Jamaa kakosea sana ila alikosea zaidi na zaidi katika kuoa. Kimisingi huyo bwana anapata tabu sana kuishi na mtu ambaye intellectually yuko chini sana kulinganisha na yeye. Kwa mfano katika hali ya kawaida tu unaweza kuacha kujadiliana na mtu kwa kugundua kwamba uwezo wake wa kuchambua mambo ni mdogo au saa nyingine unaweza kuvumilia na kujaribu kujiweka katika level ya huyo mtu. Sasa fikiria kama unapaswa kufanya hivyo kila siku na mtu huyo huyo!!! Ni wazi baada ya kujitahidi kwa miaka 3 kuna mahali itafika lazima ushindwe.
Hii mara nyingi inatokea kwa sababu mwanzo mwanaume anaweza kugubikwa na mapenzi moto moto na pia wanakuwa hawapati muda wa kukaa pamoja kwa muda mrefu. Zaidi mume anaweza kutegemea mke atakua kiakili na kimaarifa lakini kwa bahati mbaya inaweza isiwe hivyo kwa kuwa watu tunatofautiana uwezo. Kuna wengine hata ufanye vipi hawawezi kufika kiwango anachotamani mume. Sasa ukute mume anataka kujadili kuhusu uchumi wa Uingereza, Marekani, Tanzania na Brazil hapo anakuja na habari za GDP, PPP, per capita, FDI na habari za sekta za dhahabu, wese na wenzao, ukigeuka kidogo anataka kuzungumzia import/export tax, custom duties na visa issues. Hujakaa sawa anataka kuongelea U.S foreign policy in the middle east. Kabla hujajikuna vizuri anakuletea habari za investment and planning ukichanganya na expanding and dreaming big. Sasa kama ndoto zako ni kuishi kwenye nyumba ya vyumba vitatu na gari ya kutembelea lazima mambo yatakuzidi kimo sana. Na ukichanganya na tabia ya watz wengi tulivyo wavivu wa kujifunza mambo mapya ndio kabisa lazima uchemshe. Ndo hapo sasa mume anakuona kilaza bab kubwa. Lazima nyumba uione chungu.
Ila hata hivyo mimi huwa naona watu wanalazimisha mambo. Kuna siku niliwahi kusema maisha yanaweza kuwa magumu sana kama badala ya kutafuta mke unatafuta business partner. Inapofikia mahali huyo mke akashindwa kuwa business partner inakuwa shida kubwa sana.
Inabidi ifike mahali watu kama huyo jamaa inabidi wajue kuwa mke ni mke tu. Kuna majukumu yake kama mke kama anayaweza hayo basi inatosha. Ikitokea akaweza kusimamia na mambo mengine nje ya yale ya msingi na wajibu basi ni vizuri lakini kama hawezi basi si budi kumlazimisha asichokiweza.