Queen Horse
JF-Expert Member
- Sep 12, 2013
- 414
- 317
- Thread starter
-
- #121
Queen Horse umenipasua pwaaaaa......
Kumbe rafiki yako kaja kukuambia yoote? Leo atanitambua na tabia yake ya kuanika mambo ya ndani..... Hivi vyuo vya katavinatuharibia wanawake..
Atakuja kufarijiwa na mchepuko soonNakwambia acha bibie mpaka kaloose weight chezea manyanyaso ya kauli wewe.. Anakula vizuri, analala vizuri, usafiri upo ila akimfikiria mumewe nguvu zinaishaa anakosa hata amani ya kumwambia mambo yanayomuhusu
Badilika mkuu siyo poa unavyomtendea wife...Queen Horse umenipasua pwaaaaa......
Kumbe rafiki yako kaja kukuambia yoote? Leo atanitambua na tabia yake ya kuanika mambo ya ndani..... Hivi vyuo vya katavinatuharibia wanawake..
Mwidiwee.. Namahorooo wana JF
Bado Niko najiuliza maswali juu ya wanaume wasomi hasa hasa kuanzia level ya masters, PhD hadi kule kwenye ukuta ulioandikwa elimu tena basi kwanini wengi wao wanakuwa wanatabia ya kupenda kuwadharau wake zao hasa ukikuta wamewapita kiwango cha elimu mfano mke ana diploma yake ya ualimu au digrii yake ya course ya kuchechemea.
Naongea hivi kwa experience kwa sababu nimekutana na kesi kama tatu zenye kufanana lakini hii ya nne too much.
Haya yamemkuta shosty wangu mmoja hivi mwenye degree yake ya sociology na GPA ya kuchechemea na mchuchu wake mwenye PHD ya mambo ya planning.
Sikutaka kuchukua details nyingi kwa sababu elimu yake hainisaidii wala kuniletea hela ya ugali
Back to the topic, shosty kipindi kabla hajaolewa mapenzi yamechanua kama maua ya saa nne alikuwa anajisifia kweli na mchuchu wake mara wanaume waliosoma sana waelewa sana, Mara mimi degree holder wenzangu nimpeleke wapi.
Maneno kibao kudharau waume za wenzie na kujifanya wa kwake ndio bora sana kama tunavyojua masikini akipata masaburi hulia mbwata, sie tena wenye vicertificate holder vyetu tukawa tuna zip our mouth shut tunajipa moyo maisha hayapimwi kwa wingi Wa makaratasi ya vyeti.
Basi bwana Shoga yule mwaka juzi kaolewa kwa shangwe na vigelele na sisi mashabiki kama kawa tupo mbele kumpa kampani, ndoa sasa ina miaka mitatu ndo anaona chungu ya ndoa mkaka kawa na dharau kila analoliongea mkewe sharti liwe prove intelectually with high thinking capacity, akikosea kidogo matusi najuta kukuoa kilaza mkubwa wewe degree yenyewe umeipata kwa bahati, mara mimi siwezi kukaa na kujadili maisha na watu ambao sio ma critical thinker, mara sasa utanishauri nini wewe na akili yako ndogo na maneno mengine ya maudhi.
Sasa juzi ndo ilikuwa komesha shoga kaingiza loss katika biashara ya familia ambayo mkaguzi ni Mr.
Alioona junijulai alitukanwa mpaka aliiona ardhi ngumu kuikanyaga kupooza machungu kabaki anatupigia simu mashoga zake kutupa mkasa na maneno ya najuuta kibao nikamwambia shoga vumilia ndo ndoa ilivyo vumilianeni kila mtu ana kasoro zake.
Back to my question: kwani mahusiano yanahitaji akili ya kukariri vitabu?
Kama mnaona vitabu ni mali si mngekaa single mkaendelea kukariri.
Najua wengi mko humu wenye hizo tabia acheni dharau ishini na familia zetu kwa amani, kama mkeo ana weakness mu encourage aweze vile unavyotaka kumnyanyasa kisaikolojia sio vizuri.
Unasababishia makovu moyoni ambayo inawezekana hata we huyajui.
sa kama amekosea asiambiwe, umeleta hasara kwenye biashara unataka nikubembeleze tena.... hiyo kitu haipo, tusipokuwa wakali mtatupanda kichwani, lazima upige biti ata kidogo!!! Ilitakiwa ampe na vibao hata viwili kabisa sio maneno matupu
Ni kweli kabisa nimeshuhudia hii kitu. Alafu mtu wa namna hii si kwa mkewe tu ila mkewe ndio anakua mhanga namba moja. Na mtu wa namna hii kila kosa hata la kibinadamu ambalo naye humtokea huwaona wengine wajina ila akifanya yeye atalaumu mwingine sababu yeye hawezi kukosea. Na hata siku moja hawezi kuwa na kasoro kwamba inabidi ajirekebishe hapana, wengine ndio inabidi wajirekebishe na wengine ndio wanamuhitaji hata mkewe yeye hana shida nao. Ila malezi pia huchangia, na umasikini sababu mwengine si msomi ila ametokea kwenye ufukara lakini akafanikiwa alafu aoe mke aliyetoka tu hata familia ya kawaida basi atamnyanyasa mpaka basi. Kikubwa wanawake tuchunguze kabla ya kuingia ndoani, na mtu anayekudharau na kukuabuse kwa maneno au vipigo kamwe hawezi badilika hivyo ukiona dalili hizi ni vema kusonga mbele unaweza kuumizwa mpaka ukajiua kwa depression.Aise mpe pole sana, kuna watu wapo hivyo, ni selfish na insecure, yaani ni mtu kasoma lkn ana low self esteem kwa hiyo ili ajiskie vizuri na kujiamini lazima atafute mtu wa kumput dowm sasa yeye kaona ni mke, na watu wa mimi, mimi, mimi, hawafanyi effort yeyote kusaidi wanaonaga matatizo yapo kwa mtu mwingine, hata kitandani wakiunder perform ni rahisi kusema mwanamke ndo anasababisha ila wao hawana kasoro..
Kumbe BAKITA nao wamo humu.... safi sana.
Yaani kama uliingia mdomoni kwa huyo mkaka uka copy na kupaste.... Yaan anajiona yeye ndo muhimili wa Shoga angu mie bila yeye nyumba itaanguka.. Inafika stage anamwambia shukuru mungu umezaa na intellect kizazi chako kitakuwa na watoto wanaojielewaa ungezaa na vilaza wenzio ungetoa waokota makopo.. Mmh kweli is it fair??
Ni kweli kabisa nimeshuhudia hii kitu. Alafu mtu wa namna hii si kwa mkewe tu ila mkewe ndio anakua mhanga namba moja. Na mtu wa namna hii kila kosa hata la kibinadamu ambalo naye humtokea huwaona wengine wajina ila akifanya yeye atalaumu mwingine sababu yeye hawezi kukosea. Na hata siku moja hawezi kuwa na kasoro kwamba inabidi ajirekebishe hapana, wengine ndio inabidi wajirekebishe na wengine ndio wanamuhitaji hata mkewe yeye hana shida nao. Ila malezi pia huchangia, na umasikini sababu mwengine si msomi ila ametokea kwenye ufukara lakini akafanikiwa alafu aoe mke aliyetoka tu hata familia ya kawaida basi atamnyanyasa mpaka basi. Kikubwa wanawake tuchunguze kabla ya kuingia ndoani, na mtu anayekudharau na kukuabuse kwa maneno au vipigo kamwe hawezi badilika hivyo ukiona dalili hizi ni vema kusonga mbele unaweza kuumizwa mpaka ukajiua kwa depression.
Mtasingizia na jirani zangu bure lkn tatizo ni huyo dada.........
Kuleta loss isiyo na maelezo ni sawa na kuukaribisha umaskini ktk familia!!!!!!!! hii ni inatokana na kutoa hela za biashara kufanyia mambo binafsi