Je Biblia ya ukweli/Halisi ni ipi?

zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Messages
10,279
Likes
11,288
Points
280
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2013
10,279 11,288 280
UTANGULIZI
Historia ya Biblia ya kikristo ni ndefu jinsi vitabu vilivyopatikana lakini ntaandika kwa kifupi sana na mengine tutaandaika tunavyozidi kuchangia kwenye uzi huu. Na pia nitoe rai mapema kuwa uzi huu sio wa kidini bali wa kielimu/historia hivyo sitegemei watu kurushiana matusi ya kuhusu dini sijui Mungu yupo au hayupo!! N.k
bible-jpg.993939

Prologue
Biblia ya kikristo ni mjumuiko wa vitabu mbalimbali vya manabii/Mitume wa Mungu ambao vimejumuishwa pamoja ili kutoa muongozo wa kiimani kwa wakristo kote ulimwenguni. Biblia inatambulika kama iliandikwa na vitabu kujumuishwa kwa uweza wa MUNGU hivyo ni kitabu kitakatifu, lakini kilichonishtua ni kugundua kwamba kati ya wakristo wanatumia Biblia tofauti kabisa yaani Wakatoliki Biblia yao ina vitabu 73, waprotestant vitabu 66, Orthodox Tawahedo (Ethiopia) ina vitabu 81 hili limenifanya nifungue uzi ili tumalize mkanganyiko huu na naomba tusome taratibu na kwakuelewa mada inazungumzia nini kabla ya kuchangia kwa kuongozwa na ushabiki au mihemko.

Historia
Wayahudi (Israel) walikuwa wanaandika maandiko wanayovuviwa na Mungu wao Yahweh tokea miaka 600 kabla ya Yesu na walikuwa na fixed canon ya vitabu 24 (39 ukivigawa) mpaka kipindi cha nabii wa mwisho Malachi 400 BC hivyo inasemekana ndio vitabu pekee vilivyokuwepo. kufikia karne ya 4 kabla ya kristo (KK) wayahudi waliokuwa uhamishoni hasa misri walitafsiri vitabu vya agano la kale vilivyoandikwa kiebrania kwenda kigiriki na kuzaa Biblia iliofahamika kama ''Septuagint''.... Biblia hii ilipata ushawishi sana kuliko ya kiebrania na ieleweke kwamba ni Biblia hii ndio imetumika mpaka na Yesu alipokuwa akinakili maandiko ya agano la kale kiufupi 70% ya quotes kutoka agano la kale kwenye vitabu vya Agano jipya vimetolewa kwenye Greek Septuagint. Kufikia hapa kukawepo na Biblia mbili kuu hivyo twende pamoja.
bible-inspiration1-jpg.993940

Mgogoro
Ikumbukwe Septuagint ilijumuisha vitabu vya kimafundisho ambavyo Hebrew bible haikuvitambua vitabu hivi vinajumuisha Macabees, Sirach,Wisdom of solomon n.k. Sasa ikafika mahali Septuagint (kigiriki) ikawa inatumika zaidi kuliko maandiko ya kiebrania (wayahudi) hivyo kwa mujibu wa mwanahistoria Heinrich Graetz ikabidi kikundi cha wayahudi kikutane kwa kilichoitwa council of Jamnia kilichofanyika 70 Baada ya kristo ambapo ndio kiliweka msimamo wa vitabu gani vya biblia ya kiebrania ndio vitambulike kwa wayahudi wote yote hii ili kuzuia upepo wa Biblia ya Greek sepruagint na hivyo hapa wakawa na msimamo wa vitabu vichache hasa vya agano la kale 39 tofauti na 46 vya septuagint. Hivyo tokea hapa madhehebu tofauti ya kikristo yakachukua Biblia mojawapo ya pande hizi mfano RC wao waliendelea na Greek Septuagint ambayo ndio ilitumiwa na mitume ila waprotestant wao waliamua kuendelea na Hebrew Bible wakiamini ndio halali na haijachakachuliwa pia madhehebu mengine kma Tawahedo Orthodox na mengineo yalikuwa na misimamo yao juu ya vitabu fulani hivyo utakuta baadhi ya makanisa yana vitabu kati ya hivyo 39 hadi 46 vya agano la kale.

Martin Luther
Karne ya 16 kiongozi wa wanamabadiliko/protestants walioamua kujitenga na ukatoliki Dr. Martin Luther naye aliamua kufanya tafsiri ya Biblia kwenda lugha ya kijerumani. Kiliandikwa 1520-34 na katika kuifanyia majumuisho naye alitaka kupunguza vitabu 7 vya agano jipya vikiwemo Ufunuo,Yuda,Waebrania na Yakobo n.k kwa kile alichokiita kwamba "havikuwa na uvuvio wa Roho mtakatifu" na hata leo hii kwenye Luther bible cha waprotestant hivyo vitabu 4 vimewekwa vya mwisho kabisa katika biblia yao na nakala za mwanzoni viliwekwa kundi moja na vitabh vilivyoitwa ''apocrypha''.

Pia luther alikipinga vikali kitabu cha esther nakutaka kifutwe kutoka kwa Biblia. Alisema hakina uvuvio wa Roho mtakatifu maana hakuna mahala kinamtaja MUNGU!! Martin luther alipinga pia uwepo wa kitabu cha James/Yakobo kwenye Biblia sabau kwanza kiliandikwa karne ya 2 ambapo muandishi wanayedai ni Yakobo kaka yake yesu alishakuwa amekufa toka mwaka 67 BK hivyo aliona kma ni kilifojiwa tu.
images-91-jpg.993938

HITIMISHO
Sasa baada ya kuwa nimepitia baadhi ya hoja za wana JF humu hasa zinazogusa maslahi ya kikristo huwa wana conclude kuwa Biblia haina makosa maana ilivuviwa na Roho mtakatifu sasa nilikuwa nataka wajuzi mnisaidia maswali yafuatayo

1.je kauli hii inapotolewa huwa ina maana ya Biblia ipi ambayo ilivuviwa na Roho?

2. Je Biblia gani ni halali

3. Manabii wanasema usiongeze au kupunguza neno kwenye Vitabu vyao sasa Je kama mmoja ndio yupo sahihi ina maana wengi wamepotoshwa??

4. Na kama wamepotoshwa je nini hatma ya ukristo kama wahuni wachache wanaweza ongeza maneno au kupunguza kwenye Biblia

5. Swali la mwisho naamini MUNGU anaona haya makosa Je ina maana karuhusu neno lake lipotoshwe?? Na kama sio kwanini mpaka sasa kaacha wahuni wachezee NENO lake.

Naomba kuwasilisha

Cc: ningeomba Moderator kina Active na Mhariri msihamishe uzi huu jukwaa la dini ili niweze kupata mawazo ya wana JF wote hta wasio na access na jukwaa la dini, nitashukuru kwa hilo.
 
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Messages
10,279
Likes
11,288
Points
280
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2013
10,279 11,288 280
lifecoded chabuso Malcom Lumumba ElungataMshana Jr Eiyer Vi rendra N J subi Bujibuji Kipanga boy Kiranga Che mittoga Ip man 3 mitale na midimu Mzee wa Torano Blaki Womani Grahnman za chembe jimmykb197 911sep11 afsa Francis3 mtu chake NJOLO Msolo Shubiri Pori Pendael24 Mr Miller Elli Khalifavinnie Kennedy Son of Gamba Kanungila Karim Daimler Mr FCB Mr Q geesten66 Jerry Ekky Mnabuduhe Chrisvern Dabby Jr kibuyu180@IGWE SALA NA KAZI Wick Da'Vinci Kudo salaniatz Jokajeusi
 
buzitata

buzitata

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2017
Messages
1,306
Likes
4,896
Points
280
buzitata

buzitata

JF-Expert Member
Joined Apr 11, 2017
1,306 4,896 280
Nawasubiri waanzae kuchangia na mm nishushe nondo zangu
 
ndege JOHN

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2016
Messages
5,604
Likes
8,796
Points
280
ndege JOHN

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined Aug 31, 2016
5,604 8,796 280
Sijasoma bandiko lako kwa sababu ya kuwa busy Sana lakini sitegemei mtu kushindwa kujua ule ujumbe muhimu wa ndani yaani hekima ya bure kabisa katika vitabu vilivyoko kwenye biblia na badala yake kuanza kulalamika kuhusu Aina za maneno ambaye kimsingi ziko wazi pia..Mimi binafsi napenda kutumia biblia ya ulimwengu mpya inapatikana JW library lakini pia biblia yoyote tu nailewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
oscarsolomon

oscarsolomon

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2017
Messages
1,953
Likes
2,783
Points
280
oscarsolomon

oscarsolomon

JF-Expert Member
Joined Apr 8, 2017
1,953 2,783 280
Sijasoma bandiko lako kwa sababu ya kuwa busy Sana lakini sitegemei mtu kushindwa kujua ule ujumbe muhimu wa ndani yaani hekima ya bure kabisa katika vitabu vilivyoko kwenye biblia na badala yake kuanza kulalamika kuhusu Aina za maneno ambaye kimsingi ziko wazi pia..Mimi binafsi napenda kutumia biblia ya ulimwengu mpya inapatikana JW library lakini pia biblia yoyote tu nailewa

Sent using Jamii Forums mobile app
Biblia ipi unaitumia kati ys hizo hapo juu tajwa na mtoa mada?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wordsworth

Wordsworth

Member
Joined
Jan 14, 2019
Messages
48
Likes
122
Points
40
Wordsworth

Wordsworth

Member
Joined Jan 14, 2019
48 122 40
Mimi ni Mkristu Mkatoliki na ukweli utabaki pale pale kuwa dini ni njia ya binadamu kufikia muumba wake. Hivyo basi, watu wali 'edit' Biblia kwa jinsi waonavyo wao ni sawa, na kujua ukweli halisi wa kitabu hiki ni ngumu. Kila mtu aamini tu Biblia anayoona ni sawa bila kuona kwamba wengine wanakosea au wajinga.
 
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Messages
10,279
Likes
11,288
Points
280
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2013
10,279 11,288 280
Sijasoma bandiko lako kwa sababu ya kuwa busy Sana lakini sitegemei mtu kushindwa kujua ule ujumbe muhimu wa ndani yaani hekima ya bure kabisa katika vitabu vilivyoko kwenye biblia na badala yake kuanza kulalamika kuhusu Aina za maneno ambaye kimsingi ziko wazi pia..Mimi binafsi napenda kutumia biblia ya ulimwengu mpya inapatikana JW library lakini pia biblia yoyote tu nailewa

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hoja ya bandiko langu sio version ya maneno bali content.... Ufunuo wa Yohana inakataza mtu kuongeza au kupunguza maneno ya maandiko sasa basi nmeweka mfano kuwa makanisa tofauti yanatumia namba tofauti ya vitabu ikimaanisha wote hawawezi kuwa sahihi maana tayari wameongeza/kupunguza namba ya vitabu

Sasa swali langu linakuja.... Je Biblia gani ndio sahihi ( at least kwa namba ya vitabu) maana kuna hoja huwa zikiibuliwa humu juu ya Biblia watu wanakimbilia kusema tusihoji maana waliocompile Biblia waliongozwa na Roho mtakatifu Je ina maana Roho mtakatifu anakinzana kiasi awape vitabu pungufu baadhi ya makanisa??

Karibu kunielewesha
 
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Messages
10,279
Likes
11,288
Points
280
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2013
10,279 11,288 280
Mimi ni Mkristu Mkatoliki na ukweli utabaki pale pale kuwa dini ni njia ya binadamu kufikia muumba wake. Hivyo basi, watu wali 'edit' Biblia kwa jinsi waonavyo wao ni sawa, na kujua ukweli halisi wa kitabu hiki ni ngumu. Kila mtu aamini tu Biblia anayoona ni sawa bila kuona kwamba wengine wanakosea au wajinga.
Lakini hili jibu lako linakinzana na maneno ya walioandika Biblia... Mfano Mtume Yohana wa ufunuo alisema msiongeze au kupunguza neno kwenye maandiko ya Mungu sababu mtatupwa KUZIMU..... sasa basi huoni makanisa mengine kuwa na vitabu pungufu au nyongeza tayari wamekinzana na maandiko hivo kufanya Biblia zao kuwa batili

Karibu
 
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Messages
10,279
Likes
11,288
Points
280
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2013
10,279 11,288 280
Mkuu kwenye bible kuna mstari unasema hivi "kila neno lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa mafundisho "
Kwa iyo wanaotumia vitabu vingi/ vichache wote wapo sawa.
....
Torati 12:32
32 Neno niwaagizalo lo lote liangalieni kulifanya; usiliongeze, wala usilipunguze.

Je huu mstari unaopinga kupunguza au kuongeza maneno kwa Bible unauzungumziaje ?
 
Emerald47

Emerald47

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2016
Messages
241
Likes
271
Points
80
Emerald47

Emerald47

JF-Expert Member
Joined Dec 16, 2016
241 271 80
Torati 12:32
32 Neno niwaagizalo lo lote liangalieni kulifanya; usiliongeze, wala usilipunguze.

Je huu mstari unaopinga kupunguza au kuongeza maneno kwa Bible unauzungumziaje ?
Torati 4:2
'Msiliongeze neno niwaamurulo wala msilipunguze, mpate kuzishika amri za Bwana, Mungu wenu , niwaamuruzo '
..... Unaweza kunipa utofauti wa neno hili na ulilolitoa
....
 
Wordsworth

Wordsworth

Member
Joined
Jan 14, 2019
Messages
48
Likes
122
Points
40
Wordsworth

Wordsworth

Member
Joined Jan 14, 2019
48 122 40
Lakini hili jibu lako linakinzana na maneno ya walioandika Biblia... Mfano Mtume Yohana wa ufunuo alisema msiongeze au kupunguza neno kwenye maandiko ya Mungu sababu mtatupwa KUZIMU..... sasa basi huoni makanisa mengine kuwa na vitabu pungufu au nyongeza tayari wamekinzana na maandiko hivo kufanya Biblia zao kuwa batili

Karibu
Ndio ni kweli lakini vitabu hvi mwisho wa siku viliandikwa na watu ingawa wanasema kuna uwezo wa Roho Mtakatifu. Hata kama ni kwenda kuzimu, wataenda waliovitoa kwa nia zisizo nzuri au maslahi yao binafsi.
 
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Messages
10,279
Likes
11,288
Points
280
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2013
10,279 11,288 280
Torati 4:2
'Msiliongeze neno niwaamurulo wala msilipunguze, mpate kuzishika amri za Bwana, Mungu wenu , niwaamuruzo '
..... Unaweza kunipa utofauti wa neno hili na ulilolitoa
....
Mkuu yote yanafanana lakini muongozo,sheria,Amri,maagizo ya Mungu n.k yapo katika kila kitabu cha Nabii au Mtume.... Sasa kimoja kinapoachwa na kanisa fulani huoni kuna maagizo ya Mungu yataachwa?? Je huoni tayari wanakinzana na mistari hii miwili
 
dog 1

dog 1

Senior Member
Joined
Nov 20, 2015
Messages
106
Likes
124
Points
60
Age
30
dog 1

dog 1

Senior Member
Joined Nov 20, 2015
106 124 60
Biblia ina historia ndefu sana. kwa mtumiaji wa kawaida inabidi tu aiache kama ilivyo na aamini kilichopo.
Maandiko ya kale yaliandikwa na wafuasi wa musa, amabavyo ndiyo vitabu vitano vya kwanza vya biblia, vinaitwa PENTATUCH. hivi ni vitabu vya mwanzo, kutoka, walawi, hesabu na kumbukumbu la torati.

Baadae walikuja manabii kama vile isaya, Amosi n.k. Inasadikiwa Amosi ndio kitabu kikongwe kabisa miongoni mwa vitabu vya manabii. sitaki kuandika kuhusu mgawanyiko wa vitabu vya biblia maana si mada husika hapa.

Biblia ilikuja kutafsiriwa kwenda kigiriki, kama mleta mada alivyopambanua. Hapa mkanganyiko ndio ulipoanzia. Walikuwepo watafsiri wengi na kwa awamu mbalimbali waliotafsiri biblia kutoka kiebrania hadi kigiriki. Ikumbukwe kuwa Tafsiri zingine zote za biblia zilitafsiriwa kutoka machapisho (tafsiri) ya kigiriki.

katika kutafsiri maandiko kwenda kigiriki, wapo waliotafsiri wakiwa mashariki ya kati (samahani mji nimeusahau) na wapo waliotafsiri wakiwa katika mji wa Alexandria- Misri. Hapa ndipo kulipotokea mkanganyiko wa vitabu vya biblia kutofautiana katika tafsiri. Mfano wayahweist (YAHWEST) wana tafsiri yao na wapo wengine (da, ukilaza wangu umesababisha nisahau majina ya watafsiri wengine, mtanisamehe) wana tafsiri tofauti. Hadi leo ukiangalia vitabu vya biblia vina tafsiri mbalimbali, mfano kitabu cha mwanzo katika biblia ya KING JAMES VERSION ni tofauti na kitabu cha mwanzo katika biblia zingine. Kiuhalisia hizi ni tafsiri tu, si aina za biblia, kulingana na origin ya watafsiri.

sasa basi, baada ya utawala wa RUMI kushiaka hatamu, watawala wa kipindi hicho walikuwa na mamlaka makubwa ya kuchagua tafsiri na vitabu vya kutumia. Kuna vitabu vingi sana ambavyo vimetelekezwa au kuachwa kwa sababu ya matakwa ya watawala. mfano mdogo na hai ni vitabu vya deutorokanoni (kanuni ya pili) vinavyotumika na madhehebu ya kikatoliki duniani kote lakini havitumiki na madhehebu mengine.

Hebu nijaribu kujibu maswali ya mleta hoja japo kidogo...

1.je kauli hii inapotolewa huwa ina maana ya Biblia ipi ambayo ilivuviwa na Roho?
Biblia ni mkusanyiko wa vitabu mbalimbali, vipo vya manabii, vya historia, injili, barua za mitume n.k. Ukiachilia mbali tafsiri mbalimbali za biblia, kiujumla biblia ni moja. tofauti iliyomo katika tafsiri haiondoi uhalisia wa biblia. Pia vitabu vingine kutotumika na madhehebu mengine, pamoja na ukweli kwamba kuna vitabu vingine vimepotea kabisa (vingine inasadikiwa vimefichwa na ROMA) bado msingi wa biblia unabaki pale pale.

vitabu visivyokuwa maarufu au vilivyopotea (mfano vitabu vya matendo ya YESU na mataendo ya PETRO) au vinavyotumiwa na baadhi ya madhehebu (mfano vitabu vya sira, wamakabayo, Thobiti, n.k) havina misingi mikubwa ya kiimani au kiroho, zaidi vinasaidia kufundisha historia ya wahusika au matukio flani. mfano kuna kitabu kinaeleza namna yesu alivyokua, yaani matendo yake akiwa kijana. Kinasema mengi kama vile jinsi mama yake yesu (mariam) alivyokuwa akitembea na yesu sehemu mbalimbale wakitenda miujiza na kuponya watu. Pia kitabu cha matendo ya petro kinatoa hadithi moja inayosema petro alikuwa na mtoto mlemavu lakini petro mwenyewe alikataa katakata kumponya... kitafute ukisome mwenyewe utafurahia hadithi hizi.

kwa kifupi, vitabu vya kiroho ni vile vya musa (pentatuch) na vya manabii. vingine ni vya Ayubu, methali, maombolezo n.k na vitabu vinne vya injili. Kuna barua za mtume paul pia vinasaidia kirao, bila kusahau kitabu cha waebrania.

2. Je Biblia gani ni halali
Biblia halali ni ile inayozingatia tafsiri halali, bila kujali ni nani alitafsiri au ilitafsiriwa wapi na lini. Kwa maana nyingine hakuna biblia haramu. Biblia ni mkusanyiko wa vitabu rasmi vilivyotokana na tafsiri rasmi.

3. Manabii wanasema usiongeze au kupunguza neno kwenye Vitabu vyao sasa Je kama mmoja ndio yupo sahihi ina maana wengi wamepotoshwa??
Ukiachana na kitabu cha ufunuo, ambacho mwandishi wake anajiita Yohane na kilichoandikwa katika kisiwa cha kupro, hakuna kitabu kingine kinachozungumzia kuongeza ua kuongeza neno. Kinachoepukwa ni kupotosha au kotoa tafsiri isiyo sahihi. Biblia imetoa wigo mkubwa kwa watafsiri, si kama Quran ambayo imekataza kabisa mchezo wowote wa kuchezea maandishi yake.

Katika tafsiri za biblia, hakuna atakaesema yuko sahihi au hayuko sahihi. Kimsimngi maana haijapotoshwa, isipokuwa watumiaji ndo hupotosha maana kutokana na imani zao au namna ya kutafsiri maandiko hayo.

4. Na kama wamepotoshwa je nini hatma ya ukristo kama wahuni wachache wanaweza ongeza maneno au kupunguza kwenye Biblia

5. Swali la mwisho naamini MUNGU anaona haya makosa Je ina maana karuhusu neno lake lipotoshwe?? Na kama sio kwanini mpaka sasa kaacha wahuni wachezee NENO lake.

Kwa maelezo hayo bila shaka hakuba haja ya kujibu maswali namba nne na tano.
cc zitto junior
 
dog 1

dog 1

Senior Member
Joined
Nov 20, 2015
Messages
106
Likes
124
Points
60
Age
30
dog 1

dog 1

Senior Member
Joined Nov 20, 2015
106 124 60
Torati 12:32
32 Neno niwaagizalo lo lote liangalieni kulifanya; usiliongeze, wala usilipunguze.

Je huu mstari unaopinga kupunguza au kuongeza maneno kwa Bible unauzungumziaje ?
Torati 4:2
'Msiliongeze neno niwaamurulo wala msilipunguze, mpate kuzishika amri za Bwana, Mungu wenu , niwaamuruzo '
..... Unaweza kunipa utofauti wa neno hili na ulilolitoa
....
ENYI ndugu zangu katika bwana. Maneno haya yana maana moja tofauti yake vinatokana na tafsiri tofauti au toleo tofauti la biblia. Maana ya maneno haya si kupunguza au kubadili neno katika biblia, isipokuwa jamii ilikuwa inaaswa kuzingatia mafundisho yatolewayo pasipo kuongeza sheria zao au kupunguza baadhi ya maagizo. Hapa waisrael walitakiwa kufuata sheria walizopewa kama zilivo bila kuzipuuza au kuzibadili.
 
Emerald47

Emerald47

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2016
Messages
241
Likes
271
Points
80
Emerald47

Emerald47

JF-Expert Member
Joined Dec 16, 2016
241 271 80
ENYI ndugu zangu katika bwana. Maneno haya yana maana moja tofauti yake vinatokana na tafsiri tofauti au toleo tofauti la biblia. Maana ya maneno haya si kupunguza au kubadili neno katika biblia, isipokuwa jamii ilikuwa inaaswa kuzingatia mafundisho yatolewayo pasipo kuongeza sheria zao au kupunguza baadhi ya maagizo. Hapa waisrael walitakiwa kufuata sheria walizopewa kama zilivo bila kuzipuuza au kuzibadili.
Nadhan hapa zitto junior atakua amekuelewa.
Labda niongezee kidogo, kuna kupunguza maneno na kutafsiri maneno, nadhan bwana Zitto atakua amejichanganya katika hilo
 
Emerald47

Emerald47

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2016
Messages
241
Likes
271
Points
80
Emerald47

Emerald47

JF-Expert Member
Joined Dec 16, 2016
241 271 80
ENYI ndugu zangu katika bwana. Maneno haya yana maana moja tofauti yake vinatokana na tafsiri tofauti au toleo tofauti la biblia. Maana ya maneno haya si kupunguza au kubadili neno katika biblia, isipokuwa jamii ilikuwa inaaswa kuzingatia mafundisho yatolewayo pasipo kuongeza sheria zao au kupunguza baadhi ya maagizo. Hapa waisrael walitakiwa kufuata sheria walizopewa kama zilivo bila kuzipuuza au kuzibadili.
Alaf mkuu bible ninayosoma Mimi ndio anayosoma zitto junior
 
Forum statistics

Threads 1,262,497
Members 485,587
Posts 30,123,850