Mwidiwee.. Namahorooo wana JF
Bado Niko najiuliza maswali juu ya wanaume wasomi hasa hasa kuanzia level ya masters, PhD hadi kule kwenye ukuta ulioandikwa elimu tena basi kwanini wengi wao wanakuwa wanatabia ya kupenda kuwadharau wake zao hasa ukikuta wamewapita kiwango cha elimu mfano mke ana diploma yake ya ualimu au digrii yake ya course ya kuchechemea.
Naongea hivi kwa experience kwa sababu nimekutana na kesi kama tatu zenye kufanana lakini hii ya nne too much.
Haya yamemkuta shosty wangu mmoja hivi mwenye degree yake ya sociology na GPA ya kuchechemea na mchuchu wake mwenye PHD ya mambo ya planning.
Sikutaka kuchukua details nyingi kwa sababu elimu yake hainisaidii wala kuniletea hela ya ugali
Back to the topic, shosty kipindi kabla hajaolewa mapenzi yamechanua kama maua ya saa nne alikuwa anajisifia kweli na mchuchu wake mara wanaume waliosoma sana waelewa sana, Mara mimi degree holder wenzangu nimpeleke wapi.
Maneno kibao kudharau waume za wenzie na kujifanya wa kwake ndio bora sana kama tunavyojua masikini akipata masaburi hulia mbwata, sie tena wenye vicertificate holder vyetu tukawa tuna zip our mouth shut tunajipa moyo maisha hayapimwi kwa wingi Wa makaratasi ya vyeti.
Basi bwana Shoga yule mwaka juzi kaolewa kwa shangwe na vigelele na sisi mashabiki kama kawa tupo mbele kumpa kampani, ndoa sasa ina miaka mitatu ndo anaona chungu ya ndoa mkaka kawa na dharau kila analoliongea mkewe sharti liwe prove intelectually with high thinking capacity, akikosea kidogo matusi najuta kukuoa kilaza mkubwa wewe degree yenyewe umeipata kwa bahati, mara mimi siwezi kukaa na kujadili maisha na watu ambao sio ma critical thinker, mara sasa utanishauri nini wewe na akili yako ndogo na maneno mengine ya maudhi.
Sasa juzi ndo ilikuwa komesha shoga kaingiza loss katika biashara ya familia ambayo mkaguzi ni Mr.
Alioona junijulai alitukanwa mpaka aliiona ardhi ngumu kuikanyaga kupooza machungu kabaki anatupigia simu mashoga zake kutupa mkasa na maneno ya najuuta kibao nikamwambia shoga vumilia ndo ndoa ilivyo vumilianeni kila mtu ana kasoro zake.
Back to my question: kwani mahusiano yanahitaji akili ya kukariri vitabu?
Kama mnaona vitabu ni mali si mngekaa single mkaendelea kukariri.
Najua wengi mko humu wenye hizo tabia acheni dharau ishini na familia zetu kwa amani, kama mkeo ana weakness mu encourage aweze vile unavyotaka kumnyanyasa kisaikolojia sio vizuri.
Unasababishia makovu moyoni ambayo inawezekana hata we huyajui.