Jamii imempora mwanamke nafasi yake

Jamii imempora mwanamke nafasi yake

Truee
Hata Rebeca 83 amesema the same thing

Huyu kijana mwenye mada ana bias flani hivi abnormal unaiona kabisa kwny mada zake

Na mada zake zote ni about women...women this women that..
U can tell the frustration...

Ni km vile binti ambae mada zake mda wote ziwe about men..tena in a demeaning tone..utapata msg flani..ana maumivu abt men..

Nyenyere soothe ur soul bruhh..ts the soul that needs a surgery

Kumbe kuiongelea sana jinsia fulani ni viashiria vya chuki/maumivu fulani dhidi ya jinsia hiyo?

Fikra zingine hizi
 
Uelewa wako ndio umefikia mwisho, we dont have to agree on everything. Wewe una malezi yako so endelea hivyo. Mambo ya kuchukia wanawake eti kwa kukataliwa san na kukejeliwa ni ramli za kichawi ambazo hazinihusu, nimevuka huo upuuzi na siwezi kujisifia mambo machafu. Hao unaowawazia hivyo ni wale walioishi maisha ya kihuni na kuhusiana na makahaba, nawezaje kujisifia ujinga huo?

I am happy kwa jinsi nilivyo hata kama hufurahii, but FACT: wanawake mmeahama kwenye nafasi zenu na kujiweka kwenye majukumu ya wanaume.
Here is another fact for you: Enzi za kumnyima mwanamke elimu na mali ili mwanaume amtawale zimeisha
 
Mimi sio muandishi mzuri lakini napenda nichangie kwa kusema miongoni mwa mada ambazo zimenigusa ni hii, na mimi ni muhanga wa mfumo huu ulioasisiwa huko Beijing nchini China wakiwiita haki sawa kati ya mwanamke na mwanume, nimesoma wachangiaji wengi kiukweli ninawaunga mkono. Jamii yetu imeingia kwenye shida kubwa ikiamini kumuelimisha mtoto wa kike ndio suluhisho la kuondokana na kunyanyaswa, kudhurumiwa, kuonewa na mengine yanayofanana na hayo.
Lakini matokeo yake Jamii imejaza wanawake wenye kiburi na jeuri kwa sababu tu wanaamini kupitia elimu (kazi) zao wanaweza kufanya wanachokitaka wao hivyo ile heshima ya mwanamke kwa mwanume haipo tena.
Pia mmomonyoko wa maadili kwa watoto umekuwa mkubwa kwani malezi ya wazazi hayapo tena zaidi ya kutegemea wasichana wa kazi kwa wale walioko majumbani lakini pia kutegemea walimu na walezi walioko mashuleni hususani kwenye shule za boarding.
Hii inaendelea kutengeneza wanawake ambao sio wife materials kwani unaweza kuta mtoto wa kike mpaka anafika form4 hajui hata kupika wala kufua nguo zake kwakuwa tayari ameshajengewa mfumo wa kuwa yeye ni mtafutaji na sio mtu wa kufanya kazi fulani, kwakuwa muda wote huo majukumu ama kazi alizopaswa kufanya km mtoto wa kike zinafaywa na walezi a wapo shuleni ama mdada wa kazi a wapo nyumbani.
Inasikitisha sana kuona Jamii yetu inapotea huku tukiendelea kupiga makofi kwa kuimba wimbo wa haki sawa, tuombe neema ya Mungu watu wapate ufunuo kufunuliwa juu ya angamizo hili. Mwenye masikio na asikie.
 
Mkuu umeongea ukweli mtupu hawa viumbe likija suala la pesa kwao ni km hakuna mwisho wa dunia wala hawatakuja kuiacha hii dunia.
Maandiko yanasema nchi na vyote viijazavyo ni Mali ya Mungu dunia na wote wakaao ndani yake.
So wanawake wanapaswa kufahamu kuwa pesa na mali ni vitu vya kupita na mwisho wa siku tutaviacha hapahapa duniani lkn je heshima ya mwanamke katika family na jamii kwa ujumla iko wapi.
Utafutaji huu wa mwanamke umempa kiburi kiasi kwamba yeye haoni umuhimu wa kuwa na mume isipokuwa tu pale ambapo anaweza kutumia nguvu yake ya kiuchumi kummiliki mtu anayemtaka. Inasikitisha sana.
Nioneshe hiyo self-contradiction ilipo kwenye maalezo yangu.

Money is Power ndio hatukatai, lakini je unaitumiaje hiyo power? Hii Ndio hoja kuu iliyopo mezani.

Hata hao wanaume wanaotumia pesa/mali kuwanyanyasia wanawake ni wanachangia kuiharibu jamii.

Halafu nyie wanawake hasa mliochangia huu uzi naona mna ulimbukeni sana, nyie ni ma HEDONISTS mnaoamini maisha ni hela tu na ukishakuwa nazo basi hata mambo mengine ni ya ziada tu.

Ndio maana mpaka mnaona mnaweza kuwanunua wanaume kisha mkawatumia mtakavyo.
 
Hii mambo ya kutaka kuwa sawa na wanaume mimi inipite tuu kwa kweli.
Niacheni mimi niendelee kundeka na kudekezwa, ndio raha ya uanamke wangu... nyie endeleeni kutunishiana misuli na wanaume muone mtakavyoachiwa majukumu ya kiume....
Halafu muanze kulialia wakati mmeyataka wenyewe
Madam katika jamii yetu hii ni ukweli ulio wazi wanawake wanaoishi maisha ya furaha na uhuru wa nafsi ni wanawake wa aina yako ambao wanakubali kukaa kwenye nafasi yao ya uanamke na sio hawa ambao wako bize kutunishiana misuli na wanaume.

Hawa wanawake wenzio wanaojifanya ni ma Alpha females wengi wao wamejaa visirani, uchungu rohoni na chuki kali sanan dhidi ya watu wengine hususani wanaume. Kwa sababu muda wote wako kwenye battle of Supremacy na pale inapotokea jamii kuwachukulia hawana kitu chochote special kulinganisha na wanawake wengine hali hiyo uwajaza hasira sana, maana akilini mwao wanajiona sio wanawake wa kawaida tena.

Mwenyezi Mungu hakuwa mjinga kutuumba tukiwa na hizi tofauti tulizonazo, kuna mambo ambayo yapo kwa ajili ya kufanywa na mwanamke tu, pia kuna mambo ambayo yapo kwa ajili ya mwanaume tu na kwenda kinyume na hapo ni kuishi kinyume na makusudi yake.
FB_IMG_1571433177943.jpeg
 
Mkuu umeongea ukweli mtupu hawa viumbe likija suala la pesa kwao ni km hakuna mwisho wa dunia wala hawatakuja kuiacha hii dunia.
Maandiko yanasema nchi na vyote viijazavyo ni Mali ya Mungu dunia na wote wakaao ndani yake.
So wanawake wanapaswa kufahamu kuwa pesa na mali ni vitu vya kupita na mwisho wa siku tutaviacha hapahapa duniani lkn je heshima ya mwanamke katika family na jamii kwa ujumla iko wapi.
Utafutaji huu wa mwanamke umempa kiburi kiasi kwamba yeye haoni umuhimu wa kuwa na mume isipokuwa tu pale ambapo anaweza kutumia nguvu yake ya kiuchumi kummiliki mtu anayemtaka. Inasikitisha sana.
Asante mkuu kwa kulitambua hilo.

Hawa wanaamini pesa na mali ndio kusudio la wanawake wengi kuolewa, kwa hiyo akiwa navyo hivyo basi hata mwanaume/kuolewa kwake sio suala muhimu tena.

Yaani iko hivi pesa/mali=mwanaume

Ukiwa navyo hivyo basi tayari una mwanaume ndani. Inafurahisha na inasikitisha.

Si umeona kuna mmoja kule mwanzo kasema ukishakuwa na uhuru wa kiuchumi tu(pesa) unaweza hata kumnunua mwanaume, haya ndio mawazo ya wanawake wa kileo kwamba tafuta pesa mambo mengine yatakuwa ni ya ziada tu.

Cha kushangaza pamoja na pesa zao lakini kuna mambo mbali mbali ya Kijamii kama malezi wamefeli vibaya mno.
 
Mimi sio muandishi mzuri lakini napenda nichangie kwa kusema miongoni mwa mada ambazo zimenigusa ni hii, na mimi ni muhanga wa mfumo huu ulioasisiwa huko Beijing nchini China wakiwiita haki sawa kati ya mwanamke na mwanume, nimesoma wachangiaji wengi kiukweli ninawaunga mkono. Jamii yetu imeingia kwenye shida kubwa ikiamini kumuelimisha mtoto wa kike ndio suluhisho la kuondokana na kunyanyaswa, kudhurumiwa, kuonewa na mengine yanayofanana na hayo.
Lakini matokeo yake Jamii imejaza wanawake wenye kiburi na jeuri kwa sababu tu wanaamini kupitia elimu (kazi) zao wanaweza kufanya wanachokitaka wao hivyo ile heshima ya mwanamke kwa mwanume haipo tena.
Pia mmomonyoko wa maadili kwa watoto umekuwa mkubwa kwani malezi ya wazazi hayapo tena zaidi ya kutegemea wasichana wa kazi kwa wale walioko majumbani lakini pia kutegemea walimu na walezi walioko mashuleni hususani kwenye shule za boarding.
Hii inaendelea kutengeneza wanawake ambao sio wife materials kwani unaweza kuta mtoto wa kike mpaka anafika form4 hajui hata kupika wala kufua nguo zake kwakuwa tayari ameshajengewa mfumo wa kuwa yeye ni mtafutaji na sio mtu wa kufanya kazi fulani, kwakuwa muda wote huo majukumu ama kazi alizopaswa kufanya km mtoto wa kike zinafaywa na walezi a wapo shuleni ama mdada wa kazi a wapo nyumbani.
Inasikitisha sana kuona Jamii yetu inapotea huku tukiendelea kupiga makofi kwa kuimba wimbo wa haki sawa, tuombe neema ya Mungu watu wapate ufunuo kufunuliwa juu ya angamizo hili. Mwenye masikio na asikie.
Umeongea vitu vizito sana bro!! Yaani vizito mno ni maneno machache tu lakini yamekusanya scenarios kibao zenye ukweli mtupu.
 
Wanawake tunapoteza nafasi yetu na tunakosa haki na vipaumbele vya msingi kwa kulazimisha kuwa sawa na wanaume.
Huu usawa unaenda hata kinyume na dini zetu..Je Mungu alikosea kumwambia adam atakula kwa jasho? Hivi kwanini hili hakumwambia Hawa?

Sisemi kwamba wanawake wanatakiwa wasitoke jasho ila hata Mungu alijua kwamba hatuwezi kuwa sawa ila tunaweza kuwa wasaidizi wazuri sana
Madam kama Mungu angekuwa anataka tuwe sawa basi hakuwa na haja ya kutuumba na hizi tofauti zetu tulizonazo ambazo ndio zimekuwa msingi wa mgawanyo wa kimajukumu.

Kama angetaka tuwe sawa hakuwa na haja ya kumfanya mmoja awe dhaifu kimwili kuliko mwingine.

Kama angetaka tuwe sawa basi wote angetupa adhabu zinazofanana.

Leo hii tunalazimisha usawa lakini nature inatuhukumu. Na uzuri wa nature inatuumbua bila kificho.

Sasa hivi yale masuala ya kupewa vipaumbele kwa kuangalia jinsia hayapo tena kwenye matukio mbali mbali. Na hata kama yapo basi ni kidogo na yanaenda yanaisha.

Kadri siku zinavyozidi kwenda wanaume nao wanajifunza kwenda sawa na huu mfumo mpya.

Wanawachukulia wanawake kama wanaume tu. Mimi mwenyewe ni mmoja wapo ambaye tayari nimeanza kuwachukulia wanawake kama ninavyowachukulia wanaume tu.

Leo hii ikitokea vita ya tatu ya dunia nakuhakikishia kila mtu anapigania kuokoa maisha yake tu.

Na wala hakuna mwanaume atakaye sacrifice maisha yake kwa ajili ya wanawake na watoto kama ilivyokuwa imezoeleka miaka ya nyuma.

Huu mfumo umekuja kutusaulisha kabisa kama kuna dini na kuna wengine umewaondolea dini kabisa, wanaona dini ni nyenzo ya ukandamizaji, utakuta wanakwambia vitabu vya dini vimeandikwa na mwanaume kwa maslahi yake binafsi halafu cha ajabu hawawezi hata kuthibitisha haya madai yao.
 
Nimesikitishwa sana na hiki kipande cha bandiko lako inaonesha wazi kabisa haujui kabisa athari za huu mfumo unaompedelea mwanamke.

Ndugu huu mfumo unaofanya dunia ya sasa kumpendelea mwanamke sio wa kushabikia hata kidogo, maana athari zake ni kubwa mno na zinatulenga jinsia zote mbili.

Ulimwengu wa sasa unampendelea zaidi mwanamke kwa kumpa umuhimu mkubwa kuliko jinsia nyingine. Kuna taasisi nyingi sana duniani zimeanzishwa kwa ajili ya kushughulika na masuala ya wanawake, sheria zetu zenyewe zina mpendelea zaidi mwanamke na hata ukija kwenye jumuiya kubwa za kimataifa zinalinda sana maslahi ya wanawake kuliko wanaume mfano kama UN kuna departments zaidi ya 8 ambazo ni mahususi kwa kushughulika na women issues lakini hakuna hata moja inayoshughulika na wanaume.

Kutokana na hali hii ya mwanamke kupendelewa na kuaminishwa kuwa anaweza kuwa sawa na mwanaume imepelekea kutokea kwa gender isolation.

Siku hizi ni matukio ya wanaume kusingiziwa kesi za ubakaji na wanawake yamekuwa mengi sana, na sababu kuu hasa ni huu upendeleo wa kijinsia tulionao kwenye dunia ya leo.

Na hii imepelekea wanaume kutengeneza distance baina yao na wanawake kutokana na hofu pamoja na kutoona hawana umuhimu kwa wanawake. Yaani imefikia hatua mwanaume anaona yuko salama zaidi asipojihusisha na mwanamke kwa jambo lolote lile.

Ni kwa bahati mbaya sana waathirika wakuu wa hii gender isolation ni wanawake. Na tayari athari hii imeshaanza kuonekana huko ambako haya mambo yameanzia.

Nchini Sweden matukio ya uhalifu ikiwemo ubakaji yamekuwa mengi sana miaka hii ukilinganisha na miaka ya nyuma. Na waathirika wakuu wa matukio haya ni wanawake.

Mwaka juzi wanawake wa Sweden waliandamana wakiwalaumu wanaume wa nchi hiyo kwamba wamejitenga sana na ndio maana wanawake wengi wamekuwa wakibakwa na kufanyiwa matukio mengine ya kihalifu.

Kwa madai yao ni kwamba endapo kama wanaume wa kiswedish wangekuwa karibu na wanawake basi kusingekuwepo na matukio ya ubakaji kwa kiasi kikubwa hivi.

Cha kushangaza hao hao wanawake ndio chanzo cha wanaume kujitenga na wao mpaka wanakutwa na hayo maswahibu.

Kuna tukio lingine lilitokea huko Italy miaka ya nyuma kidogo linaloonesha jamii yetu imefikia pabaya sana kutokana na huu mfumo unaoufurahia na kuupigia debe. Ngoja nikuwekee kipande cha hiyo habari..

PASSENGERS of the Costa Concordia, the cruise ship that sunk off an Italian island on Friday [13th January 2012], told The Daily Mail that in the chaos after the ship was wrecked, men rushed for the lifeboats and gave no priority to women and children.

As she [one of the survivors ] waited for a flight home from Rome, grandmother Sandra Rogers, 62, told the Daily Mail: ‘There was no “WOMEN and CHILDREN FIRST” policy. There were big men, crew members, pushing their way past us to get into the lifeboats. It was DISGUSTING.’


Kwa kuangalia hiyo scenario hapo utaona wanaume wa leo sio wale wa zama zile za TITANIC, wanaume wa siku hizi hata wao wamejifunza kwenda na huu mfumo wenu mpya, yale masuala ya wanawake na wanawake kwamba ndio wanapewa kipaumbele kwenye kuokolewa pale yanapotokea majanga hayapo tena. Maana hata wanawake pia wanaweza kufanya chochote ambacho wanaume wanafanya ikiwemo kujiokoa wenyewe kwenye ajali.

Hivi umewahi kujiuliza siku Ikitokea vita ya tatu ya dunia hali itakuwaje?

Wewe unahisi kwa huu utengano na ubinafsi tuliojengewa na huu mfumo wenu wa haki sawa wanaume watakuwa tayari kujitoa kwa ajili ya wanawake kama walivyo fanya miaka ya nyuma??

Dunia ya sasa inajaribu kukuaminisha kwamba huko sawa na mwanaume kwa kila kitu, lakini hicho kitu hakipo na wala hakitakuja kutokea. Uking'ang'ania sana utajikuta wewe ndio unayepoteza pakubwa.

Tunaweza kuandika maelezo mengi hapa ukaona kama ni stress tu ndio zinazoandika lakini nikwambie kwa mawazo hayo uliyonayo unastahili kupewa pole sababu unashabikia na kufurahia kitu usichokijua madhara yake.
Umeongea point aisee....umetema madini
 
Mkuu Nyenyere kuna mada Fulani ulipost hapo nyuma na kwa kweli nilitofautiana sana na mtizamo wako(na mpaka sasa natofautiana na wewe)

Lakini kwa mada hii ya leo nakuunga mkono asilimia mia moja na naomba niongezee hoja kadhaa hapa chini kuunga mkono mada yako

Mkuu kwa sababu ya mapinduzi yalifofanyika na yanayoendelea kufanyika kila siku,leo hii tunapata familia na vizazi vibovu kuwahi kutokea,kwa nini?

leo hii baba na mama wote ni wafanyakazi kuondoka aubuhi kurudi usiku,watoto wameshakula wamelala,anayeshinda na watoto ni dada wa kazi ambaye haijulikani anashindaje na kuwatendeaje watoto,mama anapoondoka anaacha tu maagizo dada utampa mtoto uji,utamwekea katuni,utahakikisha anafanya homework,mtoto ni wa dada wa kazi?dada wa kazi anajua thamani ya yule mtoto?akiharibika dada ana hasara yeyote?na akiwa mtu mzuri kioo cha jamii,ni kwa namna gani dada wa kazi anafaidika hivi kwamba atajitahidi kwa kadri awezavyo kumlea mtoto ipasavyo?

kwa mfano huo mdogo tu wale ambao wamewahi kuona madhara ya aina hi ya Maisha wataelewa nachokisema ila kwa wale ambao wanaamini njii hii ya Maisha ni sawa si ajabu huko mbeleni watu watakuja kuconfess humu (painful ad regret Confession)

Kiasili na kulingana na uumbaji mwanaume aliumbwa kutafuta kwa maana ya kwamba mke alipaswa akae nyumbani atunze watoto muda wote baba anapokuwa katika mihangaiko ya kutafutia riziki mke na watoto wake,ni aina hii yamaisha iliyofanya familia kadhaa za miaka kadhaa kuwa bora na kutokeza vijana wa kiume na mabinti wa kike wenye kutegemeka na kujiheshimu,mama walikuwa wakitumia muda wao mwingi kutunza watoto wao na kuwafundisha lilo sawa na lilo na kosa pia,haikuwa rahisi kwa binti au kijana kuharibika na mama shindwe kuona mbadiliko hayo na kutoa ripoti kwa baba ambaye angeshughulikia hali hiyo kabla mambo hayajaharibika kabisa

lakini leo poor us kuna uwezekano mtoto kashaharibika sana tu (labda kawa mvuta bangi,katoa mimba za kutosha,kawa shoga,kawa mlevi) na bado mama au baba hajui kuhusu yote hayo,watajua saa ngapi wakati wote wako kazini bize kutafuta pesa?nani atampa mwenzie ripoti kuhusiana na maendeleo ya mtoto? dada wa kazi? dada wa kazi wanawajua vizuri watoto wenu? inauma lakini kutokana na aina yetu ya Maisha ya siku hizi,inakuja kujulikana kuwa mtoto kafikia stage ya point of no return na hakuna kinachoweza kufanyika kumsaidia tena just kwa sababu mama na baba wote walikuwa bize kuzitafuta pesa,what for? Maisha bora,,,,Maisha bora yapi?kupoteza watoto wenu mkiwa mmebaki na pesa zenu nyingi??
Mkuu umeongea mambo halisia yanaendelea kwenye baadhi ya familia zetu. Binafsi sometimes huwa na-regret kuoa mke msomi, maana sioni faida yake kiukweli masaa mengi yuko bize na mambo yake hana muda hata na watoto. Lakini pia mwisho wa siku faida ya kazi zake hizo kwa familia ni very negligible.

Yaani kwa uzembe wake kwa watoto ilifika pahala nikahamua kuwa narudi nyumbani mwenyewe mapema ili nikague school works na kuwasimamia watoto wafanye homeworks.

Nilifikia uhamuzi huu baada ya kumsihi afanye hivyo yeye bila mafanikio, wakati huo mimi navipenda kweli vitoto vyangu hivi vi3 na pia ninavilipia hela yangu nyingi ninayopata kwa shida ili visome!

Nikaona bora nijitoe tu muhanga nivisaidie maana kwa upande wangu kama ni kukosea/kupatia maisha kidogo kuna muelekeo ila kwa hawa watoto bado sana kulijua hilo hivyo inabidi kuwasaidia kadri iwezekanavyo hata kama ushirikiano wa bibie ni mdogo.
 
Mimi sitaki uchokozi na mtu siku hizi.
Mnanichokoza lakini hamnipati ng'oo!

Wewe Rebeca 83 na wenzako mnachokitafuta kwangu mtakipata.

Khantwe
Karma ambaye ndiye Marianah
Lady Red
Hamnipati ng'ooo.

Kwanza Rebeca Njoo Pm
Aah na mimi tena
 
Back
Top Bottom