Je, Bado Una Imani na Jason Bourne?

Omutwale

JF-Expert Member
Feb 4, 2008
1,431
1,045
Soma hii series kisha uamue mwenyewe!

Hadithi inaanzia hapa:

Jason Bourne
RIPOTI YA UCHUNGUZI BINAFSI JUU YA UGONJWA WA DR HARISON MWAKYEMBE 12/10/ 2011 (Kama hukupata kuisoma, isome hapo chini mwisho kabla Invisible haja iondoa tena)


Ikafuatiwa na…


HALI YA WAGONJWA DR MWAKYEMBE, MWANDOSYA NA ZITTO -INDIA

JASON BOURNE
TEL:
ID :
Hali ya Mwakyembe
Katika jamii inayoamini maombi kuwa ni sehemu ya uponyaji, basi yatupasa watanzania wenye mapenzi mema na Mh Mwakyembe tufanye hivyo tena haraka sana. Kwa mda wa dk20 nizokaa ndani ya chumba chake maalumu chenye vihami sumu, kwakweli nilitokwa na machozi.

Mh hali yake ni mbaya! Nadhani mtu mzima akisema hali ni maya bila shaka mnatambua.

Hali ya Mwandosya:
Mh Mwandosya sikuweza kumuona live hii ni kutokana na mahali alipolazwa kuwa mbali kidogo na hapo alipo Mwakyembe, Taarifa nilizo zipatata kutoka kwa Daktari Virmandh Gaemr mmoja wa madaktari wanaomtibu Mwandosya ni kuwa hali yake haina tofauti sana na ya Mwakyembe.

Hayo ndiyo niliyoyaona kwa macho yangu!
Asanteni sana.

Nini kikafuata?

…… hatimae yale maneno mengi na kelele za wizara ya afya leo zimezimwa pale shangingi liliposogelea ndege ya Emirates na huku gari la kubebea wagonjwa kutoka Swiss port likijisogeza kwa ukaribu zaidi, kuashiria kuna mtu anashuka akiwa ndani ya wheelchair ama stretcher.

Hatimae gari likajisogeza pembeni na kukaribia kwenye Landcruiser gafla mikono ya shupavu Prof Mwandosya ikajitokeza kushukuru watanzania
na kwa maombi yao na ukarimu wao.

Na sasa:


Monday, 12 December 2011 20:42
Naibu Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe

Patricia Kimelemeta

NAIBU Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe, amerejea nchini akitokea Hospitali ya Apollo nchini India alikolazwa kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa wa ngozi. …..

Kiambatanisho

Jason bourne said:


Ripoti ya Uchunguzi Binafsi juu ya Ugonjwa wa DR HARISON MWAKYEMBE 12/10/ 2011


Baada ya kushauriwa na afisa mwandamizi wa JF bwana PAW kuwa niifanyie marekebisho kidogo hii ripoti na mimi bila hiyana nimefanya hivyo. Ni matumaini yangu kuwa japo uhalisia kamili wa ripoti utakuwa umepungua lakini nitawaomba kuweni wavumilivu.Vilevile nitawaomba radhi wale mtakao kerwa na mpangilio mbovu wa hii ripoti, hii ni kwa kuwa mimi si mtaalamu sana wa uandaaji wa ripoti.
RIPOTI YA UCHUNGUZI BINAFSI JUU YA UGONJWA WA DR HARISON MWAKYEMBE 12/10/ 2011
JASON BOURNE
TEL:*********
ID************Hatua ya kwanza:
Niliamua kujua kama ni kweli kalishwa sumu au laa. Na watu nilio wahusisha katika kujua huko ni TISS.
Katika uchunguzi niliweza kuzungumza na LTK wapatao kumi na tano.

  1. Maboharia wawili
  2. Wapanga mikakati wawili
  3. Mkuu wa LTK
  4. Vijana wa kazi kumi
Wote maelezo yao yalifanana kwa maana ya (walishiriki kupanga na kutekeleza kumlisha sumu Dr Harison Mwakyembe) Hatua walizopitia:
Kwa mujibu wa maelezo ya LTK/D00/B1 mkuu wa kitengo hicho ambae kwa kweli niliongea nae kama rafiki yangu wa karibu ndie aliyenipa mwangaza wakufanikisha kazi yangu.
Katika misheni hii watu wengi wanatakiwa KUFA, nitawataja wale muhimu tu:
1. Wilblod Slaa
2. Samweli Sitta
3. Harison Mwakyembe
4. Said Kubenea
5. Mark Mwandosya Mnamo ijumaa ya tarehe 01/10/2010 saa 4:25, kikao kikuu cha mikakati kilikalika Moven Pick kikihudhuriwa na watu sita,

  1. TISS/A001 XXX
  2. TISS/B1
  3. TISSB32
  4. TISS/B5
  5. TISS/A6
  6. TISS/F5
Baada ya mjadala wa saa moja uliogusa magumu inayokumbana serikali na watu walio waona wao ni vikwazo na waliosababisha magumu hayo, ndipo wakaibuka na listi ya wanaotakiwa kusalimisha uhai wao:Bada ya hapo kesho yake TISS/B1 alikutana na LTK/D00/B1 na kumpa amri ya misheni hiyo na orodha kamili ya watuhumiwa bila kumwambia sababu za mauaji hayo, zaidi alisema "nahitaji ripoti ya utekelezaji".

.....

Je, sasa unamwamini Jason Bourne walau katika hili?
 
Tusubiri,chochote chaweza tokea ni swala la mda tu

kuna mawili kukubaliana nae ama kutokukubaliana nae,je umeziona picha za Mh wakati anasguka uwanja wa ndege DSM? jE UMEIONA AFYA YAKE IKOJE?

nadhani tumwombee awesalama ktk hilo la sumu na kama Madokta wake wangekuwa wa kweli wangetuwekea taarifa za ugonjwa wake na hapo ndipo tungeweza kuwa na maamuzi mengine
 
Pamoja na yote aliyoyaandika, lakini usisahau kuwa aliwataka watanzania kuwaombea hao viongoizi wetu, na kwa jinsi watanzania walivyo na imani za dini zao bila shaka walimuombea, na Mungu akasikia maombi yao na kuwaponya viongozi hao, sioni kama kuna nongwa hapo.

Au wewe huamini kwamba Mungu ana uwezo wa kuwaponya??
 
Ni vigumu sana kuniamini lakini ni rahisi mno kunipinga!

Je ripoti ya madaktari pale india inasomekaje? Je mwakyembe mwenyewe anasemaje? Uhalisia wa hali yake kwa sasa ukoje? Wizara ya afya inasemaje? Serikali yake inasema? Je kila aliyelishwa sumu hufa hata akitibiwa na madaktari bingwa?

Mimi nishatoa ripoti na kwangu mimi itasimama kuwa ndio kauli na ukweli niliouona katika uchunguzi!

Mwenye ripoti ya madaktari wa india aiweke hapa!!
 
mi bado namwamini JB, kwani kama ukipewa sumu ukatibiwa huwezi kupona? kwani kwa kupona kwao inaondoa ukweli kwamba walipewa sumu na mafisadi na wasioitakia mema nchi yetu? sijaelewa mantik ya maneno yako.
 
Imani ni nini?

Kidini (UKRISTO) Imani ni nini?
Waebrania 11:1 inajibu " Imani ni kuwa na uhakika wa mambo yatarijiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana".


Kidunia na haswa katika mada hii, kuwa na imani na mtu ni kuwa na utayari wa kuyakubali au kuyaafiki yale yote anayoyasema au kuyaandika huku ukiwa huna jinsi ya kuyathibitisha mpaka muda umetimia kuthibitisha aliyoyasema au kuyaandika.

Naomba kukosolewa!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom