Lizarazu
JF-Expert Member
- Aug 23, 2015
- 6,331
- 7,885
Lakini ktk kufanya kazi huko tusisahau tu kuwa watoto wetu wanatuhitaji sana..
Kwenye bandiko lako lote hiki ndio cha msingi ulichoandika.
Lakini ktk kufanya kazi huko tusisahau tu kuwa watoto wetu wanatuhitaji sana..
Hata mimi nimepigwa butwaa!!
Sio nyie tu wakuu, hata mie binafsi nimebaki hoi...!!Nimeshangazwa na kusikitishwa sana na mawazo ya huyu mwanamama.
Wanawake tufanye kazi tu jamani maana tusipofanya hakuna rangi tutaacha kuona. Kama mnavyojua wanaume wengi wamekuwa mafurushi hivyo za kuambiwa changanya na zako.
Lakini ktk kufanya kazi huko tusisahau tu kuwa watoto wetu wanatuhitaji sana.
Hakuna mfumo usio na faida ukakosa hasara.
Niliwahi andika andiko jinsi jamii ilivyopotezwa kwa kumuondoa mwanamke katika mfumo wake
Wemgi sana walipinga
Ila naona kumbe wapo wanaojua na kuyatambua haya
Andiko lako limenigusa sana mkuu, nikupe pole kwa yote yaliyokufika. Umenena kweli kabisa, ni kosakubwa sana kwa mwanamke kuiacha nafasi yake. Kazi ya malezi ya watoto ni jukumu la msingi la mke. Hili ni jukumu kutoka kwa muumba, ingawa leo hii wanawake hawalitaki kabisa. Biblia imeweka wazi kuwa wataokolewa kwa hilo:Sio nyie tu wakuu, hata mie binafsi nimebaki hoi...!!
Lakini sio jambo la kushangaa sana, maana wao wenyewe kujimwambafy ndio wanaona ufahari wenyewe!! So hivyo wanavyoleta leagues na waume zao, ndio mioyo yao inasema safi-nimefaulu!!
Na niwe tu mkweli, mie mwenzenu nimekuwa na chuki kubwa sana, juu ya huu upumbavu unaoendelea dhidi ya hawa viumbe!!.
Hakika huu upumbavu, unaharibu sana familia zetu...bila shaka waliouleta, walilenga kuisambaratisha kabisa jamii kwa ujumla. Maana unapomuharibu mwanamke mmoja psychologically, ni sawa na umeharibu wastani wa kuanzia watu wa3, katika jamii husika. Na hii yote inatokana na kwamba, kiumbe huyo ndio mwenye karama ya malezi ya watoto na faraja ya mumewe....sasa ikitokea ndio ameoza, hipi itakuwa fate ya hao watoto na baba yao?.
Hakika jamii inateketea sana, kwa matokeo ya hii hali. Na sisi wenyewe ni wetness wa hilo, hakika tumeona watoto wakiharibika kimalezi, huku wababa wakizidi kupukutika siku hadi siku!!
For sure inaumiza sana, honestly hata me binafsi ni mmoja wa waanga wa hii kitu. Hii kitu imeacha alama kubwa sana, katika familia yangu! Hapa nilipo now nimebakiza only one mechanism defence, dhidi ya sumu hiyo...and i don't know if nitaweza au nitachemka!
Ila very sad, hawa viumbe wenyewe hawayaoni hayo! Na hiyo yote inatokana na kwamba, udhaifu wao wa kwanza hupo kwenye UPOFU WA MAONO.
Hakika siku zote, hawa viumbe sio watu wanaoweza kukaa chini na kuliangalia well, jambo moja in and out. Then wakanyanyuka na ujumbe uliokamilika....
Ndio maana M/Mungu, hakawapa wao jukumu la malezi ya familia na sio uongozi wa familia. Maana uongozi wowote, unahitaji nguvu ya maono!
Sasa ukichukua hiyo hali ya upofu walionao, uka-plus na msimamo wa ubishi (msingi mkuu wa feminism), matokeo yake ndio hii hatari tunayoiona sasa. Hapo ni sawa sawa na kipofu, anayekataa kushikwa mkono na kuongozwa kule aendapo.......in fact you can guess, ni nini kitakachompata mtu huyo!
Lakini tusilahumu sana, maana tunaweza tukajikuta tunakufuru bure!
Why nasema hivyo?.
Hakika nasema hivyo, kwa sababu ukiangalia hili suala lilivyo.....unaona kama ni matimisho ya maandiko matakatifu ya kidini.
Mfano mzuri kwetu sisi wakristo:-
1: Tunaona zipo sehemu mbalimbali, zinazo muimiza mwanaume kuishi na mwanamke kwa akili.
Sasa jiulize kwanini mwanaume...??
2: Mwanamke upumbavu uvunja.....kwa mikono yake mwenyewe!
Pia jiulize, ni kwanini mwanamke...??
Note:
Tukumbuke kwamba hata yale, yaliokuwa yanaendelea kule Salem, yalikuwa ni part of plan ya Mungu wetu. Na ndio maana, hata msaliti....alitabiriwa kabisa kwamba atafanya utasaliti.!!
Basi kwa msingi huo, nadhani sisi wachache tulio angalau na mwanga, juu ya hiki kinachoendelea. Tujitaidi kufanya kadili tuwezavyo, kuzikumbusha jamii zetu juu ya nini kinaendelea. Na tusihishie tu hapo, inatubidi pia kuwekeza nguvu kubwa ya kuhakikisha, watoto wetu pia hawaji kuharibika na wao.
Ingawa its hard, lakini tujipe moyo.....we can. God is Good!
Mkuu, wapinzani wengi wametekwa na elimu mpya, hawayaoni maisha katika uhalisia wake. Wacha wapinge lakini ukweli utasimama tu.Niliwahi andika andiko jinsi jamii ilivyopotezwa kwa kumuondoa mwanamke katika mfumo wake
Wemgi sana walipinga
Ila naona kumbe wapo wanaojua na kuyatambua haya
Mkuu Lizarazu, dunia ya leo imajaa watu wanaofanana na wanawake, lakini si wake wa ndoa. Wengi wamejipa daraja ya vyombo vya starehe, hawajitambui wala hawayatambui na kuyakubali majukumu yao ya msingi.Wewe tayari inaonesha wazi mind yako iko crippled na misconception. Angalia jinsi unavyoutafsiri utumwa inashangaza kweli kweli.
Kwamba mwanamke yoyote asiyesoma basi huyo ni wa kuwa mtumwa tu na utumwa wenyewe ni ile hali ya kuwa tegemezi.. Very wonderful idea.
Kumbe mwanaume anayeoa mke atakaye mtegemea kama maandiko yanavyoelekeza basi mwanaume huyo aoi mke bali anaoa mtumwa.
Kwa maana hiyo kwa mwanamke kusoma ni kuukimbia utumwa na kutosoma ni kuukubali utumwa.
This is the most bizarre concept i have ever come across in my entire life and here is where I rest my case.
Nyenyere na hawa ndio wake zetu wasomi tulioandaliwa na wakwe zetu.
Hakika hawa wakwe zetu wanakwama sana kwenye malezi yao.
Hawa viumbe wenyewe, wanavielewa hata hivyo vifungu basi?!!Andiko lako limenigusa sana mkuu, nikupe pole kwa yote yaliyokufika. Umenena kweli kabisa, ni kosakubwa sana kwa mwanamke kuiacha nafasi yake. Kazi ya malezi ya watoto ni jukumu la msingi la mke. Hili ni jukumu kutoka kwa muumba, ingawa leo hii wanawake hawalitaki kabisa. Biblia imeweka wazi kuwa wataokolewa kwa hilo:
1 Timotheo 2
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹² Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu.
¹³ Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye.
¹⁴ Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa.
¹⁵ Walakini ataokolewa kwa uzazi wake, kama wakidumu katika imani na upendo na utakaso, pamoja na moyo wa kiasi.
Uzazi kwa mwanamke ni jambo muhimu kabisa baada ya ndoa, ndio maana kama hashiki mimba atahangaika mpaka kwawaganga kutafuta mimba. Uzazi wake utamuunganisha zaidi na mumewe na kumpa amani na furaha ya ndoa.
Neno linasema ataokolewa kwa uzazi wake, naam ndivyo ilivyo. Kwamba akijitahidi kuwalea na kuwafunza watoto wake kwa kadri ya njia ya kimungu. Watoto wake wakikua katika kumcha Mungu ni thawabu kubwa kwa mwanamke, ndipo waswahili pia wakasema asiyefunzwa na mamaye....
Mafunzo kwa mtotoni jukumu la msingi la mke wa ndoa, ndio maana ya neno hili:
Mithali 10
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹ Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye; Bali mwana mpumbavu ni mzigo wa mamaye.
Well said.Mkuu Lizarazu, dunia ya leo imajaa watu wanaofanana na wanawake, lakini si wake wa ndoa. Wengi wamejipa daraja ya vyombo vya starehe, hawajitambui wala hawayatambui na kuyakubali majukumu yao ya msingi.
Niseme wazi tu, mwanamke yeyote aliyelelewa kwenye misingi ya "ukombozi wa mtoto wa kike" amepoteza sifa ya kuwa mke wa ndoa. Huyu amelelewa kuwaindependent, hivyo hafai kumweka chini ya mamlaka, labda asubiri upepo wa kisulisuli ambako ataolewa bila sifa za mke.
Bahati mbaya kwao, wanawake wana wakati mgumu sana kuchagua destiny. Kadri anavyozidi kusoma sana ndivyo nafasi yake ya kuolewa inavyozidi kupungua. Na huu ni ujweli mchungu.
Kadri mwanamke anavyopata madaraka ya juu ndivyo nafasi yake kuolewa inavyopungua, anazidi kuwa lonely. Huu pia ni ukweli mchungu.
Kadri mwanamke anavyozidi kujikita kwenye biashara ndivyo nafasi yake kuolewa inavyozidi kupotea. Ni ngumu kwa mwanamke wa namna hii kumpata mume afaaye.
Mambo haya anayoyakimbilia mwanamke wa leo yamepishana na ndoa, ndio maana mabinti wengi wamebaki kusubiri upepo wa kisulisuli.
Kweli kabisa mkuu, tatizo ninaloliona kwenye nyumba za ibada ni mapato makubwa yanayotoka kwa wanawake. Kwa sababu ya uwezo wao mdogo kufanya reasoning, wamekuwa target ya watumishi wengi. Hii ni mbaya sana lakini ukweli inabido usemwe tu.Hawa viumbe wenyewe, wanavielewa hata hivyo vifungu basi?!!
Wengi wamebakia kuudhuria misa tu....na wengine wamefika mbali zaidi, hata kuona ya kwamba haya maandiko ya kidini, yapo outdated! Hivyo wao wanafata yale wayaonayo.....!!
Na naweza kusema shida inaanzia, kwenywe hizi nyumba zetu za ibada. Maana binafsi naamini, if kama hili suala lingepewa nguvu ya uratibu na nyumba hizo, am sure kwa kiwango kikubwa sana....jambo hili lingepungua au kupotea kabisa, kwenye uso wa dunia.
Na wala sitaki kuamini kwamba, hawa watumishi.....hawaelewi nini kinaendelea katika jamii zinazowazunguka.
Bali mie naona ni matokeo tu, ya mbegu ya ukengemfu ya ibilisi....!!
Honestly inaumiza sana....!!
Kwahio mie furushi tena?😃😃😃Wanawake tufanye kazi tu jamani maana tusipofanya hakuna rangi tutaacha kuona. Kama mnavyojua wanaume wengi wamekuwa mafurushi hivyo za kuambiwa changanya na zako.
Lakini ktk kufanya kazi huko tusisahau tu kuwa watoto wetu wanatuhitaji sana.
Hakuna mfumo usio na faida ukakosa hasara.
Umeolewa kwani? Hebu tuanzie hapoGombeni sana na kulalama sana ila mkumbuke mfumo usio wa haki unaoitwa mfumo dume ndiyo uliomfanya mwanamke kutafuta jinsi ya kujikomboa. Mfumo mpya mnaoulilia kuwa ni mbaya siyo mpya bali ni ule ule sema sasa una jinsi zote mbili na mkuki kwa nguruwe unakuwa mchungu. Huyu Mungu tunayemtaja hapa kuwa alimweka mwanaume kuwa mtawala na mwanamke mtawaliwa (if at all maana nakumbuka aliwatuma kutawala/kutiisha nchi) hakusema kumtawala mwanamke ni kumnyanyasa na kumdharau. Angetaka iwe hivyo angeumba mwanamke ambaye hana akili wala vipawa na angeweza kabisa kulea watoto wake kama wafanyavyo hayawani. Lakini kitendo cha kuwapa wote ufahamu na jukumu la kutiisha nchi alitaka hawa watu washirikiane kwa upendo kila mmoja katika nafasi yake na waheshimiane.
Kilichotokea ni mtawala kuwa mbinafsi na kutawala kidikteta - kusahau kuwa mwenzie ni binadamu kamili mwenye utashi na matamanio ya asili ya upendo na uhuru. Vipigo ni vya mwanamke, uduni ni wa mwanamke, kazi duni ni za mwanamke, matusi ya kudhalilisha ni ya kike. Yaani chochote cha mwanamke ni duni. Mwanaume akikosea anaambiwa anafanya mambo ya kike na akiambiwa hivi anaumia; mwanamke akifanya yampasayo mwanadamu kufanya anaambiwa anaigiza uanaume! Mwanaume ni mtu, mwanamke ni kiumbe. Kiumbe dhaifu. Mwanamke si kiumbe cha kufananishwa nacho. Ni fahari kufananishwa na simba au jogoo lakini si mwanamke.
Sasa mambo yamebadilika. Maendeleo ya Sayansi na uchumi yanasukuma mabadiliko katika mahusiano ya kijamii. Mfumo wa sasa hauruhusu mahusiano ya mtawala asiyejitambua na mtawaliwa asiyejitambua. Kujitambua ndo habari yenyewe - mtu mmoja mmoja mpaka taifa. Ukila na kipofu vizuri utakula muda mrefu na yeye ataridhika. Ukimdhulumu utampa fursa ya kujihoji na kuhoji kisha nafasi yako itatikiswa maana hukutumia maarifa bali kiburi cha kumiliki nyenzo za kutawalia (mali na elimu). Sasa huyu mnyonge baada ya kujitambua kuwa hastahili kutendewa vibaya anaanza harakati za kujikomboa. Naye anaanza kutaka kukaa alipo mtawala ili naye apate ahueni. Na ahueni anaipata kweli wala tusidanganyane kuwa mwanamke mwenye uhuru wa kimaarifa na kiuchumi ana tabu kama mwanamke ambaye hana hivi vitu na anajitambua lakini hana jinsi. Asiyejitambua hana shida. Jambo usilolijua halikusumbui. Ndiyo wife material naskia.
Sasa mwanamke akishapata nyenzo za uhuru hawezi kuenenda tofauti na mfumo kandamizi uliopo. Naye atakuwa mkandamizaji. Kwa hiyo mfumo dume na mfumo jike yote ni mifumo kandamizi. Watanyanyasika wanawake na wanaume wote ambao hawana nyenzo za uhuru. Kimsingi wanaume ni waathirika wakubwa zaidi kwani si rahisi kukaa kwenye nafasi ya "mtu duni" kwani anaathirika mara mbili: hana vyenzo za uhuru wala urahisi wa kupata mwenzi kwani nyenzo hizo ni vigezo vikuu. Mwanamke mwenye nyenzo za uhuru akikosa mwenzi anakuwa amekosa kitu moja, si vyote, na kama amevuka kiwango cha kushikiliwa kimaadili na jamii anaweza kutumia nyenzo zake kuwachezea wanaume walio kwenye nafasi duni. Uhuru si sawa na upweke. Sasa mwanaume ukose nyenzo za uhuru - upweke utakuhusu, manyanyaso yatakuhusu maana anayekuweka mjini ndiye anakuendeshea maisha. KILA MWANAMKE NA KILA MWANAUME ATAFUTE SANA KUJITEGEMEA KIAKILI NA KIUCHUMI.
Mwisho, mfumo sahihi wa kijamii ni mfumo wa haki (just). Tunaposema haki sawa kwa wote tunamaanisha binadamu wote ni sawa bila kujali ulemavu au jinsi ya mtu. Mfumo unaoheshimu utu wa mtu kwanza kabla ya kuja kwenye uanamke, ulemavu, utoto au uzee ndiyo mfumo bora. Mwanamke angechukuliwa kama mtu kwanza halafu mwanamke baadae tusingefika hapa. Pia tusichanganye mabadiliko ya kiuchumi na mabadiliko ya nafasi ya mwanamke. Mwanamke miaka mingi huko nyuma na mpaka sasa ni mzalishaji mkuu. Wa wakati ule alikuwa akizalisha karibu na nyumbani na anakwenda shamba na mtoto anamchimbia shimo anamuweka au anamuweka mgongoni. Lakini sasa shughuli za kiuchumi zimepanuka na makazi yamekuwapo ya vijiji na miji. Si jambo geni kwa mwanamke kuacha mtoto nyumbani na kwenda kutafuta. Mimi nina miongo minne sasa na niliachwa sana kwa mama mkubwa mpaka mama atakaporudi toka shambani au sokoni na alipokwenda kujiendeleza kielimu niliachwa kwa babu na bibi. Mama yangu mwenyewe mwenye miongo 7 alianza shule akiwa na miaka 10 kwa kuwa alikuwa akimlea mdogo wake wakati mama yake akizalisha mali. Tusichanganye mada. Kazi ndiyo utu. Tujipange upya zama zimebadilika.