Jamani wanaume wasomi mna nini?

Jamani wanaume wasomi mna nini?

Jamaa kakosea sana ila alikosea zaidi na zaidi katika kuoa. Kimisingi huyo bwana anapata tabu sana kuishi na mtu ambaye intellectually yuko chini sana kulinganisha na yeye. Kwa mfano katika hali ya kawaida tu unaweza kuacha kujadiliana na mtu kwa kugundua kwamba uwezo wake wa kuchambua mambo ni mdogo au saa nyingine unaweza kuvumilia na kujaribu kujiweka katika level ya huyo mtu. Sasa fikiria kama unapaswa kufanya hivyo kila siku na mtu huyo huyo!!! Ni wazi baada ya kujitahidi kwa miaka 3 kuna mahali itafika lazima ushindwe.

Hii mara nyingi inatokea kwa sababu mwanzo mwanaume anaweza kugubikwa na mapenzi moto moto na pia wanakuwa hawapati muda wa kukaa pamoja kwa muda mrefu. Zaidi mume anaweza kutegemea mke atakua kiakili na kimaarifa lakini kwa bahati mbaya inaweza isiwe hivyo kwa kuwa watu tunatofautiana uwezo. Kuna wengine hata ufanye vipi hawawezi kufika kiwango anachotamani mume. Sasa ukute mume anataka kujadili kuhusu uchumi wa Uingereza, Marekani, Tanzania na Brazil hapo anakuja na habari za GDP, PPP, per capita, FDI na habari za sekta za dhahabu, wese na wenzao, ukigeuka kidogo anataka kuzungumzia import/export tax, custom duties na visa issues. Hujakaa sawa anataka kuongelea U.S foreign policy in the middle east. Kabla hujajikuna vizuri anakuletea habari za investment and planning ukichanganya na expanding and dreaming big. Sasa kama ndoto zako ni kuishi kwenye nyumba ya vyumba vitatu na gari ya kutembelea lazima mambo yatakuzidi kimo sana. Na ukichanganya na tabia ya watz wengi tulivyo wavivu wa kujifunza mambo mapya ndio kabisa lazima uchemshe. Ndo hapo sasa mume anakuona kilaza bab kubwa. Lazima nyumba uione chungu.

Ila hata hivyo mimi huwa naona watu wanalazimisha mambo. Kuna siku niliwahi kusema maisha yanaweza kuwa magumu sana kama badala ya kutafuta mke unatafuta business partner. Inapofikia mahali huyo mke akashindwa kuwa business partner inakuwa shida kubwa sana.

Inabidi ifike mahali watu kama huyo jamaa inabidi wajue kuwa mke ni mke tu. Kuna majukumu yake kama mke kama anayaweza hayo basi inatosha. Ikitokea akaweza kusimamia na mambo mengine nje ya yale ya msingi na wajibu basi ni vizuri lakini kama hawezi basi si budi kumlazimisha asichokiweza.[/QU
Sasa ndio umeshajua tayari mkeo ana akili ndogo kumnyanyasa kisaikolojia ndo unajenga au unaharibu?? Hakuna binadam ambaye haelewi pale anapoelekezwa tena especially na mtu ambaye yuko close nae to that extent.. Ina maana maswala ya kifamilia nayo yanahitaji critical thinking..utajisikiaje siku ukigundua mkeo mambo mengi yanayomuhusu yeye tena mengine ya privacy yanayotakiwa mujadili nyinyi kaenda kuyaomba ushauri nje??
 
sa kama amekosea asiambiwe, umeleta hasara kwenye biashara unataka nikubembeleze tena.... hiyo kitu haipo, tusipokuwa wakali mtatupanda kichwani, lazima upige biti ata kidogo!!! Ilitakiwa ampe na vibao hata viwili kabisa sio maneno matupu

Hapo kwenye vibao umeniwahi mkuu.
 
sa kama amekosea asiambiwe, umeleta hasara kwenye biashara unataka nikubembeleze tena.... hiyo kitu haipo, tusipokuwa wakali mtatupanda kichwani, lazima upige biti ata kidogo!!! Ilitakiwa ampe na vibao hata viwili kabisa sio maneno matupu

Hakuna alikataa kuambiwa lakini unamwambia mtu kwa style IPI???.. Imagine unamfokea mkeo mbele ya house gal na ndugu zako unataka wao wamchukuliejee??
 
kuna wakina dada wanabahati mbaya wanakutana na wanaume ambao 'selfish' hiyo ni shida mnao...yaani mtu mimi, mimi, hela zangu, mimi nimesoma, magari yangu, mimi utaniambia nini nimesoma..ukidate na mtu wa mmimi, mimi, mimi,mimi kimbia ufe...

Yaani kama uliingia mdomoni kwa huyo mkaka uka copy na kupaste.... Yaan anajiona yeye ndo muhimili wa Shoga angu mie bila yeye nyumba itaanguka.. Inafika stage anamwambia shukuru mungu umezaa na intellect kizazi chako kitakuwa na watoto wanaojielewaa ungezaa na vilaza wenzio ungetoa waokota makopo.. Mmh kweli is it fair??
 
Nameza...murahoo

Kabla hata Mr. PhD hajamdharau we mwenyewe ulishamdharau shost yako mpaka hana hamu, umetumia kivumishi sifa..ka na ki (kadiploma, kidegree...GPA ya kuchechemea) kuelezea udogo kitaaluma kati ya diploma na degree dhidi ya Masters na PhD.

Umetumia mfumo kuendelea kumshusha hadhi ya mwanamke na hukuacha hisia zako za kukerwa (wivu) na dharau ya mwanamke mwenzio ulipo kosoa majigambo yake...

Nanukuu "kipindi kabla hajaolewa mapenzi yamechanua kama maua ya saa nne alikuwa
anajisifia kweli na mchuchu wake Mara ooh wanaume waliosoma sana waelewa sana, Mara ooh mi kadegree holder kenzangu nikapeleke wapi,maneno kibao kudharau waume za wenzie na
kujifanya Wa kwake ndio bora sana kama tunavyojua masikini akipata masaburi hulia mbwata..sie tena wenye vicertificate holder vyetu tukawa tuna zip our mouth shut tunajipa moyo maisha hayapimwi kwa wingi Wa makaratasi ya vyeti.." mwisho wa kunukuu.

Katika uandishii huu wa kuuma na kupuliza, ambao mwishoni unatoa wito...kwa Mr. PhD dhamira yake bado inatia shaka na inamapungufu hamtetei mlengwa mwanamke msomi...bila kujali kozi yake inakumbatia mfumo dume.

Jibu la swali lako wanaume wasomi wana nini? Utalipata ukibadili dhamira ya uandishi. Tofauti na hapo tarajia michango ya uzoefu badala ya suluu.
 
Yaani kama uliingia mdomoni kwa huyo mkaka uka copy na kupaste.... Yaan anajiona yeye ndo muhimili wa Shoga angu mie bila yeye nyumba itaanguka.. Inafika stage anamwambia shukuru mungu umezaa na intellect kizazi chako kitakuwa na watoto wanaojielewaa ungezaa na vilaza wenzio ungetoa waokota makopo.. Mmh kweli is it fair??

Mi nadhaniw ana matatizo zaidi ya hayo ya "intellectual capacity" kwenye ndoa. Si bure.
 
PhD yenyewe ya planning nayo anajiita msomi...mie nikajua labda engineer hivi, mahisabati nk nk...nahisi atakuwa nshomire, maana wale wanaweza kukudharau hadi ukatamani umkabe shingo!
 
Mimi nahisi nyuma ya pazia kuna kitu. Either huyo dada Kuna kitu aliharibu, na mwanzo wa kudhsrauliwa au huyo PHD holder ameruka ukuta, kuna sehemu anapooza na ndo kuanza kumdharau mwenzake.

Hiyo ya kudharau kwa sababu ya tofauti za kielimu ni kujikweza tu hamna lolote.
 
PhD yenyewe ya planning nayo anajiita msomi...mie nikajua labda engineer hivi, mahisabati nk nk...nahisi atakuwa nshomire, maana wale wanaweza kukudharau hadi ukatamani umkabe shingo!

Hili kabila la nshomire mnalipenda sana enheee!!hata mjui ni kabila gani lakn mishono inawawasha kutaja makabila ya watu!!!nyambafuuuu
 
Ndo maana nikaamua kuolewa na asiyesoma kabisa,tabu za kudharauliana za nini!!
 
Kabla hata Mr. PhD hajamdharau we mwenyewe ulishamdharau shost yako mpaka hana hamu, umetumia kivumishi sifa..ka na ki (kadiploma, kidegree...GPA ya kuchechemea) kuelezea udogo kitaaluma kati ya diploma na degree dhidi ya Masters na PhD.

Umetumia mfumo kuendelea kumshusha hadhi ya mwanamke na hukuacha hisia zako za kukerwa (wivu) na dharau ya mwanamke mwenzio alipo kosoa majigambo yake...

Nanukuu "kipindi kabla hajaolewa
mapenzi yamechanua kama
maua ya saa nne alikuwa
anajisifia kweli na mchuchu
wake Mara ooh wanaume
waliosoma sana waelewa sana, Mara ooh mi kadegree
holder kenzangu nikapeleke
wapi, maneno kibao kudharau
waume za wenzie na
kujifanya Wa kwake ndio bora
sana kama tunavyojua masikini akipata masaburi
hulia mbwata..sie tena wenye
vicertificate holder vyetu
tukawa tuna zip our mouth
shut tunajipa moyo maisha
hayapimwi kwa wingi Wa makaratasi ya vyeti.." mwisho wwa kunukuu

Hizo Ka, ke, Ki nimeziongelea in a positive way kutokana na hali halisi ya Matatizo yao... But suala LA dharau cijajua though hata nikimdharau, dharau yangu Mimi haina effect ya kumfanya ugali usipite kooni vizuri cz Mimi ni Shoga tu Leo tunaweza kuwa karibu kesho nat.. Maumivu ya dharau ya mtu unayelaa nae kitanda kimoja ambaye umempa uhimili Wa maisha yako yote muishi kwa shida na raha huwez kucompare na maneno ya wapita njia
 
Ni asili tu watu wa namna hii wapo wengi tu hata asingekua na hiyo phd angetafuta njia nyingine kumuundermine huyo mwanamke,
Mimi nahisi nyuma ya pazia kuna kitu. Either huyo dada Kuna kitu aliharibu, na mwanzo wa kudhsrauliwa au huyo PHD holder ameruka ukuta, kuna sehemu anapooza na ndo kuanza kumdharau mwenzake.

Hiyo ya kudharau kwa sababu ya tofauti za kielimu ni kujikweza tu hamna lolote.
 
Hili kabila la nshomire mnalipenda sana enheee!!hata mjui ni kabila gani lakn mishono inawawasha kutaja makabila ya watu!!!nyambafuuuu

Babu mbona waja juu kama moshi wa kifuu! Hili kabila mie binafsi lilishanitenda sana sana ni mambo mazito hata kusimulia siwezi...kwa hiyo you shshhh!
 
Mtoa kwanza wewe mwenyewe inaonekana una gubu sana, nimekiona kijicho chako kibaya kwa shoga yako kuolewa na jamaa wa PHD...

Ikiwa kweli huyo mwanamme anafanya mambo hayo nadiriki kusema elimu haijamkomboa kifikra...

Mara nyingi hii huwa ni Kujishtukia tu kwa mwanamke, kwa kila anachogombezwa kuhisi anagombezwa pengine kwa sababu ana elimu kidogo kuliko jamaa...eg ilishawahi kunitokea miaka hiyo huko kijijini kwetu nikikosea jambo basi lazima watalihusisha na elimu yangu ya kadegree niliyokuwa nayo...kumbe hawakujua hata Mimi ni binadamu nakosea kitabia kama ambavyo wengine ambao hawakusoma hukosea...

Ila we mtoa mada kama ilivyo kwa wanawake wote duniani ni kama vile unafurahia matatizo ya mwenzako, acha hizo kitu
 
Mkuu hiyo sui tabia ya kisomi, huyo mwanaume anamnyanyasa mke wake sio kwa sababu kasoma sana ila ndo alivyo, usomi hauwezi kuwa ndo sababu ya kumnyanyasa, mbona kuna wanaume hawana elimu na wananyanyasa wake zao, me nafikiri hiyo ni tabia ya mtu wala haina uhusiano na elimu
 
Mtoa kwanza wewe mwenyewe inaonekana una gubu sana, nimekiona kijicho chako kibaya kwa shoga yako kuolewa na jamaa wa PHD...

Ikiwa kweli huyo mwanamme anafanya mambo hayo nadiriki kusema elimu haijamkomboa kifikra...

Mara nyingi hii huwa ni Kujishtukia tu kwa mwanamke, kwa kila anachogombezwa kuhisi anagombezwa pengine kwa sababu ana elimu kidogo kuliko jamaa...eg ilishawahi kunitokea miaka hiyo huko kijijini kwetu nikikosea jambo basi lazima watalihusisha na elimu yangu ya kadegree niliyokuwa nayo...kumbe hawakujua hata Mimi ni binadamu nakosea kitabia kama ambavyo wengine ambao hawakusoma hukosea...

Ila we mtoa mada kama ilivyo kwa wanawake wote duniani ni kama vile unafurahia matatizo ya mwenzako, acha hizo kitu
Kwanza suala la gubu ni shani ambayo mungu hakunijaalia nayo kwa kuwa naridhika na nilichonacho na sina mda Wa kumuonea mtu kijicho..don judge me behind my writings...pia sifurahii Matatizo ya mwenzangu dats y nilimwambia avumilie ndan ya ndoa yakimkifu ashirikishe familia labda wanaweza kumsaidia.. Cz hata mi Nina yangu najua changamoto ni nyingi..ntafurahije msiba Wa jirani wakati Israel hana ndugu..
 
inawezekana huyo jamaa back ground yake ni mbaya wale wa ghetto fabolous wale waliokuwa maisha magumu sana hivyo hali hii huchangia wanakuwa na matatizo ya saikolojia

au kabila letu lile la kujivuna la huku kagera nshomile
 
Back
Top Bottom