Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,341
- 51,907
KAMA KIJANA MTAFUTAJI NI MUHIMU KUJIUNGA NA JUMUIYA MAHALI UNAPOISHI
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
Umeenda mbali na nyumbani, ni aidha kutafuta maisha au umepelekwa na serikali. Moja ya mambo muhimu kabisa ya kufuata ni pamoja na kujiunga na jumuiya za kijamii.
Kama ni mkristo nenda Kanisani. Kama ni muislamu nenda msikitini huko. Fuata mambo ya dini yako kwa bidii na juhudi huku ukiendelea na harakati zako za maisha.
Kama wewe sio muumini wa mambo ya dini. Jiunge na jumuiya za kabila lenu ambalo lipo mahali anapoishi. Changia kulingana na uwezo wako.
Ni kweli unahitaji faradha lakini hiyo haimaanishi ati ujifiche kwa kiwango cha kutisha.
Ni kweli labda mahali anapoishi sio pazuri. Haujajipata vizuri kiasi kwamba unaona aibu kukaribisha wanajumuiya wenzako Ghettoni kwako. Lakini hiyo haikuzuii kutojiunga na jumuiya.
Jumuiya zinafaida na hasara zake. Lakini faida ni nyingi zaidi.
Ni rahisi kupata msaada ukiwa ndani ya jumuiya kuliko ukiwa jeshi la mtu mmoja.
Vijana wengi ambao wanaomba pesa mitaani au kwenye mitandao ya kijamii wengi wao hawapo katika jumuiya hizi aidha za kidini au kikabila.
Shughuli za mtaani kwenu hushiriki. Viongozi wa serikali za mtaa hawakujui kwa sababu hushiriki wala huna Tija yoyote kwenye huo mtaa. Haipo hivyo vijana. Kijana lazima uwe na Tija.
Kijana unajifanya unataka kuishi maisha ya kijasusi wakati majasusi wote moja ya kanuni zao ni kushiriki na kujichanganya na jamii. Ati wewe unajifanya hutaki mazoea na Watu wa mtaani kwako. Kwa kipi hasa?
Ukitoka Kanisani au msikitini, Nduki! Hutaki hata Watu wasalimiane na wewe na wala wewe huna habari za Watu. Umechizika wewe. Mantiki ya jambo hilo ukifuatilia ni kutokujiami, na inferiority complex ya kutotaka Watu wakujue kwamba wewe bado hujajipata, wewe bado ni njaa.
Hivi unafikiri ukiwa hujajipata ni siri? Au unafikiri ukijipata nako ni Siri.
Kuwa na Tija. Hakikisha Watu wanafurahia uwepo wako. Wajue huyu ni kijana/ Binti Haswa.
Hata wazee wakikuona watamani uoe binti zao. Au uolewe na vijana wao.
Sio upoupo tuu. Mambo hayaendi hivyo.
Kufanya kazi zenye kipato duni haikupunguzii heshima yako. Ifanye kwa furaha na kuipenda Watu nao wataipenda na kukupenda. Sasa unaishi mtaani hutaki Watu wajue unafanya kazi gani kwa mantiki ipi? Unaogopa dharau, ukiwa na akili hizo bado utaonekana haujakua.
Moja ya dalili kuwa umekua Watu wanachoangalia ni ufanyaji wa kazi. Je unafanya kazi? JE unafanya kazi kwa weledi, je unaipenda kazi yako?
Unajificha nini? Hujafunzwa kujiamini sio? Unaogopa hutapata Mwanamke mzuri wa kumwoa. Mbona sisi wengine tumeoa wake wazuri pasipo hizo kazi nzuri, pasipo hizo pesa ambazo wengi wanasema wakizipata ndio waoe Wanawake wazuri. Hatuna magari wala nyumba lakini tunafurahia maisha.
Vijana hakuna mtu anayeweza kukudharau kwa kufanya kazi halali. Hakuna mtu atakayeweza kukudharau kwa kuwa muadilifu. Hakuna! Wewe tuu ndio haujiamini.
Tumia kila kipaji, Karama, ujuzi uliojaliwa na Mungu uwe na Tija katika jamii yako.
Elewa, unapoanza utaanzia chini, chini ndipo utakapojitambulisha.
Ukipatwa na shida ni rahisi kusaidiwa na kusaidika. Unapiga simu moja tuu. Kila mtu anatamani kukusaidia na anajisikia raha kuwa moja ya Watu aliokusaidia.
Zingatia, haufanyi hayo ili upate faida ya msaada baadaye siku yakikukuta. Bali unafanya hivyo kwa sababu unapenda kuwa na Tija. Yaani uwepo wako uwe na Matokeo chanya kwa wengine bila kujali watakusaidia au laa.
Acha Nipumzike sasa.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam