Mpango wa maendeleo ya nchi ni lazima uzingatie mkakati wa kutatua suala la ukosefu wa ajira

ong'wafaza

JF-Expert Member
Apr 30, 2012
243
100
Nimekuwa nikifuatilia mjadala wa Mpango wa maendeleo uliosomwa Bungeni katika kikao kinachoendelea hivi sasa huko Dodoma.

Pamoja na mambo mengi mazuri ambayo mpango umekuja nayo, ningeshauri swala la ukosefu wa ajira liwekewe mkakati maalumu wa kulitatua.

Itakumbukwa kuwa Serikali imewekeza sana kwenye swala la elimu kwa wananchi wake kupitia ujenzi wa shule na vyuo vya elimu katika ngazi mbalimbali nchini. Matokeo ya hili ni kutengeneza taifa lililoelimika na ni jambo jema.

Lakini tukumbuke pia kwamba hakuna jambo jema lisilokuwa na mabaya yake, kadhalika hakuna jambo baya lisilokuwa na neema.

Je, tulishawahi kujiuliza na kupata jibu ni madhara gani kuwa na taifa la wasomi wasiokuwa na ajira?
Pengine ni vigumu kuwa na jibu la moja kwa moja kwenye hili bila kufanya utafiti.

Lakini kwa tuliosoma Cuba tunafahamu kuwa Taifa lenye wasomi wengi wasiokuwa na ajira za uhakika ni hatari zaidi kuliko lile lenye wajinga wengi hata kama hawana ajira.

Kwa mkhtaza huo,napenda kutoa angalizo pia kwamba ajira chache zinazopatikana zisilenge kundi au jamii fulanifulani tu kwani kuna hatari pia ya kujikuta jamii inagawanyika katika makundi ya walio nacho na wasio nacho, hata kama ni baada ya miaka mingi ijayo.

Kwa hiyo, nashauri katika Mpango wa maendeleo uje na sera zinazolenga kukuza ajira na pia kuunda mfumo mzuri wa kusambaza ajira hizo miongoni mwa Watazania wote tofauti na jinsi ilivyo sasa.
Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom