Mi Mara nyingi nakaaga na wanawake wenzangu loh!
Ilaaa....
Kuna kipindi nilikaa kwenye basi na mkaka pande la mtu, nikajisemea....mhh, kumbe limeoa, kuangalia kidole lina Pete, niliiskia hasira.
Alipo niomba no nikamwambia sitowagi no kwa waume za watu[emoji23].tena hapo Niko serious[emoji16]
Siku nyingine nasafiri na fast jet, kuingia Nina vibegi vitatu vidogo, kufika kwenye siti yangu, hakuna mtu, nikiangalia wengine wamekaa na watu, nikafyonza kimoyo moyo.
Nikaanza kuweka vibegi vyangu kule juu, si kimoja kikawa kinagoma, najaribu kuongeza urefu wapi, basi mkaka katoka siti Jiran kaja kunisaidia, loh nilicheka kama fala alivyokuwa smart sasa.
Nikajisemea kimoyomoyo huyu boya lazima aniombe no, maana safari yote alikuwa ananikodolea macho.
Wakati wa kushuka, akaja akanitolea vibegi vyangu, nimkamzoom kama ana Pete hana,
Akanisaidia ki bag kimoja kufika nje nikawa nawasiliana na anaekuja kunifata, yule kaka yupo pembeni mwangu ananikodolea haniombi no ,
Yaani alikuwa domo zege, nikawaza Wenda msukuma. Mpaka natoka pale ananikodolea aongei kitu dah!
Sijui aliogopa watu wasimsikie akiomba no, jinga sana yule boya.
Kuna mida ulinambia simama nikasima, alipofika hukunambia kitu.jinga sana.