Jamani, mtoto anatuchonganisha familia nzima!

Jamani, mtoto anatuchonganisha familia nzima!

Pole ila punguza hasira mkuu!
Mtoto akichafua mkono haukatwi bali unasafishwa tu. Naamini watoto wako ni wadogo bado ila trust me,ulezi una challenges sana na si watoto wote ni rahisi kuwalea.
Kakae na dada yako uombe radhi yaishe na muongee na huyo mtoto kwa upendo muendelee kumlea kwa upendo na amani.
Sidhani kama angekuwa wako wa kumzaa ungemsusa pia.
Watoto wanakosea na wakikosea wanaonywa na kusamehewa ili maisha yaendelee.
Mungu awaongoze mkalimalize hili kwa busara ya kujishusha na kuchukuliana.
 
Kula wali maharage ukasome............wali samaki wanakula wenye ajira zao bibie. Ukitaka boom likulipie kila kitu unachopenda unapotea saaaaana. Ukijaliwa wazazi wenye pesa za kutosha kula unachotaka na utapewa back up ya financial assistance kutoka home. Usijilinganishe na wengine

Kula wali maharage kila siku? Hapana kwakweli....kama kipo kinatumika. Ndio maana natumia
 
  • Thanks
Reactions: amu
Hlf hyo dada yko usimuendekeze akili za wanawake wote tunazijua kashikiliwa maskio na bwana mdogo bila hta ya kupima kakurupuka kukulaum cha msingi mtafute sister muongee asipokuelewa mpotezee

Nimekusoma sana mkuu. Ngoja na mie hizi hasira zangu zikate then nitajaribu kumfuata dada nijue nini msimamo wake na pia kujaribu kufukia mashimo. Ahsante kwa ushauri wako.
 
Hapo ni mjini kaka yangu.
Vyuo vyetu vilivyo mbali na mji ni majanga.
Wali samaki tu 5000. Hapo hujanywa hata maji. Asubuhi hujanywa chai na jioni hujala. Kuondoa mahitaji mengine ya stationary. ... elfu 10 kwa siku ni kwa kujibana sana kaka. Majanga.

Hakuna hii Tanzania mahali ambapo chakula cha wanafunzi kina bei zaidi ya IFM.

Wali samaki 5,000? Hizi ni bei za canteen kubwa kubwa mjini ambazo wafanyakazi wanakula, tena sio wafanyakazi wote nakwambia.

Kubali kwamba ile umeweka kama story tu, laki 200,000/- juu ya boom! Hostel umelipiwa, stationery umelipiwa.
 
Hakuna hii Tanzania mahali ambapo chakula cha wanafunzi kina bei zaidi ya IFM.

Wali samaki 5,000? Hizi ni bei za canteen kubwa kubwa mjini ambazo wafanyakazi wanakula, tena sio wafanyakazi wote nakwambia.

Kubali kwamba ile umeweka kama story tu, laki 200,000/- juu ya boom! Hostel umelipiwa, stationery umelipiwa.

No research no right to speak. Don't conclude because you don't know.
Njoo Mzumbe main campus uone.....hiyo ni bei ya muso canteen. Canteen ya chuo
 
Hlf hyo dada yko usimuendekeze akili za wanawake wote tunazijua kashikiliwa maskio na bwana mdogo bila hta ya kupima kakurupuka kukulaum cha msingi mtafute sister muongee asipokuelewa mpotezee

Nimekusoma sana mkuu. Ngoja na mie hizi hasira zangu zikate then nitajaribu kumfuata dada nijue nini msimamo wake na pia kujaribu kufukia mashimo. Ahsante kwa ushauri wako.
 
habari za usiku huu wanajamvi? Poleni sana kwa mihangaiko ya siku nzima ya leo pia kwa wale wakazi wa dar poleni sana kwa foleni ya siku ya leo. Hope baada ya kufika now tupo kwenye jukwaa letu pendwa.

Now back to the topic, hapa nilipo nina kisirani na kero ambayo hata imechangia kuharibu siku yangu tangu usiku wa jana, kisa mtoto wa ,marehemu kaka yetu. Ipo hivi; kaka yetu mkubwa alibahatika kuzaa akiwa shuleni miaka hiyo.

Huyo mtoto nimepishana naye kama miaka mitano so kwa kiasi fulani nimekua naye kabisa kama mdogo wangu wa kunifuata maana mie die kitinda mimba katika familia yetu. Huyu mtoto amekuwa na tabia za ajabu sana tangu akiwa mdogo kama vile ubinafsi, matumizi mabaya ya fedha, uchonganishi, kiburi na mengineyo mengi ambayo hata kwa sasa ndio yamenipelekea naandika uzi huu.

Tumeanza kumlea tangu tangu akiwa na umri wa miaka mitatu baada ya wazazi wa mama yake kutuzilia hapo ndio ikawa hadi wazazi wake wanafariki katikati na mwishoni mwa miaka ya tisini. So hadi wazazi wetu nao pia wanafariki alikuwa ni mdogo sana ndio kwanza yupo form one wakati mie nipo form six. In short baada ya mie kumaliza chuo na kuanza kazi ikawa ni jukumu letu na dada yangu kumsomesha huyo mtoto ili nae apate msingi bora wa maisha ingawa alikuwa na usumbufu ila darasani hakuwa haba kwa kweli.

Nakumbuka mwaka juzi alichaguliwa kujiunga na chuo kikuu kimoja hivi cha binafsi hapa nchini, kweli tulijipinda na kumpeleka. Akiwa huko vibweka havikuisha kabisa kwa kupiga vibomu vikubwa vikubwa huku na huku (kwangu na sister). Baada ya kushitukia hila zake dada alipendekeza mie kuwa ndie in charge bila ya kujua kuwa naingia kwenye shimo la moto nikakubali.

Akiwa chuo alipiga bomu moja kubwa sana akijumlishia na gharama za medical capitation, wakati huo bima anatumia kadi ya bima ya afya ya kwangu niliomkatia. Nijuavyo ni kuwa chuoni kama mtu una bima ya afya ya shirika fulani unaweza usichangie hiyo medical capitation given kuwa umeweka taarifa zako bayana kuwa una bima gani na ni mwanachama hai
so baada ya hiko kibomu nikiwa pamoja dada yangu nilimpa taratibu za kufuata ili kuweza kuweka mambo yake sawa ili kupunguza gharama zisizokuwa za lazima kwangu na dada. Alionekana dhahiri kutoridhika na ile proposal yangu ila nikakomaa nae nikamwambia kuwa nampa siku tatu afanye follow up then when he is done anambie alipofikia kama kaweza au la. Basi ile kumwambia vile ndio ikawa kama nimekata undugu maana sikupata hata missed call kutoka kwake hadi wiki inaisha. Nikaona sasa isiwe taabu maana shida zake yeye anataka tena alete kiburi, so na mie nikawa jeuri nikakaa kimya.

Amini msiamini ilikuwa ni mwezi wa 9 mwaka jana alikaa kimyaaaa hadi mwezi wa 12 tarehe 31 aliponitumia message inasema “hello papaa! Happy new year. Yo ma dad and am ya son. I always love you ila kama ni shida zangu nitajitahidi kutokukushirikisha…” hiyo text nimecopy na kupaste kama alivyotuma nothing added or removed. Kwa kweli ilinikera na nikaona kama anajiona tayari kajipanga kimaisha, let him be. Niliendelea na ukimya wangu ili kuepusha shari na wala sikutaka kumwambia mtu.

Jana usiku wa saa nne nilimpigia dada simu kumjulia hali ndio hapo ikawa balaa sasa. Dada aliuliza “mara ya mwisho ni lini ilikuwa kuongea na mwanao?”

nilimwambia kila kitu juu ya misbehavior za mtoto. Alichonambia ni kuwa mie nakuwa mjinga na katili. Akaendelea kuwa kama hapo ukiambiwa mwanao anaumwa je? Nikajibu kuwa kwa kuwa ana bima ya afya basi mie wala sitokuwa na wasi na kama akihitaji msaada kama kweli nitatoa msaada wangu kwa kadiri niwezavyo.

Basi hapo dada yangu aliwaka vibaya mno kuwa mie katili, mtoto wiki ya tatu hii anaumwa halafu mie natoa majibu mepesi… what i told her ni kuwa je ningeota au ningejuaje kama yeye aliamua kukaa kimya.
Dada aliendelea kuwaka na kunivisha kila aina ya ubaya akimtetea mtoto. (sijui wana ajenda gani ya siri maana it seems wao wana mawasiliano ya karibu ambayo mie siyajui na sijui wanaongea nini).

Baada ya kuona vile dada anakuja juu nilikata simu kwa hasira. Hakuishia hapo, alituma message ikisema “ahsante umekuwa nashukuru, nakuacha kama ulivyosema ndugu zako ni hao wa mkeo ila…”

hapo pia nilishindwa kuelewa mke wangu anaingilia wapi jamani? Yaani usiku wa jana ulikuwa mchungu, kazi hazikwenda leo na hata sasa nipo mood less.

Hapa nashindwa kuelewa kosa langu lipo wapi? Je mwisho wa haya yote ni nini? Huyu mtoto nimfanyaje? Naombeni ushauri na maoni yenu wadau na pia samahani kwa posti ndefu namna hii but i was trying to explain the situation exhaustively.

Karibuni.

pole sana ndugu yangu. Asiyekupa support katika hili atakuwa mtu wa ajabu au naye ana tabia kama za huyu mtoto. Binafsi nimelea wengi tena wenye tabia chafu kuliko huyo wa kwako. Haya mambo bwana yanahitaji busara sana. Huyo dadaako ni rahisi kukulaumu kwa kuwa kalishwa maneno na mtoto huyo. Angekuwa na akili angejiuliza pale alipokuambia umsimamie yeye alikuwa wapi?


Kaa zako kimya endelea na maisha yako. Fanya yaliyo sahihi. Wakikua hao watapata akili. Time is the best teacher.

Peace!
 
Hakuna kitu kigumu kama kulea mtoto asiye wa kwako. Binafsi nalea watoto wa mume wangu wawili yaani ni kero hawana jema hata uwafanye nini. Mi nimeamua kutimiza wajibu wangu sitaki kesho kwa Mungu nikahukumiwe. Mi nafanya yangu wao shauri yaom
pole sana ndugu yangu. Asiyekupa support katika hili atakuwa mtu wa ajabu au naye ana tabia kama za huyu mtoto. Binafsi nimelea wengi tena wenye tabia chafu kuliko huyo wa kwako. Haya mambo bwana yanahitaji busara sana. Huyo dadaako ni rahisi kukulaumu kwa kuwa kalishwa maneno na mtoto huyo. Angekuwa na akili angejiuliza pale alipokuambia umsimamie yeye alikuwa wapi?


Kaa zako kimya endelea na maisha yako. Fanya yaliyo sahihi. Wakikua hao watapata akili. Time is the best teacher.

Peace!
 
Natamani sana ningevaa uhusika wako. Huyo dogo ni malipo ya malezi mliyo mlea hapo hawali. Imekwisha kuwa to late. Ila kwangu mimi ningewanyorotesha wote yeye na Dada.
 
Kwanza mkuu Nyaupindo hongera sana kwa Moyo wako wa dizain hiyo inamFinance mtu ambaye anapata boom na nina ya Afya juu,,atake nini zaidi? Maisha haya ya sasa hivi yanajulikana jinsi yalivyo magumu ukizingatia una familia yako unayoiangalia.

Huyo kijana ajue kuwa YATIMA HADEKI.
 
Last edited by a moderator:
umenikumbusha kuna mmoja nimekutana naye kama mwezi mmoja hivi, hanijui simjui, ile tumekaa pamoja for drinks and the like basi ndio ana birthday kesho kutwa yake, na kesho anaenda saloon , maana yake nimsupport, hivi mbona hawadaigi hela za vitabu au umnunulie kitabu?

Watoto wa siku hizi ndo ivo anataka aishi kama meneja wa CRDB hivi au TRA, ila kwa fedha za wengine!
Shemeji
Shemeji

Ila bado nawaza kijana anatumia 100,000 kwa wiki?

Hahahahah hajui mshahara gross ni 400,000?? Hapo kama atabahatika kupata ajira??
 
Are you serious:what:😱
Laki moja inaisha kwa wiki 2:what:...trust me anajibana sana....mimi laki moja natumia kwa wiki moja tu mkuu. Enzi wewe unasoma chuo vitu vilikua bei chee compared na sasa.... kwa sasa bila anasa mwanachuo kwa siku anatumia sh10000...nakushangaa huyo dogo anawezaje kutumia laki moja kwa wiki 2. Mimi ni mwanachuo...natumia laki 1 kwa wiki 1.
Wewe kwa maelezo tu unaonekana kabisa ni kiburi na don't care. Jitafakari upya bro.

Matumizi mabaya ya pesa
Na kwa sababu huitafuti wewe
 
Kijana ana kiburi
Na atawaaumbua sana wakimuendekeza
Maisha sio lele mama
Na show off A kijinga za chuo aache
Alipaswa kujua kua baba yake mdogo anamsaidia tu na sio wajibu wake, hilo lingemfanya ashike na atunze sana anachokipokeA

Pila hana uchungu na baba yeke mdogo ndo maana haoni hasara kutapanya na inawezekana kijana hajali kwa kuwa sio baba yake mzazi?
Yaani uchungu hana

Hata hivyo yeye kama baba mlezi lazima awe firm
Maisha sio lele mama wakimuendekeza sasa hivi atawasumbua
Na kijana ajifunze discipline

Anajua ni vingapi baba yake mdogo amejinyima ili yeye asome?

La hasha huyo kijana sio wa kumuendekeza





duh....hili suala ni very sensitive jamani...

mjue pamoja na yote mleta mada ana familia yake na watoto

Huyu mtoto wa kaka yake kwa upande wake alipaswa atambue kwamba kwa mazingira yalivyo anatakiwa awe mtiifu na aridhike kuliko kuonyesha kiburi hivi na kumchunia baba yake mdogo.

Kama wamemfanyia yote hayo anapaswa kuwa myemyekevu na aonyeshe adabu hata pale anapoona kwamba 'ameonewa'
nakubali kwamba tunawiwa kuwasaidia ndugu zetu lakini hiyo isiwe sababu ya kukoseshana furaha, kuwekeana visasi na vinyongo n.k. mleta mada anayo haki pia ya kufurahia maisha yake hapa duniani regardless of what happened .....ni Mungu alimwita kaka yake sio yeye

sasa angalia...kijana ana Boom, bado anapewa financial assistance, anasema hazitoshi,,,anaumwa, hasemi, na huku ana kadi ya bima ya Afya? ni wangapi kati yetu hapa ambao tuna wazazi wote wawili na bado hatuwezi kuafford maisha haya ya hivi? Yaani laki kwa mbili apart from boom wengine mnaona ndogo, je tunajua mleta mada analipwa mshahara kiasi gani? Maana kama tunazungumzia lki moja kwa wiki ni laki nne kwa mwezi......huo ni zaidi ya mshahara wa TGS D! familia yake je anaihudumiaje?

Mi nadhani mleta mada na dada yake wakae pamoja...wayaongee kisha wamwonye dogo kwa upendo....maisha haya sio kama zamani mambo yametight sana
BADILI TABIA nimekusoma shemeji
 
Last edited by a moderator:
Kijana ana kiburi
Na atawaaumbua sana wakimuendekeza
Maisha sio lele mama
Na show off A kijinga za chuo aache
Alipaswa kujua kua baba yake mdogo anamsaidia tu na sio wajibu wake, hilo lingemfanya ashike na atunze sana anachokipokeA

Pila hana uchungu na baba yeke mdogo ndo maana haoni hasara kutapanya na inawezekana kijana hajali kwa kuwa sio baba yake mzazi?
Yaani uchungu hana

Hata hivyo yeye kama baba mlezi lazima awe firm
Maisha sio lele mama wakimuendekeza sasa hivi atawasumbua
Na kijana ajifunze discipline

Anajua ni vingapi baba yake mdogo amejinyima ili yeye asome?

La hasha huyo kijana sio wa kumuendekeza

You just nailed it shemeji BADILI TABIA
 
Last edited by a moderator:
Dogo kiburi
Komaa nae
Hata kama atajifunza the hard way
Ipo siku atakujumbuka



sio makosa ya kununa na kuwafanyia kiburi wakubwa zangu. hii sio mara ya kwanza dogo kuninunia na kukata mawasiliano na mie ndio nakuwa wakwanza kumtafuta, kuna kipindi akiwa shule alianza makundi mabaya akaanza kuweka wave kwenye nywele, mikorogo (kumbuka ni mtoto wa kiume huyu) na mengine.
nilipomsema alinuna so ikabidi mie tena nimtafute na kuongea nae kwa upole na kuyamaliza, ingawa hata mawasiliano ya simu yalikata. So mtu kama huyo ni wa kumpa nini au upendo wa aina gani?
 
Kwa siku HESLB wanatupatia 7500 ya kujikimu. Pesa hiyo haitoshi coz wameangalia gharama za vyakula vya kawaida tu.
Kwa chuo nachosoma....wali samaki tu ni sh. 5000
Hapo sijanywa maji wala asubuhi sijanywa chai wala jioni sijala. Kwa kujibana sana huwa natumia 10000 kwa siku minimum....... be reasonable


Khaaa hebu niambie mfano wa chuo wanachouza kwenye Cafteria wali Samaki 5000?
 
Hata mimi nimeshangaa laki mtu analalamika niliwahi kuomba budget ya laki kwa mwezi mzee aliuliza natumia nini alilalamika uzuri wana mitazamo hasi na chanya bi mkubwa alishangaa ninawezaje kuishi kwa laki moja kwa mwezi mzima tena Maisha ya Dar alikataa. Jamani kwa maisha ya chuo laki kwa week mbili ni sawa na sawa na 7000 kila siku uweke voucher hujala cjui u print mi assignment nauli sijui ki mchango cha ka saccos au mwenzio kaumwa yaani laki kusema ukweli anajibana amekuhurumia watoto wa mjini wanasema laki si pesa hiyo ni sawasawa na kiingilio cha kuangalia wanamziki au mashindano ya miss Tanzania

----- nini?kumbuka ana boom huyo.
 
umenikumbusha kuna mmoja nimekutana naye kama mwezi mmoja hivi, hanijui simjui, ile tumekaa pamoja for drinks and the like basi ndio ana birthday kesho kutwa yake, na kesho anaenda saloon , maana yake nimsupport, hivi mbona hawadaigi hela za vitabu au umnunulie kitabu?

Watoto wa siku hizi ndo ivo anataka aishi kama meneja wa CRDB hivi au TRA, ila kwa fedha za wengine!

Kaka, sentenso ya mwisho umesamaraisi kila kitu. Na wadau naona wanamtetea dogo kwa nguvu zote, hivi ndio tunatakiwa tuwalee vijana kwa jinsi hii just because tulichukua jukumu la kuwatunza?
 
Back
Top Bottom