Mkuu
Nyenyere kuna mada Fulani ulipost hapo nyuma na kwa kweli nilitofautiana sana na mtizamo wako(na mpaka sasa natofautiana na wewe)
Lakini kwa mada hii ya leo nakuunga mkono asilimia mia moja na naomba niongezee hoja kadhaa hapa chini kuunga mkono mada yako
Mkuu kwa sababu ya mapinduzi yalifofanyika na yanayoendelea kufanyika kila siku,leo hii tunapata familia na vizazi vibovu kuwahi kutokea,kwa nini?
leo hii baba na mama wote ni wafanyakazi kuondoka aubuhi kurudi usiku,watoto wameshakula wamelala,anayeshinda na watoto ni dada wa kazi ambaye haijulikani anashindaje na kuwatendeaje watoto,mama anapoondoka anaacha tu maagizo dada utampa mtoto uji,utamwekea katuni,utahakikisha anafanya homework,mtoto ni wa dada wa kazi?dada wa kazi anajua thamani ya yule mtoto?akiharibika dada ana hasara yeyote?na akiwa mtu mzuri kioo cha jamii,ni kwa namna gani dada wa kazi anafaidika hivi kwamba atajitahidi kwa kadri awezavyo kumlea mtoto ipasavyo?
kwa mfano huo mdogo tu wale ambao wamewahi kuona madhara ya aina hi ya Maisha wataelewa nachokisema ila kwa wale ambao wanaamini njii hii ya Maisha ni sawa si ajabu huko mbeleni watu watakuja kuconfess humu (painful ad regret Confession)
Kiasili na kulingana na uumbaji mwanaume aliumbwa kutafuta kwa maana ya kwamba mke alipaswa akae nyumbani atunze watoto muda wote baba anapokuwa katika mihangaiko ya kutafutia riziki mke na watoto wake,ni aina hii yamaisha iliyofanya familia kadhaa za miaka kadhaa kuwa bora na kutokeza vijana wa kiume na mabinti wa kike wenye kutegemeka na kujiheshimu,mama walikuwa wakitumia muda wao mwingi kutunza watoto wao na kuwafundisha lilo sawa na lilo na kosa pia,haikuwa rahisi kwa binti au kijana kuharibika na mama shindwe kuona mbadiliko hayo na kutoa ripoti kwa baba ambaye angeshughulikia hali hiyo kabla mambo hayajaharibika kabisa
lakini leo poor us kuna uwezekano mtoto kashaharibika sana tu (labda kawa mvuta bangi,katoa mimba za kutosha,kawa shoga,kawa mlevi) na bado mama au baba hajui kuhusu yote hayo,watajua saa ngapi wakati wote wako kazini bize kutafuta pesa?nani atampa mwenzie ripoti kuhusiana na maendeleo ya mtoto? dada wa kazi? dada wa kazi wanawajua vizuri watoto wenu? inauma lakini kutokana na aina yetu ya Maisha ya siku hizi,inakuja kujulikana kuwa mtoto kafikia stage ya point of no return na hakuna kinachoweza kufanyika kumsaidia tena just kwa sababu mama na baba wote walikuwa bize kuzitafuta pesa,what for? Maisha bora,,,,Maisha bora yapi?kupoteza watoto wenu mkiwa mmebaki na pesa zenu nyingi??