JamiiForums Issues an Official Responce to CCM allegations: (Press Release)

JamiiForums Issues an Official Responce to CCM allegations: (Press Release)

Status
Not open for further replies.
Mtandao wa Kijamii wa Jamii Forums, umekanusha madai yaliyotolewa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Pius Msekwa, kuwa umeanzishwa na vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kwamba unatumiwa na chama hicho katika harakati zake za kisiasa hapa nchini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jamii Forums, unafanya kazi kwa kujitegemea na kwamba haumilikiwi na chama chochote cha kisiasa wala kufadhiliwa na Chadema kama alivyodai Msekwa.

Taarifa hiyo ilisema Msekwa alitoa madai hayo wiki iliyopita wakati akitambulisha Sekretarieti mpya ya CCM mjini Dodoma ambapo alitumia muda wake kushutumu mtandao huo.

Mtandao huo ulisema kwa sasa una wanachama 40,000 waliojiandikisha na kwamba unafanya kazi kama chanzo huru cha habari bila kutumiwa na mtu wala chama chochote cha siasa.

Shutuma hizo za Msekwa zilitolewa Aprili 14, mwaka huu mjini Dodoma ambapo pia mwanasiasa huyo alisema mtandao huo ulichangia kukikosesha kura CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Taarifa hiyo iliongeza kwamba shutuma zinazotolewa dhidi yao kwamba unatumika kuivuruga CCM na serikali yake sio za kweli na kwamba zinalenga kuukwamisha mtandao huo katika harakati zake za kuielimisha jamii na kuipasha habari.

Mtandao huo ulisema CCM unawaandama kutokana na wao kuwa mstari wa mbele katika kupiga vita vitendo vya rushwa ambavyo hivi karibuni vimekichafua chama hicho na serikali yake.

Shutuma hizo zimewasababishia usumbufu kutoka kwa wanachama wao walioenea kona zote za nchi na nje ya nchi na kwamba hatua hiyo ya CCM ni ishara kuwa kimeanza kuuogopa mtandao huo.
CHANZO: NIPASHE
 
Noana kila mwanaharakati anaetaka mageuzi ya kiuchumi,kijamii na kisiasa hapa Tanzania anaonekana ni mpinzani na mwanachadema.sasa wanataka tuwaangalie ,tuwapigie makofi,tuwasifu kwa madudu yao?? Tunachotaka ni maendeleo kwa kila nyanja,kukomesha ufisadi na maovu mengineyo yanayoligharimu Taifa.kwani wao wanatakiwa kutawala milele? kwani wana hati miliki na Taifa kuwa ni lao pekee??? watakoma mwaka huu na baado vijana wanazinduka kwa kasi kubwa kutaka mageuzi.mwisho wa yote umewadia wakitaka na wao waanzishe blog itakayosifu maovu yao watuachie forum yetu inayomulika maovu na kuyaanika.sasa wamewasha moto sijui kama wataweza kuuzima????
 
From Fikra Pevu - Political Paranoia? Tanzania's Ruling Party threatens online social media | Fikra Pevu | Kisima cha busara!

The following is the statement issued earlier today by JamiiForums - the most prominent Tanzanian online social gathering. The popular political forum played a crucial role in a lead up to the General Elections in October 2010 by being the most authoritative source of politica news, discussion and debate. However, few days ago JamiiForums came under a well calculated and targeted attack by the ruling party - Chama cha Mapinduzi - which accused the forum for being "anti-CCM" and "anti-government".

The statement was distributed to a variety of media outlets in the country and abroad as well as to a number of interested parties.

Do not worry colleagues; the role of JF and the the Civil Society world is "TO CIVILIZE THE GOVERNMENT AND OTHER DUTY BEARERS FOR AND ON BEHALF OF RIGHT HOLDERS, THE WANANCHI" Kama hawataki shauri yao. Kama yupo mpinzania na apinge.
Kama katika kutekeleza jukumu hilo mawazo yamefananishwa na chama au taasisi nyingine hakuna shida yoyote.
Mwendo MDUNDO FICHUA MAFISADI.
 
Sioni tatizo la members wa JF kuwa wapenzi wa CHADEMA kama ilivyo wale wa vyama vingine, ila naona tatizo la watu ninaowaheshimu kama Msekwa kudhani jamii forum ni taasisi kama CCM

Kwa taarifa yao, JF ni mimi, wewe, yule na hata msekwa.... JF ni kioo tu cha jamii, kama ni mbuzi basi utajiona ukiwa mbuzi na kama ni mtu utajiona ukiwa mtu

Huwezi kulaumu kioo kwa kuwa sura yako haina mvuto

Eniweis
 
Sasa kama chama tawala kinaendeshwa kwa majungu kama hayo wananchi watarajie kupata maendeleo gani?
 
Chama Cha Magamba.

or, Magamba ya chama cha magamba kilichodai kujivua magamba na bado kikabaki na magamba, it's like kumuondoa Makamba(Gamba-Yussuf) na kumvika the same gamba another Makamba(February), from old gamba to the new gamba, trully ccm is full of magamba!
 
lol. If u did, your Chadema could be in power right now. Lets be honest baab, you are making a living off CCM being in power. Otherwise, your megaphone is impotent.

I remember perusing JF right before election and reading this space you would think Chadema will win a landslide, they ended up losing big. Reading it right now you would think Chadema will take over a country in 3 weeks.

Someni Tanzania literature, Kezilahabi, Mtobwa na wengine ili mupate uelewa wa society ya WaTanzania tulivyo. We are all talk. Read anthropology work in Tanganyika. Heck, even Germany East Africa had to be subsidized from Berlin, the colony was not making any monies. British didn't even bother messing with Tanganyika. Read David Landes' masterpiece on why countries are rich and others a poor.

Throngs of threads about CCJ came and go. At that time you would have thought it was Qiyama for CCM.

InshaAllah November 2015 we will be here. Millions threads will be read and forgotten, and you will probably author few thousands. You candidate will loose. And the society will be better off. Jamii Forum and family will continue to cash up "donors' money.

Life goes on.

Perhaps your reading and literature about Tanzania has made you see just few meters ahead....read, reflect and meditate big...regimes come and go, kingdoms rise and fall....ideologies embraced for some time and then change come....societies are better off only when true democracy is embraced. Big up JF for the contribution toward true change in this society....But I feel sorry for those who embrace evil for few peanuts...keep dreaming my friend, the wind of change is everywhere and it is here, and lives will never be the same especially for many citizens who are living in abject poverty, wewe na wachache may enjoy the crumbs under the tables of wafisadi unaowakumbatia
 
Hapo sasa ndio wameupandisha zaidi, kama Msekwa alifikiri kuutaja mtandao huo ni bora atashangaa baada ya kauli yake utakuwa na wanachama mamilioni hii ni kwa sababu kuwa hata wale ambao walikuwa hawaufuatilii dsasa watataka kujua ni nini kilichomo hadi CCM inaulalamikia?. Nijuavyo mimi mtandao huu ni huru kila mmoja anatoa maoni yake. Msekwa ajiulize badala ya kulaumu tu. Mbona hata vyuo vikuu viongozi wa serikali unapaogopa na hata shule za kata? nawashauri wajiangalie upya na sikujivua gamba tu.
 
Super Man,
Kwanza nakupongeza sana kwa juhudi zako kuhakikisha jf, inapata haki dhidi ya shutuma hizi.

Naunga mkono asilimia 100%, kwenda mahakamani kudai fidia, lengo letu likiwa sio kupata mafao ya tozo, bali kulinda heshima yetu.
Tanzania hatu legistalation yoyote ya cyber law. Sheria zetu zote, zimetokana na sheria za Mwingereza, comon law ambazo walizikopi na kuzipeleka Afrika kusini ilipopata uhuru wake 1912, na baadaye India ikazikopi ilipopata uhuru wake 1948, na Tanzania tocacopy zile sheria za India para-material (neno kwa neno bila kubadili kitu). Wenzetu India, wameshazibadili za kwao na kujumuisha cyber law, sisi bado.

Pamoja na kutokuwa na specific cyber law, tumeshapitisha vifungu kadha wa kadha vyenye kuruhusu prosecution ya cyber crimes kupitia several The Written Laws (Miscellaneous Amendments) na pia kupitia baadhi ya shria mpya tulizoshinikizwa ikiwemo anti-terrosism act.

Wanasheria wamegawanyika sehemu nyingi, wale wenye kushughulikia kesi mbalimbali za madai ya mahakamani, wanaitwa wanasheria waitwa wanasheria wa litigations, na miongoni mwa kesi zinazosumbua mahakamani kuliko kesi nyingine zote, ni kesi za madai ya defamation na libel, zinapoteza muda mrefu na nyingine huishia kutoshinda. Mawakili wa kesi za namna hii nchi za wenzetu, wanatumia mtindo unaitwa 'No Win No Fee', yaani wakili atalipwa tuu baada ya kushinda kesi, ila mgao wake unakuwa ni mkubwa hadi kufikia kugawana nusu kwa nusu (fifty fifty).

Kinachazifanya kesi hizi ziwe sumbufu, ni jinsi ya kuthibitisha umeumizwaje kiuchumi, mfani JF ikidai fidia ya bilioni 100, inatakiwa kuthibitisha kwanza thamani yake, is it woth 100 bilions?, pili kuthibitisha njia za mapato za jf zinatirisha mabilioni hayo, halafu ndipo una prove kuwa matamshi yale yameiangusha jf kimapato hivyo kustahili fidia husika.

Kwa vile lengo letu sio kupata faida ya kuichumi, bado tunaweza kufungua kesi kama ya Mengi na Manji, ambayo Manji anadai Shilingi Moja Tuu (1/=) ili kumthibitishia Mengi, lengo sio mafao bali kulinda heshima.

Gharama za wakili, sio issue sana, mimi naamini kuna mawakili watajitolea kyuibeba hii kesi free of charge. Kwa wenzetu ulaya, ili uweze kujenga jina, mawakili wanaochipukia, hujitolea kubeba complex cases wakishinda ndipo wanapotokea.

Mimi binafsi, sikuwahi kuwa na mpango wa kuwa wakili, lakini jf, ime ni inspire sana, mpaka nimetamani, ningekuwa wakili, ningeibeba hii kesi free of charge, na ninaamini kwa asilimia 100 tungeshinda!.

Mkuu Pasco;

Kwa hili nakupongeza sana. Ni mtazamo wa kijasiri na uzalendo wa hali ya juu if you truly mean it. tuko pamoja Mkuu.

Nakubaliana na maoni yako kwa kiasi kikubwa sana.

Wale Advocates pia wanajaribu kupitia vifungu vya sheria ambavyo vinaweza kutumika in connection with Cyber isuues. will keep u posted.

Nadhani sasa ni Busara au Hekima tu ya Uamuzi kutoka Uongozi wa JF.

Peace & Love.

Respect.
 
Hao attorneys watafanya kaza pro bono? Kama si hivyo sidhani kama kuna attorney ambaye atakataa kuichukua hii kesi hata kama haina mshiko. Vipi wameshakuomba retainer?
 
Kweli nakubaliana na wewe kuwa busara lazima itumike vinginevyo mnataka kuuelekeza uongozi wa JF kwenye moto.
 
Hawana shukurani hawa - kwa hakika kujivua gamba kunakoendelea ni matokeo ya free speech wanayoipiga vita.
 
Thanks Maxcence and the whole JF Technical Team.

The so called "Chama cha Magamba" has a cronic illiness!!! They need to know that JF was there before, is there and will be there, come rain come sunshine!!! JF hosts members and visitors from all angles and pheres of life, including members of Chama cha Magamba and Intelligence!!! JF gives a room for everyone to post and share his/her feelings, suggestions, etc through a key board!!!! We invite newly elected NEC members, if at all not members to join here.

Their existence in the JF will help them learn more from we the Jamii, of our discontents we have for their Chama cha Magamba and the Government it is rulling!!!! Real elites welcome critisms to allow improvements. Tanzanians of today are never those of yesterday and the future ones will never be of Today. We are not Fools anymore!!!!

Long Live JF!
 
Hao attorneys watafanya kaza pro bono? Kama si hivyo sidhani kama kuna attorney ambaye atakataa kuichukua hii kesi hata kama haina mshiko. Vipi wameshakuomba retainer?

LOL

Mkuu, Ni PM tuwekane sawa. Ni vema nieleweke maana naona unashabikia sana mshiko. Sisi nia yetu ni kujisafisha na kujijengea muhimili kama tutashinda na kama itakubalika.

SM
 
Nice piece of writing. Imenifanya nianze kuamni kuwa kumbe hapa kwetu kuna watabiri na wasoma nyota smarter than Sheik Yahya. Eventually tunaweza kumpata Paul the Octopus wetu.
So while others are embarking on investigative and analytical jounalism, you give it something of a surprise rather, an astrological eye! Lol!
We have read mwanakijiji, bring in yours if you want to counter him. A series of book titles - which we never know if you have read already - followed by some fortune telling, will not help,for sure!

Back
Top Bottom