Jamani, mtoto anatuchonganisha familia nzima!

Nyaupindo

Member
Joined
Mar 24, 2014
Posts
43
Reaction score
30
Habari za usiku huu wanajamvi? Poleni sana kwa mihangaiko ya siku nzima ya leo pia kwa wale wakazi wa Dar poleni sana kwa foleni ya siku ya leo. Hope baada ya kufika now tupo kwenye jukwaa letu pendwa.

Now back to the topic, hapa nilipo nina kisirani na kero ambayo hata imechangia kuharibu siku yangu tangu usiku wa jana, kisa mtoto wa ,marehemu kaka yetu. Ipo hivi; kaka yetu mkubwa alibahatika kuzaa akiwa shuleni miaka hiyo.

Huyo mtoto nimepishana naye kama miaka mitano so kwa kiasi Fulani nimekua naye kabisa kama mdogo wangu wa kunifuata maana mie die kitinda mimba katika familia yetu. Huyu mtoto amekuwa na tabia za ajabu sana tangu akiwa mdogo kama vile ubinafsi, matumizi mabaya ya fedha, uchonganishi, kiburi na mengineyo mengi ambayo hata kwa sasa ndio yamenipelekea naandika uzi huu.

Tumeanza kumlea tangu tangu akiwa na umri wa miaka mitatu baada ya wazazi wa mama yake kutuzilia hapo ndio ikawa hadi wazazi wake wanafariki katikati na mwishoni mwa miaka ya tisini. So hadi wazazi wetu nao pia wanafariki alikuwa ni mdogo sana ndio kwanza yupo form one wakati mie nipo form six. In short baada ya mie kumaliza chuo na kuanza kazi ikawa ni jukumu letu na dada yangu kumsomesha huyo mtoto ili nae apate msingi bora wa maisha ingawa alikuwa na usumbufu ila darasani hakuwa haba kwa kweli.

Nakumbuka mwaka juzi alichaguliwa kujiunga na chuo kikuu kimoja hivi cha binafsi hapa nchini, kweli tulijipinda na kumpeleka. Akiwa huko vibweka havikuisha kabisa kwa kupiga vibomu vikubwa vikubwa huku na huku (kwangu na sister). Baada ya kushitukia hila zake dada alipendekeza mie kuwa ndie in charge bila ya kujua kuwa naingia kwenye shimo la moto nikakubali.

Akiwa chuo alipiga bomu moja kubwa sana akijumlishia na gharama za medical capitation, wakati huo bima anatumia kadi ya bima ya afya ya kwangu niliomkatia. Nijuavyo ni kuwa chuoni kama mtu una bima ya afya ya shirika Fulani unaweza usichangie hiyo medical capitation given kuwa umeweka taarifa zako bayana kuwa una bima gani na ni mwanachama hai
So baada ya hiko kibomu nikiwa pamoja dada yangu nilimpa taratibu za kufuata ili kuweza kuweka mambo yake sawa ili kupunguza gharama zisizokuwa za lazima kwangu na dada. Alionekana dhahiri kutoridhika na ile proposal yangu ila nikakomaa nae nikamwambia kuwa nampa siku tatu afanye follow up then when he is done anambie alipofikia kama kaweza au la. Basi ile kumwambia vile ndio ikawa kama nimekata undugu maana sikupata hata missed call kutoka kwake hadi wiki inaisha. Nikaona sasa isiwe taabu maana shida zake yeye anataka tena alete kiburi, so na mie nikawa jeuri nikakaa kimya.

Amini msiamini ilikuwa ni mwezi wa 9 mwaka jana alikaa kimyaaaa hadi mwezi wa 12 tarehe 31 aliponitumia message inasema “hello papaa! Happy new year. Yo ma dad and am ya son. I always love you ila kama ni shida zangu nitajitahidi kutokukushirikisha…” Hiyo text nimecopy na kupaste kama alivyotuma nothing added or removed. Kwa kweli ilinikera na nikaona kama anajiona tayari kajipanga kimaisha, let him be. Niliendelea na ukimya wangu ili kuepusha shari na wala sikutaka kumwambia mtu.

Jana usiku wa saa nne nilimpigia dada simu kumjulia hali ndio hapo ikawa balaa sasa. Dada aliuliza “mara ya mwisho ni lini ilikuwa kuongea na mwanao?”

Nilimwambia kila kitu juu ya misbehavior za mtoto. Alichonambia ni kuwa mie nakuwa mjinga na katili. Akaendelea kuwa kama hapo ukiambiwa mwanao anaumwa je? Nikajibu kuwa kwa kuwa ana bima ya afya basi mie wala sitokuwa na wasi na kama akihitaji msaada kama kweli nitatoa msaada wangu kwa kadiri niwezavyo.

Basi hapo dada yangu aliwaka vibaya mno kuwa mie katili, mtoto wiki ya tatu hii anaumwa halafu mie natoa majibu mepesi… what I told her ni kuwa je ningeota au ningejuaje kama yeye aliamua kukaa kimya.
Dada aliendelea kuwaka na kunivisha kila aina ya ubaya akimtetea mtoto. (sijui wana ajenda gani ya siri maana it seems wao wana mawasiliano ya karibu ambayo mie siyajui na sijui wanaongea nini).

Baada ya kuona vile dada anakuja juu nilikata simu kwa hasira. Hakuishia hapo, alituma message ikisema “Ahsante umekuwa nashukuru, nakuacha kama ulivyosema ndugu zako ni hao wa mkeo ila…”

Hapo pia nilishindwa kuelewa mke wangu anaingilia wapi jamani? Yaani usiku wa jana ulikuwa mchungu, kazi hazikwenda leo na hata sasa nipo mood less.

Hapa nashindwa kuelewa kosa langu lipo wapi? Je mwisho wa haya yote ni nini? Huyu mtoto nimfanyaje? Naombeni ushauri na maoni yenu wadau na pia samahani kwa posti ndefu namna hii but I was trying to explain the situation exhaustively.

Karibuni.
 
Kama uliamua kubeba jukumu kama mzazi, hukutakiwa kumuacha mtoto peke yake kwa kipindi chote hicho bila kumjulia hali mtoto No matter how stubborn he is, ebu jiulize angekuwa mtoto wako wa kumzaa ungemfanyia hivyo?, watoto yatima ni ngumu sana kuishi nao, wana uchungu sana. Ushaur wangu kaeni kama familia ombaneni msamaha muyamalize full stop. Usichoke kutenda wema
 
Mkuu kusema ukweli sijaona kosa la mtoto na pia dada yako yuko sahihi. Yaani kuanzia mwezi wa 9 mwaka jana mpaka leo hujui mtoto anaishije kisa alikuomba hela unayosema ni nyingi.

Unadiriki kusema eti "shida zake akuletee kibri" which means you don't care. Kwanini kama unaona anamapungufu usimwambie ili ayarekebishe. Mwanafunzi wa chuo siyo mtoto mdogo ni mtu mzima bana.

Nadhani sms aliyokutumia mwezi dec ni kaa la moto moyoni kwako ila jitahidi ubadirike.

Hata wewe hukuzaliwa na pesa mkuu, Mtafute muongee mmalize tofauti zenu pia uendelee kumhudumia kama mwanafamilia.

Kumbuka hata yeye hakupenda kupoteza wazazi wake na pia wewe siyo jiwe wala mlima kwamba utaishi milele. Just imagine umepass away then wanao wakawa wanahitaji msaada wa namna hiyo.

Anyway naomba nikuulize. If that was your own son, would you have abandoned him like that just because of begging you money?
 
Kama uliamua kubeba jukumu kama mzazi, hukutakiwa kumuacha mtoto peke yake kwa kipindi chote hicho bila kumjulia hali mtoto No matter how stubborn he is, ebu jiulize angekuwa mtoto wako wa kumzaa ungemfanyia hivyo?, watoto yatima ni ngumu sana kuishi nao, wana uchungu sana. Ushaur wangu kaeni kama familia ombaneni msamaha muyamalize full stop. Usichoke kutenda wema

I second you mkuu, jamaa amfuate dada yake wakae na wamkalishe mtoto warekebishe tofauti zao., though sometimes inakera.
 
Ulipopewa jukumu la kuwa in-charge haina maana ya kutoa pesa tu lakini ni pamoja na kuhakikisha mtoto wenu anapata malezi.

Kwa bahati mbaya umekuwa irresponsible guardian, na hata dada yako amaliona hilo. Kama mtu mzima ulipoona mtoto ana tatizo kwa nini hujachukua hatua ya 'kumsimamia' badala ya kulalama pembani?

Kama uliona jukumu ulilopewa ni zito kwa nini ulikubali kulipokea.
 
  • Thanks
Reactions: amu
Jamani ndugu zangu naona wengi mmeangalia upande mmoja ti wa mtoto na pia baadhi ya tabia bado hamjazijua kiasi cha mie kufikia kuchoka namna hiyo. ngoja niwaambie kitu.
kijana anapokea boom na pia all the way nimekuwa nampa financial back up regardless kuwa yeye anapokea boom ila mind you wakati mie nasoma sikupokea financial assistance ya mtu yeyoye maana dada alikuwa masomoni na pia hilo hilo bum langu nilikuwa namtumia na yeye. Nikiwa chuoni nilifanya kila aina ya kazi kujikimu.
Ila kwa huyu kijana yeye ni the opposite. Maana laki moja inaisha ndani ya wiki 2!!
So inapotokea mtu unakuwa mfuatiliaji wa masuala yako ya kifedha ndio unakuwa mbaya jamani?
Alikataa shule ya serikali tukampeleka private. Mbona mie nimesoma serikalini huko huko. Tena alingoja hadi kafanyiwa shopping yote na kaenda ndio kaleta ujinga wake.
Jamani yaani ni mengi huyu mtoto kayafanya yanayoumiza tangu na tangu na muda wote huo nimekuwa nampa second chance.
what else should I do now? so isiwe kuwa nashambuliwa kuwa mie ni irresponsible wakati I have done all I could tangu nasoma hadi naingia kazini.
 
Hakuna kitu kigumu kama kuishi na mtoto wa mtu tena aliyefiwa na wazazi wake wote wawili. Hawa watoto wanakuwa na msongo mkubwa wa mawazo, vichwani mwao wameshajiwekea ulonlyness. Mimi nadhani ulipaswa kujiuliza endapo mwanao angefanya hivyo, wewe ungechukua uamuzi wa kumchunia?
Mimi nadhani, inapaswa kuwekwa elimu juu ya kuishi na watoto yatima.
 
You have made a point man The Donchop
 
maisha mafupi
mtu asikustress
hao ndugu ni magunia tu (baadhi)
kuna ndugu tumeuza nyanya ili wasome leo wanatutukana

hivyo ushauri ninaokupa kutokana na eksipiriensi yangu

let them be

siku wakiamua kukufuata kuyaongea mtayaongea

wasipotaka wale kona

Jamani ndugu zangu naona wengi mmeangalia upande mmoja ti wa mtoto na pia baadhi ya tabia bado hamjazijua kiasi cha mie kufikia kuchoka namna hiyo. ngoja niwaambie kitu.
kijana anapokea boom na pia all the way nimekuwa nampa financial back up regardless kuwa yeye anapokea boom ila mind you wakati mie nasoma sikupokea financial assistance ya mtu yeyoye maana dada alikuwa masomoni na pia hilo hilo bum langu nilikuwa namtumia na yeye. Nikiwa chuoni nilifanya kila aina ya kazi kujikimu.
Ila kwa huyu kijana yeye ni the opposite. Maana laki moja inaisha ndani ya wiki 2!!
So inapotokea mtu unakuwa mfuatiliaji wa masuala yako ya kifedha ndio unakuwa mbaya jamani?
Alikataa shule ya serikali tukampeleka private. Mbona mie nimesoma serikalini huko huko. Tena alingoja hadi kafanyiwa shopping yote na kaenda ndio kaleta ujinga wake.
Jamani yaani ni mengi huyu mtoto kayafanya yanayoumiza tangu na tangu na muda wote huo nimekuwa nampa second chance.
what else should I do now? so isiwe kuwa nashambuliwa kuwa mie ni irresponsible wakati I have done all I could tangu nasoma hadi naingia kazini.
 
Jamani ndugu zangu naona wengi mmeangalia upande mmoja ti wa mtoto na pia baadhi ya tabia bado hamjazijua kiasi cha mie kufikia kuchoka namna hiyo. ngoja niwaambie kitu.
kijana anapokea boom na pia all the way nimekuwa nampa financial back up regardless kuwa yeye anapokea boom ila mind you wakati mie nasoma sikupokea financial assistance ya mtu yeyoye maana dada alikuwa masomoni na pia hilo hilo bum langu nilikuwa namtumia na yeye. Nikiwa chuoni nilifanya kila aina ya kazi kujikimu.
Ila kwa huyu kijana yeye ni the opposite. Maana laki moja inaisha ndani ya wiki 2!!
So inapotokea mtu unakuwa mfuatiliaji wa masuala yako ya kifedha ndio unakuwa mbaya jamani?
Alikataa shule ya serikali tukampeleka private. Mbona mie nimesoma serikalini huko huko. Tena alingoja hadi kafanyiwa shopping yote na kaenda ndio kaleta ujinga wake.
Jamani yaani ni mengi huyu mtoto kayafanya yanayoumiza tangu na tangu na muda wote huo nimekuwa nampa second chance.
what else should I do now? so isiwe kuwa nashambuliwa kuwa mie ni irresponsible wakati I have done all I could tangu nasoma hadi naingia kazini.

Better act like a woman and think like a men,be a man and be responsible usilalamike km mke Hapa,mpe hela akasome fanya yako and stop being selfish it's the only way
 
Mmmh nasikia harufu ya wewe kushikwa na mkeo juu ya malezi ya huyo mtoto ,hii ni kutokana na majibu ya huyo dada ako!!..but its not fair wewe ni kama baba yake no matterwhat mtoto akinyea mkono !!!...
 
  • Thanks
Reactions: amu
Hakuna kitu kigumu kama kuishi na mtoto wa mtu tena aliyefiwa na wazazi wake wote wawili. Hawa watoto wanakuwa na msongo mkubwa wa mawazo, vichwani mwao wameshajiwekea ulonlyness. Mimi nadhani ulipaswa kujiuliza endapo mwanao angefanya hivyo, wewe ungechukua uamuzi wa kumchunia?
Mimi nadhani, inapaswa kuwekwa elimu juu ya kuishi na watoto yatima.

On point yaani mavi lazima yashike chupi,well said mkuu
 
Jamani ndugu zangu naona wengi mmeangalia upande mmoja ti wa mtoto na pia baadhi ya tabia bado hamjazijua kiasi cha mie kufikia kuchoka namna hiyo. ngoja niwaambie kitu.
kijana anapokea boom na pia all the way nimekuwa nampa financial back up regardless kuwa yeye anapokea boom ila mind you wakati mie nasoma sikupokea financial assistance ya mtu yeyoye maana dada alikuwa masomoni na pia hilo hilo bum langu nilikuwa namtumia na yeye. Nikiwa chuoni nilifanya kila aina ya kazi kujikimu.
Ila kwa huyu kijana yeye ni the opposite. Maana laki moja inaisha ndani ya wiki 2!!
So inapotokea mtu unakuwa mfuatiliaji wa masuala yako ya kifedha ndio unakuwa mbaya jamani?
Alikataa shule ya serikali tukampeleka private. Mbona mie nimesoma serikalini huko huko. Tena alingoja hadi kafanyiwa shopping yote na kaenda ndio kaleta ujinga wake.
Jamani yaani ni mengi huyu mtoto kayafanya yanayoumiza tangu na tangu na muda wote huo nimekuwa nampa second chance.
what else should I do now? so isiwe kuwa nashambuliwa kuwa mie ni irresponsible wakati I have done all I could tangu nasoma hadi naingia kazini.

Are you serious:what:😱
Laki moja inaisha kwa wiki 2:what:...trust me anajibana sana....mimi laki moja natumia kwa wiki moja tu mkuu. Enzi wewe unasoma chuo vitu vilikua bei chee compared na sasa.... kwa sasa bila anasa mwanachuo kwa siku anatumia sh10000...nakushangaa huyo dogo anawezaje kutumia laki moja kwa wiki 2. Mimi ni mwanachuo...natumia laki 1 kwa wiki 1.
Wewe kwa maelezo tu unaonekana kabisa ni kiburi na don't care. Jitafakari upya bro.
 
Back
Top Bottom