Mbunge Mnzava Asisitiza Kuwa na Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi ili Kumaliza Migogoro ya Ardhi Nchini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

MHE TIMOTHEO MNZAVA ASISITIZA KUWA NA MPANGO WA MATUMIZI BORA YA ARDHI ILI KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI NCHINI

"Nampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya ya kujali maisha ya wananchi wa nchi hii. Maazimio haya ni ushahidi wa namna Rais anavyowasikiliza watanzania" - Mhe. Timotheo Mnzava, Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini

"Nampongeza Waziri wa Maliasili na Utalii, Naibu Waziri kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuchakata maazimio na kuleta mchakato kujadiliwa katika Bunge. Nakupongeza Spika wa Bunge mpaka kufikia hapa tulipo" - Mhe. Timotheo Mnzava, Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini

"Serikali na Wizara ya Maliasili na Utalii kwenye mgawanyo wa hifadhi ya Kigosi imefanya Umakini mkubwa sana kwa kuangalia maslahi ya Taifa na kuangalia maisha ya watanzania. Niombe waheshimiwa wabunge tuunge mkono maazimio ya Wizara ya Maliasili na Utalii" - Mhe. Timotheo Mnzava, Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini

"Katika eneo la kuigawa hifadhi ya Ruaha Elimu kwa wananchi ni muhimu sana. Serikali iendelee kukubali na kufikiria maisha ya watu katika hifadhi ya Ruaha" - Mhe. Timotheo Mnzava, Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini

"Kazi iliyofanywa na timu ya Mawaziri Nane mapendekezo yaliyotolewa kushughulikia suala la Ruaha, yako baadhi ya maeneo machache ambayo taarifa iliyotumika kufikia maamuzi yale hazikuwa sahihi kule chini. Naishukuru Serikali kuona haja ya kuongeza vitu vya ziada" - Mhe. Timotheo Mnzava, Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini

"Tanga, Wilaya ya Mkinga na Wilaya ya Korogwe eneo Mto Umba, Bonde la Umba eneo Kata ya Mwakijembe, Kata ya Kalalani Wataalam wakienda uwandani watakuja na picha kamili ya kusaidia kutatua mgogoro na kuwanufaisha wananchi" - Mhe. Timotheo Mnzava, Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini

"Waziri wa Maliasili na Utalii tutume tena timu ya Wataalam kwenye maeneo ambayo hayajarudiwa kwa mara ya pili wakafanye uhakika wa hali ilivyo. Pia, tujitahidi kuongeza kasi ili maeneo yaliyopitiwa na timu ya Mawaziri Nane ikamilike tupate utatuzi wa Kudumu tumalize migogoro" - Mhe. Timotheo Mnzava, Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini

"Mwaka 2019 nikiwa Mjumbe wa Kamati niliweka mezani taarifa ya Maoni ya Kamati kupandisha hadhi hifadhi ya Kigosi na Ugara. Wabunge wa maeneo haya waliomba maeneo haya yasipandishwe hadhi ili wananchi wapate mahali pa kufanya shughuli zao. Namshukuru Rais jambo hili limewezekana" - Mhe. Timotheo Mnzava, Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini

"Tuna hifadhi nyingi za Taifa lakini hifadhi nyingi halifanyi vizuri. Hifadhi ya Taifa ndiyo hifadhi ya juu kabisa kwenye uhifadhi ambapo shughuli za kibinadamu haziruhusiwi kabisa. Ni wakati kama Taifa tufanye tathimini sahihi ya uhifadhi wa Taifa" - Mhe. Timotheo Mnzava, Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini

"Maazimio katika Wizara ya Maliasili na Utalii yanatusaidia kupunguza migogoro kati ya wananchi na hifadhi, wananchi na Serikali. Waziri tafakari namna ya kuimarisha Jeshi la Usu ili kulipa Weledi na Elimu zaidi liwe rafiki kwa wananchi tupunguze migogoro kwenye maeneo ya uhifadhi" - Mhe. Timotheo Mnzava, Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini

"Kama nchi tujizatiti katika eneo la Mipango Bora ya Ardhi. Siyo kweli tuna uhaba wa maeneo ya kufanya shughuli za Kilimo na Ufugaji. Changamoto ni hatujatengeneza Mipango vizuri ya Matumizi ya Ardhi" - Mhe. Timotheo Mnzava, Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2021-11-06 at 6.36.02 PM.jpeg
    WhatsApp Image 2021-11-06 at 6.36.02 PM.jpeg
    60.2 KB · Views: 1

Similar Discussions

Back
Top Bottom