Je, Biblia ya ukweli/Halisi ni ipi?

Mpaka hapo hauoni kuwa dini haina mahusiano na kuzuia maendeleo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kitendo cha kuua taratibu desturi za sehemu husika na kusambaza desturi ngeni ni kuua maendeleo. Walitumia diini kuua mila na desturi zetu - leo hii tunaamini kwenye madawa yao, kila kitu chao hata nyimbo. Alafu unasema dini haina mahusiano na kuua maendeleo ya sehemu husika? Think twice Tz mbongo.
 
Ni mila na desturi zipi zilizoharibiwa na zingesaidia vp katika kuleta maendeleo?
Hebu fafanua mkuu maana haya mambo huwa hamtoi ufafanuzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya tumeona ngoja wajuvi wa mambo waje.

Sent using Jamii Forums mobile app
Labda niandike kitu tu kwasababu nilikuwa nimepita hapa. Nina umri miaka 60 sasa na hilo nimeanza kulisikia zaidi ya miaka 40 iliyopita.

Mimi ni mkristo, nakushauri swali la 2 usingeliweka.
Maana wakujibu swali hilo ni Mungu tu.
Maana yeye ndio ungeaandika vyoote akwambie kipi ni halali na kipi sio halali
Nashangaa hilo swaki limeelekezwa kwa wasomaji ambao bila shaka kila mtu ana dini yake ndio waseme Biblia ni Halali au sio halali

Pili. Katika vitabu vyote vya dini karibu zote tu kuna maaandiko mengi na hadithi pia ambapo Mungu ameonyesha maamuzi yake hayazingatii "wengi wape".

Kwa hiyo watu woote wakisema ni halali hiyo haiifanyi Biblia kuwa halali na watu woote wakisema sio halali haiifanyi isiwe halali maana Mhusika Mkuu mpaka kitabu kikaitwa kitakatifu hayupo. Tunaongea sisi kwa sisi.

Uwe na Amani Bw.Mdogo
 
Ingekuwa ni katiba ningechangia kwani ni kanuni tumetunga wenyewe ila Biblia ni hadithi zilizoandikwa na wasiojulikana . Kwangu neno lililobarikiwa ni yale yanayotuongoza katika katiba . Hakika ukiifuata katiba yako mliokubaliana utauona ufalme wa Mungu . Samahani kwa kutoka nje ya mada .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ndio napojiuliza ina maana kila kitabu cha Biblia ni kisiwa?? Yaani Musa akikataza uzinzi basi anaongea na waisrael sio watanzania au wakristo?? Tukienda kwa staili hii ina maana hata amri 10 za Mungu kwakuwa zilitolewa kwa Waisrael basi watanzania hazituhusu si ndio maana yake mkuu ??
Hapana kiongozi aya ni mambo mawili tofauti! Mfano wako kwenye sheria unatofautiana na kile nachokizungumzia! Ukisoma ilo Katazo la Yohana anasema "husiongeze/kupunguza chochote katika unabii wa kitabu ichi"
Kwahiyo ndugu huwezi nambia mfano; warumi au wakoritho kwamba na hizo nyaraka ni unabii, maana kwenye biblia kuna vitu vingi kuna unabii, nyaraka, injili na Sheria!
Sasa ukifanya nyongeza au punguzo lolote katika unabii ina maana unavuruga mantiki nzima, maana unabii ni fumbo au lugha ya picha kwahiyo yampasa kila mtu afumbue ilo fumbo kwa jinsi alivyojaliwa kivyake na siyo kutafuniwa.
Lakini ili liko kinyume na injili au nyaraka maaana unapomtuma mtu afundishe jambo fulani lazima akifika uko atoe ufafanuzi wa jambo ilo na kwa kufanya ivyo atakuwa kaongeza/ kapunguza kitu ili aeleweke. Ukienda site unakutana na changamoto mpya zinazoitaji ufafanuzi wa ziada lakini kama ni Unabii utaupeleka kama ulivyo huwezi fanya nyongeza yoyote wala ufafanuzi wowote maana ata ww unakuwa umefumbwa.
Sijui kama tuko wote mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hoja ya bandiko langu sio version ya maneno bali content.... Ufunuo wa Yohana inakataza mtu kuongeza au kupunguza maneno ya maandiko sasa basi nmeweka mfano kuwa makanisa tofauti yanatumia namba tofauti ya vitabu ikimaanisha wote hawawezi kuwa sahihi maana tayari wameongeza/kupunguza namba ya vitabu

Sasa swali langu linakuja.... Je Biblia gani ndio sahihi ( at least kwa namba ya vitabu) maana kuna hoja huwa zikiibuliwa humu juu ya Biblia watu wanakimbilia kusema tusihoji maana waliocompile Biblia waliongozwa na Roho mtakatifu Je ina maana Roho mtakatifu anakinzana kiasi awape vitabu pungufu baadhi ya makanisa??

Karibu kunielewesha
Unaelewa maana ya kuongeza maneno au kupunguza?

Elewa hivi kwamba Biblia ni Maktaba Ambayo ina Vitabu vingi! Hivyo msomaji anachagua vitabu vya kusoma!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ingekuwa ni katiba ningechangia kwani ni kanuni tumetunga wenyewe ila Biblia ni hadithi zilizoandikwa na wasiojulikana . Kwangu neno lililobarikiwa ni yale yanayotuongoza katika katiba . Hakika ukiifuata katiba yako mliokubaliana utauona ufalme wa Mungu . Samahani kwa kutoka nje ya mada .

Sent using Jamii Forums mobile app
Katiba ipi sasa ndio ungechangia maana kila nchi ina katiba yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana kiongozi aya ni mambo mawili tofauti! Mfano wako kwenye sheria unatofautiana na kile nachokizungumzia! Ukisoma ilo Katazo la Yohana anasema "husiongeze/kupunguza chochote katika unabii wa kitabu ichi"
Kwahiyo ndugu huwezi nambia mfano; warumi au wakoritho kwamba na hizo nyaraka ni unabii, maana kwenye biblia kuna vitu vingi kuna unabii, nyaraka, injili na Sheria!
Sasa ukifanya nyongeza au punguzo lolote katika unabii ina maana unavuruga mantiki nzima, maana unabii ni fumbo au lugha ya picha kwahiyo yampasa kila mtu afumbue ilo fumbo kwa jinsi alivyojaliwa kivyake na siyo kutafuniwa.
Lakini ili liko kinyume na injili au nyaraka maaana unapomtuma mtu afundishe jambo fulani lazima akifika uko atoe ufafanuzi wa jambo ilo na kwa kufanya ivyo atakuwa kaongeza/ kapunguza kitu ili aeleweke. Ukienda site unakutana na changamoto mpya zinazoitaji ufafanuzi wa ziada lakini kama ni Unabii utaupeleka kama ulivyo huwezi fanya nyongeza yoyote wala ufafanuzi wowote maana ata ww unakuwa umefumbwa.
Sijui kama tuko wote mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hoja yako naielewa kabisa ila nachosimamia mimi ni kwamba Je katazo la kitabu kimoja haliwezi kuwa applicable kwenye maandiko mengine mfano

Torati 4:2
2 Msiliongeze neno niwaamurulo wala msilipunguze, mpate kuzishika amri za BWANA, Mungu wenu, niwaamuruzo

Sasa basi hapa Mungu anasema tusipunguze maneno anayotuamuru na wote tunaamini vitabu vya Biblia vinatoa muongozo na maagizo ya Mungu kwetu sasa basi kanisa fulani kupunguza vitabu na kanisa jingine kuongeza vitabu huoni wanakuwa wamekiuka hii Torati 4:2

Okay hapa pia unaweza sema alikuwa anaongea na wayahudi tu na sio watanzania..... Hivyo swali langu je ina maana basi hata maagizo mengine ya Torati na mwanzo au agano la kale lote tusiyachukue sababu alikuwa anaadress wayahudi pekee?
 
Elewa hivi kwamba Biblia ni Maktaba Ambayo ina Vitabu vingi! Hivyo msomaji anachagua vitabu vya kusoma!

Sent using Jamii Forums mobile app
Torati 4:2
2 Msiliongeze neno niwaamurulo wala msilipunguze, mpate kuzishika amri za BWANA, Mungu wenu, niwaamuruzo

Mstari huu unakataza tusipunguze maagizo ya Mungu.... Sasa kama unaamini Biblia ina maagizo ya Mungu je huoni kupunguza vitabu ni kukiuka hii Torati 4:2?? Na kama sio inamaana leo hii naweza tengeneza Biblia yenye kitabu cha mwanzo pekee na nitakuwa sahihi??
 
Unaelewa maana ya kuongeza maneno au kupunguza?

Sent using Jamii Forums mobile app
Yes naelewa mfano Biblia ya orthodox ya Ethiopia ina vitabu 81 meaning kuna maneno ya Mungu ya vitabu zaidi ya Biblia ya RC yenye vitabu 73 pekee.... Je hapo huoni maneno ya Mungu yameongezwa na kupunguzwa??

Pia kuna hoja inasema Biblia ilikuwa compiled kwa msaada wa Roho mtakatifu sasa inakuaje Roho awaambie Orthodox wawe na vitabu vingi alafu protestants wawe na vichache?? Na kama sio ningependa utumie fursa hii kukanusha rasmi kwamba kuna Biblia ambazo hazijawa compiled kwa msaada wa Roho ili iwe mwanzo na mwisho kwa wakristo wa JF kuja na hoja hiyo kwenye mada za humu

Ubarikiwe
 
Kama kuna agano la kale na agano jipya basi kuna agano la mwisho.

Si lingine ni Qur'an. Kitabu pekee duniani kilichohifadhiwa kwenye mioyo ya watu wengi zaidi duniani na kitabu pekee duniani ambacho aya zake husomwa kwa ghaibu (bila kufungua kitabu) kila siku mara tano na Waislam wasiopungua billion moja duniani.

Hakika Qur'an ni muujiza unaoishi.
 
Tz mbongo , umeuliza ni katiba ya nchi gani ? Maadam mimi ni Mtz ni katiba ya nchi yangu , na nikiwa nje nafuata katiba ya nchi husika . Kwangu mimi katiba hasa ya nchi yangu ni kitabu kitakatifu kwani muongozo wote na kanuni za kuishi zipo pale . Watu walioandaa na kuipitisha kwa wananchi wanajulikana na tukakubaliana nao .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UTANGULIZI
Historia ya Biblia ya kikristo ni ndefu jinsi vitabu vilivyopatikana lakini ntaandika kwa kifupi sana na mengine tutaandaika tunavyozidi kuchangia kwenye uzi huu. Na pia nitoe rai mapema kuwa uzi huu sio wa kidini bali wa kielimu/historia hivyo sitegemei watu kurushiana matusi ya kuhusu dini sijui Mungu yupo au hayupo!! N.k
View attachment 993939
Prologue
Biblia ya kikristo ni mjumuiko wa vitabu mbalimbali vya manabii/Mitume wa Mungu ambao vimejumuishwa pamoja ili kutoa muongozo wa kiimani kwa wakristo kote ulimwenguni. Biblia inatambulika kama iliandikwa na vitabu kujumuishwa kwa uweza wa MUNGU hivyo ni kitabu kitakatifu, lakini kilichonishtua ni kugundua kwamba kati ya wakristo wanatumia Biblia tofauti kabisa yaani Wakatoliki Biblia yao ina vitabu 73, waprotestant vitabu 66, Orthodox Tawahedo (Ethiopia) ina vitabu 81 hili limenifanya nifungue uzi ili tumalize mkanganyiko huu na naomba tusome taratibu na kwakuelewa mada inazungumzia nini kabla ya kuchangia kwa kuongozwa na ushabiki au mihemko.

Historia
Wayahudi (Israel) walikuwa wanaandika maandiko wanayovuviwa na Mungu wao Yahweh tokea miaka 600 kabla ya Yesu na walikuwa na fixed canon ya vitabu 24 (39 ukivigawa) mpaka kipindi cha nabii wa mwisho Malachi 400 BC hivyo inasemekana ndio vitabu pekee vilivyokuwepo. kufikia karne ya 4 kabla ya kristo (KK) wayahudi waliokuwa uhamishoni hasa misri walitafsiri vitabu vya agano la kale vilivyoandikwa kiebrania kwenda kigiriki na kuzaa Biblia iliofahamika kama ''Septuagint''.... Biblia hii ilipata ushawishi sana kuliko ya kiebrania na ieleweke kwamba ni Biblia hii ndio imetumika mpaka na Yesu alipokuwa akinakili maandiko ya agano la kale kiufupi 70% ya quotes kutoka agano la kale kwenye vitabu vya Agano jipya vimetolewa kwenye Greek Septuagint. Kufikia hapa kukawepo na Biblia mbili kuu hivyo twende pamoja.
View attachment 993940
Mgogoro
Ikumbukwe Septuagint ilijumuisha vitabu vya kimafundisho ambavyo Hebrew bible haikuvitambua vitabu hivi vinajumuisha Macabees, Sirach,Wisdom of solomon n.k. Sasa ikafika mahali Septuagint (kigiriki) ikawa inatumika zaidi kuliko maandiko ya kiebrania (wayahudi) hivyo kwa mujibu wa mwanahistoria Heinrich Graetz ikabidi kikundi cha wayahudi kikutane kwa kilichoitwa council of Jamnia kilichofanyika 70 Baada ya kristo ambapo ndio kiliweka msimamo wa vitabu gani vya biblia ya kiebrania ndio vitambulike kwa wayahudi wote yote hii ili kuzuia upepo wa Biblia ya Greek sepruagint na hivyo hapa wakawa na msimamo wa vitabu vichache hasa vya agano la kale 39 tofauti na 46 vya septuagint. Hivyo tokea hapa madhehebu tofauti ya kikristo yakachukua Biblia mojawapo ya pande hizi mfano RC wao waliendelea na Greek Septuagint ambayo ndio ilitumiwa na mitume ila waprotestant wao waliamua kuendelea na Hebrew Bible wakiamini ndio halali na haijachakachuliwa pia madhehebu mengine kma Tawahedo Orthodox na mengineo yalikuwa na misimamo yao juu ya vitabu fulani hivyo utakuta baadhi ya makanisa yana vitabu kati ya hivyo 39 hadi 46 vya agano la kale.

Martin Luther
Karne ya 16 kiongozi wa wanamabadiliko/protestants walioamua kujitenga na ukatoliki Dr. Martin Luther naye aliamua kufanya tafsiri ya Biblia kwenda lugha ya kijerumani. Kiliandikwa 1520-34 na katika kuifanyia majumuisho naye alitaka kupunguza vitabu 7 vya agano jipya vikiwemo Ufunuo,Yuda,Waebrania na Yakobo n.k kwa kile alichokiita kwamba "havikuwa na uvuvio wa Roho mtakatifu" na hata leo hii kwenye Luther bible cha waprotestant hivyo vitabu 4 vimewekwa vya mwisho kabisa katika biblia yao na nakala za mwanzoni viliwekwa kundi moja na vitabh vilivyoitwa ''apocrypha''.

Pia luther alikipinga vikali kitabu cha esther nakutaka kifutwe kutoka kwa Biblia. Alisema hakina uvuvio wa Roho mtakatifu maana hakuna mahala kinamtaja MUNGU!! Martin luther alipinga pia uwepo wa kitabu cha James/Yakobo kwenye Biblia sabau kwanza kiliandikwa karne ya 2 ambapo muandishi wanayedai ni Yakobo kaka yake yesu alishakuwa amekufa toka mwaka 67 BK hivyo aliona kma ni kilifojiwa tu.
View attachment 993938

HITIMISHO
Sasa baada ya kuwa nimepitia baadhi ya hoja za wana JF humu hasa zinazogusa maslahi ya kikristo huwa wana conclude kuwa Biblia haina makosa maana ilivuviwa na Roho mtakatifu sasa nilikuwa nataka wajuzi mnisaidia maswali yafuatayo

1.je kauli hii inapotolewa huwa ina maana ya Biblia ipi ambayo ilivuviwa na Roho?

2. Je Biblia gani ni halali

3. Manabii wanasema usiongeze au kupunguza neno kwenye Vitabu vyao sasa Je kama mmoja ndio yupo sahihi ina maana wengi wamepotoshwa??

4. Na kama wamepotoshwa je nini hatma ya ukristo kama wahuni wachache wanaweza ongeza maneno au kupunguza kwenye Biblia

5. Swali la mwisho naamini MUNGU anaona haya makosa Je ina maana karuhusu neno lake lipotoshwe?? Na kama sio kwanini mpaka sasa kaacha wahuni wachezee NENO lake.

Naomba kuwasilisha

Cc: ningeomba Moderator kina Active na Mhariri msihamishe uzi huu jukwaa la dini ili niweze kupata mawazo ya wana JF wote hta wasio na access na jukwaa la dini, nitashukuru kwa hilo.
Wengine tuko hapa kufundishwa nawewe hivo hata majibu hatuna.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom