Jambo lipi ni muhimu kufanya ili kumuinua kielimu kijana ambaye ni taifa la kesho?

Really Kamodo

New Member
Jun 8, 2020
1
0
Tumekua tukikalilishwa sana Watanzania kwamba elimu ni ufunguo wa maisha. NDIYO Elimu ni ufunguo wa maisha, lakini pia tukumbuke kwamba Elimu hiyo tunayowapa vijana wetu inawajenga vipi kifikra vijana wetu.

Je, inawasaidia au ndio inawaharibu kisaikorojia?

Tunajua hakuna jambo lenye faida tu, pia tuna takiwa tujue hasara ya kua na elimu. Kwasababu, elimu ni kupandikiza kitu ambacho hakipo kwenye kichwa cha mtu. Sasa kama ni hivyo, Je tukipandacho kitamea kwenye mazangira salama?

Na je, kitakua na faida pande zote? Nina maana kwa muhusika pamoja na jamii yake inayomzunguka.

Lakini pia tunatakiwa tujue je muhusika amapokeaje kile anachopewa(anachofundishwa).

Kwasababu tunapotoa elimu yoyote ile tunatoa bila kutoa faida na hasara zake kwa tunaowapa elimu.

Yaani tunawapa faida ya elimu bila ya kuwajulisha pia kua kuna hasara zake. Naamini elimu ina hasara zake pia pamoja na kwamba ni ufunguo.

images (54).jpeg


Serikali ifanye mpango kuandaa elimu ambayo itakua na faida za moja kwa moja kwa kijana taifa la kesho, ili kujua moja kwa moja kijana anahitaji nini ili aendelee kuona faida zaidi za elimu yake.

Kuliko kukandamizwa asome masomo tisa ambayo baadae yatamfanya ashindwe kujua yeye ni nani haswa na anatakiwa afanye nini. Tofauti na mfumo wa sasa ulivyo. Hadi ukifika chuo hujui kitu halisi ambacho ndio maana halisi ya wewe.
 
Back
Top Bottom