Munkari
JF-Expert Member
- Feb 9, 2013
- 8,084
- 4,363
I have masters my wife is std 7 and respect her seriously and she understands it.
Congratulation.!!
I have masters my wife is std 7 and respect her seriously and she understands it.
Cku zote maisha ya mke na mume yanatakiwa yaanzishwe na watu wawili wenye uwiano unaokaribiana kimtazamo, Socially,Agewise, Spiritually, Education wise na mengine mengi ,Ili mnapoishi muweze kuendana.Mfano labda wewe elimu ndogo kiasi halafu tena ukaoa mke ambaye hata smart phone hawezi kutumia!Ni wazi kuwa mtatofautiana.Suala la kuoa hatuangalii mapenzi tu .Inashauriwa uchumba uchukue muda mrefu kiasi ili kujuana kwa undani.
Mi nafikiri hiyo dharau na majigambo haitokani na hiyo elimu ni tabia tu mtu anakuwa nayo sema huyo elimu ndo imekuwa fimbo ya kumchapia mkewe.
Tatizo huja hivi, kwanza rafiki yako kutokana na digrii yake alijiona mjuaji tangu awali. Alipokutana na huyo mumewe akaendeleza ujuaji japo jamaa bila shaka alikuwa akimsoma. Kwa kuwa hawakuwa wakiishi pamoja jamaa hakujua undani wa mwanamke. Walipooana ndio jamaa akaanza kumjua. Pengine alimvumilia awali lakini bado mwanamke alileta ujuaji. Wanawake wasomi wajuaji sana hata kama hawajui. Sasa naona jamaa kachoka ujinga wa mkewe na kumtolea uvivu.
tatizo laweza kuwa huyo dada hajajua tatizo lake ambalo ni kujikweza. Sasa bahati mbaya alimpata mtu wa kumshusha, so kama hajajitambua na akienda kwa mwingine ni shida. Pia na jamaa nae aliyidisha chumviKama kamchoka basi amuache tu ndio suluhisho la kudumu kama sio kumuendeleza naye apate elimu inayoitwa ya juu!!!!
Sio maneno na manyanyaso kwa dada wa watu, amteme akiwa bado anatazamika watu wajitoe muhanga kabla ya lala salama
Nameza...murahoo
Kabla hata Mr. PhD hajamdharau we mwenyewe ulishamdharau shost yako mpaka hana hamu, umetumia kivumishi sifa..ka na ki (kadiploma, kidegree...GPA ya kuchechemea) kuelezea udogo kitaaluma kati ya diploma na degree dhidi ya Masters na PhD.
Umetumia mfumo kuendelea kumshusha hadhi ya mwanamke na hukuacha hisia zako za kukerwa (wivu) na dharau ya mwanamke mwenzio ulipo kosoa majigambo yake...
Nanukuu "kipindi kabla hajaolewa mapenzi yamechanua kama maua ya saa nne alikuwa
anajisifia kweli na mchuchu wake Mara ooh wanaume waliosoma sana waelewa sana, Mara ooh mi kadegree holder kenzangu nikapeleke wapi,maneno kibao kudharau waume za wenzie na
kujifanya Wa kwake ndio bora sana kama tunavyojua masikini akipata masaburi hulia mbwata..sie tena wenye vicertificate holder vyetu tukawa tuna zip our mouth shut tunajipa moyo maisha hayapimwi kwa wingi Wa makaratasi ya vyeti.." mwisho wa kunukuu.
Katika uandishii huu wa kuuma na kupuliza, ambao mwishoni unatoa wito...kwa Mr. PhD dhamira yake bado inatia shaka na inamapungufu hamtetei mlengwa mwanamke msomi...bila kujali kozi yake inakumbatia mfumo dume.
Jibu la swali lako wanaume wasomi wana nini? Utalipata ukibadili dhamira ya uandishi. Tofauti na hapo tarajia michango ya uzoefu badala ya suluu.
Exactly.Utakuwa hujaeleimika kama utataka kuongea mambo ya bond cleaving na mtu wa historia au utake kumuambia mambo ya meli kuelea mtu wa anthropology by the way hujaoa mke ili uzungumze naye ma GDP na vitu kama hivyo!!!!
Tukiamua kuoa basi tukubali hizo tofauti zetu, hivi we ukiwa na PhD mkeo mpishi kila uchao akuletee stori za recipes mpya utaona sawa!!!
Tuzungumze yenye kuhusu familia zetu na hao tuliowaoa italeta amani na upendo na penzi shirikishi!!!
Queen kama umesoma vizuri bandiko langu nimesema jamaa kakosea sana. Hayuko sahihi hata kidogo. ila nimejaribu kuonesha ni kwa nini inakuwa hivyo.Jamaa kakosea sana ila alikosea zaidi na zaidi katika kuoa. Kimisingi huyo bwana anapata tabu sana kuishi na mtu ambaye intellectually yuko chini sana kulinganisha na yeye. Kwa mfano katika hali ya kawaida tu unaweza kuacha kujadiliana na mtu kwa kugundua kwamba uwezo wake wa kuchambua mambo ni mdogo au saa nyingine unaweza kuvumilia na kujaribu kujiweka katika level ya huyo mtu. Sasa fikiria kama unapaswa kufanya hivyo kila siku na mtu huyo huyo!!! Ni wazi baada ya kujitahidi kwa miaka 3 kuna mahali itafika lazima ushindwe.
Hii mara nyingi inatokea kwa sababu mwanzo mwanaume anaweza kugubikwa na mapenzi moto moto na pia wanakuwa hawapati muda wa kukaa pamoja kwa muda mrefu. Zaidi mume anaweza kutegemea mke atakua kiakili na kimaarifa lakini kwa bahati mbaya inaweza isiwe hivyo kwa kuwa watu tunatofautiana uwezo. Kuna wengine hata ufanye vipi hawawezi kufika kiwango anachotamani mume. Sasa ukute mume anataka kujadili kuhusu uchumi wa Uingereza, Marekani, Tanzania na Brazil hapo anakuja na habari za GDP, PPP, per capita, FDI na habari za sekta za dhahabu, wese na wenzao, ukigeuka kidogo anataka kuzungumzia import/export tax, custom duties na visa issues. Hujakaa sawa anataka kuongelea U.S foreign policy in the middle east. Kabla hujajikuna vizuri anakuletea habari za investment and planning ukichanganya na expanding and dreaming big. Sasa kama ndoto zako ni kuishi kwenye nyumba ya vyumba vitatu na gari ya kutembelea lazima mambo yatakuzidi kimo sana. Na ukichanganya na tabia ya watz wengi tulivyo wavivu wa kujifunza mambo mapya ndio kabisa lazima uchemshe. Ndo hapo sasa mume anakuona kilaza bab kubwa. Lazima nyumba uione chungu.
Ila hata hivyo mimi huwa naona watu wanalazimisha mambo. Kuna siku niliwahi kusema maisha yanaweza kuwa magumu sana kama badala ya kutafuta mke unatafuta business partner. Inapofikia mahali huyo mke akashindwa kuwa business partner inakuwa shida kubwa sana.
Inabidi ifike mahali watu kama huyo jamaa inabidi wajue kuwa mke ni mke tu. Kuna majukumu yake kama mke kama anayaweza hayo basi inatosha. Ikitokea akaweza kusimamia na mambo mengine nje ya yale ya msingi na wajibu basi ni vizuri lakini kama hawezi basi si budi kumlazimisha asichokiweza.[/QU
Sasa ndio umeshajua tayari mkeo ana akili ndogo kumnyanyasa kisaikolojia ndo unajenga au unaharibu?? Hakuna binadam ambaye haelewi pale anapoelekezwa tena especially na mtu ambaye yuko close nae to that extent.. Ina maana maswala ya kifamilia nayo yanahitaji critical thinking..utajisikiaje siku ukigundua mkeo mambo mengi yanayomuhusu yeye tena mengine ya privacy yanayotakiwa mujadili nyinyi kaenda kuyaomba ushauri nje??