Jamii imempora mwanamke nafasi yake

Jamii imempora mwanamke nafasi yake

Sio nyie tu wakuu, hata mie binafsi nimebaki hoi...!!

Lakini sio jambo la kushangaa sana, maana wao wenyewe kujimwambafy ndio wanaona ufahari wenyewe!! So hivyo wanavyoleta leagues na waume zao, ndio mioyo yao inasema safi-nimefaulu!!

Na niwe tu mkweli, mie mwenzenu nimekuwa na chuki kubwa sana, juu ya huu upumbavu unaoendelea dhidi ya hawa viumbe!!.

Hakika huu upumbavu, unaharibu sana familia zetu...bila shaka waliouleta, walilenga kuisambaratisha kabisa jamii kwa ujumla. Maana unapomuharibu mwanamke mmoja psychologically, ni sawa na umeharibu wastani wa kuanzia watu wa3, katika jamii husika. Na hii yote inatokana na kwamba, kiumbe huyo ndio mwenye karama ya malezi ya watoto na faraja ya mumewe....sasa ikitokea ndio ameoza, hipi itakuwa fate ya hao watoto na baba yao?.

Hakika jamii inateketea sana, kwa matokeo ya hii hali. Na sisi wenyewe ni wetness wa hilo, hakika tumeona watoto wakiharibika kimalezi, huku wababa wakizidi kupukutika siku hadi siku!!

For sure inaumiza sana, honestly hata me binafsi ni mmoja wa waanga wa hii kitu. Hii kitu imeacha alama kubwa sana, katika familia yangu! Hapa nilipo now nimebakiza only one mechanism defence, dhidi ya sumu hiyo...and i don't know if nitaweza au nitachemka!

Ila very sad, hawa viumbe wenyewe hawayaoni hayo! Na hiyo yote inatokana na kwamba, udhaifu wao wa kwanza hupo kwenye UPOFU WA MAONO.
Hakika siku zote, hawa viumbe sio watu wanaoweza kukaa chini na kuliangalia well, jambo moja in and out. Then wakanyanyuka na ujumbe uliokamilika....
Ndio maana M/Mungu, hakawapa wao jukumu la malezi ya familia na sio uongozi wa familia. Maana uongozi wowote, unahitaji nguvu ya maono!

Sasa ukichukua hiyo hali ya upofu walionao, uka-plus na msimamo wa ubishi (msingi mkuu wa feminism), matokeo yake ndio hii hatari tunayoiona sasa. Hapo ni sawa sawa na kipofu, anayekataa kushikwa mkono na kuongozwa kule aendapo.......in fact you can guess, ni nini kitakachompata mtu huyo!

Lakini tusilahumu sana, maana tunaweza tukajikuta tunakufuru bure!

Why nasema hivyo?.

Hakika nasema hivyo, kwa sababu ukiangalia hili suala lilivyo.....unaona kama ni matimisho ya maandiko matakatifu ya kidini.
Mfano mzuri kwetu sisi wakristo:-

1: Tunaona zipo sehemu mbalimbali, zinazo muimiza mwanaume kuishi na mwanamke kwa akili.
Sasa jiulize kwanini mwanaume...??

2: Mwanamke upumbavu uvunja.....kwa mikono yake mwenyewe!
Pia jiulize, ni kwanini mwanamke...??

Note:
Tukumbuke kwamba hata yale, yaliokuwa yanaendelea kule Salem, yalikuwa ni part of plan ya Mungu wetu. Na ndio maana, hata msaliti....alitabiriwa kabisa kwamba atafanya utasaliti.!!

Basi kwa msingi huo, nadhani sisi wachache tulio angalau na mwanga, juu ya hiki kinachoendelea. Tujitaidi kufanya kadili tuwezavyo, kuzikumbusha jamii zetu juu ya nini kinaendelea. Na tusihishie tu hapo, inatubidi pia kuwekeza nguvu kubwa ya kuhakikisha, watoto wetu pia hawaji kuharibika na wao.

Ingawa its hard, lakini tujipe moyo.....we can. God is Good!
Hili bandiko limejaa mambo mazito na umeandika kwa hisia sana mpaka mimi mwenyewe limenipa msisimko. Pole sana kiongozi kwa yale unayopitia ila ninaamini kwa upeo na uwezo ulio nao utayashinda.

Hawa binadamu wenzetu walinyimwa MUONO na hii ni tatizo kubwa kwao. Uwezo wa kung'amua jambo kiundani na kubaini kama lina hasara na hasa kama hasara hizo ni za muda mrefu hawana kabisa.

Wameletewa elimu(kitu ambacho ni kizuri) lakini elimu hiyo imekuwa twisted kwa namna fulani kiasi kwamba inawajenga wakati huo huo inawabomoa bila ya wao kujua.

Angalia leo hii mwanamke anasoma hili aje ashindane na mwanaume na sio kuja kushirikiana na mwanaume kwenye ujenzi wa jamii iliyobora. Na hili tunaweza kuliona hata hapa kwenye huu uzi, wao wanaona elimu ni nyenzo ya kupambana na mwanaume.. Inasikitisha kweli.

Sipingani na mwanamke kuelimika ila napingana na namna ambavyo elimu inatumiwa na mwanamke hasa kwenye ushirikiano wake na mwanaume kijamii. Wengi wanaweza wakaniona kama mtu fulani niliyechanganyikiwa kwa kuongea hivi lakini hapa kunaa tatizo na linahitaji kuangaliwa.

Mfumo wa haki sawa(gender equality) hapo awali ulikuwa na dhamira nzuri sana tofauti na ilivyo leo hii, ililenga kumpa mwanamke uhuru sawa na mwanaume na access ya mambo ya msingi kama elimu. Lakini haukulenga kumbadilishia mwanamke majukumu au kumpora nafasi yake ya asili.

Leo hiii mfumo huo jinsi unavyokuwa practiced ni kama umekuja kumfanya mwanamke kuwa mshindani wa mwanaume, na matokeo yake umetuvurugia familia na jamii nzima kwa ujumla.

Na kwa bahati mbaya sana hawa wenzetu wao hawalioni hili kama lina athari na badala yake wanaona ndio matokeo ya ukombozi wenyewe.

Waanzilishi wa huu mfumo wana ajenda zao za siri ambazo zinahitaji jamii iliyopalanganyika hili ziweze kupenyezwa kwa urahisi. Na mfumo huu ni nyenzo sahihi ya kutimiza ajenda hizo.

Ukiangalia jamii yetu ya sasa hivi sio sawa na zamani kimaadili na hata kuroho. Na kupitia mabadiliko haya kuna watu wananufaika bila ya tulio wengi kujua.

Siku hizi kuna mambo mengi sana ya ajabu ajabu yanaonekana ya kawaida tangu tuingie kwenye huu mfumo unaosemwa kwamba umeleta uhuru.

Acha tuendelee kuwakumbusha na wale ambao bado hawajajua nini kimaendelea kupitia forums kama hizi.
 
Mkuu Lizarazu, dunia ya leo imajaa watu wanaofanana na wanawake, lakini si wake wa ndoa. Wengi wamejipa daraja ya vyombo vya starehe, hawajitambui wala hawayatambui na kuyakubali majukumu yao ya msingi.

Niseme wazi tu, mwanamke yeyote aliyelelewa kwenye misingi ya "ukombozi wa mtoto wa kike" amepoteza sifa ya kuwa mke wa ndoa. Huyu amelelewa kuwaindependent, hivyo hafai kumweka chini ya mamlaka, labda asubiri upepo wa kisulisuli ambako ataolewa bila sifa za mke.

Bahati mbaya kwao, wanawake wana wakati mgumu sana kuchagua destiny. Kadri anavyozidi kusoma sana ndivyo nafasi yake ya kuolewa inavyozidi kupungua. Na huu ni ujweli mchungu.

Kadri mwanamke anavyopata madaraka ya juu ndivyo nafasi yake kuolewa inavyopungua, anazidi kuwa lonely. Huu pia ni ukweli mchungu.

Kadri mwanamke anavyozidi kujikita kwenye biashara ndivyo nafasi yake kuolewa inavyozidi kupotea. Ni ngumu kwa mwanamke wa namna hii kumpata mume afaaye.

Mambo haya anayoyakimbilia mwanamke wa leo yamepishana na ndoa, ndio maana mabinti wengi wamebaki kusubiri upepo wa kisulisuli.
Wao wanaita ukombozi yaani Ukiskiliza fikra zao utafikiri labda wanaume ni wanyama fulani hivi wasiokuwa na uhuruma hata kidogo na muda wote wao ni kunyanyasa tu wanawake.

Yaani elimu inamfanya aone kwamba Mwanaume alikuwa ni adui yake na muda wote alikuwa amemuweka kwenye cage.

Wakati hao hao wanaume ndio wamekuwa waki sacrifice maisha yao kwa ajili ya wanawake tangu kuumbwa kwa huu ulimwengu.

Mwanamke mwenye fikra zilizopinduliwa na elimu yake hafai kuwa mke.
 
Gombeni sana na kulalama sana ila mkumbuke mfumo usio wa haki unaoitwa mfumo dume ndiyo uliomfanya mwanamke kutafuta jinsi ya kujikomboa. Mfumo mpya mnaoulilia kuwa ni mbaya siyo mpya bali ni ule ule sema sasa una jinsi zote mbili na mkuki kwa nguruwe unakuwa mchungu. Huyu Mungu tunayemtaja hapa kuwa alimweka mwanaume kuwa mtawala na mwanamke mtawaliwa (if at all maana nakumbuka aliwatuma kutawala/kutiisha nchi) hakusema kumtawala mwanamke ni kumnyanyasa na kumdharau. Angetaka iwe hivyo angeumba mwanamke ambaye hana akili wala vipawa na angeweza kabisa kulea watoto wake kama wafanyavyo hayawani. Lakini kitendo cha kuwapa wote ufahamu na jukumu la kutiisha nchi alitaka hawa watu washirikiane kwa upendo kila mmoja katika nafasi yake na waheshimiane.

Kilichotokea ni mtawala kuwa mbinafsi na kutawala kidikteta - kusahau kuwa mwenzie ni binadamu kamili mwenye utashi na matamanio ya asili ya upendo na uhuru. Vipigo ni vya mwanamke, uduni ni wa mwanamke, kazi duni ni za mwanamke, matusi ya kudhalilisha ni ya kike. Yaani chochote cha mwanamke ni duni. Mwanaume akikosea anaambiwa anafanya mambo ya kike na akiambiwa hivi anaumia; mwanamke akifanya yampasayo mwanadamu kufanya anaambiwa anaigiza uanaume! Mwanaume ni mtu, mwanamke ni kiumbe. Kiumbe dhaifu. Mwanamke si kiumbe cha kufananishwa nacho. Ni fahari kufananishwa na simba au jogoo lakini si mwanamke.

Sasa mambo yamebadilika. Maendeleo ya Sayansi na uchumi yanasukuma mabadiliko katika mahusiano ya kijamii. Mfumo wa sasa hauruhusu mahusiano ya mtawala asiyejitambua na mtawaliwa asiyejitambua. Kujitambua ndo habari yenyewe - mtu mmoja mmoja mpaka taifa. Ukila na kipofu vizuri utakula muda mrefu na yeye ataridhika. Ukimdhulumu utampa fursa ya kujihoji na kuhoji kisha nafasi yako itatikiswa maana hukutumia maarifa bali kiburi cha kumiliki nyenzo za kutawalia (mali na elimu). Sasa huyu mnyonge baada ya kujitambua kuwa hastahili kutendewa vibaya anaanza harakati za kujikomboa. Naye anaanza kutaka kukaa alipo mtawala ili naye apate ahueni. Na ahueni anaipata kweli wala tusidanganyane kuwa mwanamke mwenye uhuru wa kimaarifa na kiuchumi ana tabu kama mwanamke ambaye hana hivi vitu na anajitambua lakini hana jinsi. Asiyejitambua hana shida. Jambo usilolijua halikusumbui. Ndiyo wife material naskia.

Sasa mwanamke akishapata nyenzo za uhuru hawezi kuenenda tofauti na mfumo kandamizi uliopo. Naye atakuwa mkandamizaji. Kwa hiyo mfumo dume na mfumo jike yote ni mifumo kandamizi. Watanyanyasika wanawake na wanaume wote ambao hawana nyenzo za uhuru. Kimsingi wanaume ni waathirika wakubwa zaidi kwani si rahisi kukaa kwenye nafasi ya "mtu duni" kwani anaathirika mara mbili: hana vyenzo za uhuru wala urahisi wa kupata mwenzi kwani nyenzo hizo ni vigezo vikuu. Mwanamke mwenye nyenzo za uhuru akikosa mwenzi anakuwa amekosa kitu moja, si vyote, na kama amevuka kiwango cha kushikiliwa kimaadili na jamii anaweza kutumia nyenzo zake kuwachezea wanaume walio kwenye nafasi duni. Uhuru si sawa na upweke. Sasa mwanaume ukose nyenzo za uhuru - upweke utakuhusu, manyanyaso yatakuhusu maana anayekuweka mjini ndiye anakuendeshea maisha. KILA MWANAMKE NA KILA MWANAUME ATAFUTE SANA KUJITEGEMEA KIAKILI NA KIUCHUMI.

Mwisho, mfumo sahihi wa kijamii ni mfumo wa haki (just). Tunaposema haki sawa kwa wote tunamaanisha binadamu wote ni sawa bila kujali ulemavu au jinsi ya mtu. Mfumo unaoheshimu utu wa mtu kwanza kabla ya kuja kwenye uanamke, ulemavu, utoto au uzee ndiyo mfumo bora. Mwanamke angechukuliwa kama mtu kwanza halafu mwanamke baadae tusingefika hapa. Pia tusichanganye mabadiliko ya kiuchumi na mabadiliko ya nafasi ya mwanamke. Mwanamke miaka mingi huko nyuma na mpaka sasa ni mzalishaji mkuu. Wa wakati ule alikuwa akizalisha karibu na nyumbani na anakwenda shamba na mtoto anamchimbia shimo anamuweka au anamuweka mgongoni. Lakini sasa shughuli za kiuchumi zimepanuka na makazi yamekuwapo ya vijiji na miji. Si jambo geni kwa mwanamke kuacha mtoto nyumbani na kwenda kutafuta. Mimi nina miongo minne sasa na niliachwa sana kwa mama mkubwa mpaka mama atakaporudi toka shambani au sokoni na alipokwenda kujiendeleza kielimu niliachwa kwa babu na bibi. Mama yangu mwenyewe mwenye miongo 7 alianza shule akiwa na miaka 10 kwa kuwa alikuwa akimlea mdogo wake wakati mama yake akizalisha mali. Tusichanganye mada. Kazi ndiyo utu. Tujipange upya zama zimebadilika.
Kwa kweli nimejitaidi kupitia article yako vizuri, lakini nasikitika kusema sijaona uliposimama na hoja. Naona kama umekuja tu, kuendeleza mvutano usio na tija.

Anyway, tunakushukuru kwa mchango wako. Ni imani yetu, ipo siku isiyo na jina....mtaelewa vizuri athari za hiki, kinachoongelewa hapa.
 
Well said....thanks.
Kuhusu uhusiano wa mwanamke na mwanaume katika ndoa; mwanaume anajukumu la KUMPENDA mke wake, naye mke analojukumu la KUMTII mume wake (Wakolosai 3:18-25, Waefeso 5:22-23).

Lakini pia, mwanamke ni msaidizi wa mwanaume (Mwanzo 2:18). Kumbe huo ndio mpango wa Mungu tangu mwanzo alipowaumba mwanaume na mwanamke.

Ndio maana hata Historia inatufundisha kuwa; tangu mwanzo wa jamii zetu zilizokuwa primitive, bado kulikuwa na mgawanyo wa majukumu.

Kazi ya mwanaume ilikuwa ni kutafuta kipato kwa kuchimba mizizi, kuvuna matunda, na baadae kuwinda na kulima huku mwanamke alikaa na watoto nyumbani kuwalea na kutunza familia.

Mungu hajaweka usawa kati ya mwanaume na mwanamke. Ndio maana mwanaume analinganishwa na kichwa na mwanamke analinganishwa na mwili. Utofauti huu unatufanya tuhitajiane.

Kichwa hakiwezi kufanya kitu bila mwili, wala mwili bila kichwa. Utofauti huu ndio unatufanya tukamilishane. Wala usichukuliwe kama utumwa.
 
Mkuu Nyenyere kuna mada Fulani ulipost hapo nyuma na kwa kweli nilitofautiana sana na mtizamo wako(na mpaka sasa natofautiana na wewe)

Lakini kwa mada hii ya leo nakuunga mkono asilimia mia moja na naomba niongezee hoja kadhaa hapa chini kuunga mkono mada yako

Mkuu kwa sababu ya mapinduzi yalifofanyika na yanayoendelea kufanyika kila siku,leo hii tunapata familia na vizazi vibovu kuwahi kutokea,kwa nini?

leo hii baba na mama wote ni wafanyakazi kuondoka aubuhi kurudi usiku,watoto wameshakula wamelala,anayeshinda na watoto ni dada wa kazi ambaye haijulikani anashindaje na kuwatendeaje watoto,mama anapoondoka anaacha tu maagizo dada utampa mtoto uji,utamwekea katuni,utahakikisha anafanya homework,mtoto ni wa dada wa kazi?dada wa kazi anajua thamani ya yule mtoto?akiharibika dada ana hasara yeyote?na akiwa mtu mzuri kioo cha jamii,ni kwa namna gani dada wa kazi anafaidika hivi kwamba atajitahidi kwa kadri awezavyo kumlea mtoto ipasavyo?

kwa mfano huo mdogo tu wale ambao wamewahi kuona madhara ya aina hi ya Maisha wataelewa nachokisema ila kwa wale ambao wanaamini njii hii ya Maisha ni sawa si ajabu huko mbeleni watu watakuja kuconfess humu (painful ad regret Confession)

Kiasili na kulingana na uumbaji mwanaume aliumbwa kutafuta kwa maana ya kwamba mke alipaswa akae nyumbani atunze watoto muda wote baba anapokuwa katika mihangaiko ya kutafutia riziki mke na watoto wake,ni aina hii yamaisha iliyofanya familia kadhaa za miaka kadhaa kuwa bora na kutokeza vijana wa kiume na mabinti wa kike wenye kutegemeka na kujiheshimu,mama walikuwa wakitumia muda wao mwingi kutunza watoto wao na kuwafundisha lilo sawa na lilo na kosa pia,haikuwa rahisi kwa binti au kijana kuharibika na mama shindwe kuona mbadiliko hayo na kutoa ripoti kwa baba ambaye angeshughulikia hali hiyo kabla mambo hayajaharibika kabisa

lakini leo poor us kuna uwezekano mtoto kashaharibika sana tu (labda kawa mvuta bangi,katoa mimba za kutosha,kawa shoga,kawa mlevi) na bado mama au baba hajui kuhusu yote hayo,watajua saa ngapi wakati wote wako kazini bize kutafuta pesa?nani atampa mwenzie ripoti kuhusiana na maendeleo ya mtoto? dada wa kazi? dada wa kazi wanawajua vizuri watoto wenu? inauma lakini kutokana na aina yetu ya Maisha ya siku hizi,inakuja kujulikana kuwa mtoto kafikia stage ya point of no return na hakuna kinachoweza kufanyika kumsaidia tena just kwa sababu mama na baba wote walikuwa bize kuzitafuta pesa,what for? Maisha bora,,,,Maisha bora yapi?kupoteza watoto wenu mkiwa mmebaki na pesa zenu nyingi??
 
Kuhusu uhusiano wa mwanamke na mwanaume katika ndoa; mwanaume anajukumu la KUMPENDA mke wake, naye mke analojukumu la KUMTII mume wake (Wakolosai 3:18-25, Waefeso 5:22-23).

Lakini pia, mwanamke ni msaidizi wa mwanaume (Mwanzo 2:18). Kumbe huo ndio mpango wa Mungu tangu mwanzo alipowaumba mwanaume na mwanamke.

Ndio maana hata Historia inatufundisha kuwa; tangu mwanzo wa jamii zetu zilizokuwa primitive, bado kulikuwa na mgawanyo wa majukumu.

Kazi ya mwanaume ilikuwa ni kutafuta kipato kwa kuchimba mizizi, kuvuna matunda, na baadae kuwinda na kulima huku mwanamke alikaa na watoto nyumbani kuwalea na kutunza familia.

Mungu hajaweka usawa kati ya mwanaume na mwanamke. Ndio maana mwanaume analinganishwa na kichwa na mwanamke analinganishwa na mwili. Utofauti huu unatufanya tuhitajiane.

Kichwa hakiwezi kufanya kitu bila mwili, wala mwili bila kichwa. Utofauti huu ndio unatufanya tukamilishane. Wala usichukuliwe kama utumwa.
Good note mkuu Dutu J

kulingana na maandiko uliyoyataja hapo huo ni mgawanyiko ulio fair kabisa,na amini nakwambia yeyote anayeyaishi maandiko hayo,maisha yake ni mfano kwa wengine na kwao furaha ni kitu cha kawaida kabisa

be blessed mkuu
 
Hawa viumbe wenyewe, wanavielewa hata hivyo vifungu basi?!!

Wengi wamebakia kuudhuria misa tu....na wengine wamefika mbali zaidi, hata kuona ya kwamba haya maandiko ya kidini, yapo outdated! Hivyo wao wanafata yale wayaonayo.....!!

Na naweza kusema shida inaanzia, kwenywe hizi nyumba zetu za ibada. Maana binafsi naamini, if kama hili suala lingepewa nguvu ya uratibu na nyumba hizo, am sure kwa kiwango kikubwa sana....jambo hili lingepungua au kupotea kabisa, kwenye uso wa dunia.

Na wala sitaki kuamini kwamba, hawa watumishi.....hawaelewi nini kinaendelea katika jamii zinazowazunguka.
Bali mie naona ni matokeo tu, ya mbegu ya ukengemfu ya ibilisi....!!

Honestly inaumiza sana....!!
Kweli kabisa mkuu, tatizo ninaloliona kwenye nyumba za ibada ni mapato makubwa yanayotoka kwa wanawake. Kwa sababu ya uwezo wao mdogo kufanya reasoning, wamekuwa target ya watumishi wengi. Hii ni mbaya sana lakini ukweli inabido usemwe tu.
Hawa watumishi wenyewe ni perpetrators wa huu mfumo haribifu na una maslahi sana kwao sio wa kuwaamini kabisa.

Yaani hawa sijui wanasaiokolojia,wachungaji, wahamasishaji, wasululishi wa migogoro ya ndoa ni washirika wazuri sana wanao prolog huu unaoitwa ukombozi wa mwanamke.

Na tusigemee kabisa kama watasaidia hata kupunguza athari zitokanazo na huu mfumo maana unafaida kwao.

Uwepo wa matatizo yetu ya kijamii hususani ya mahusiano ndio uhai wa maslahi yao, siku matatizo hayo yakiisha hata maslahi yao pia yatakuwa hatarini.

Kama umewahi kuwafuatilia hawa akina Chris mauki,Eddy makenge na wengineo mara nyingi huwa wanaongea vitu ambavyo wanawake wanapenda kuviskia. Mara nyingi wanaongelea sana makosa ya wanaume na kufunika funika makosa ya wanawake na hata ushauri wanaoutoa ni ushauri unaoharibu zaidi kuliko kujenga sema wanajitahidi kucheza na saikolojia ya wanawake.

Na wanafanya vile makusudi kabisa ila wanachoangalia wao ni account zao kuongezeka unene.
 
ujinga huu, kama tukianza kufuata ujinga wa kizamani hata utumwa ulihalalishwa. Kma hutaki mwanamke afanye kazi wafanyie hivyo wanao wa kike, ni dunia huru hii, fursa sawa kwa kila mtu
Huko Ulaya kuna conservatives wanaoitwa far right ambao wana mawazo kama yako, wanashangaa pia kwa nini watu weusi wanapewa nafasi kubwa hadi wengine kuwa Rais kwenye nchi za wazungu, lakini hawashindi watabaki kuumia tu kama wewe unavyoumia
 
Hili bandiko limejaa mambo mazito na umeandika kwa hisia sana mpaka mimi mwenyewe limenipa msisimko. Pole sana kiongozi kwa yale unayopitia ila ninaamini kwa upeo na uwezo ulio nao utayashinda.

Hawa binadamu wenzetu walinyimwa MUONO na hii ni tatizo kubwa kwao. Uwezo wa kung'amua jambo kiundani na kubaini kama lina hasara na hasa kama hasara hizo ni za muda mrefu hawana kabisa.

Wameletewa elimu(kitu ambacho ni kizuri) lakini elimu hiyo imekuwa twisted kwa namna fulani kiasi kwamba inawajenga wakati huo huo inawabomoa bila ya wao kujua.

Angalia leo hii mwanamke anasoma hili aje ashindane na mwanaume na sio kuja kushirikiana na mwanaume kwenye ujenzi wa jamii iliyobora. Na hili tunaweza kuliona hata hapa kwenye huu uzi, wao wanaona elimu ni nyenzo ya kupambana na mwanaume.. Inasikitisha kweli.

Sipingani na mwanamke kuelimika ila napingana na namna ambavyo elimu inatumiwa na mwanamke hasa kwenye ushirikiano wake na mwanaume kijamii. Wengi wanaweza wakaniona kama mtu fulani niliyechanganyikiwa kwa kuongea hivi lakini hapa kunaa tatizo na linahitaji kuangaliwa.

Mfumo wa haki sawa(gender equality) hapo awali ulikuwa na dhamira nzuri sana tofauti na ilivyo leo hii, ililenga kumpa mwanamke uhuru sawa na mwanaume na access ya mambo ya msingi kama elimu. Lakini haukulenga kumbadilishia mwanamke majukumu au kumpora nafasi yake ya asili.

Leo hiii mfumo huo jinsi unavyokuwa practiced ni kama umekuja kumfanya mwanamke kuwa mshindani wa mwanaume, na matokeo yake umetuvurugia familia na jamii nzima kwa ujumla.

Na kwa bahati mbaya sana hawa wenzetu wao hawalioni hili kama lina athari na badala yake wanaona ndio matokeo ya ukombozi wenyewe.

Waanzilishi wa huu mfumo wana ajenda zao za siri ambazo zinahitaji jamii iliyopalanganyika hili ziweze kupenyezwa kwa urahisi. Na mfumo huu ni nyenzo sahihi ya kutimiza ajenda hizo.

Ukiangalia jamii yetu ya sasa hivi sio sawa na zamani kimaadili na hata kuroho. Na kupitia mabadiliko haya kuna watu wananufaika bila ya tulio wengi kujua.

Siku hizi kuna mambo mengi sana ya ajabu ajabu yanaonekana ya kawaida tangu tuingie kwenye huu mfumo unaosemwa kwamba umeleta uhuru.

Acha tuendelee kuwakumbusha na wale ambao bado hawajajua nini kimaendelea kupitia forums kama hizi.
Asante mkuu,

Hakika umejazia mambo ya muhimu sana, hongera kwako chief.

Kikubwa tuendelee tu kukumbushana ya kwamba, waathirika wa hii kitu sio tu wanawake. Bali pia tufahamu kwamba, lipo kundi kubwa la wanaume wenzetu, walio-affected kwenye hili suala...!!

Hivyo tunavyojivalisha mabomu ya kuliteketeza suala hili, katika jamii zetu. Tunatakiwa tufahamu kabisa, tunaenda kupambana na makundi yote mawili ya waathirika (mwanaume & mwanamke).

Kwa msingi huo ni wazi tunaona kwamba, ili kufanikisha kuijenga jamii mpya, ni lazima tujidhatiti kwa hali na mali......a part from that, ni lazima TUTASHINDWA!
 
ujinga huu, kama tukianza kufuata ujinga wa kizamani hata utumwa ulihalalishwa. Kma hutaki mwanamke afanye kazi wafanyie hivyo wanao wa kike, ni dunia huru hii, fursa sawa kwa kila mtu
Huko Ulaya kuna conservatives wanaoitwa far right ambao wana mawazo kama yako, wanashangaa pia kwa nini watu weusi wanapewa nafasi kubwa hadi wengine kuwa Rais kwenye nchi za wazungu, lakini hawashindi watabaki kuumia tu kama wewe unavyoumia
Ujinga uko wapi hapo?

Nani kasema hapa kwamba mwanamke asifanye kazi?

Umeelewa content ya mada lakini au umekurupuka tu kutoka huko ulipokuwa na kuja ku blab hogwash hapa?

Huko ulaya na Marekani conservatives bado wana family stability kuliko hata hao wapumbavu wa liberals ambao wanaonekana kukuharibu akili. Tafakari kuhusu hili
 
Upo sahihi kabisa, kiongozi.

Ni kweli huu uharibifu wa jamii zetu unaofanyika, una faida kubwa sana kwa baadhi ya watu! Na hii inajidhihirisha wazi, kutokana na mambo yanayofanywa/kuongelewa na watu hao, ambao wengi wao wapo kwenye makundi haya ya wachungaji, makungwi, wanasaikolojia, waongeaji n.k

Simply, still tuna safari ndefu....!!
Hawa watumishi wenyewe ni perpetrators wa huu mfumo haribifu na una maslahi sana kwao sio wa kuwaamini kabisa.

Yaani hawa sijui wanasaiokolojia,wachungaji, wahamasishaji, wasululishi wa migogoro ya ndoa ni washirika wazuri sana wanao prolog huu unaoitwa ukombozi wa mwanamke.

Na tusigemee kabisa kama watasaidia hata kupunguza athari zitokanazo na huu mfumo maana unafaida kwao.

Uwepo wa matatizo yetu ya kijamii hususani ya mahusiano ndio uhai wa maslahi yao, siku matatizo hayo yakiisha hata maslahi yao pia yatakuwa hatarini.

Kama umewahi kuwafuatilia hawa akina Chris mauki,Eddy makenge na wengineo mara nyingi huwa wanaongea vitu ambavyo wanawake wanapenda kuviskia. Mara nyingi wanaongelea sana makosa ya wanaume na kufunika funika makosa ya wanawake na hata ushauri wanaoutoa ni ushauri unaoharibu zaidi kuliko kujenga sema wanajitahidi kucheza na saikolojia ya wanawake.

Na wanafanya vile makusudi kabisa ila wanachoangalia wao ni account zao kuongezeka unene.
 
Ujinga uko wapi hapo?

Nani kasema hapa kwamba mwanamke asifanye kazi?

Umeelewa content ya mada lakini au umekurupuka tu kutoka huko ulipokuwa na kuja ku blab hogwash hapa?

Huko ulaya na Marekani conservatives bado wana family stability kuliko hata hao wapumbavu wa liberals ambao wanaonekana kukuharibu akili. Tafakari kuhusu hili
Ujinga huo aliouandika
Nadhani wewe ndio hujamuelewa mleta mada, pengine kamsome tena
Dunia imebadilika, kila mtu ana haki ya kupata fursa ya elimu na kufanya kazi yoyote kama anaweza kuifanya
Kama hupendi pole, ndio mambo yalivyo na yataendelea kuwa hivyo, haturudi karne ya 19 tena
 
ujinga huu, kama tukianza kufuata ujinga wa kizamani hata utumwa ulihalalishwa. Kma hutaki mwanamke afanye kazi wafanyie hivyo wanao wa kike, ni dunia huru hii, fursa sawa kwa kila mtu
Huko Ulaya kuna conservatives wanaoitwa far right ambao wana mawazo kama yako, wanashangaa pia kwa nini watu weusi wanapewa nafasi kubwa hadi wengine kuwa Rais kwenye nchi za wazungu, lakini hawashindi watabaki kuumia tu kama wewe unavyoumia
Nimepitia article yako vizuri, lakini nasikitika kupata ukakasi juu ya msingi mzima wa ufahamu...

Nadhani ni vyema, ukapitia tena uzi huu kiutaratibu na kwa umakini.....ili uweze kung'amua msingi mkuu wa kinachoongelewa hapa.

Asante.
 
article yangu ipi? sijaandik article mimi, nime comment. Msingi wa kinachoongelewa nimekielewa, anasema mwanamke arudi kwenye majukumu yake ya ki traditional kama kupika na kulea watoto, na mwanaume ndio awe mtafuta kipato
 
Hapawezi kuwa na usawa kati ya mwanaume na mwanamke maisha yakaenda....
Wamama na wadada tunaweza kuwa na haki sawa ya kupata huduma za kijamii kama elimu, ajira, biashara, burudani etc lakini hatuwezi kuwa sawasawa na wanaume wala wanaume hawaezi kuwa sawa na wanawake kwani kila mmoja ana majukumu ambayo aliumbiwa

Kwenye imani zetu tumejifunza toka awali kabisa kwenye uumbaji mwanaume ni nani na mwanamke ni nani pamoja na majukumu yao. Pia desturi zetu hazikua mbali na imani zetu kuhusu hili.

Mambo yale ya Beijing tuyaache Beijing, sisi tuishi kwa asili yetu binadamu ilivyo na pia miongozo ya imani zetu

Maoni yangu binafsi
 
Safi, umenena vizuri sana!

Endapo kila kitongoji katika jamii zetu, kikawa na wanawake kama wewe kumi tu. Aiseeh bila ubishi tutapiga hatua kubwa sana za kimaendeleo, kuanzia kwenye msingi wa familia mpaka nchi kwa ujumla.

Asante sana Dada, ubarikiwe!
Hapawezi kuwa na usawa kati ya mwanaume na mwanamke maisha yakaenda....
Wamama na wadada tunaweza kuwa na haki sawa ya kupata huduma za kijamii kama elimu, ajira, biashara, burudani etc lakini hatuwezi kuwa sawasawa na wanaume wala wanaume hawaezi kuwa sawa na wanawake kwani kila mmoja ana majukumu ambayo aliumbiwa

Kwenye imani zetu tumejifunza toka awali kabisa kwenye uumbaji mwanaume ni nani na mwanamke ni nani pamoja na majukumu yao. Pia desturi zetu hazikua mbali na imani zetu kuhusu hili.

Mambo yale ya Beijing tuyaache Beijing, sisi tuishi kwa asili yetu binadamu ilivyo na pia miongozo ya imani zetu

Maoni yangu binafsi
 
ujinga huu, kama tukianza kufuata ujinga wa kizamani hata utumwa ulihalalishwa. Kma hutaki mwanamke afanye kazi wafanyie hivyo wanao wa kike, ni dunia huru hii, fursa sawa kwa kila mtu
Huko Ulaya kuna conservatives wanaoitwa far right ambao wana mawazo kama yako, wanashangaa pia kwa nini watu weusi wanapewa nafasi kubwa hadi wengine kuwa Rais kwenye nchi za wazungu, lakini hawashindi watabaki kuumia tu kama wewe unavyoumia
Umepoteana huelewi maudhui,by the way sina tabia ya kunuku kila kitokacho ulaya. Mmelishwa matango pori nasasa hamna furaha kama ilivyokuwa zamani. Kama unabisha angalia waliokimbilia upepo wa kisulisuli, ni aibu kwa janga mnalotengeneza wenyewe.

Habari ya ulayawaachie wenyewe, tujadili ya kwetu. Elimu haikupaswa kumwondoa mwanamke kwenye majukumu yake ya msingi, lakini kilichopo sasa ni nini? Naamini wazazi wako walikulea vema ingawa wewe hutaki kuwatendea hivyo wanao, ubataka walelewe na dunia. Ni upuuzi usiomithilika.

Kama unadhani mimi nanung'unika basi umepotea, mimi najaribu kushauri kuhusu maadili na sababu ya wanawake kujikuta wakiwa na wanyonge pale ujana wapo unapoondoka. Wanawake ni short sighted hata kama utabisha, wanasombwa hovyo na kila upepo unaokuja na ndio maana ni target kubwa ya kila jambo jipya, iwe fashion, urembo, mavazi, imani mpya n.k. Akili zao zinavutwa kila kinachoonekana ni kitamu machoni hata kama mwisho wake ni mchungu, hawana uwezowa kuchuja mambo. Ndivyo walivyoumbwa.

Starehe na kujidanganya hudumu kwa muda mfupi sana kwa mwanamke wa kizazi kipya, asiyeheshimu kuumbwakwake kama mwanamke, ambaye anadhani ushindani na walioumbwa wanaume ni jambo la kutukuzwa, lakini mwanamke anayeijua nafasi yakeana chance kubwa ya kuwana furaha idumuyo maisha yake yote. Mwanamke hakuumbwakushindana na mwanamume bali kumsaidia kufikia malengo ya maishawakiwa kama familia moja. Sasa wanawake waliojanjaruka kama wewe na kujiona ni wenye kupambana na wanaume hupigana na vivuli vyao wenyewe kwani watacheka mwanzoni, tena kwa muda mfupi sana, lakini mwisho wao huwa ni kilio na majuto makuu.

Elimu ilikusudiwa kumtoa mtu kwenye ujinga na kumpeleka kwenye hekima na busara, lakini badala yake imefanya kinyume chake. Wacha mtumike kwa starehe na kuwaburudisha walioharibika akili pia, lakini usisahau kuwawakati ukuta.

Amina.
 
Inapendeza kama hata wewe unafahamu fika kwamba huu mfumo tunaoambiwa kwamba umeletwa kwa ajili ya kuwasaidieni nyie wanawake kwa namna jinsi unavyo kuwa practiced unaleta athari nyingi kuliko faida kwa walengwa.

Athari zake zinaweza zisionekane kwa urahisi sasa hivi lakini tukaziona hapa baadae au hata kwenye matukio mbali mbali mfano kama kwenye ajali kama ulivyo ona kwenye comment yangu iliyopita.

Sasa nije kwenye hiyo kauli ya baba yako aliyokwambia juzi.

Juzi juzi baba yangu amenitamkia kuwa alinisomesha nisiwe mtumwa. Naamini wengi wanaonekana hivi wakiwa nyumbani wanalea. Hebu niambie ni nani anayependa utumwa.

Kwa kuangalia tu hii kauli baba yako Nathubutu kusema yeye ni aina ya wazazi ambao wameshiriki kikamilifu kuharibu kizazi cha wanawake wa sasa.

Baba yako anaamini mwanamke asiyesoma ni lazima atakuwa ni tegemezi tu kwa mwanaume na huo utegemezi yeye anauona ni utumwa, sasa hili asiingie kwenye huo utumwa basi lazima asome sana...INASIKITISHA SANA KWA KWELI.

Naamini kabisa tangu udogoni kwako amekuwa akikujengea hii mindset kwamba kusoma=kuepuka manyanyaso ya mwanaume na mpaka sasa hivi umekuwa nayo na hujawahi kuona tatizo kwenye hilo.

Mbali na huu mfumo tulionao wazazi pia wamechangia sana kuwaharibu wanawake hasa nyie wasomi kwa namna jinsi walivyowalea.

Mzazi anampa binti yake elimu hili aje aitumie kama mbadala wa kuishi bila mwanaume. Yaani elimu inakuwa ni replacement ya mwanaume maishani mwake.. Very pathetic mindset.

Umewahi kujiuliza ni kwanini wanawake wengi wasomi ndoa zinawashinda? Sababu moja wapo kubwa ni kuwa na hii mindset waliojazwa na wazazi wa aina ya baba yako.

Wanawake wengi wasomi wawapo ndoani wakikutana na changamoto hawaitumii elimu yao kama nyenzo ya kutatua changamoto hizo na badala yake elimu hiyo wanaifanya plan B(mbadala wa mume baada ya kuachika) pale mambo yasivyoenda jinsi wanavyotaka wao.

wanawake hao wasomi ni rahisi sana kusema maneno kama "tuachane" "usinibabaishe" "ninaweza kuishi bila wewe" hata pale changamoto ndogo tu inapojitokeza. Yote hii ni kwa sababu tu wanaweza kujitegemea kupitia elimu zao na wameshaukimbia ule utegemezi(utumwa) na hii tafsiri ya neno utumwa kwao inaenda mpaka kwenye utii.

Elimu zao zinawaondolea ile haiba na nafasi ya mwanamke kwa mwanaume na kujikuta anakuwa mshindani badala ya msaidizi ndio maana ni ngumu sana kwao kuwa na ndoa thabiti, sululisho pekee la kukabiliana na changamoto za ndoa huwa wanaona ni kuvunja ndoa.

Nadhani umewahi kuona comments zangu humu nikisistiza kuwa mwanamke msomi hafai kuwa mke. Ninasema vile kwa kumaanisha wala sio maigizo.

Na ni kweli hamfai kuwa wake.

Angalia mfano kama wewe hapo tayari sasa hivi unaona eti mwanamke anayefanya kazi ya kulea tu watoto nyumbani huyo ni mtumwa!!! How?

Kwa maana nyingine unaniambia kwamba mwanamke anayechakalika sawa na mwanaume huyo ndio kajikomboa toka utumwani kitu ambacho si sahihi kabisa.

MWENYEZI MUNGU hakuwa mjinga kumfanya mwanamke kuwa tegemezi wa mwanaume na kumuepusha na shuruba zote za kazi kama ambavyo wazazi wa siku wanavyowaaminisha nyie mabinti.

Haya sasa hivi mmetoka kwenye huo utumwa mmeingia kwenye kushindana na wanaume Nadhani athari zake wewe mwenyewe unaziona.

Kushindana kwenu na wanaume kumepelekea wengi wenu kuishi bila wenza na mnajikuta mna majukumu mengi sana ya kuyakabili kuliko hata wale mnaowaona wako utumwani(tegemezi).

Na majukumu hayo mazito mliyojipachika yanawaleteeni athari za kiakili kwanzia nyie mpaka kwenye familia zenu.

Kuna observation moja ilifanyika nchini UK watoto waliolelewa na single parents na wale waliolelewa na wazazi wote wawili walikuwa wanaulizwa kama wanatamani kuishi maisha wanayoishi wazazi wao pale watakapokuwa watu wazima.

Karibia watoto wote wanaolelewa na single parents walisema hawatamani kabisa kuishi maisha ya wazazi wao, kwa sababu wazazi wao(single parents) wana struggle sana namna ya kubalance familia na careers zao, na hivyo watoto hao kujikuta muda mwingi wanauokosa ule ukaribu wa mzazi.

Na hii ni ukweli mtupu single mothers wengi(ambao hawako tena utumwani) hawana muda wa kukaa na familia sababu ya kukimbizana na majukumu.

Haya yote yameletwa na huu mfumo unaoshabikiwa na wengi ambao umefanya wengi kuwa na mentality kama hii aliyonayo baba yako ya kuamini utegemezi ni utumwa.
Sasa unashauri wa kike wakizaliwa wasipelekwe shule wasubiri ndoa ama?.

What is your solution?.
Tatizo tumeliona
 
Back
Top Bottom