Jamii imempora mwanamke nafasi yake

Jamii imempora mwanamke nafasi yake

ivi kweli mimi nitake kuwa sawa na mwanaume nianze kufanya kazi ngumu kama za ukuli labda bandarini, nianze kubeba gunia la mahindi begani wakati nimepewa mbavu 01 tuu kati ya mbavu 12
Wacha niendelee na majukumu yangu ya kuzaa kwa uchungu, kupamba nyumba na kupika
Madam huu usawa wengi wanaufurahia sana lakini niamini mimi athari zake zitawakumba zaidi wanawake kuliko wanaume.

Wewe si unajifanya uko sawa mwanaume!!? Basi na mimi nakuchukulia kama mwanaume mwenzangu katika situation yoyote ile. Hebu soma hiki kipande cha habari, Kwenye hii ajali waliokufa wote ni wanawake na watoto.

PASSENGERS of the Costa Concordia, the cruise ship that sunk off an Italian island on Friday [13th January 2012], told The Daily Mail that in the chaos after the ship was wrecked, men rushed for the lifeboats and gave no priority to women and children.

As she [one of the survivors ] waited for a flight home from Rome, grandmother Sandra Rogers, 62, told the Daily Mail: ‘There was no “WOMEN and CHILDREN FIRST” policy. There were big men, crew members, pushing their way past us to get into the lifeboats. It was DISGUSTING.’

Na huku ndio tulipofikia.. Naamini kabisa hata ile ajali ya TITANIC ingetokea leo hii wangekufa wanawake tupu.
 
Nataja walio wengi, exception cases zipo ila majority.

Nimepata kuzungumz na wanawake wengi waliohesabika kufanikiwa, wote walonyesha kuumizwa na kutokuwa na ndoà. Mfano mwingine ni Sophia Simba aliwahi kuhojiwa live kwenye TV na alikiri hayo. Wanawake waliojiendeleza na wakawa na ndoa imara wana furaha kuliko waliojiendeleza na kubaki kudanga mitaani. Kuna tofauti kati ya mwanamke mwenye ndoa na asiye na ndoa, hata heshima yao ni tofauti, huo ndio ukweli.

Sina bias, nayatazama maisha katika uhalisia. Mwanamume akiamua kuoa anaoa, mwanamke akiamua kuolewa anasuniri ampate mwanamume, the difference is clear. Wote wakishatumikia anasa wakaamua kuingia kwenye ndoa, mwanamke atategemea bahati wakati mwanamume atachagua amtakaye. Nimekosea wapi hapo?

Kukimbilia upepo w kisulisuli sio kipimo cha godly women. Mwanamke mcha Mungu hawezi kuwemo kwenye kundi lile la wanawake walio desperate. Huyu hufichwa katika Bwana na mwanamume amwonaye ni yule aliye sahihi tu, that is the Bible. Uliowaona hapo ni wale waliokwenda kanisani kutafuta muujiza wa ndoa.
Ndoa ni jambo zuri mnoooo

Na ndoa ingekua rahisi kiasi hicho kwa wanaume basi mabachelor wasingekua wanapata tabu wamuoe nani...ts a struggle eitherways..nadhani anaechagua anapata tabu zaidi cz he has to choose well..and the woman can also say no if she wants..ts not like inakuaga smooth sail tushapita tunajua sio kila mtu alokutamkia ndoa ulimkubalia..u had to choose pia ktk hao...

Na mwanamke asipoolewa na mwanaume mmoja haimaanishi hatoolewa na mwanaume mwingine

Furaha ya mwanamke na ndoa ipo karibu sana mana ndo jukumu la tangu kuumbwa dunia alikua asubirie ndoa tu azae alee afe...mindset na setting kijamii iko hivyo
sikuhizi vyanzo vya furaha ni vingi..vingi sana...ndoa inakuja kama icing on the cake and not the whole cake...si kwa mwanamke tu hata mwanaume...there is life beyond
Maisha yanakua ss muunganiko wa yote hayo
 
Kwa vipi sasa.
Kuchagua aina ya kazi/biashara utakayofanya
Mfano:iwe flexible, masaa machache kazini ama kwny biashara,kuwa na wasaidizi wa kazi nyumbani mgawane kazi nk

Maadam upate kazi/biashara inayokupa nafasi kuattend majukumu ya familia na yako binafsi as a human being/woman
 
Wanaume wote wanabeba mizigo kwani?.

Hamna softer works that u can also do uingize kipato?
Hiyo mizigo sio lazima iwe anafanya ili apate kuongeza kipato ni majukumu waliyopewa na aliyewaumba
Juzi nilikua nahamisha makabati makubwakubwa mbona wanawake4 tulishindwa hadi wakaja wanaume2 na kazi ikaenda fasta
Hapa ndio nasemaga hakuna usawa ila kuna haki sawa
Issue hapa sio vyanzo vya kipato bali ni wanawake kujiona wana vifua sawa na wanaume, yaani kuwa na ile mentality ya "what a man can do, a woman can do better" mpaka wanafikia hatua ya kutamka maneno kama "i don't need a man in my life so long as I'm financially independent". Sasa na sisi muda sio mrefu tutasitisha generous gestures kama hizi na kisha tutaanza kutembelea kwenye haki sawa kweli°
9740920_images20190701t075056_079_jpeg_jpeg2d7954450fdab878c3d33c2d424379cc.jpeg
 
Mkuu Nyenyere kuna mada Fulani ulipost hapo nyuma na kwa kweli nilitofautiana sana na mtizamo wako(na mpaka sasa natofautiana na wewe)

Lakini kwa mada hii ya leo nakuunga mkono asilimia mia moja na naomba niongezee hoja kadhaa hapa chini kuunga mkono mada yako

Mkuu kwa sababu ya mapinduzi yalifofanyika na yanayoendelea kufanyika kila siku,leo hii tunapata familia na vizazi vibovu kuwahi kutokea,kwa nini?

leo hii baba na mama wote ni wafanyakazi kuondoka aubuhi kurudi usiku,watoto wameshakula wamelala,anayeshinda na watoto ni dada wa kazi ambaye haijulikani anashindaje na kuwatendeaje watoto,mama anapoondoka anaacha tu maagizo dada utampa mtoto uji,utamwekea katuni,utahakikisha anafanya homework,mtoto ni wa dada wa kazi?dada wa kazi anajua thamani ya yule mtoto?akiharibika dada ana hasara yeyote?na akiwa mtu mzuri kioo cha jamii,ni kwa namna gani dada wa kazi anafaidika hivi kwamba atajitahidi kwa kadri awezavyo kumlea mtoto ipasavyo?

kwa mfano huo mdogo tu wale ambao wamewahi kuona madhara ya aina hi ya Maisha wataelewa nachokisema ila kwa wale ambao wanaamini njii hii ya Maisha ni sawa si ajabu huko mbeleni watu watakuja kuconfess humu (painful ad regret Confession)

Kiasili na kulingana na uumbaji mwanaume aliumbwa kutafuta kwa maana ya kwamba mke alipaswa akae nyumbani atunze watoto muda wote baba anapokuwa katika mihangaiko ya kutafutia riziki mke na watoto wake,ni aina hii yamaisha iliyofanya familia kadhaa za miaka kadhaa kuwa bora na kutokeza vijana wa kiume na mabinti wa kike wenye kutegemeka na kujiheshimu,mama walikuwa wakitumia muda wao mwingi kutunza watoto wao na kuwafundisha lilo sawa na lilo na kosa pia,haikuwa rahisi kwa binti au kijana kuharibika na mama shindwe kuona mbadiliko hayo na kutoa ripoti kwa baba ambaye angeshughulikia hali hiyo kabla mambo hayajaharibika kabisa

lakini leo poor us kuna uwezekano mtoto kashaharibika sana tu (labda kawa mvuta bangi,katoa mimba za kutosha,kawa shoga,kawa mlevi) na bado mama au baba hajui kuhusu yote hayo,watajua saa ngapi wakati wote wako kazini bize kutafuta pesa?nani atampa mwenzie ripoti kuhusiana na maendeleo ya mtoto? dada wa kazi? dada wa kazi wanawajua vizuri watoto wenu? inauma lakini kutokana na aina yetu ya Maisha ya siku hizi,inakuja kujulikana kuwa mtoto kafikia stage ya point of no return na hakuna kinachoweza kufanyika kumsaidia tena just kwa sababu mama na baba wote walikuwa bize kuzitafuta pesa,what for? Maisha bora,,,,Maisha bora yapi?kupoteza watoto wenu mkiwa mmebaki na pesa zenu nyingi??
Hivi mnamaanisha kuwa watoto waliolelewa na mamazao kwa kukaa nyumbani ndo watoto walio Bora zaidi katika jamiii?.... Ina maana watoto waliolelewa na mama na baba Ni wafanya kazi ndo watoto wahovyo?... Nadhani huu mtizamo Ni umegeneralize na Wala hauna ukweli wowote.
 
Issue hapa sio vyanzo vya kipato bali ni wanawake kujiona wana vifua sawa na wanaume, yaani kuwa na ile mentality ya "what a man can do, a woman can do better" mpaka wanafikia hatua ya kutamka maneno kama "i don't need a man in my life so long as I'm financially independent". Sasa na sisi muda sio mrefu tutasitisha generous gestures kama hizi na kisha tutaanza kutembelea kwenye haki sawa kweli°View attachment 1237595
Imeanzia kwa wanaume
Women are just victims of copying what men did bila kuchuja..kila kitu kina madhara ukizidisha..balance is key

Baadhi ya wanaume ndo vinara wa mwanamke ni nini.?maadam ana pesa thats all that matters...
 
Hivi mnamaanisha kuwa watoto waliolelewa na mamazao kwa kukaa nyumbani ndo watoto walio Bora zaidi katika jamiii?.... Ina maana watoto waliolelewa na mama na baba Ni wafanya kazi ndo watoto wahovyo?... Nadhani huu mtizamo Ni umegeneralize na Wala hauna ukweli wowote.
Thank you

We all know hamna watu wanapeta sana kwenye maisha kama wale ambao baba na mama wote wako vizuri kiuchumi
 
Wakuu niwatakieni weekend njema na yenye amani tele. Leo nitaandika kifupi tu kwani wengi wamekuwa wakilalamika mada ziwapo ndefu. Tuendelee na mada:

Mwanamke na mwanamume wameumbwa tofauti kwa malengo tofauti. Utofauti huo haufanyi mmoja awe inferior kwa mwenzake bali wawe umoja ili kutimiliza malengo ya uwepo wao duniani ambayo lengo kuu ni kuendeleza kizazi (procreation). Nasema wameumbwa tofauti kw malengo tofauti kwa sababu zifuatazo:

1. Maisha ya kijamii
Mfumo wa maisha wa mwanamke umetofautiana kwa kiasi kikubwa na mwanamume. Mwanamke amepewa maisha ya kuhusiana na jamii inayomzunguka, ndio maana utaona wanawake wanakuwa na makundi mtaani, kwamba huyu ni rafiki yangu w karibu huyu sio. Wanakutana kupeana simulizi za kuhusu maisha ya wengine, nani kapigwa na mume, nani hajui kuvaa, nani kanyang'anya mchumba wa mwingine n.k. Kama huamini fuatilia aina ya maongezi y wanawake wote bila kujali elimu zao. Hili si baya hata kidogo, ndivyo walivyoumbwa. Mwanamke ni kiumbe anayestahili kuwa kwenye mazingiri ya nyumbani kwake kwa muda mwingi zaidi, ni mlezi.

Mwanamume kwa upande wake ameumbiwa maisha ya kutangatanga. Maongezi yao mengi ni kuhusu nani kapataje utajiri, nani kamtapeli mwingine, nani kavusha mzigo nje ya nchi n.k. Mwanamume ni mtafutaji, kwa ajiki na mke na watoto, tena kwa ajili ya wazazi. Mwanamume ni mlezi wa jamii kwa ujumla wake na ndio maana akili yake imeumbwa kufikiri namna ya kupata mali kwa ajili ya familia. Hivi umewahi kujiuliza ni kwa nini hatuna majambazi wanawake?

Uumbaji
Mwanamke na mwanamume hushiriki uumbaji kwa kuunganisha mbegu na yai. Kwa sababu mwanamke sio mtafutaji kiasili, yeye amewekewa mfuko wa uzazi na mfumo wa uleaji wa mtoto mpaka awapo mtu mzima. Mwanamume hajapewa mfumo huo ili awe mtafutaji, amepewa kuwa na nguvu zake mwaka mzima apate kumtunza mke na familia. Kila mfumo uliwekwa kwa kusudi lake.

Jinsi jamii ilivyopora nafasi ya mwanamke
Mapinduzi ya wanawake kuingia kwenye majukumu ya kufanya kazi yalianza wakati wa vita kuu ya pili ya dunia. Hapa kuna hoja nyingi mno lakini siongelei kwa sasa kwa kuogopa kuifanya thread kuwa ndefu. Lakini niseme tu, tuchunguze mfumo wa elimu sasa na kabla.

Zamani mtoto wa kike alipewa elimu yenye ubora wa hali ya juu, iliyomjenga vema kutambua majukumu yake. Shule yak kuu ilikuwa ni wazazi wake ambao aliumia muda mwingi kuwa nao nyumbani. Elimu hii ilimfanya kuwa mwanamke bora aliyejitambua nafasi yake na majukumu yake pia. Mwanamke ni mlazi wa familia, hivyo elimu ililenga kumjengea uwezo kwenye eneo hilo.

Kwa mtoto wa kiume elimu yake iliendana na majukumu yake pia, utafutaji. Kwa kuwa kiasili mwanamume ni mtafutaji, jamii ilijikita kumpatia elimu itakayomwezesha kutafuta mali ili kumudu majukumu ya kumtunza mke na watoto. Ndio maana zamani mtoto wa kiume alipewa nafasi kubwa kusoma elimu ya kizungu (mashuleni na vyuoni). Wapi mambo yalipobadilika?

Pale dunia ilipobadili mfumo na kuanza kuwajengea mtazamowanawake na jamii kwa ujumla kuwa mwanamke anastahili kuwa na kipato chake, asiwe tegemezi kwa mume (hoja inayoondoa kabisa maana ya ndoa na majukumu yaliyomo humo), ndoa zikatazamwa kama gereza la mwanamke. Kwamba mwanamke anapoingia kwenye ndoa kwa mtazamo wa zamani ananyimwa uhuru wa kujitafutia kipato chake mwenyewe. Ndipo likaja swala la elimu.

Mwanamke akatakiwa kupatiwa elimu sawa na mwanamume, mambo ya haki sawa. Hili lilikuwa jambo jema kwa kulitazama kwa juu juu, lakini ukiangalia kwa undani, mwanamke kupatiwa elimu ya utafutaji ni kumwondoa kwenye nafasi yake kama mke. Elimu iliyolenga kutafuta mali tangu awali ilimlenga mtafutaji, mwanamume. Sasa badala ya dunia kuleta elimu inayolenga kuboresha nafasi ya mwanamke, ikaleta elimu inayolenga kumfanya mwanamke awe sawa na mwanamume. Mwanamke hawezi kuwa sawa na mwanamume na ndio maana kinachotokea ni kuigiza kuwa kama mwanamume.

Wanawake wamekuwa wakiishi maisha ya uigizaji, na hii imewafanya kutokujitambua, kutokujua thamani yao na nafasi yao katika jamii. Jamii imemshusha hadhi mwanamke na kumfanya kama mwanamume, isipokuwa tu ameshindwa kabisa kuenenda kwa jinsia hiyo. Matokeo yake wanawake wamegeuzwa kuwa chombo cha starehe, matangazo ya biashara. Mwanamke ambaye zamani alikuwa akiishi na jamii iliyomzunguka huku akijiweka kumliwaza mume, sasa anaishi na jamii za mbali kwa sababu ni mfanya biashara ama mfanyakazi. Zamani alivaa kuteka hisia za mume leo anavaa kuteka hisia za watu wa nje kwa sababu ndiko anakotumia muda wake mwingi. Zamani alikuwa na marafiki waliomzunguka anapoishi leo ana marafiki wa mbali, ambao wana nafasi ya kumjengea mtazamo tofauti.

Mwanamke ameondolewa kwenye nafasi yake ambapoalikuwa chombo cha thamani kubwa na sasa amegeuka mshindani na wanaume. Jamii imemshusha hadhi mwanamke naye amefumbwa macho kuikubali hali hihyo, ndio maana anaishi maisha yasiyo na malengo na matokeo yake ni kuishia kwenye majuto makuu.

Najua mada kama hizi ni ngumu lakini lazima tuangalie ni wapi tulipojikwaa. Feminism ilipaswa kuboresha majukumu ya mwanamke, badala yake imefanya mwanamke awe kama mwanamume.
Wewe Anza na familia yako..mke wako akae nyumbani...watoto wa kiume wasome, wakike waishie lasaba... Usilazimishe kuwa mtizamo wako Ni mzuri na kwamba unajenga familia Bora kuliko wengine...haimaanishi kwa mkewako kukaaa nyumbani watoto wako ndo watakua Bora zaidi kuliko watoto wa watu wengine. Usilazimishe mtizamo wako was ki conservative kwamba Ndo mtizamo iliobora zaidi...
 
Hao unaosema hawa exist wapo sana tu, God fearing women waliotunza asili yao. Nami nikuambie tu I have a happy marriage contrary to what you wish. Mtoto katika miaka yake ya awali atahusiana na mama zaidi kwa sababu ana muda naye mwingi hata baada ya kumwachisha ziwa. Kijana wa kiume akikua huambatana na baba yake zaidi lakini pia atakuwa na muda na mama yake, ndivyo ilivyo kwa mtoto wa kike kwa mama.

Mmhhhh children needs to bond with BOTH parents,hii ya kusema mtoto wa kike na mama na mtoto wa kiume na baba, ni PROOF tosha ulilelewa kwenye isolation......

Watu ambao nyie mnatafuta walikufa na kizazi chao!..demands from the environment wants us women to get education and get jobs..sasa we are responding to the environment which means mtapata tabu sana nyie mnaodhania a woman's place is in the kitchen!....

You are happily married??? I DONT THINK SO!...usingekua unaleta kila siku mada za wanawake,lol..we can smell trouble from very far,lol....Jiangalie mwenyewe topics ngapi in total ulizozianzisha kuhusu wanawake..kisha jiulize tena 'am i happily married'?lol

Social skills zinakuwa imparted hivyo, kila mzazi ana nafasi yake kwa wakati wake. Sisi tuliolelewa kwenye maisha hayo unayoyakashifu tuna amani sana kuliko hiki kizazi cha nyoka, kinachokidai kuzibuka lakini wanaishia kunasa kwenye tundu bovu.

Mnhhh mna amani indeed,kila siku wanawake this wanawake that humu...Mmepata Platform ya kutolea frustrations zenu kuhusu wanawake...in short hamna amani when it comes to women,to you educated ,working lady tayari ni mwiba kwako..tayari ni challnge hutaki kukabiliana nayo..lol...social skills ni BOTH parents playing their role well tangu mkiwa wadogo, na sio kwa njia uliyoiweka hapo!

Na kama unaamini mwanamume ndiye mwenye kuumia kwenye huu upuuzi, basi kweli haimo ndani yako. Hayuko mwanamume aliyekwenda kutafuta dawa ya kupata mke, ama kwenye nyumba za ibada, ama kwa waganga. Waganga wa jadi wamezidi kuwa wengi kwa sababu ya wanawake kuhitaji huduma, hawana amani tena. Bisha na hili

MNhhhhhh sijui hata haya yametoka wapi?
 
Mbona unataja wanawake wenye shida tu ?
Hamna wanaume wenye shida?

Na hamna wanawake wanaofurahia maisha simply bcz wamejiendeleza kwa namna flani?.

Naona una bias flani hivii
Mwanaume kutokuoa sio hoja he also remains single like the woman..
Na siku akioa ataoa mwanamke na si mwanaume mwenzake..ts even..ndoa ya wawili jmn..y u feel women always loose and men always win?..reality haiko hivo

If Godly women were only the happiest wasingekimbilia upepo wa kisulisuli vile😅
Ujue mwanzoni niliposoma hii mada nilidhani huyu mtoa mada ni wale wahafidhina,(wanaoamini katika utamaduni na desturi za kale)
Ok nikaheshimu mtazamo wake, nikajisemea sio mbaya mtu kuamini hivyo, anaweza akawa yupo sahihi kwa watu wengi tu, maana na mimi pia kuna mambo mengi ya kisasa huwa siyaungi mkono
Lakini nilivyozidi kumsoma na comments zake, nikaona kumbe hata mada yake haihusu conservatism, naona huyu tatizo lake ni kuwa anachukia wanawake, misogynist
Maana hao wanawake ambao anataka wanawake wote wafanane hivyo (ambao ni dependant, mission yao kwenye maisha ni kuolewa na kwenda kukaa nyumbani) bado huyu mtoa mada anawakejeli tena, yaani anataka wanawake wote wawe hivyo, ila wale wanawake ambao wapo hivyo ambao wametokana na mfumo wa maisha anaoupigia debe kwenye uzi wake, bado anawakejeli
So tatizo lake sio mfumo wa maisha tatizo lake ni wanawake, pengine alikejeliwa ama kukataliwa sana na wanawake ikamuathiri akawa anawachukia wanawake wote
 
Ndoa ni jambo zuri mnoooo

Na ndoa ingekua rahisi kiasi hicho kwa wanaume basi mabachelor wasingekua wanapata tabu wamuoe nani...ts a struggle eitherways..nadhani anaechagua anapata tabu zaidi cz he has to choose well..and the woman can also say no if she wants..ts not like inakuaga smooth sail tushapita tunajua sio kila mtu alokutamkia ndoa ulimkubalia..u had to choose pia ktk hao...

Anayechagua hapatintabu kama unavyodhani kwake wife material wamejitenga wazi. Anayesubiri kuchaguliwa ndiye mwenye pressure. Kwa leo hii ni nadra mwanamke kisema no, isipokuwa wale waliomezwa na starehe za ujana wakidhani watadumu hivyo milele. Mwanamke wa leo analilia ndoa, na ndio kisa cha wwnaume wenye nia ovu kuwarubuni na kulimega tunda kiulaini.

Na mwanamke asipoolewa na mwanaume mmoja haimaanishi hatoolewa na mwanaume mwingine

Ni kweli haimaanishi hivyo, lakini kuolewa kwa mwanamke kunategemea sana mtazamo wake kwenye ndoa, ndio malezi yenyewe. Wengi wasiotambua thamani ya ndoa huishia kwenye upepo wa kisulisuli wakitaka kuolewa bila sifa

Furaha ya mwanamke na ndoa ipo karibu sana mana ndo jukumu la tangu kuumbwa dunia alikua asubirie ndoa tu azae alee afe...mindset na setting kijamii iko hivyo
sikuhizi vyanzo vya furaha ni vingi..vingi sana...ndoa inakuja kama icing on the cake and not the whole cake...si kwa mwanamke tu hata mwanaume...there is life beyond
Maisha yanakua ss muunganiko wa yote hayo

Hiyo habari ya mindset au jamii ni uongo, hayo ni maandiko kw wanaoamini. Tunaamini ni maagizo ya Mungu Mwenyezi. Ndoa ndio msingi wa kujenga familia, sio kama leo hii inavyosemwa hovyo hovyo. Na furaha ya ndoa ni kuu kuliko hivyo vyanzo unavyosema ambavyo ni vya muda tu
 
Its twisted simply because men twisted it first

It used to be kisa mwanaume ana elimu na pesa mwanamke utaisoma namba..utanyanyasika mana jamaa anakupangia anavotaka yeye smtimes bila kujali how you feel...japo sio wote ila baadhi
Ss sikuhz women have that pia naona ndo mana wanaume mnateseka...

Afterall si wanawake wote wanatumia elimu zao vibaya..jifunzeni kuchagua tu vizuri
Ndio nnachokisema hiki, wanawake kuamini kwamba elimu na pesa ni nyenzo ya kumnyanyasia mtu kitu ambacho si kweli, sasa kwa sababu na nyie siku hizi mnazo nyenzo hizo basi ni mwendo wa mashindano tu hata pasipokuwa na ulazima.

Kwakuwa na nyinyi mna mali/pesa basi mmekuwa alpha females. Naona mpaka kuna mmoja wenu hapo juu anasema pesa zimempa uwezo wa kuwachezea wanaume kadri anavyotaka. .

Nakubali wanawake walikandamizwa karne hizo lakini si kwa sababu ya kutokuwa na pesa/mali kama ambavyo wengi mnaamini. Mgawanyo wa kimajukumu ndio ulitoa mwanya huo wa mwanamke kukandamizwa napenyewe si kwa kiasi ambacho kinaongelewa siku hizi.

Ni kweli nakubaliana na wewe sio wanawake wako hivyo ila bahati mbaya sana wengi ndio wako hivi
 
Wewe Anza na familia yako..mke wako akae nyumbani...watoto wa kiume wasome, wakike waishie lasaba... Usilazimishe kuwa mtizamo wako Ni mzuri na kwamba unajenga familia Bora kuliko wengine...haimaanishi kwa mkewako kukaaa nyumbani watoto wako ndo watakua Bora zaidi kuliko watoto wa watu wengine. Usilazimishe mtizamo wako was ki conservative kwamba Ndo mtizamo iliobora zaidi...
Asante kwa mchango, tumekusikia
 
Kwani la saba sio elimu? Wasisome kabisa, aee you happy now?
 
Kuchagua aina ya kazi/biashara utakayofanya
Mfano:iwe flexible, masaa machache kazini ama kwny biashara,kuwa na wasaidizi wa kazi nyumbani mgawane kazi nk

Maadam upate kazi/biashara inayokupa nafasi kuattend majukumu ya familia na yako binafsi as a human being/woman
Hicho ndicho tukisemacho, mwanamke asihame kwenye majukumu yake ya msingi, nurturing. Hii haimfanyi kuwa mtumwa hata kidogo bali inamfanya mwenye jukumu jema la malezi.
 
Madam huu usawa wengi wanaufurahia sana lakini niamini mimi athari zake zitawakumba zaidi wanawake kuliko wanaume.

Wewe si unajifanya uko sawa mwanaume!!? Basi na mimi nakuchukulia kama mwanaume mwenzangu katika situation yoyote ile. Hebu soma hiki kipande cha habari, Kwenye hii ajali waliokufa wote ni wanawake na watoto.

PASSENGERS of the Costa Concordia, the cruise ship that sunk off an Italian island on Friday [13th January 2012], told The Daily Mail that in the chaos after the ship was wrecked, men rushed for the lifeboats and gave no priority to women and children.

As she [one of the survivors ] waited for a flight home from Rome, grandmother Sandra Rogers, 62, told the Daily Mail: ‘There was no “WOMEN and CHILDREN FIRST” policy. There were big men, crew members, pushing their way past us to get into the lifeboats. It was DISGUSTING.’

Na huku ndio tulipofikia.. Naamini kabisa hata ile ajali ya TITANIC ingetokea leo hii wangekufa wanawake tupu.

Wanawake tunapoteza nafasi yetu na tunakosa haki na vipaumbele vya msingi kwa kulazimisha kuwa sawa na wanaume.
Huu usawa unaenda hata kinyume na dini zetu..Je Mungu alikosea kumwambia adam atakula kwa jasho? Hivi kwanini hili hakumwambia Hawa?

Sisemi kwamba wanawake wanatakiwa wasitoke jasho ila hata Mungu alijua kwamba hatuwezi kuwa sawa ila tunaweza kuwa wasaidizi wazuri sana
 
kiazi mbatata wee ....navyompenda Mama yangu, na ninvyosimaam kwa ajili ya mama yangu..

Niwe nmekosa nn?? Hihihi kaone ,kapanya weee
Mimi Nadhani hata kumuita Kiazi mbatata umempa heshima sana ambayo hastahili kuwa nayo. Kiazi mbatata ni chakula chenye manufaa mengi sana mwilini, usilinganishe chakula hiki na vitu vya kipuuzi kabisa.

Huyo ni kokwa la embe tena tena lile ambalo limeshaanza kuoza kiini chake kiasi kwamba halina matumizi tena kwenye uso wa hii dunia.
 
Ndio nnachokisema hiki, wanawake kuamini kwamba elimu na pesa ni nyenzo ya kumnyanyasia mtu kitu ambacho si kweli, sasa kwa sababu na nyie siku hizi mnazo nyenzo hizo basi ni mwendo wa mashindano tu hata pasipokuwa na ulazima.

Kwakuwa na nyinyi mna mali/pesa basi mmekuwa alpha females. Naona mpaka kuna mmoja wenu hapo juu anasema pesa zimempa uwezo wa kuwachezea wanaume kadri anavyotaka. .

Nakubali wanawake walikandamizwa karne hizo lakini si kwa sababu ya kutokuwa na pesa/mali kama ambavyo wengi mnaamini. Mgawanyo wa kimajukumu ndio ulitoa mwanya huo wa mwanamke kukandamizwa napenyewe si kwa kiasi ambacho kinaongelewa siku hizi.

Ni kweli nakubaliana na wewe sio wanawake wako hivyo ila bahati mbaya sana wengi ndio wako hivi
Unajicontradict

Money is power
Kinachowapa jeuri wanaume si pumbu tu
Ni hio hali ya kuwa na kipato ama kupata access zaidi ya wanawake over the years

Na truth be told..imetumika kuwaonea wanawake mara nyingi..wanayotenda wanawake ni matokeo ya walichoona kwa wanaume
Alpha females ni trait tu mana Beta Males wapo pia
Kila mtu na mbuyu wake
 
Hivi mnamaanisha kuwa watoto waliolelewa na mamazao kwa kukaa nyumbani ndo watoto walio Bora zaidi katika jamiii?.... Ina maana watoto waliolelewa na mama na baba Ni wafanya kazi ndo watoto wahovyo?... Nadhani huu mtizamo Ni umegeneralize na Wala hauna ukweli wowote.
Kuna exceptions mkuu, lakini hoja ni kuwa watoto waliolelewa na mama zao ni bora mno na huwezi kuwalinganisha na waliolelewa na mahouse girls. Ni nini hoja yako katika hilo?
 
Back
Top Bottom