni nani?

Je, Captain Tesha ni nani?

Kachafua hali ya hewa sana leo hapa nchini

Hayupo pekee yake, wapo wengi kwa mujibu wa historia, captain lazima kuna wengi wanaunga mkono maoni yake.

Kutaka mabadiliko na kutoka hadharani maana yake kuna wengi ndani ya jeshi wanaongea kuhusu kutofurahia kinachoendelea nchini awamu ya 6 hadi leo tarehe 04 October 2025 kapteni Tesha kuongea na umma

TOKA MAKTABA 1986
Rais Ali Hassan Mwinyi awaachia huru maofisa wa jeshi waliokuwa kizuizini kwa tuhuma za uhaini :

President Ali Hassan Mwinyi frees 14 from detention ,

From NATION Correspondent
in Dar es Salaam, Tanzania. Sunday

Fourteen people , detained on suspicion of being implicatedin the attempted plot to
overthrow the government of the now-retired Tanzanian President Julius Nyerere three years ago, were freed yesterday.

Their freedom, announced today by the government-owned .Sunday News, followed President Ali Hassan Mwinyi's decision to resciud their detention order. According to the list, seven were armymen and five civilians. The names of the remaining two people were not given.

The freed armymen were identified as Lieutenant-Colonel M a r t i n P e t e r Msami.
Lieutenant - Colonel Martin Ngalomba, Lieutenant-Colonel Protas Bachibila Muchwampika
.

Captain Harry Hanspoppe, Captain Manyama Athumani oazukainwe, Lieutenant John Mhelwa Mzimba and Sergeant Michael Mwigulu.

The five civilians were Messrs Robert Bayona, Thadeo Boniface, Mtakyama Bugingo, Ramadhani Shabani Otto and Sulemani Nassor Seif. The remaining two names were not released.

The 14 were among scores of people detained without trial in early 1983 on suspicion that they were connected with the coup plot which the government claimed was planned to take place between June, 1982, and Jan 1983

Of the convicted for planning the coup attempt, One of them was the alleged ring leader, Mr Pius Mtakubwa Lugangira who, together with Hatty McGhee, escaped from the maximum security remand prison in June, 1984, and fled to Kenya.

Hatibu Gandhi alias Captain Hatty Macghee; others were Captain Christopher Kadego alias Chriss; Lieutenant Eugene Maganga; Captain Metusela Suleiman Kamando; Captain Vitalis Gabriel Mpunda; Captain Rodrick Roushan Roberts; Captain Dietrich Oswald Mbogoro; Captain Zacharia Hanspoppe and P3794 Lieutenant Badru Rwechungura Kajaja. Mr McGhee was subsequently returned to Tanzania in exchange for two Kenya Air Force men whowere in Tanzania as political refugees.

Last year, a well known local industrialist, Jayantlal Rajani, was released after being detained in connection with the 1983 plot. Against Mr Nyerere, AFP writes. During a treason trial last December for some of those implicated in the plot, nine People were jailed for life and six others were acquitted by the Tanzanian High Court.

During a treason trial last December for some of those implicated in the plot, nine
People were jailed for life and six others were acquitted by the Tanzanian High Court.


At the time when the country was facing this economic crisis in 1982, the second, third,
fourth, fifth, sixth, seventh, eighth and ninth appellants held military commissions in the
Tanzania Peoples' Defence Forces, that is TPDF.

At the time material to this case in 1982, the second appellant was stationed in a tank unit in Dar es Salaam, whereas the third appellant was pursuing higher studies at Dar es Salaam University. He was in his final year reading for a BA degree in Political Science.

The fourth appellant was a pilot in the TPDF Airwing at Ukonga in Dar es Salaam, and so were the fifth and sixth appellants. As far as the seventh appellant is concerned, he was in the Air Defence Regiment and was in charge of Battery No 2 in Dar esSalaam; similarly, the eighth appellant was in the same regiment as Chief Engineer.

As for the ninth appellant, he happened to be stationed in a military unit at Nachingwea, but was in Dar es Salaam in December 1982. All appellants are Tanzanians by nationality.
Thereafter, during the same month of December 1982, the first appellant and the fourth
appellant visited Zanzibar on several occasions. At about this time the first appellant received a number of guests at house No 80B Drive-In.

He, and a number of friends, also used to visit a house at Kinondoni Mkwajuni, that is, house No 65--32P along Livingstone Street in Dar es Salaam, where he and his friends used to have lunch and indulge in heavy drinking. That house belonged to PW38, that is, Zahara Abdulla Sengumba, who rented it from the National Housing Corporation. She was in some way related to the first appellant.

She had agreed to allow the first appellant and his friends to have their lunch there as and when they wished. For most of the time, material to this case, the first appellant travelled in the city by taxi which he hired from PW1, that is, Abdallah Mhando. Towards the end of December 1982, the first appellant hired another taxi driven by PW45, that is, Nassor Sultan Seif, apparently because PW1 had travelled outside the country to Harare in Zimbabwe.

During this time, Pius Lugangira alias Father Tom was not sitting idly by at Motel Agip, but made a number of contacts in the city, including a visit to house No 1127 Chole Road at
Source: IFRA Press Archive
 
kipindi cha uchaguzi hiki
Sawa kaka.Kwahiyo jamaa ni afande wa mchongo(hebu nisaidie nisije ingia chaka hapa).

Raia anamwandikia barua CDF au anatamka wazi kwamba kamwandikia CDF kumpatia ushauri pia nini kifanyike?(ndio sio mwanajeshi lakini sasa uone nchi ilivyokuwa na jeshi la hovyo kama hadi raia wanapata sare wanaingia live ujue Rwanda hiko njiani kutwaa ardhi ya taifa hili.Maana hapa jeshi hakuna tena)
 
😂 😂 😂
Sasa itakuwaje jeshi lisipokuwa upande wa samia?

Maana yake samia anabaki kuwa kama msanii wa bongofleva tu, sio Amiri jeshi tena.

Watamfurumusha, bora ajiondokee zake kwa heshima apewe hata kiinua mgongo [Japo najua kwa sasa ana mahela mengi ameyajaza kwenye makontena].

Akikaza shingo ataburuzwa mkuku mkuku mpaka kwa pilato wa Kisutu mwendo wa kijeshi.

Sijui atavaa ushungi au watamvua??? WE HUOGOPI?
 
Unafikiri Kissu ni kama Mbowe! Ambaye ukimuwekea hela mezani hachomoki? Muulize Abdul alipokwenda na begi la hela nyumbani kwa Lissu kwa lengo la kumziba mdomo, tena akisindikizwa na Wenje! Halafu nini kilitokea.
ipo sku utahuzunika ukija kujua za ndan kwa sasa we komaa ivo ivo
 
Sasa itakuwaje jeshi lisipokuwa upande wa samia?

Maana yake samia anabaki kuwa kama msanii wa bongofleva tu, sio Amiri jeshi tena.

Watamfurumusha, bora ajiondokee zake kwa heshima apewe hata kiinua mgongo.

Akikaza shingo ataburuzwa mkuku mkuku mpaka kwa pilato wa Kisutu mwendo wa kijeshi.

Sijui atavaa ushungi au watamvua??? WE HUOGOPI?
😂 😂 tesha ashasema mjitokeze tar 29 na ametoa onyo ole wa mtu aguse mtu anaandamana tar 29
 
Mazingira na visababishi vya fukuto ndani ya jeshi ni kama ilivyokuwa mwaka 1985.

Hii 2025 kuna mazingira na visababishi kutaka mabadiliko turejee historia :


TOKA MAKTABA: KESI YA UHAINI

Kapteni Mstaafu Rodrick Roberts : Sitasahau nilipohukumiwa maisha jela

1759584182684.jpeg

Kapteni mstaafu Rodrick Roberts

Rubani wa ndege aliyeonja kifo kwa ajali ya ndege na kifungo cha maisha, Rubani huyu ni Kapteni Mstaafu Rodrick Roberts (69). Picha na Maktaba

Na Lauden Mwambona, Mwananchi

Posted Alhamisi, Novemba 28 2013 saa 13:0 PM

KWA UFUPI

Rubani huyu ni Kapteni Mstaafu Rodrick Roberts (69) mrefu, mweupe ambaye si mnene na wala si mwembamba akiwa na nywele laini zinazoashiria wazi kwamba mmoja wa wazazi wake alikuwa mtu wa nje ya Bara la Afrika.
Nje kidogo ya Mji wa Songea, kipo kijiji kinachoitwa Mateka. Bila shaka jina la kijiji hicho lina historia yake, lakini kubwa ni kwamba ndiko anakoishi rubani wa ndege aliyeonja kifo kwa ajali ya ndege na kifungo cha maisha.

Rubani huyu ni Kapteni Mstaafu Rodrick Robert (69) mrefu, mweupe ambaye si mnene na wala si mwembamba akiwa na nywele laini zinazoashiria wazi kwamba mmoja wa wazazi wake alikuwa mtu wa nje ya Bara la Afrika.

Ni mara ya kwanza kumwona alipokuwa akifungua mlango, lakini anatoka na tabasamu baada ya kuona wageni nje wakiwa na mkewe aitwaye May Daud Robert aliyeniongoza kufika hapo mara ya pili baada ya kumwomba aachie kidogo kazi yake mjini Songea na kunipeleka nyumbani kwake nikaonane na mumewe.

Kwa kweli ilikuwa mara ya pili kwangu kufika pale saa 11.00 jioni baada ya mara ya kwanza ya saa 4.00 asubuhi ya siku hiyo kuwakosa nilipopelekwa na msamaria kwa pikipiki mbili.

Robert anatukaribisha ndani huku akisema alipata taarifa za kuwapo kwa wageni wanaomtafuta tangu asubuhi. Tunaingia ndani na kufika kwenye sebule ikiwa na makochi ya kawaida na hatimaye Robert, mkewe na mimi tunaketi.

Akiwa anamwangalia mkewe aliyeketi upande wa kushoto kwake, Rubani Robert ananikaribisha.

Anasimulia kidogo historia yake.

Rubani: Nilizaliwa Mtaa wa Mtini mjini Songea mwaka 1944 na baba yangu alikuwa mhandisi wa kujenga barabara na nyumba za Serikali na alishiriki kujenga Uwanja wa Ndege za Jeshi Dar es Salaam.

Nilisoma chekechea mjini Songea, Shule ya Msingi Songea na Peramiho baadaye Sekondari ya Wavulana Songea kabla ya kujiunga St Michael ya Iringa ambayo baadaye ikawa Mkwawa Sekondari na sasa ni chuo.

Baada ya kumaliza Mkwawa nilingia Chuo Kikuu cha Dar e Salaam kuchukua Sayansi ya Jamii, lakini nilisoma mwaka mmoja nikaacha.

Mwandishi:Ni sababu zipi zilikuachisha chuo?

Rubani: Sikumbuki.

Mwandishi:Baada ya kuacha chuo kikuu ulikuwa unafanya nini?

Rubani:Nilikuwa nyumbani nikijishughulisha na uandishi na pia kuchora jambo ambalo lilinifanya niitwe kwenye mafunzo ya siku sita kuhusu uandishi Chuo Kikuu cha Makerere ambako nikawa mmoja wa watu wa kwanza tulioandika jarida la kwanza la chuo hicho. Niliporudi nchini nilipata kazi kwenye Shirika la British America Tobacco Company (BAT) ambako nilifanya kazi karibu mwaka mmoja na baadaye niliacha.

Mwandishi: Ni kwa nini uliacha?

Rubani: Sikumbuki.

Mwandishi: Baada ya hapo ulikwenda wapi?

Rubani: Nakumbuka mwaka 1970 nikiwa nyumbani Songea, alikuja Jenerali Luis ambaye alikuwa mwenyeji wa Mkoa wa Rukwa na kuniambia kwamba walikuwa wakihitaji vijana waliosoma ili wawe marubani wa jeshi. Hoja hiyo niliipenda na nikakubali, hivyo aliniandikisha na kunitaka niende kwenye mafunzo ya kijeshi (TMA) Dar es Salaam kwa ajili ya uofisa.

Nilimaza mafunzo kwenye kikosi cha anga Dar es Salaam na baada ya hapo pamoja na wenzangu karibu 14 tuliendelea na mafunzo ya kuendesha ndege kwa chini (Ground School) kwa mwaka mmoja na baada ya hapo tulianza mafunzo ya awali ya kurusha ndege.

Mwandishi: Tangu mafunzo hadi kuanza kazi, je uliwahi kupata ajali?

Rubani: Ndiyo, nilipata ajali mwaka 1978 nikiwasafrisha askari 26 kutoka Dar es Salaam kwenda Beira Nover Freesco Msumbiji ingawa sikujua askari wale walikuwa wakienda nchi gani. Sijui walikuwa wa Zimbabwe au Angola sijui. Injini ya kushoto ilizimika ghafla na baadaye injini ya kulia ikazima hivyo nililazimika kutua kwenye shamba dogo porini na askari wote tulitoka salama isipokuwa mmoja alipata michubuko kutokana na bawa la ndege kugonga kichuguu. Kipande hiki (anainuka kuchukua na kukionyesha kichuma cha bawa la ndege) nilipewa kama kumbukumbu.

Baada ya ajali hiyo, mwishoni mwa mwaka 1978 nilikwenda Uingereza kusoma utaalamu wa ndege aina ya Hauca Cidre748.

Mwandishi:Je, vita dhidi ya Idd Amin Dada ulishiriki?

Ruban: Tangu mwanzo hadi mwisho mimi nilikuwa mmoja wa walioshiriki mchana na usiku hadi vilipoisha.

Mwandishi: Unakumbuka nini kwenye vita hivyo?

Rubani: Nakumbuka siku moja nilikuwa off (napumzika kidogo), nikaamua kunywa bia. Na ratiba ilikuwa ikionyesha nitakuwa kazini kesho yake. Lakini ghafla kiongozi wangu alinijia na kunitaka nirushe ndege. Mimi nilikataa katakata kwa sababu nilikuwa nimekunywa pombe. Niliwahi kumwendesha Nyerere.

Mwandishi: Je, ni kweli ulimwendesha Nyerere? Na kazi ya jeshi iliendelea hadi lini?

Rubani: Ni kweli baada ya vita vya Amini niliendelea kurusha ndege za jeshi na pia kufanya kazi ya kuendesha ndege ya Rais Nyerere. Mwaka 1983 Januari 7, nilikamatwa na wanajeshi wengine wengi kwa tuhuma za uhaini. Tulidaiwa tulitaka kumuua Rais Julius Nyerere. Nilikamatwa nikiwa eneo la Airwing Dar es Salaam. Tulikaa kizuizini hadi Julai mwaka 1983 Mahakama ilipotangaza kwamba hatukuwa na kesi ya kujibu. Lakini cha kushangaza mwaka 1984 watu tisa kati ya wale walioshikiliwa mara ya kwanza, tulikamatwa tena na kufikishwa mahakamani kwa kosa la kutaka kumuua Rais Nyerere.

Mwandishi: Je, kiukweli mpango huo ulikuwapo?

Rubani. Aaa...ulikuwapo haukuwapo, it was planned by high official (ulipangwa na baadhi ya maofisa za ngazi za juu), unajua baada ya vita vya Uganda nchi ilikuwa imefilisika. Haikuwa na unga, sabuni, sukari na hata nguo, karibu kila kitu hakikuwapo. Hivyo Watanzania wengi walikuwa wamechanganyikiwa na hali ile.

Mwandishi: Kwa maana hiyo mpango huo ungefanikiwa je bidhaa hizo zingeonekana?

Rubani: Rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi aliiokoa nchi baada ya kuruhusu kila kitu kiingie nchini hata bila ya kutoza kodi. Mwinyi aliituliza nchi. Pia Serikali iligundua kwamba waliokamatwa walitaka mfumo wa vyama vingi vya siasa ili kuishtua CCM ambayo ilikuwa imejisahau na hivyo kuanzishwa kwa vyama vingi jambo ambalo lilitekelezwa baadaye.

Mwandishi: Matatizo yaliyokuwapo enzi hizo na sasa unatofautishaje?

Rubani:Kama nilivyosema, enzi za Nyerere nchi ilifilisika, Mzee Mwinyi aliiokoa nchi, Rais Mkapa akaweka msingi wa kukusanya kodi, hivi sasa sijui kinachoendelea kwa kuwa sisomi sana magazeti kwani sina fedha za kununua.

Mwandishi: Mama Robert ulifanikishaje safari yako kurudi Songea. ?

Mkewe: Mimi niliposikia anafungwa maisha nilipigwa na butwaa na simanzi kubwa. Hivyo sikuwa na nguvu, lakini cha ajabu, baada ya saa 12 kupita, mkuu wa kikosi aliniita na kunitaka niondoke kwenye nyumba ndani ya saa 24. Kumbuka wakati ule mimi nilikuwa nafundisha Chuo Cha Utumishi Magogoni Dar es Salaam, hivyo nilihitaji kupata nafasi ya kuomba uhamisho na kufunga mizigo. Lakini mambo ya jeshi ni amri na nilitolewa mizigo ili nisafirishwe kwa ndege ya Jeshi ambayo nayo iliharibika. Lakini kwa bahati ilipona kabla ya saa 12 kumalizika, nikatakiwa nitaje niende wapi.

Suala hilo lilinifanya nitaje Songea kwa vile nilikuwa na watoto sita na Robert na watoto walikuwa wakiwafahamu ndugu wa Songea.

Hivyo mizigo na watoto walisafiri kwa ndege mimi nikabaki Dar es Salaam nikiomba uhamisho wa kwenda kufundisha Shule ya Sekondari ya Songea Wasichana.

Kwa kweli ilikuwa fedheha kubwa. Serikali inampenda mfanyakazi mzuri, lakini huyohuyo akiteleza kidogo ni takataka. Ipo haja ya kubadilisha msimamo huo.

Mwandishi: Kwako rubani, je unalo neno kwa Serikali?

Rubani:Aaaa , tangu nifike huku sijapata na wala sina senti ya Serikali. Wapo wenzangu waliosema eti Serikali inafikiria kutupatia chochote, lakini mpaka sasa sijasikia lolote.

Mwandishi: Kwa sasa afya yako ikoje na unajishughulisha na nini?

Rubani. Afya yangu nashukuru Mungu naendelea vyema, mambo mengine Mungu anasaidia.

Kapteni Mstaafu Rodrick Robert anasema ni suala la msingi kwa watu kuwa na moyo wa kulitumikia taifa kwani ndio msingi wa kuhakikisha tunakuwa na taifa lenye maendeleo makubwa.

Jambo la msingi ambalo napenda kusisitiza ni moja tu kwamba kwa kila kitu ambacho mtu anafanya, anapaswa kuweka mbele maslahi ya taifa kwanza, anasisitiza akiwaasa Watanzania kujenga tabia ya kuheshimu mila na tamaduni za taifa, pia kujali maadili ya uongozi.

Aidha anawashauri vijana kufanya kazi kwa bidii ili kuharakisha maendeleo nchini, kwani vijana ndio tegemeo kubwa kwa taifa na ulimwengu kwa ujumla kwa vile wana nguvu za kutosha.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi
 
Back
Top Bottom