Jamii imempora mwanamke nafasi yake

Jamii imempora mwanamke nafasi yake

MKUU LIZARAZU PUNGUZA HASIRA, MAANA HATA KOKWA LA EMBE LIKIOZA LINAKUWA NDIO CHANZO CHA KUOTA MWEMBE MWINGINE
Kwa maana hiyo hata hapo bado ni mahali asipostahili.
FB_IMG_1571179274220.jpeg
 
Habari Wakuu na wachangiaji wote, Binafsi nimesoma bandiko hili na yafuatayo ndiyo maoni yangu:-

Nakubaliana na ukweli kwamba Mwanaume (Adam) ndiye aliyekuwa wa kwanza kuumbwa na baadaye Mwanamke (Eva/Hawa) alifuatia baada ya Adamu kulazwa usingizi na kutolewa sehemu ya mbavu yake ya kushoto ambayo ilitumika kumuumba aliyekuja kuwa msaidizi wake (Yaani Hawa/Eva)

Kabla ya kuumbwa Hawa/Eva. Adamu tayari alikwisha pewa mamlaka ya kuvitawala viumbe vyote vilivyopo chini ya jua (Pamoja na Hawa/Eva) pia alipewa na maagizo ya namna ya kuishi katika bustani ya Eden nini ale/afanye na nini asile/asifanye. maagizo hayo yote Adamu aliyashika na kuyaelewa ipasavyo. Binafsi nahisi hata shetani alijaribu kumshawishi Adamu lakini alishindwa.

Baada ya kuumbwa Hawa na kukabidhiwa kwa Adamu kama msaidizi ndipo vioja vilianza. Adamu aliona ya kuwa Eva/Hawa ni mzuri hivyo alichizika na uzuri wake na hatimaye kusahau kanuni na maagizo (Rules of Engagement) aliyopewa kuhusu Eden na shetani kwa kuwa alikuwa mjanja akaona kuwa Eva ni njia sahihi ya kufanikisha kusudi lake.

Baada ya Shetani kufanikiwa kumrubuni Hawa naye Hawa alikwenda kumwambia maneno hayo Adamu ambaye tayari alikwishachizika na uzuri wake jambo ambalo lilipelekea kumuamini pasina shaka. baada ya kula tunda ndipo walijikuta wakiwa uchi na kwenda kujificha. Baadae MUNGU alikuja kuwatafuta na kukuta wamejificha kwa kuwa wapo uchi alipouliza kama wamekula tunda la mti wa katikati na kwa nini ndipo Adamu akamtupia lawama MUNGU kwa kusema kuwa "Ni huyu Mwanamke uliyenipa" (kwa maoni yangu Adamu alitakiwa kukiri kosa na kuomba msamaha, kumlaumu Hawa haikuwa sahihi maana yeye ndiye alikuwa kiongozi)

Wanaume wa leo tumekuwa waoga wengi wetu tunakwepa kuwajibika na badala yake pale tunapokosea huishia kurushia lawama wanawake. Maandiko yalishatuambia kuwa wanawake ni viumbe dhaifu tuishi nao kwa akili (Kuishi nao kwa akili ni kuhakikisha wanapata mahitaji muhimu, kuwasikiliza, kuwaelekeza na kuwarekebisha pale wanapokosea) lakini baadhi ya sisi Wanaume tumeshindwa kutimiza wajibu wetu na badala yake tumekuwa watu wa kuwasonta vidole wanawake na kuwalaumu, ndiyo maana yanaibuka haya tuonayo sasa.

Kuhusu kuporomoka kwa maadili tatizo siyo Mwanamke mchawi wa mmomonyoko wa maadili ni Technologia hasa ya mawasiliano ambayo pia wagunduzi na waasisi wake ni Wanaume wenzetu wa bara la America na Asia hivyo hata wao (Wanawake) na sisi wote ni .wahanga.

Kuhusu elimu kwa mtoto wa kike siyo jambo baya japokuwa si kila aliyesoma ameelimika, Baadhi ya wanawake waliosoma kisha wakaelimika wametumia elimu yao kuisaidia familia na hakika maisha yao na waume zao ni mazuri na yenye mafanikio maana wanawake hao wamekuwa watii na kuwa wasaidizi hasa kwa wale Wanaume waliobahatika kuwaoa. Wale waliosoma wakashindwa kuelimika ndio pasua kichwa na ndio hupenda kusema "usinibabaishe nina elimu yangu".

Wito wangu ni kuwa tatizo limekwishatokea kulaumu, kukejeli na kudhihaki hakubadilishi chochote. sisi kama viongozi tunatakiwa kuangalia wapi tulikosea, turekebishe kisha tusonge mbele. Maisha ya ndoa hayahitaji uhana harakati bali nidhamu iliyotukuka na upendo wa kweli baina ya wanandoa lakini hii inatakiwa ianzishwe na mume kisha mke afuate.

NINAYO MENGI LAKINI KWA LEO NAISHIA HAPA NA WENZANGU WAENDELEE!!
 
Nime quote hii point
sasa hakuna wanawake bali watafutaji

Hicho unachokisema ndio ukengeufu wenyewe. Jukumu la mwanamke ni kuzaa na kulea, hizo kazi mmepewa na wajanja na iko sababu ya kibiashara na kimapato ya serikali. Mwanamke anagawana majukumu na mune, mmoja nyumbani mwingine kazini. Ndio maana watoto wa siku hizi hawana malezi bora, kwa sababu mama anarudi saa nne usiku na baba pia. Wanawake mmejitwisha jukumu la wanaume, mkaacha jukumu lenu.

Kwamba wasio na kazi wana maisha mabaya si kweli, inategemea unatazasha vipi maisha. Wanawake wasio na waume nilioongea nao mimi hawana furaha wala amani hata kama wana kazi. Kazi sio kila kitu kwa mwwnamke ila dunia imejaribu kumwaminisha hivyo. Kwa mfumo sasa hakuna mwanamke tena, wote ni watafutaji tu. Mwanamke halisi atawazia malezi ya famikia bora kuliko kutafuta mali binafsi ndani ya ndoa.

Ukahaba kuwepo tangu kale ni kwa sababu wako wachache ambao hawakuzingatia maonyo. Na hiyo sio sababu ya kuendeleza ukahaba, misingi ya zama hizo haikushabikia ukahaba bali ilipinga kabisa, hivyo kauli yako ni mfu. Wanawake wengi wanaji expose kwenye system ya elimu, wanajikuta wameingia kwenye vitendo vya ukahaba kwani wanaanza kujitegemea wakiwa bdo hawako tayari.
 
Mkuu umeongea mambo halisia yanaendelea kwenye baadhi ya familia zetu. Binafsi sometimes huwa na-regret kuoa mke msomi, maana sioni faida yake kiukweli masaa mengi yuko bize na mambo yake hana muda hata na watoto. Lakini pia mwisho wa siku faida ya kazi zake hizo kwa familia ni very negligible.

Yaani kwa uzembe wake kwa watoto ilifika pahala nikahamua kuwa narudi nyumbani mwenyewe mapema ili nikague school works na kuwasimamia watoto wafanye homeworks.

Nilifikia uhamuzi huu baada ya kumsihi afanye hivyo yeye bila mafanikio, wakati huo mimi navipenda kweli vitoto vyangu hivi vi3 na pia ninavilipia hela yangu nyingi ninayopata kwa shida ili visome!

Nikaona bora nijitoe tu muhanga nivisaidie maana kwa upande wangu kama ni kukosea/kupatia maisha kidogo kuna muelekeo ila kwa hawa watoto bado sana kulijua hilo hivyo inabidi kuwasaidia kadri iwezekanavyo hata kama ushirikiano wa bibie ni mdogo.
pole sana mkuu

ila hiyo ndio hali haslisi kabisa mkuu

yaani nawashangaa sana vijana wa siku hizi eti katika vigezo wanavyotaka mke awe navyo ni elimu au kipato cha kutosha,ndugu yangu elimu au pesa ya mwanamke haijengi mji,haitunzi watoto hiyo

yaani mkuu kama mke anajua kazi za nyumbani vizuri kabisa huyo ndo wa kuoa na sio ana elimu kiasi gani au pesa kiasi gani,ni shida mkuu shida mnoo basi tu watu huwa hatulijui hilo au tunaamua tu kulifumbia macho

pole sana mkuu kwa shida unayoyapitia kwa sasa,kaza moyo tu mkuu labda itafika siku ambayo atashtuka kwamba anachokifanya sio sawa,plus watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu so we endelea tu kukomaa nao wasipoteze mwelekeo,maana wakipoteza mwelekeo maumivu yake hayana kifani,keep the spirit kaka.
 
Hivi mnamaanisha kuwa watoto waliolelewa na mamazao kwa kukaa nyumbani ndo watoto walio Bora zaidi katika jamiii?.... Ina maana watoto waliolelewa na mama na baba Ni wafanya kazi ndo watoto wahovyo?... Nadhani huu mtizamo Ni umegeneralize na Wala hauna ukweli wowote.
mkuu kagebby labda hujaelelewa maana niliyoipresent hapo juu

naomba nikusaidie uelewe

Mkuu nini maana ya malezi?

jukumu la malezi ni la nani?baba,mama,housegirl au baba na mama?

nini kinamsaidia mtoto kujengeka vizuri kifikra,kihisia na hata kitabia?kazi ya mama na baba? au nini kinahsukia mkuu?

tuanzie hapo kwanza ndo mengine yafuate.
 
Wakuu niwatakieni weekend njema na yenye amani tele. Leo nitaandika kifupi tu kwani wengi wamekuwa wakilalamika mada ziwapo ndefu. Tuendelee na mada:

Mwanamke na mwanamume wameumbwa tofauti kwa malengo tofauti. Utofauti huo haufanyi mmoja awe inferior kwa mwenzake bali wawe umoja ili kutimiliza malengo ya uwepo wao duniani ambayo lengo kuu ni kuendeleza kizazi (procreation). Nasema wameumbwa tofauti kw malengo tofauti kwa sababu zifuatazo:

1. Maisha ya kijamii
Mfumo wa maisha wa mwanamke umetofautiana kwa kiasi kikubwa na mwanamume. Mwanamke amepewa maisha ya kuhusiana na jamii inayomzunguka, ndio maana utaona wanawake wanakuwa na makundi mtaani, kwamba huyu ni rafiki yangu w karibu huyu sio. Wanakutana kupeana simulizi za kuhusu maisha ya wengine, nani kapigwa na mume, nani hajui kuvaa, nani kanyang'anya mchumba wa mwingine n.k. Kama huamini fuatilia aina ya maongezi y wanawake wote bila kujali elimu zao. Hili si baya hata kidogo, ndivyo walivyoumbwa. Mwanamke ni kiumbe anayestahili kuwa kwenye mazingiri ya nyumbani kwake kwa muda mwingi zaidi, ni mlezi.

Mwanamume kwa upande wake ameumbiwa maisha ya kutangatanga. Maongezi yao mengi ni kuhusu nani kapataje utajiri, nani kamtapeli mwingine, nani kavusha mzigo nje ya nchi n.k. Mwanamume ni mtafutaji, kwa ajiki na mke na watoto, tena kwa ajili ya wazazi. Mwanamume ni mlezi wa jamii kwa ujumla wake na ndio maana akili yake imeumbwa kufikiri namna ya kupata mali kwa ajili ya familia. Hivi umewahi kujiuliza ni kwa nini hatuna majambazi wanawake?

Uumbaji
Mwanamke na mwanamume hushiriki uumbaji kwa kuunganisha mbegu na yai. Kwa sababu mwanamke sio mtafutaji kiasili, yeye amewekewa mfuko wa uzazi na mfumo wa uleaji wa mtoto mpaka awapo mtu mzima. Mwanamume hajapewa mfumo huo ili awe mtafutaji, amepewa kuwa na nguvu zake mwaka mzima apate kumtunza mke na familia. Kila mfumo uliwekwa kwa kusudi lake.

Jinsi jamii ilivyopora nafasi ya mwanamke
Mapinduzi ya wanawake kuingia kwenye majukumu ya kufanya kazi yalianza wakati wa vita kuu ya pili ya dunia. Hapa kuna hoja nyingi mno lakini siongelei kwa sasa kwa kuogopa kuifanya thread kuwa ndefu. Lakini niseme tu, tuchunguze mfumo wa elimu sasa na kabla.

Zamani mtoto wa kike alipewa elimu yenye ubora wa hali ya juu, iliyomjenga vema kutambua majukumu yake. Shule yak kuu ilikuwa ni wazazi wake ambao aliumia muda mwingi kuwa nao nyumbani. Elimu hii ilimfanya kuwa mwanamke bora aliyejitambua nafasi yake na majukumu yake pia. Mwanamke ni mlazi wa familia, hivyo elimu ililenga kumjengea uwezo kwenye eneo hilo.

Kwa mtoto wa kiume elimu yake iliendana na majukumu yake pia, utafutaji. Kwa kuwa kiasili mwanamume ni mtafutaji, jamii ilijikita kumpatia elimu itakayomwezesha kutafuta mali ili kumudu majukumu ya kumtunza mke na watoto. Ndio maana zamani mtoto wa kiume alipewa nafasi kubwa kusoma elimu ya kizungu (mashuleni na vyuoni). Wapi mambo yalipobadilika?

Pale dunia ilipobadili mfumo na kuanza kuwajengea mtazamowanawake na jamii kwa ujumla kuwa mwanamke anastahili kuwa na kipato chake, asiwe tegemezi kwa mume (hoja inayoondoa kabisa maana ya ndoa na majukumu yaliyomo humo), ndoa zikatazamwa kama gereza la mwanamke. Kwamba mwanamke anapoingia kwenye ndoa kwa mtazamo wa zamani ananyimwa uhuru wa kujitafutia kipato chake mwenyewe. Ndipo likaja swala la elimu.

Mwanamke akatakiwa kupatiwa elimu sawa na mwanamume, mambo ya haki sawa. Hili lilikuwa jambo jema kwa kulitazama kwa juu juu, lakini ukiangalia kwa undani, mwanamke kupatiwa elimu ya utafutaji ni kumwondoa kwenye nafasi yake kama mke. Elimu iliyolenga kutafuta mali tangu awali ilimlenga mtafutaji, mwanamume. Sasa badala ya dunia kuleta elimu inayolenga kuboresha nafasi ya mwanamke, ikaleta elimu inayolenga kumfanya mwanamke awe sawa na mwanamume. Mwanamke hawezi kuwa sawa na mwanamume na ndio maana kinachotokea ni kuigiza kuwa kama mwanamume.

Wanawake wamekuwa wakiishi maisha ya uigizaji, na hii imewafanya kutokujitambua, kutokujua thamani yao na nafasi yao katika jamii. Jamii imemshusha hadhi mwanamke na kumfanya kama mwanamume, isipokuwa tu ameshindwa kabisa kuenenda kwa jinsia hiyo. Matokeo yake wanawake wamegeuzwa kuwa chombo cha starehe, matangazo ya biashara. Mwanamke ambaye zamani alikuwa akiishi na jamii iliyomzunguka huku akijiweka kumliwaza mume, sasa anaishi na jamii za mbali kwa sababu ni mfanya biashara ama mfanyakazi. Zamani alivaa kuteka hisia za mume leo anavaa kuteka hisia za watu wa nje kwa sababu ndiko anakotumia muda wake mwingi. Zamani alikuwa na marafiki waliomzunguka anapoishi leo ana marafiki wa mbali, ambao wana nafasi ya kumjengea mtazamo tofauti.

Mwanamke ameondolewa kwenye nafasi yake ambapoalikuwa chombo cha thamani kubwa na sasa amegeuka mshindani na wanaume. Jamii imemshusha hadhi mwanamke naye amefumbwa macho kuikubali hali hihyo, ndio maana anaishi maisha yasiyo na malengo na matokeo yake ni kuishia kwenye majuto makuu.

Najua mada kama hizi ni ngumu lakini lazima tuangalie ni wapi tulipojikwaa. Feminism ilipaswa kuboresha majukumu ya mwanamke, badala yake imefanya mwanamke awe kama mwanamume.
Fanyia hivyo mabinti zako
 
pole sana mkuu

ila hiyo ndio hali haslisi kabisa mkuu

yaani nawashangaa sana vijana wa siku hizi eti katika vigezo wanavyotaka mke awe navyo ni elimu au kipato cha kutosha,ndugu yangu elimu au pesa ya mwanamke haijengi mji,haitunzi watoto hiyo

yaani mkuu kama mke anajua kazi za nyumbani vizuri kabisa huyo ndo wa kuoa na sio ana elimu kiasi gani au pesa kiasi gani,ni shida mkuu shida mnoo basi tu watu huwa hatulijui hilo au tunaamua tu kulifumbia macho

pole sana mkuu kwa shida unayoyapitia kwa sasa,kaza moyo tu mkuu labda itafika siku ambayo atashtuka kwamba anachokifanya sio sawa,plus watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu so we endelea tu kukomaa nao wasipoteze mwelekeo,maana wakipoteza mwelekeo maumivu yake hayana kifani,keep the spirit kaka.
Mkuu ni kweli kabisa uliyoyaandika. Asante sana kwa ushauri mzuri, nimeuchukua.
 
Nyenyere hii ni mada ambayo nashukuru kusema kuwa ndiyo mada Bora ambayo mwaka huu unaoishia masaa matatu mbele nimeiona Bora kabisa sijui uliwaza nini yaani ni unbelievable big up wachangiaji wote

Sent from my itel S32 using Tapatalk
 
jukumu la malezi ni la mwanamke, naye ameliacha na kukimbilia majukumu ya mwanamume
Sasa mwanamke huyu afanyaje endapo ana mwanaume ambaye hatimizi majukumu yake kama baba,hafanyi chochote kwa ajili ya kutunza familia yake??
 
Wakuu niwatakieni weekend njema na yenye amani tele. Leo nitaandika kifupi tu kwani wengi wamekuwa wakilalamika mada ziwapo ndefu. Tuendelee na mada:

Mwanamke na mwanamume wameumbwa tofauti kwa malengo tofauti. Utofauti huo haufanyi mmoja awe inferior kwa mwenzake bali wawe umoja ili kutimiliza malengo ya uwepo wao duniani ambayo lengo kuu ni kuendeleza kizazi (procreation). Nasema wameumbwa tofauti kwa malengo tofauti kwa sababu zifuatazo:

Maisha ya kijamii
Mfumo wa maisha wa mwanamke umetofautiana kwa kiasi kikubwa na mwanamume. Mwanamke amepewa maisha ya kuhusiana na jamii inayomzunguka, ndio maana utaona wanawake wanakuwa na makundi mtaani, kwamba huyu ni rafiki yangu wa karibu huyu sio. Wanakutana kupeana simulizi za kuhusu maisha ya wengine, nani kapigwa na mume, nani hajui kuvaa, nani kanyang'anya mchumba wa mwingine n.k. Kama huamini fuatilia aina ya maongezi ya wanawake wote bila kujali elimu zao. Hili si baya hata kidogo, ndivyo walivyoumbwa. Mwanamke ni kiumbe anayestahili kuwa kwenye mazingiri ya nyumbani kwake kwa muda mwingi zaidi, ni mlezi.

Mwanamume kwa upande wake ameumbiwa maisha ya kutangatanga. Maongezi yao mengi ni kuhusu nani kapataje utajiri, nani kamtapeli mwingine, nani kavusha mzigo nje ya nchi n.k. Mwanamume ni mtafutaji, kwa ajili ya mke na watoto, tena kwa ajili ya wazazi. Mwanamume ni mlezi wa jamii kwa ujumla wake na ndio maana akili yake imeumbwa kufikiri namna ya kupata mali kwa ajili ya familia. Hivi umewahi kujiuliza ni kwa nini hatuna majambazi wanawake?

Uumbaji
Mwanamke na mwanamume hushiriki uumbaji kwa kuunganisha mbegu na yai. Kwa sababu mwanamke sio mtafutaji kiasili, yeye amewekewa mfuko wa uzazi na mfumo wa uleaji wa mtoto mpaka awapo mtu mzima. Mwanamume hajapewa mfumo huo ili awe mtafutaji, amepewa kuwa na nguvu zake mwaka mzima apate kumtunza mke na familia. Kila mfumo uliwekwa kwa kusudi lake.

Jinsi jamii ilivyopora nafasi ya mwanamke
Mapinduzi ya wanawake kuingia kwenye majukumu ya kufanya kazi yalianza wakati wa vita kuu ya pili ya dunia. Hapa kuna hoja nyingi mno lakini siongelei kwa sasa kwa kuogopa kuifanya thread kuwa ndefu. Lakini niseme tu, tuchunguze mfumo wa elimu sasa na kabla.

Zamani mtoto wa kike alipewa elimu yenye ubora wa hali ya juu, iliyomjenga vema kutambua majukumu yake. Shule yao kuu ilikuwa ni wazazi wake ambao aliumia muda mwingi kuwa nao nyumbani. Elimu hii ilimfanya kuwa mwanamke bora aliyejitambua nafasi yake na majukumu yake pia. Mwanamke ni mlazi wa familia, hivyo elimu ililenga kumjengea uwezo kwenye eneo hilo.

Kwa mtoto wa kiume elimu yake iliendana na majukumu yake pia, utafutaji. Kwa kuwa kiasili mwanamume ni mtafutaji, jamii ilijikita kumpatia elimu itakayomwezesha kutafuta mali ili kumudu majukumu ya kumtunza mke na watoto. Ndio maana zamani mtoto wa kiume alipewa nafasi kubwa kusoma elimu ya kizungu (mashuleni na vyuoni). Wapi mambo yalipobadilika?

Pale dunia ilipobadili mfumo na kuanza kuwajengea mtazamo wanawake na jamii kwa ujumla kuwa mwanamke anastahili kuwa na kipato chake, asiwe tegemezi kwa mume (hoja inayoondoa kabisa maana ya ndoa na majukumu yaliyomo humo), ndoa zikatazamwa kama gereza la mwanamke. Kwamba mwanamke anapoingia kwenye ndoa kwa mtazamo wa zamani ananyimwa uhuru wa kujitafutia kipato chake mwenyewe. Ndipo likaja swala la elimu.

Mwanamke akatakiwa kupatiwa elimu sawa na mwanamume, mambo ya haki sawa. Hili lilikuwa jambo jema kwa kulitazama kwa juu juu, lakini ukiangalia kwa undani, mwanamke kupatiwa elimu ya utafutaji ni kumwondoa kwenye nafasi yake kama mke. Elimu iliyolenga kutafuta mali tangu awali ilimlenga mtafutaji, mwanamume. Sasa badala ya dunia kuleta elimu inayolenga kuboresha nafasi ya mwanamke, ikaleta elimu inayolenga kumfanya mwanamke awe sawa na mwanamume. Mwanamke hawezi kuwa sawa na mwanamume na ndio maana kinachotokea ni kuigiza kuwa kama mwanamume.

Wanawake wamekuwa wakiishi maisha ya uigizaji, na hii imewafanya kutokujitambua, kutokujua thamani yao na nafasi yao katika jamii. Jamii imemshusha hadhi mwanamke na kumfanya kama mwanamume, isipokuwa tu ameshindwa kabisa kuenenda kwa jinsia hiyo. Matokeo yake wanawake wamegeuzwa kuwa chombo cha starehe, matangazo ya biashara. Mwanamke ambaye zamani alikuwa akiishi na jamii iliyomzunguka huku akijiweka kumliwaza mume, sasa anaishi na jamii za mbali kwa sababu ni mfanya biashara ama mfanyakazi. Zamani alivaa kuteka hisia za mume leo anavaa kuteka hisia za watu wa nje kwa sababu ndiko anakotumia muda wake mwingi. Zamani alikuwa na marafiki waliomzunguka anapoishi leo ana marafiki wa mbali, ambao wana nafasi ya kumjengea mtazamo tofauti.

Mwanamke ameondolewa kwenye nafasi yake ambapoalikuwa chombo cha thamani kubwa na sasa amegeuka mshindani na wanaume. Jamii imemshusha hadhi mwanamke naye amefumbwa macho kuikubali hali hihyo, ndio maana anaishi maisha yasiyo na malengo na matokeo yake ni kuishia kwenye majuto makuu.

Najua mada kama hizi ni ngumu lakini lazima tuangalie ni wapi tulipojikwaa. Feminism ilipaswa kuboresha majukumu ya mwanamke, badala yake imefanya mwanamke awe kama mwanamume.
Unapozungumzia umbaji bilashaka unaoata hii katika maandiko matakatifu ambapo Mungu alimumba Adam then akamfanyia msaidizi,Hawa

Katika hali ya kawaida neno msaidizi haliainishi aina ya kazi wala kuweka mipaka. Kimsingi utendaji kazi wa kila mmoja hutegemea na mikakati, ujuzi, elimu, tamaduni, n.k

Umesema vema kwamba Mungu akiwambia "zaeni muongezeke mkaijaze na kuitawala" it means wote wana kazi moja na jukumu moja, hakumwambia Adam pekee
 
Nimesikitishwa sana na hiki kipande cha bandiko lako inaonesha wazi kabisa haujui kabisa athari za huu mfumo unaompedelea mwanamke.

Ndugu huu mfumo unaofanya dunia ya sasa kumpendelea mwanamke sio wa kushabikia hata kidogo, maana athari zake ni kubwa mno na zinatulenga jinsia zote mbili.

Ulimwengu wa sasa unampendelea zaidi mwanamke kwa kumpa umuhimu mkubwa kuliko jinsia nyingine. Kuna taasisi nyingi sana duniani zimeanzishwa kwa ajili ya kushughulika na masuala ya wanawake, sheria zetu zenyewe zina mpendelea zaidi mwanamke na hata ukija kwenye jumuiya kubwa za kimataifa zinalinda sana maslahi ya wanawake kuliko wanaume mfano kama UN kuna departments zaidi ya 8 ambazo ni mahususi kwa kushughulika na women issues lakini hakuna hata moja inayoshughulika na wanaume.

Kutokana na hali hii ya mwanamke kupendelewa na kuaminishwa kuwa anaweza kuwa sawa na mwanaume imepelekea kutokea kwa gender isolation.

Siku hizi ni matukio ya wanaume kusingiziwa kesi za ubakaji na wanawake yamekuwa mengi sana, na sababu kuu hasa ni huu upendeleo wa kijinsia tulionao kwenye dunia ya leo.

Na hii imepelekea wanaume kutengeneza distance baina yao na wanawake kutokana na hofu pamoja na kutoona hawana umuhimu kwa wanawake. Yaani imefikia hatua mwanaume anaona yuko salama zaidi asipojihusisha na mwanamke kwa jambo lolote lile.

Ni kwa bahati mbaya sana waathirika wakuu wa hii gender isolation ni wanawake. Na tayari athari hii imeshaanza kuonekana huko ambako haya mambo yameanzia.

Nchini Sweden matukio ya uhalifu ikiwemo ubakaji yamekuwa mengi sana miaka hii ukilinganisha na miaka ya nyuma. Na waathirika wakuu wa matukio haya ni wanawake.

Mwaka juzi wanawake wa Sweden waliandamana wakiwalaumu wanaume wa nchi hiyo kwamba wamejitenga sana na ndio maana wanawake wengi wamekuwa wakibakwa na kufanyiwa matukio mengine ya kihalifu.

Kwa madai yao ni kwamba endapo kama wanaume wa kiswedish wangekuwa karibu na wanawake basi kusingekuwepo na matukio ya ubakaji kwa kiasi kikubwa hivi.

Cha kushangaza hao hao wanawake ndio chanzo cha wanaume kujitenga na wao mpaka wanakutwa na hayo maswahibu.

Kuna tukio lingine lilitokea huko Italy miaka ya nyuma kidogo linaloonesha jamii yetu imefikia pabaya sana kutokana na huu mfumo unaoufurahia na kuupigia debe. Ngoja nikuwekee kipande cha hiyo habari..

PASSENGERS of the Costa Concordia, the cruise ship that sunk off an Italian island on Friday [13th January 2012], told The Daily Mail that in the chaos after the ship was wrecked, men rushed for the lifeboats and gave no priority to women and children.

As she [one of the survivors ] waited for a flight home from Rome, grandmother Sandra Rogers, 62, told the Daily Mail: ‘There was no “WOMEN and CHILDREN FIRST” policy. There were big men, crew members, pushing their way past us to get into the lifeboats. It was DISGUSTING.’

Kwa kuangalia hiyo scenario hapo utaona wanaume wa leo sio wale wa zama zile za TITANIC, wanaume wa siku hizi hata wao wamejifunza kwenda na huu mfumo wenu mpya, yale masuala ya wanawake na wanawake kwamba ndio wanapewa kipaumbele kwenye kuokolewa pale yanapotokea majanga hayapo tena. Maana hata wanawake pia wanaweza kufanya chochote ambacho wanaume wanafanya ikiwemo kujiokoa wenyewe kwenye ajali.

Hivi umewahi kujiuliza siku Ikitokea vita ya tatu ya dunia hali itakuwaje?

Wewe unahisi kwa huu utengano na ubinafsi tuliojengewa na huu mfumo wenu wa haki sawa wanaume watakuwa tayari kujitoa kwa ajili ya wanawake kama walivyo fanya miaka ya nyuma??

Dunia ya sasa inajaribu kukuaminisha kwamba huko sawa na mwanaume kwa kila kitu, lakini hicho kitu hakipo na wala hakitakuja kutokea. Uking'ang'ania sana utajikuta wewe ndio unayepoteza pakubwa.

Tunaweza kuandika maelezo mengi hapa ukaona kama ni stress tu ndio zinazoandika lakini nikwambie kwa mawazo hayo uliyonayo unastahili kupewa pole sababu unashabikia na kufurahia kitu usichokijua madhara yake.
You real touch my heart,

Umenisaidia sana wewe na mtoa mada, hili lazima niwaambie wanafunzi wangu, lazima tuongee haijalishi litapokelewa vipi and I used to tell my students as a teacher!!

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Hicho unachokisema ndio ukengeufu wenyewe. Jukumu la mwanamke ni kuzaa na kulea, hizo kazi mmepewa na wajanja na iko sababu ya kibiashara na kimapato ya serikali. Mwanamke anagawana majukumu na mune, mmoja nyumbani mwingine kazini. Ndio maana watoto wa siku hizi hawana malezi bora, kwa sababu mama anarudi saa nne usiku na baba pia. Wanawake mmejitwisha jukumu la wanaume, mkaacha jukumu lenu.

Kwamba wasio na kazi wana maisha mabaya si kweli, inategemea unatazasha vipi maisha. Wanawake wasio na waume nilioongea nao mimi hawana furaha wala amani hata kama wana kazi. Kazi sio kila kitu kwa mwwnamke ila dunia imejaribu kumwaminisha hivyo. Kwa mfumo sasa hakuna mwanamke tena, wote ni watafutaji tu. Mwanamke halisi atawazia malezi ya famikia bora kuliko kutafuta mali binafsi ndani ya ndoa.

Ukahaba kuwepo tangu kale ni kwa sababu wako wachache ambao hawakuzingatia maonyo. Na hiyo sio sababu ya kuendeleza ukahaba, misingi ya zama hizo haikushabikia ukahaba bali ilipinga kabisa, hivyo kauli yako ni mfu. Wanawake wengi wanaji expose kwenye system ya elimu, wanajikuta wameingia kwenye vitendo vya ukahaba kwani wanaanza kujitegemea wakiwa bdo hawako tayari.
Na wamenogewa kweli kweli kiasi kwamba wanaona hata ndoa ni uzushi tu 😂😂😂
 
Maslahi ya nani inamaana haujui !?? Takwimu zinaonyesha kuwa wanawake duniani wapo wengi kuliko wanaume so kitendo cha wao kubaki nyumbani bila ya kuwa naelimu ya juu wenye dunia yao walionao kwamba Rasilimali nyingi sana zinapotea kwa wao kuweza kukosa mapato ..so wakaona kwamba endapo wanaume na wanawake wote kwa pamoja watafanya kazi pamoja Jamii itakuwa na wanataaluma na wafanyakazi wengi na serikali zitapata Kodi kwa wingi tofauti na ilivuokuwa awali ambapo kazi zilikuww zinafanya na wanaume pekee

So wenye dunia yao wao wanataka hell tu that's why waliamua iwe hivyo Kama jamii zenu zinapata hasara kwa kuzalisha jamii yenye mnyumbuliko wa kimaadili wao they don't care wanachotaka wao Ni pesa tu 😁 ili waweze kufanya mambo yao kwa wepesi
Hili linapaswa kuwa mjadala wa kitaifa na hizi taasisi za kimataifa zinazotetea huwa zinafanya hivi kwa maslahi ya nani?
 
😂😂😂😂ivi kweli mimi nitake kuwa sawa na mwanaume nianze kufanya kazi ngumu kama za ukuli labda bandarini, nianze kubeba gunia la mahindi begani wakati nimepewa mbavu 01 tuu kati ya mbavu 12
Wacha niendelee na majukumu yangu ya kuzaa kwa uchungu, kupamba nyumba na kupika🤗🤗🤗
Jina lako tu me hoi 😋😋😊
 
You real touch my heart,

Umenisaidia sana wewe na mtoa mada, hili lazima niwaambie wanafunzi wangu, lazima tuongee haijalishi litapokelewa vipi and I used to tell my students as a teacher!!

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Pamoja mkuu Sambaza ujumbe ni muhimu sana, Western world tayari imeshatoka kwenye gender balance sasa wameingia rasmi kwenye gynocentrism, na hata sisi ndio tunakoelekea huko huko.
 
Back
Top Bottom