Kwanini Ukimwi Unazidi kupungua badala Ya kuongezeka

pharao

JF-Expert Member
Jan 17, 2017
381
642
Wakuu mimi si mwanabiologia, ila Kuna mambo yananishangaza haswa kuhusu Ukimwi.

Jambo la kwanza ni ueneaji, Ukifuatilia ripoti kutoka kwa wizara ya Afya utasikia kuwa Kasi ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi Imepungua sana katika miaka ya Usoni.

SWALI LANGU HAPA NI KWANINI KASI IPUNGUE IKIWA IDADI YA WATU INAZIDI KUONGEZEKA MWAKA BAADA YA MWAKA NA UFANYWAJI NGONO ZISIZO SALAMA UNAZIDI KUTAMALAKI MARADUFU. IKIWA HAKUNA UGONJWA HAUNA TIBA KABISA KWA MIAKA ZAIDI YA 30 KWANINI KASI IPUNGUE WAKATI NGONO ZISIZO SALAMA ZINAZIDI KUONGEZEKA!? (MABINTI NA VIJANA WA MIAKA YA 2000 WAKO SPIDI MNO)

SWALI LA PILI NI KWANINI KUPIMA UKIMWI SI KIPAOMBELE HASA KWA NCHI ZA ULAYA. MNAOISHI ULAYA TUNAWAOMBA HAPA MTOE USHUHUDA KAMA MKIENDA HOSPITALI MOJA YA VIPIMO VITATU BORA NI KUPIMA HIV!?
 
Kutokana kuwepo na dawa za kufubaza ukimwi na watu kumeza na kufuatiliwa kwa karibu na dawa kutolewa bure unakuta ukimwi kwenye mwili wa binadamu au muadhirika umefubaa(Kuna viral load supression) hivyo kumwambukiza mtu mwingine inakuwa haiwezekani au kitaalamu inapungua kwa kuwa virus vimefubazwa
 
Wakuu mimi si mwanabiologia, ila Kuna mambo yananishangaza haswa kuhusu Ukimwi.

Jambo la kwanza ni ueneaji, Ukifuatilia ripoti kutoka kwa wizara ya Afya utasikia kuwa Kasi ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi Imepungua sana katika miaka ya Usoni.

SWALI LANGU HAPA NI KWANINI KASI IPUNGUE IKIWA IDADI YA WATU INAZIDI KUONGEZEKA MWAKA BAADA YA MWAKA NA UFANYWAJI NGONO ZISIZO SALAMA UNAZIDI KUTAMALAKI MARADUFU. IKIWA HAKUNA UGONJWA HAUNA TIBA KABISA KWA MIAKA ZAIDI YA 30 KWANINI KASI IPUNGUE WAKATI NGONO ZISIZO SALAMA ZINAZIDI KUONGEZEKA!? (MABINTI NA VIJANA WA MIAKA YA 2000 WAKO SPIDI MNO)

SWALI LA PILI NI KWANINI KUPIMA UKIMWI SI KIPAOMBELE HASA KWA NCHI ZA ULAYA. MNAOISHI ULAYA TUNAWAOMBA HAPA MTOE USHUHUDA KAMA MKIENDA HOSPITALI MOJA YA VIPIMO VITATU BORA NI KUPIMA HIV!?
Sababu nazoweza kutoa ni kama zifuatazo.

1. Ukimwi uliua sana hasa miaka ya nyuma kwahyo wengi wenye ukimwi walikufa kipindi kile

2. Miongoni mwa watu wanaokufa na wenye ukimwi wamo

3. Elimu juu ya faida za kutumia dawa imewaingia wengi na matumizi sahihi ya dawa huwafanya wenye ukimwi wasiambukize tena marad tu wazngatie matumiz sahihi ya dawa

4. Kuna muamko na sheria zinazowafanya watu wakapime na kugundua hali zao na inapotokea mtu akikutwa nao ananzishwa dawa mara moja
 
UKIMWI wa siku hizi hautishi. Ule wa zamani wa miaka ya 90 na mwanzoni mwa miaka ya 2000 ndio ulikuwa noma.

Yaani mtu anabaki fuvu tu, anahema ila mnafanya kuhesabu siku lazima arudi kwa muumba.

Ulikuwa unatisha kiasi mpaka mtu akiupata familia nzima watu wanainyanyapaa.

Siku hizi UKIMWI ni kama mafua tu, mtu akipiga dawa za kufubaza hamuwezi jua.

Halafu siku hizi yale matangazo ya UKIMWI naona hayapewi airtime sijui wafadhili wamekata kamba?
 
SWALI LANGU HAPA NI KWANINI KASI IPUNGUE IKIWA IDADI YA WATU INAZIDI KUONGEZEKA MWAKA BAADA YA MWAKA NA UFANYWAJI NGONO ZISIZO SALAMA UNAZIDI KUTAMALAKI MARADUFU. IKIWA HAKUNA UGONJWA HAUNA TIBA KABISA KWA MIAKA ZAIDI YA 30 KWANINI KASI IPUNGUE WAKATI NGONO ZISIZO SALAMA ZINAZIDI KUONGEZEKA!? (MABINTI NA VIJANA WA MIAKA YA 2000 WAKO SPIDI MNO)

Wenye nao wanakula mbaazi, hivyo kushusha kasi ya maambukizi
 
Watu hawakamii shoo hata kwa waathirika wanaotumia dawa ndio maana hawapati maambukizi.
Kwa nini hawakamii shoo hilo ni swala lingine.
 
Back
Top Bottom