Mie nakumbuka juzi kati nimekata ticket yangu bus fulani maarufu sana, natokea mkoa flani kanda ya ziwa naenda Dar.
Mambo yalikua poa nimefika kwenye bus nikapanda fresh tu nikakuta mtu ambae atakua jirani yangu ni njema moja kauzu kauzu.
Nilipofika nilimsalimia hakujibu (nikaona poa tu kama tutakaushiana safari nzima lazima wote tunuke midomo) nikaendelea na mambo zangu.
Gari ilipoanza kutoka tu stand yale mataa mengi mengi mle ndani yakazimwa(ilikua kumi na mbili asubuhi) ukabaki mwanga fulani hivi hafifu
Mara ghafra jamaa akaanza kuswali(hapo mie nipo seat ya dirishani)
Kuswali wakati wa safari(kuomba dua) si kitu cha ajabu hasa kwa imani ya wenzetu, ila kwa style jamaa alivyokua anaswali mie presha ikaanza( kipindi hicho ni muda mfupi tu kulitokea shambulio la magaidi hotelini Nairobi, ilikua imepita wiki nadhani)
Style ya jamaa kuswali alikua anainua mikono juu, anazungumza maneno ambayo siyaelewi kisha anapitisha mikono machoni akiendelea kutamka maneno fulani kisha akimaliza anageuka nyuma kama vile anamuangaza mtu.
Alipiga mara ya kwanza nikaona poa.
Mara ya pili nikaona poa
Mara ya tatu nywele zikaanza kusisimka.
Akili ikaniambia hebu mtazame vizuri ile namchek jamaa ana kimfuko flani hivi kakipakata, bwana bwana bwanaaaa! Shetani mbaya sana maana baada tu ya kuutazama ule mfuko akanishawishi niamini kuna kifaa kipo ndani ya ule mfuko tena kinawaka taa nyekundu.
Baada ya vile mie natetemeka na jasho linanitoka. Nikawaza fasta ni bora nipoteze hela ya nauli kuliko uhai, nikapanga nisimame nimuite konda kwa nguvu mpaka asikie akija namwambia nimepata dharula nataka kushuka hapo hapo, lakini nikajiuliza vipi kama nikitaka kutoka jamaa ndo akaamua kukibonyeza kitufe ngoma ikalipuka?
Nikasita kufanya vile, nikachukua ticket nikaangalia namba za simu kisha nikaandika meseji hahaaaaaaaa! (Siri yangu niliandika nini) Meseji haikujibiwa hahahahaaaa!
Nikakaa kama dk tano jamaa anaendelea tu na yale mambo na kumbuka hapo ni kama dk20-30 jamaa anafanya kile kitendo.
Nikaona kama mbwai mbwai,
Nikasimama nikaita kondaaa kondaaa kondaaaa! Mpaka abiria wote wakashtuka
Konda kaja mbio mbio hajui nini kinaendelea
Alipofika nikajikuta sina cha kusema, mdomo mzito watu wote basi zima wananitazama wanasubiri kujua nini kinanisibu
Konda akaniuliza vipiii?
Mie nimetoka macho namtazama tu
Abiria wa kucheka wakacheka, wengine wakasema labda nina msongo wa mawazo, na wa kutukana wakatukana sanaaaa
Ile njemba nayo ikaniuliza(nilipopiga kelele iliacha kuswali) vipi kuna tatizo, nikakataa kwa ishara tu, konda akamaind kichizi akasepa zake.
Mie nikakaa tena kwenye siti nikajiona booooonge la mjinga, njemba nayo ikaanza kunidadisi kwa maswali mengiii kama nina matatizo mie nikakaa ila tukawa washkaji tunapiga stori mpaka tunafika Dar saa saba usiku. Ila nilijiona mjinga kichizi siku hiyo