Jamii yashauriwa kuwa na tabia ya kuandika Wosia ili kupunguza migogoro kwenye familia

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Mhasibu Mwandamizi kutoka Wizara ya Fedha, CPA Jenipha Josephat Ntangeki ametoa ushauri huo wa Wosia wakati akitoa elimu kuhusu umuhimu wa jamii kuzingaia wosia alipokuwa akishiriki Kongamano la Wanamitandao ya Kijamii na Wizara ya Fedha kwenye Ukumbi wa 88 Mkoani Morogoro, Jumanne Oktoba 24, 2023.

Jenii.JPG

Mhasibu Mwandamizi wa Wizara ya Fedha, CPA Jenipha Josephat Ntangeki
Jenipha amesema “Nashauri jamii iwe na uelewa wa kuandika wosia, kuna watu wengi wamekuwa wakisababisha wategemezi wao kupoteza stahiki zao walizotakiwa kuzipata baada ya wao kutokuwepo, saabu kubwa ikiwa ni kutozingatia uandishi wa wosia.”

Amesema kuna kesi nyingi zimetokea kwa watu wengi kutopata kile walichotakiwa kukipata kwa kuwa Wasimamizi wengi kama wazazi, mzazi au walezi hawakuzingatia kuandika wosia.

Kujua zaidi kuhusu Wosia pia unaweza kusoma:
= Hatua na Taratibu za Kufungua Maombi ya kusimamia Mirathi Mahakamani
= Ijue Sheria ya MIRATHI, WOSIA na Usimamizi wa mali zitokanazo na Mirathi
= Wazazi/Walezi andikeni WOSIA muwaache wategemezi wenu salama
 
Hata usia hupingwa mahakamani kama ule wa mengi kwa hyo bado hatuja solve tatizo hapo kikubwa watu waache tamaa
 
Kwa waislam hakuna sana mizozo sheria zao ziko wazi nani anapaswa kurithi ikiwa marehemu hajuacha usia. Hii ya ndugu kuvamia mali hakuna.
 
Wangeweka Sheria kwamba unapofikisha miaka 45 ni lazima kuandika wosia.
 
Hamna kuandika wosia. Mali nitafute mwenyewe halafu waje/aje tu mtu kupata kirahisi!? Mungu ajalie niwaache wapasuane meno na watoboane macho. Kinachotakiwa wapate kwa jasho. Yaani wapigane haswa, wauane kama bob junior alivyouawa kuridhi ufalme.
 
Back
Top Bottom