Home boy anakwambia ni mali safi hata wewe huwezi kuicha
Yeees! Ni wapendanao fresh from school wakiwa na matumaini ya kutosha kabisa kuishi kwa raha katika dunia hii ya mapenzi kana kwamba mapenzi yamewachagua wao wawili tu apart from watu billion 7 na ushee
Wana kamtoi kamoja ambako wanasongesha nako baada ya kuvuna kile walichopanga
Kama kawaida walipopewa nafasi ya kuambiana maneno matamu kabla ya mbaya haijawa mbaya,kila mmoja alimuahidi mwenzie kwamba atakuwa a better partner kwa mwenzake,na watapendana for ever!
Lakini siku zote mambo huwa tofauti kwa ground,yani inasemwa "zilongwa mbali na zitendwa mbali" nadhani mmenimanya hapo au sio! Kama hujanielewa sio shida zangu
Ikafika kipindi chenyewe murua kabisa kwenye show hii,nayo ni segment ya kucheki telephone,yes segment hii ni kama kwenye sherehe inapofika segment ya maakuli, yes! Kitu cha bufee pale kati na mziki laini kabisa,hapo ndipo tunapo furahia michango tuliyotoa kwa wanandoa
Simu ya baby girl ikachekiwa kwa kutumia code zote za maneno,ikaonekana ipo gud,yes ipo gud kabisa hakuna makando kando
Ikaja zamu ya home boy mkuu wa kambi,baada ya simu kuingizwa code za maneno mbali mbali,ikapatikana na sintofahamu ndani yake
Je,mchongo mzima ulikuwaje mpaka mbanga nzima ikajulikana?
Twende kazi....
Ikasomeka meseji kutoka kwa home boy kwenda kwa brother wake,hiyo inaitwa bro to bro...
Home boy anamwambia bro wake " it was just a night stand tu lakini najuta sijui kwanini nimeingia kwenye hii trap?
Bro akareply " kwani ilikuwaje?"
Home boy " Huyu mama aliniahidi atanipe hela,halafu amesema ana prefer calls tu,na hutaka kunipigia simu muda fulani maalumu tu!
Home boy akaendelea kusema " Na amenipigia kuniambia ana mimba yangu"
Home boy akaendelea kusema " Lakini ni mali safi hata ingekuwa wewe usingeweza kuicha"
Sasa guess who was that mama?
Ni wifi wa mpenzi wake,yani mke wa brother wa mwanamke wa home boy damn!
Home boy anaulizwa of all people ukaamua kutembea na mke wa brother wangu?
Baby girl akaendelea kufungua code " yani kweli shukrani ya punda ni mateke,bro wangu baada ya kumaliza chuo akakutafutia kazi baada ya kujua upo na mimi, na leo hii unamfanyia hivi?
Home boy akajibu " sikudhamiria kufanya hivyo,ila huyo maza aliniahidi atanipa hela,nami nikataka hiyo hela nokununulie zawadi"
View: https://youtu.be/lTXGmiGq2zs?si=TQv0YIrJO_r3b6za
Baby girl akauliza " Hukuona sehemu yoyote ya kupata pesa mpaka kwa huyo mama,na mbona umesema ni mali safi?"
Guys mambo ni mengi na muda ni mchache kama vipi tuishie hapa,kwani kuna shida?
Adios!