sasa hivi kunywa hata soda ni anasaUkweli siku zote sijawahi kuwa na imani na serikali ya CCM wala stokuwa na imani na serikali ipo chini ya CCM. Jambo leo wameandika hali halisi kabisa kutokana na ugumu wa maisha kuzidi kuwa mgumu lazima watu wapoteze imani na Raisi.
Mwananchi pekee ndio wako neutral,kwa mbali labda na mtanzania.Mengine yaliyobaki Sina uhakika.Ili ujue mambo ,/facts yalivyo kwenye Siasa za Tz kukupitia media,ni lazima pia uwajue Wamiliki wa vyombohivo! Unakumbuka Jambo Leo Miezi 9 nyuma walikuwa wanaandikaje, Fuatilia pia uandishi wa Nipashe ulivobadilika miezi kama minne iliyopita! Hiyo ndiyo Siasa ,who get what,when and how! Siwapigii debe ,magazeti objective kwakiwango cha kuridhisha ni Mwananchi na Majira !na kiasi fulani Raia Mwema ! Vinginevyo fuata mrengo ima wa tanzania Daima+Mtanzania+wenzao ...au Uhuru/habari Leo+ Raia Tanzania ....!
wanajua wazee wa lumumba nyie siku zote ukweli kwenu ni sumunashukuru kwa marekebisho maana mi nilikuwa najua inaandikwa raisi, swali lipo palepale kwa nini wameandika 'rais' na sio rais wanamaanisha nini.
Kusema ukweli, maisha yamekuwa magumu maradufu kwa watu wote, watumishi wa umma ndio usiseme, wananchi wa kawaida ni kelele biashara haziendi....
Mh. Rais aangalie hali hii inakuaje, maana hali mbaya sana mitaani
mwenyewe nimeshangaa labda wamegundua wakiandika habari za kusifia serikali hawauziUmenifanya nkalitafute nijue ni nini kimo ndani maana hawa kipindi cha nyuma walkua wako side ile
Fikiri kwa mapana, 'rais'; sio rais.Kweli kabsa hatuna imani na rais
Predictability ni moja ya nguzo za kiongozi bora; kwa JPM mimi nimeachwa chaka kabisaaa!Hawajadanganya mana siku hizi hatumuelewi anachokisimamia ni kipi
Haijalishi. Wamiliki wa hili gazeti na mhariri wake ni lazima tuwasaidie kufikiri ama kwa hiari ama kwa lazima. Tanzania haiwezi kuwa kijiwe cha wakaanga sumuanza
anza na anco ben mwambie arudishe NBC yetu
Hiyo ni tricky ya lugha tu na utata huo umeachwa makusudi ili kuwaokoa kwa kile walichokihofu baadae na ni lazima ile kwao. Watachezea akili za wapuuzi na si saikolojia zetu. Kusudi la kuandikwa hivyo na nia yao ni ile ile ijapokuwa imeachwa herufi moja ili kuzugiaFikiri kwa mapana, 'rais'; sio rais.
interestingNipo huku kijijini msibani wanakijiji waliokua washabiki wa ccm kindakindaki hawana hamu na hii serikali hadi raha, wanadai no money circulation biashara zao wengi wamekata mitaji na wengine wametoa watoto wao kwenye shule binafsi kwa kuwa hawana pesa tena za kulipia ada, wananchi wengine wanalalamika ndugu zao waliokua wanawapa misaada mbalimbali baadhi yao wameacha kuwasaidia toka mjini na wengine wamepunguza misaada kwa %90 hawa waliopunguziwa misaada wengi ni wazazi wa watoa misaada na wengi hawataki kusikia hata neno magufuli, kuna jina wamempachika siwezi andika hapa make sina milioni kumi za kuchezea.
ni kweli wanakijiji wamechoka na wengi wanadai ikipigwa kura wapo radhi kumpigia hata mbwa kuliko kumchagua tena huyu tena, niliwauliza baadhi yao kwa nini walimchagua wakadai walitishwa kuwa wakimchagua mpinzani kutatokea vita na lowasa ni mwizi atawauza hadi wao na watahamishwa kusikojulikana.
Nikawauliza akitokea huyu mwizi mtamchagua? wakadai kwa hali ilivyo sasa wako Tayari kuchagua kitu chochote ili mradi huyu atoke madarakani, wewe mwanangu angalia nilivyo konda na sasa hivi ndio ana miezi nane, akimaliza miaka mitano je? Si nitakufa? Nimemnukuu mama moja wa makamo.
CCM wasipofanya marekebisho ya kiutawala natabiri hii ndiyo serikali itakayochokwa kwa mda mfupi kuliko serikali ya kikwete.
kwani walichoa andika ni uongo,labda mwenzetu unaishi new york huyaoni ya TanzaniaHaijalishi. Wamiliki wa hili gazeti na mhariri wake ni lazima tuwasaidie kufikiri ama kwa hiari ama kwa lazima. Tanzania haiwezi kuwa kijiwe cha wakaanga sumu
yawezekana mauzo ya leo yatapaa kuliko ya siku zote maana kila mtu anataka kujua nini kimeokeaHili gazeti lilikuwa linamilikiwa na Juma Pinto swahiba wa Ridhiwan sijui kama hadi leo analimiliki.
Wakati wa awamu ya nne lilikuwa pro Kikwete na serikali yake sielewi hii U-turn ya ghafula imetoka wapi ya kuanza kupingana na rais na serikali yake.
Lazima kuna maslahi ya watu yameguswa na hii tumbua tumbua.