Nimekusoma mkuu na nakupatia pole yangu ya dhati. Ninakubaliana nawe kwa kiasi kikubwa maana kwa asilimia nyingi vijana wa siku hizi wamekuwa watata hasa kwenye nidhamu na uaminifu katika pesa.
Imekuwa kama mtu anasoma ili alipwe.
Nakumbuka miaka yetu ya nyuma mtu unaenda shuleni hata Telegram ikiitwa assembly, unashangaa kuwa heee , safari hii nyumbani wamenitumia.
Lakini vijana wa sasa ni kama kusoma ni 'ajira' kumbe ni faida yake.
Vilevile, nidhamu imekuwa katika mita ya chini kabisa. Mashindano unayaona waziwazi. Uko wapi unyenyekevu jamani? Hata kama nakusaidia ndio unisemee ufedhuli?
Nasikitika wengine wanasema eti mtoto ni mtoto tu, kwakweli hapa naomba nitofautiane. Ndio maana kwenye kitabu tunachokiamini wengine, kuna amri moja kati ya zile kumi yenye ahadi , kuwa waheshimu baba na mama ili upate kuwa na siku nyingi duniani.
Sasa kama huyu ndugu (mkuu) ni 'default baba' kwa huyu kijana , anastahili heshima. Tusipende kurahisisha vitu.
Na kwenye familia pia, si kweli wakati wote kuwa dada au sibling yuko sahihi anaposema neno juu yako just kwa sababu ni sibling. Wengine ni vyanzo vya faraka kwa vile wana mashindano na pengine wivu so akipata jambo la kushikia bango, basi lazima ata -side na upande unaokupinga.
Tumeyaona haya na tunaendelea kuyaona katika familia na kwa vile wengine wamejaliwa mishipa migumu kama PVC pipes, hata anaposema neno la uongo, hakapui hata jicho, kiasi mtu mwingine anaweza dhania ni ukweli.
Mwisho, naomba pia tunaosaidiwa na hasa kama watu sio wazazi wako ( inakuwaga assumed kuwa wazazi can put up with almost every mischief ya watoto wao) , uongeze staha maana mtu anakuwa anafanya hisani kwa kweli so ni vema mtu ku ji position nafasi yako husika na sio kutaka makuu.
Ikifika hapo , nawapendaga kidogo wenzetu wazungu ambao, kiukweli, primary concern yao na gist ya maisha yao ni spouse na watoto wao. Mengine ni ziada sana na anaweza akamsaidia hata mtu baki, mradi amependa. Ndio maana hata leo hivi, hawatujui lakini bado tunapata misaada yao na grants.
Ila haya ya mtoto wa binamu sijui mtoto wa nini, asilimia kubwa mwisho wake gharama na sonona though tunaona kama ndio tunapendana na kujaliana lakini kiukweli kabisa, shukrani ni adimu sana, zaidi sana lawama, kashfa na msongo.