Niliaibika mbele ya demu wangu nikiwa form one, huyu mrembo nilimpata baada ya mhula wa kwanza kupasua marks za juu kabisa karibia masomo yote. Sasa mtoto akajirengesha mwenyewe sikutaka kuonekana mwanakijiji nikasema mungu ni mwema.
Sasa siku moja kaka yake alisafiri maana walikuwa wanaishi na kaka yake ambaye alikuwa mwalimu wetu wa physics, mrembo akasema leo wakati wa lunch lazima ukapaone kwetu, mm nikasema mbona fresh tu.
Tukaondoka zetu mdogo mdogo, kufika home mtoto akakimbia fasta duka la jirani akanunua half cake mbili zile zinakuwaga vikaratasi kwa chini na soda halafu akaingia chumbani kama dakika 5 hivi.
Aisee nilikula cake pamoja na vile vikaratasi vyake huku nashushia na soda, alitoka chumbani na kunikuta namalizia cake ya mwisho na vikaratasi vyake. Akashangaa kishenzi niligundua kuwa kuna kitu nimefeli ila ningefanyaje sasa nimeshakula tayari.