JamiiForums Usiku wa manane

JamiiForums Usiku wa manane

hivi kwanini watu wanakufa?, kuna siri gani nyuma ya kifo maana kati ya madaktari wote duniani kwanini hakuna hata mmoja aloweza kuvumbua chanzo cha kuzuia mtu asife?,

mbona wameweza kubadilisha viungo vya mwili wa binadam kwanini wameshindwa kubadili hako ka kitu kanako sababisha mtu anakufa?
Kila kitu kwenye ulimwengu kina mwisho, hata ulimwengu wenyewe.

Wakijitahidi watapunguza kasi ya uzee ila kufa kupo pale pale.
 
kwanini kifo hakizoeleki

0015
Nakumbuka mara yangu ya kwanza kuona maiti. Nilikuwa na miaka 13. Kuna mwalimu alifariki shuleni mwili wake ukaletwa tumuage.

Nilisita, lakini kuna sister mmoja alinishika bega akaniambia "Ili uelewe maisha, ni lazima uelewe kifo." Tukaongozana pale nikauaga mwili.

Nilijifunza kwamba kifo hakina maana yeyote, kifo ni kifo tu. Chenye maana ni huu muda wako uliopo hai. Tafuta furaha yako. Unaweza ukaogopa kufa kwa sababu mbalimbali ila usiiogope dhana ya kifo.
 
Back
Top Bottom