Hebu kwanza twende trtibu, kwo huyo jamaa ni wapi, ni kule tunaendaga kwa kuvuka maji baridi?!! maana msikae mnasingizia watu wenye elimu za juu kwa sample ya wajinga wawili! btw, hivi kwa nini wanawake wengi wenye elimu kubwa wameolewa na kuachika?..na wengine wameachika kimyakimya bado wanatumia majina ya waume zao?!
Tatizo mmegeuza mada na kuanza kuchomeka ambayo pengine hayana uhusiano!Hebu jaribuni kujadili nje ya kuuliza ambayo hayana uhusiano maana si mpaka utoke sehemu Fulani ndio ufanye haya!
Ukweli ni kwamba watu wanapokuwa na tofauti kubwa ya Elimu kwenye mahusiano ni tatizo kubwa na hili tatizo haliwezi kuonekana mwanzoni maana mapenzi yanakuwa moto moto!
Athari za utofauti mkubwa wa elimu huonekana pale wawili wanapo anza kukwaruzana na kujaribu kukosoana!
Mimi sio kwamba naunga mkono huyo binti kukashifiwa lakini nina uhakika kuna mengi hatujaaambiwa kwenye hii habari na lengo la hii habari ni kuhakikisha kila msomaji aone huyu bwana ni tatizo na mwanamke hana kosa!
Kuna uwezekano mkubwa hawa watu wanekuwa wakilumbana na kufikia kurushiana maneno na haiwezekani huyu nwanamke huwa hasemi chochote!
Muda mwingine unaweza ukawa na mtu na anakiwango Fulani cha elimu na hutegemei yeye kushindwa mambo Fulani Fulani hasa madogo na unatakiwa kujua kuwa baadhi ya wanawake ni mahodari wa kusema Mimi nina elimu .....mimi nataka mtu aina Fulani na akimpata ana anza kulialia....
Kuna mtu ana kwambia ana elimu Fulani lakini unaweza kuchoka maana hata kufikiri kwenye mambo madogo yana mshinda... na hili hata wanawake wenyewe kuwa na mwanaume wa namna hii wanaona mzigo!
Muda mwingine unaweza kukaa na mtu ukashindwa kujadili nae chochote maana kila jambo amepwaya hadi inakuwa kero!..
Kuna muda unakuwa kwenye mjadala na mtu na yeye anakuwa mtu wa ndio mzee... na hawezi kuhoji kwanini unasema hivi? Au hawezi kusema kuwa nakataa hilo sababu ya hili na hill na hakuna anayependa kuwa na akanana mzigo ambaye hawezi kutoa ushauri!
Kwa case ya huyu jamaa utaona kabisa alikuwa anategemea mkewe afanye mambo Fulani Fulani lakini si Fulani Fulani!
Swala la utofauti wa elimu linatakiwa kuzingatiwa Sana kwenye mahusiano maana lina athari kubwa!