Biblia ina historia ndefu sana. kwa mtumiaji wa kawaida inabidi tu aiache kama ilivyo na aamini kilichopo.
Maandiko ya kale yaliandikwa na wafuasi wa musa, amabavyo ndiyo vitabu vitano vya kwanza vya biblia, vinaitwa PENTATUCH. hivi ni vitabu vya mwanzo, kutoka, walawi, hesabu na kumbukumbu la torati.
Baadae walikuja manabii kama vile isaya, Amosi n.k. Inasadikiwa Amosi ndio kitabu kikongwe kabisa miongoni mwa vitabu vya manabii. sitaki kuandika kuhusu mgawanyiko wa vitabu vya biblia maana si mada husika hapa.
Biblia ilikuja kutafsiriwa kwenda kigiriki, kama mleta mada alivyopambanua. Hapa mkanganyiko ndio ulipoanzia. Walikuwepo watafsiri wengi na kwa awamu mbalimbali waliotafsiri biblia kutoka kiebrania hadi kigiriki. Ikumbukwe kuwa Tafsiri zingine zote za biblia zilitafsiriwa kutoka machapisho (tafsiri) ya kigiriki.
katika kutafsiri maandiko kwenda kigiriki, wapo waliotafsiri wakiwa mashariki ya kati (samahani mji nimeusahau) na wapo waliotafsiri wakiwa katika mji wa Alexandria- Misri. Hapa ndipo kulipotokea mkanganyiko wa vitabu vya biblia kutofautiana katika tafsiri. Mfano wayahweist (YAHWEST) wana tafsiri yao na wapo wengine (da, ukilaza wangu umesababisha nisahau majina ya watafsiri wengine, mtanisamehe) wana tafsiri tofauti. Hadi leo ukiangalia vitabu vya biblia vina tafsiri mbalimbali, mfano kitabu cha mwanzo katika biblia ya KING JAMES VERSION ni tofauti na kitabu cha mwanzo katika biblia zingine. Kiuhalisia hizi ni tafsiri tu, si aina za biblia, kulingana na origin ya watafsiri.
sasa basi, baada ya utawala wa RUMI kushiaka hatamu, watawala wa kipindi hicho walikuwa na mamlaka makubwa ya kuchagua tafsiri na vitabu vya kutumia. Kuna vitabu vingi sana ambavyo vimetelekezwa au kuachwa kwa sababu ya matakwa ya watawala. mfano mdogo na hai ni vitabu vya deutorokanoni (kanuni ya pili) vinavyotumika na madhehebu ya kikatoliki duniani kote lakini havitumiki na madhehebu mengine.
Hebu nijaribu kujibu maswali ya mleta hoja japo kidogo...
1.je kauli hii inapotolewa huwa ina maana ya Biblia ipi ambayo ilivuviwa na Roho?
Biblia ni mkusanyiko wa vitabu mbalimbali, vipo vya manabii, vya historia, injili, barua za mitume n.k. Ukiachilia mbali tafsiri mbalimbali za biblia, kiujumla biblia ni moja. tofauti iliyomo katika tafsiri haiondoi uhalisia wa biblia. Pia vitabu vingine kutotumika na madhehebu mengine, pamoja na ukweli kwamba kuna vitabu vingine vimepotea kabisa (vingine inasadikiwa vimefichwa na ROMA) bado msingi wa biblia unabaki pale pale.
vitabu visivyokuwa maarufu au vilivyopotea (mfano vitabu vya matendo ya YESU na mataendo ya PETRO) au vinavyotumiwa na baadhi ya madhehebu (mfano vitabu vya sira, wamakabayo, Thobiti, n.k) havina misingi mikubwa ya kiimani au kiroho, zaidi vinasaidia kufundisha historia ya wahusika au matukio flani. mfano kuna kitabu kinaeleza namna yesu alivyokua, yaani matendo yake akiwa kijana. Kinasema mengi kama vile jinsi mama yake yesu (mariam) alivyokuwa akitembea na yesu sehemu mbalimbale wakitenda miujiza na kuponya watu. Pia kitabu cha matendo ya petro kinatoa hadithi moja inayosema petro alikuwa na mtoto mlemavu lakini petro mwenyewe alikataa katakata kumponya... kitafute ukisome mwenyewe utafurahia hadithi hizi.
kwa kifupi, vitabu vya kiroho ni vile vya musa (pentatuch) na vya manabii. vingine ni vya Ayubu, methali, maombolezo n.k na vitabu vinne vya injili. Kuna barua za mtume paul pia vinasaidia kirao, bila kusahau kitabu cha waebrania.
2. Je Biblia gani ni halali
Biblia halali ni ile inayozingatia tafsiri halali, bila kujali ni nani alitafsiri au ilitafsiriwa wapi na lini. Kwa maana nyingine hakuna biblia haramu. Biblia ni mkusanyiko wa vitabu rasmi vilivyotokana na tafsiri rasmi.
3.
Manabii wanasema usiongeze au kupunguza neno kwenye Vitabu vyao sasa Je kama mmoja ndio yupo sahihi ina maana wengi wamepotoshwa??
Ukiachana na kitabu cha ufunuo, ambacho mwandishi wake anajiita Yohane na kilichoandikwa katika kisiwa cha kupro, hakuna kitabu kingine kinachozungumzia kuongeza ua kuongeza neno. Kinachoepukwa ni kupotosha au kotoa tafsiri isiyo sahihi. Biblia imetoa wigo mkubwa kwa watafsiri, si kama Quran ambayo imekataza kabisa mchezo wowote wa kuchezea maandishi yake.
Katika tafsiri za biblia, hakuna atakaesema yuko sahihi au hayuko sahihi. Kimsimngi maana haijapotoshwa, isipokuwa watumiaji ndo hupotosha maana kutokana na imani zao au namna ya kutafsiri maandiko hayo.
4. Na kama wamepotoshwa je nini hatma ya ukristo kama wahuni wachache wanaweza ongeza maneno au kupunguza kwenye Biblia
5. Swali la mwisho naamini MUNGU anaona haya makosa Je ina maana karuhusu neno lake lipotoshwe?? Na kama sio kwanini mpaka sasa kaacha wahuni wachezee NENO lake.
Kwa maelezo hayo bila shaka hakuba haja ya kujibu maswali namba nne na tano.
cc
zitto junior