Watu 163,131 walikutwa na Maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI mwaka 2023 Tanzania

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu @ummymwalimu leo January 10,2024 ametoa taarifa ya hali ya utoaji huduma za afya nchini kwa mwaka 2023 katika mkutano wake na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam ambapo amesema katika mwaka 2023 jumla ya Watu 8,145,576 walipima Virusi vya UKIMWI (VVU) na Watu 163,131 kati yao walingundulika kuwa na maambukizi ya virusi hivyo.

Waziri Ummy amenukuliwa akisema “Kwa upande wa ugonjwa wa UKIMWI, Serikali iliendelea kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI ambapo katika mwaka 2023 jumla ya Watu 8,145,576 walipima Virusi vya UKIMWI (VVU) kulinganisha na Watu 6,930,758 mwaka 2022 (DHIS2 2023)”

“Kati ya Watu waliopima mwaka 2023, Watu 163,131 waligundulika kuwa na maambukizi ya VVU ukilinganisha na Watu 182,095 mwaka 2022 (DHIS2 2023)”

“Waliokuwa wanatumia dawa za kufubaza virusi vya VVU walikuwa 1,663,651 December 2023 kulinganisha na Watu 1,612,512 December 2022 (DHIS2023)”

“Mwaka 2023, Vifo vitokanavyo na UKIMWI vilikuwa 22,000 kulinganisha na vifo 29,000 mwaka 2022(Spectrum 2022)”
 
Back
Top Bottom