Dk Mwakyembe arejea nchini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk Mwakyembe arejea nchini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Dec 13, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Dec 13, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Monday, 12 December 2011

  [​IMG]

  Naibu Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe

  Patricia Kimelemeta

  NAIBU Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe, amerejea nchini akitokea Hospitali ya Apollo nchini India alikolazwa kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa wa ngozi. Dk Mwakymbe aliondoka nchini Oktoba 9 mwaka huu kwenda nchini India baada ya hali yake ya afya kuzorota huku ngozi yake ikionekana kudhoofika.

  Baada ya kukaa India kwa takriban miezi miwili, jana saa 7:00 mchana, Dk Mwakyembe aliwasili nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ndege ya Shirika la Qatar Airways.

  Habari zilizolifikia gazeti hili jana mchana zilieleza kuwa baada ya kutua jijini Dar es Salaam, Dk Mwakyembe aliondoka moja kwa moja kuelekea mkoani Mbeya. Akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana, Msemaji wa Familia na Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa alisema, afya ya mbunge huyo wa Kyela, ni nzuri ndio maana ameruhusiwa kutoka hospitali.

  "Ni kweli Dk Mwakyembe amerejea nchini salama. Tunamshukuru Mungu, hii inatokana na madaktari waliokuwa wakimpatia matibabu kumpa ruhusa baada ya kuona hali yake ni nzuri na kwamba anaweza kuendelea na majukumu yake kama kawaida," alifafanua Mwambalaswa na kuongeza:

  "Kutokana na hali hiyo, tunaamini kuwa, kurudi kwake nchini, kutaleta matumaini mapya ya afya yake." Msemaji huyo wa familia alisema, baada ya kurudi, Dk Mwakyembe atapumzika kijijini kwao Kyela ili aweze kujumuika na wanafamilia katika kipindi hiki cha Sikukuu ya Chrismasi na mwaka mpya, kabla ya kuanza kazi rasmi ya ujenzi wa taifa mwakani.

  Alisema, kutokana na hali hiyo anaamini, sala za wananchi ni miongoni mwa mambo yaliyofanya apone haraka na kurudi nyumbani Kuugua
  Taarifa za kuugua kwa Dk Mwakyembe zilianza kuvuma mwanzoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu baada ya kuanza kupata matibabu nchini.

  Hata hivyo, kutokana na afya yake kuendelea kuzorota, Serikali ililazimika kumkimbiza nchini India kwa ajili ya matibabu zaidi.

  Taarifa za awali, zilisema Dk Mwakyembe alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari ambapo alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

  Lakini, taarifa hizo za ugonjwa wa kisukari zilipingwa na baadhi ya washirika wake wa karibu kisiasa, ambao waliamini Naibu waziri huyo, alilishwa sumu iliyosababisha nywele zake kunyonyoka, ngozi ya mwili wake kupepetuka na kutoa unga, huku akiwa amevimba. Hata hivyio ilielezwa kuwa, madaktari nchini India ndio pekee ambao wangeweza kuangalia namna ya kumsaidia katika ugonjwa huo.
   
 2. Matope

  Matope JF-Expert Member

  #2
  Dec 13, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 539
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Ni jambo la kumshukuru Mungu kama amerejea akiwa salama
  Dr pole sana kwa matatizo yaliyokukuta mwenyezi mungu azidi kukujalia uimalike ureje ktk mapambano!big up Bravo kaka!
   
 3. O

  Ogah JF-Expert Member

  #3
  Dec 13, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Dah......Shemeji karibu sana nyumbani......ni habari njema kusikia umerudi salama...........
   
 4. Mbugi

  Mbugi JF-Expert Member

  #4
  Dec 13, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,488
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 160
  "mungu ni mkuu atukuzwe kwa huruma na upendo wake"
   
 5. kawakama

  kawakama JF-Expert Member

  #5
  Dec 13, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,303
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Mungu akupe nguvu na akuepushe na polonium....GOD BLESS U DR
   
 6. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #6
  Dec 13, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Karibu nyumbani Dr. tunamshukuru mungu kwa kukupigania. hatutarajii ukiritimba wa habari, ukate kiu ya habari tuliyonayo watz kuhusu kuumwa kwako, usimame upande wa mungu kwa kusema kweli uepuke kuwaabudu wanadamu.
   
 7. M

  Malabata JF-Expert Member

  #7
  Dec 13, 2011
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 256
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Karibu mpiganaji,Lakini anachana siasa uchwara za magamba,Karibu sana Cdm
   
 8. n

  nnn Member

  #8
  Dec 13, 2011
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  pole sana braza mwakye
   
 9. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #9
  Dec 13, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Karibu Mkuu na Mungu akujaalie maisha marefu na yenye amani tele.
   
 10. M

  Makamuzi JF-Expert Member

  #10
  Dec 13, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 1,157
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Karibu kamanda,CCM hawakutaki,so njoo CDM
   
 11. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #11
  Dec 13, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Tunamkumbusha tu kwamba asidhani ndio amepona. Akumbuke tu 'Pollinium 310' inaua taratibu. Inaweza chukua hata miaka miwili. Sisi tulimshauri asiingize kwenye serikali ya Mk*we*re akaona tunamwonea wivu! Haya hayo ndio matokeo yake!
   
 12. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #12
  Dec 13, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Wale "wachawi" waliosema, hatarudi akiwa anaƶgea, ooh! Atarudi akiwa ndani ya boksi, nk. wako wapi?

  Mnapita kuchungulia na kwenda zenu. Shutu!!
   
 13. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #13
  Dec 13, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  Ni jambo la kushukuru...wish total recovery!
   
 14. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #14
  Dec 13, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Pole sana Mwakyembe, tunasubiri utuakikishie kweli ulipewa sumu kama anavyosema Samuel Sitta
   
 15. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #15
  Dec 13, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  tunashukuru sana Mungu kuona uko salama
  ila uwe makini na hao watu
   
 16. t

  tisa desemba JF-Expert Member

  #16
  Dec 13, 2011
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 439
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  karibu tanzania, karibu kyela.... tuko pamoja nawe katika sala.
   
 17. s

  sawabho JF-Expert Member

  #17
  Dec 13, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Mungu akiwa upande wako, mengine yote ni mapito.
   
 18. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #18
  Dec 13, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Ee Mungu endelea kumlinda.
   
 19. kaburungu

  kaburungu JF-Expert Member

  #19
  Dec 13, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,602
  Likes Received: 2,458
  Trophy Points: 280
  Atukuzwe Mungu kwa kukurejesha ukiwa salama., karibu sana dr mapambano ndo kwanza yameanza.
   
 20. W

  WildCard JF-Expert Member

  #20
  Dec 13, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Huyu amekwisha. Mbona amekimbilia Mbeya? Yeye, Sitta na Nape niliwadharau sana tangu walipomtosa Mpendazoe. Mwenzao anasota wao wamerudi kwenye magari na majumba ya viyoyozi na mishahara na posho nzitonzito.
   
Loading...