Mimi nina shida na viporo. Sikumbuki ni kati ya 2001 au 2002 nilikuwa naelekea mbeya nikitokea dar,.asubuhi hiyo sikuwa na mpango wowote wa kusafiri nivyo nikaamka na kiporo cha ndizi nikafanya yangu, namaliza tu, kaka mkubwa ananiambia dogo jiandae nikuagize mbeya mara moja, yaani utadhani ananiagiza kimara tu, nikaona huyu mkubwa vipi? Ila ndo mkubwa sikupinga, c najua naenda na kesho narudi nikachomoka vile vile nilivyo, sasa nilipofika ubungo tumbo likaanza udwanzi, nikanunua konyag nikapiga nusu, likatulia, dah kufika kibaha ndugu msomaji vile virasta kipindi kile bado vimedinda, gari ikipita juu ya rasta naskia kama vitu vinatoka, nilikuwa nimekaa na afande mmoja pembeni yangu, ananichora tuu, mimi nimefungua kio mpaka mwisho upepo wa kutosha lakini natoka jasho mpaka nguo zimeloana nimetoa macho kama kasa, situlii, yule afande anauliza bwa mdogo vipi? Namjibu poa tumbo lanisumbua, sasa muonekano wangu kidogo ulikuwa sio, kwanza nilikuwa nimebana manywele kwa nyuma, jicho nyanya sasa yule bwana akajua mimi nimebeba mzigo, chombo ilipofika Chalinze ikaamliwa niingie kule kituoni nikachekiwe kidogo maana sieleweki, dah basi ile kushuka tu nikapokelewa na pomoka kama nne hivi, dah sitosahau nimeingia toilet nimesimamiwa na mtutu, wao wanajua nna mzigo kumbe mwenzao kiporo kinaniendesha...kifupi safari yangu iliishia chalinze hata huko mbeya si kufika