SoC01 Jamii ya sasa na njia za kukabiliana dhidi ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI na ugonjwa wa UKIMWI

Stories of Change - 2021 Competition

Paul_123

Member
Aug 10, 2021
49
56
Kwa jamii yetu ya Sasa ni ngum Sana kumtambua mtu anayeishi na maambukizi ya virusi vya ukimwi, au mgonjwa ukimwi kwa kumuangalia kwa macho ya kawaida bila kufanya vipimo vya kisayansi

MAKUNDI AMBAYO YAPO HATARINI SANA KUPATA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI;

1. Watu wanao tumia madawa ya kulevya na walevi.
Kisayansi huonesha mtu anayetumia vilevi hasahasa pombe Mara nyingi Sana hupelekea hamu ya kufanya ngono, kutokana na wote wawili kutokuwa katika Hali yao ya ufahamu hivyo hupekea hawa watu kushiriki ngono pasipo kutumia Kinga. Pia watu wanao tumia madawa ya kulevya kwaktumia shindano nao wapo hatarin Sana kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi kutokana na kutumia shindano moja kwa zaidi ya watu wawili

2. Wanafunzi wa vyuoni.
Hili kundi huambukizwa virusi vya ukimwi kwasababu mbalimbali; kwanza ni ugumu wa maisha, pili kukosa uaminifu, tatu kuishi maisha yasiyo na uhalisia wao na mwisho ni kuongozwa na hamasa ya marafiki

3. Watoto wa dogo.
kwanza kabisa huweza kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, hii hutokea Kama mama hajachukua hatua za awali za kuzuia maambukizi kutoka kwake kwenda kwa mtoto. Pili, huweza kutokea pale watoto wanapo chezea vitu vyenye ncha ambavyo si salama Kama vile shindano au uwembe

4. Watu wanaofanyiwa ukatili wa kingono.
Hili kundi nalo pia lipo katika hatari kubwa sana ya kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi, mfano kuingiliwa kinyume na jinsia au kuingiliwa kinguvu.

JE, NI NINI KIFANYIKE KWA JAMII YA SASA, HILI KUZUIA KASI YA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI?

1. Elimu itolewe juu ya matumizi ya dawa ya kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi ndani ya masaa 72, kwa mtu aliyefanyiwa ukatili wa kingino, mtu ambaye hajatumia Kinga kwa mtu asiye muamini au aliye ingiliwa kinguvu (kubakwa). Dawa hizo zinaitwa; LAMIVUDINE, ZIDOVUDINE na NIVERAPINE ambazo zitakukinga kwa asilimia mia moja kwa kuzuia virusi kushindwa kuingia ndani ya seli na kuzaliana. kumbuka masaa 72 yakipita dawa hii haitafanya kazi yeyote.

2. Elimu itolewe kuhusu madhara yatokanayo na virusi vya ukimwi.
Mfano kupata kansa ya koo endapo muasirika akichelewa kupata dawa (ARVs), Kifo na hata kupoteza uwezo wa kufanya kazi kwa umakini. Haya madhara hutokea Kama muhusika hajatuma dawa za kufubaza virusi vya ukimwi

3. Kuongeza ukaribu na uangalizi mkubwa kwa watoto.
Hii itasaidia kuwazuia watoto kuchezea vitu vyenye ncha kali. Pia kuzuia kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

4. Kuanzisha vipindi maalumu ambavyo vitakuwa vinahusika na utoaji wa elimu na ushauri kuhusu ugonjwa wa ukimwi.

USHAURI KWA VIJANA.

1. UKIMWI upo na unaua, hivyo Kama kijana inabidi uongeze kujijali na kujali wengine. Mfano, kuwa na mpenzi mmoja na kupima afya kila baada ya miezi mitatu

2. Na Kama unaishi ma virusi vya ukimwi huo sio mwisho wa maisha yako bado unayo nafasi ya kuishi Kama kawaida, muhimu ni kuzingatia matumizi mazuri ya dawa ya kufubaza virusi vya UKIMWI na kula vizuri

3. UKIMWI hauonekani kwa macho, hivyo ukipata mwenza nenda naye mkapime afya zenu wote wawili

4. Kuishi vyema na kuwajali watu wote wanao ishi na virusi vya UKIMWI, hatupaswi kuwa nyanyapaa au kuwatenga. Sisi ni tumaini lao kesho yao ipo kwetu

5. Pia kuepuka mazingira hatarishi yanayoweza sababisha maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Mfano kuwa mlevi kupita kiasi au matumizi mabaya ya madawa

MWISHO.
Tukpaime hili tulinde afya zetu na uhai wetu. Usipo pima unahatarisha afya yako na maisha yako
 
Reason kubwa ni kuwa waschana wanawakataa wavulana wakawaida na kupelekea vijana hao kwenda kununua Malaya barabarani.

Tuwafundishe mabinti zetu kuwa na uhusiano sio kosa ,kosa ni kutangatanga katika mahusiano
 
Reason kubwa ni kuwa waschana wanawakataa wavulana wakawaida na kupelekea vijana hao kwenda kununua Malaya barabarani.

Tuwafundishe mabinti zetu kuwa na uhusiano sio kosa ,kosa ni kutangatanga katika mahusiano
Wazo zuri mkuu. Hapa inabidi njia mbadara ihusike. Mfano serikali ianzishe somo la JINSI NA UJINSIA MASHULENI
 
Wazo zuri sana, Kikubwa nikujikinga zaidi na kuelimisha kwani jamii ya sasa inahitaji uwazi zaidi katika kila jambo.
 
Back
Top Bottom