Jamani, mtoto anatuchonganisha familia nzima!

Jamani, mtoto anatuchonganisha familia nzima!

Kuna watoto wanasoma kwenye mazingira magumu na wana wazazi lakn mzazi hana huo uwezo wa kumpa hela ya ziada kwahyo wanatumia hilo hilo boom sembuse huyo yatima kapata familia inamjali kiasi hicho pamoja na madhaifu yake lakn bado analeta jeuri anataka kuwaendesha atajavyo, hapana its time apewe tough love ili ajifunze, me nazan endelee tu kuwa kimya usimuulize dada yako kitu chochote kuhusiana na huyo mtoto waache waendelee wenyewe na kwa tabia za huyo mtoto sasahv dada yako nae atajionea na yatamshinda
Kweli muu huyo kijana hajitambui eti 10,000 kwa siku haitoshi kwani watoto wa wauza maji hawasomi , mbona wanasoma kwa hela ya boom na kusaidia wadogo zao. Huyo kijana ni mgombaishi na sasa atawachanganya zaidi kwani ameshapata wa kumtetea . Huyo dada mtu aachwe ili aje ajionee kwani vijana wa tabia hizi huwa hawaachi kufanya mazoea yao. Jambo la maana ni huyu mkaka kuendelea na maisha yake , hivi vitu vidogo ukivipa nafasi moyoni mwako lazima vitakusumbua binadamu wengie hata uutoe uhai wako bado wataona ulipaswa kufanya zaidi. Kijana mkubwa namna hii anashinddwa kutoa taarifa kwa walezi wake kama anaumwa??????????????????????????
 
Ni sahihi usemayo mi sidhan kama huyu kijana angetoa taarifa kwa huyu kaka anaumwa angemshiti mbona anaonekana anaroho nzuri sana jaman tena huyo mvulana anajidekeza watu wanaishi chuo only booom ni kwa kila kitu pia ifike wakati asitakke kuwa kama mtoto wa mwenyenyumba lzma ajifunze kitu watu wanahangaika kutafuta eneo lenye chakula bei nafuu ili waweze kubana bajet hata kama mi siamin mvulana mwenye miaka 25 hajui bajet ni makusudi anafanya makusudi hawa ndo vyuon akina sharo mambo mengiiii ka mtoto wa raus duuuh haya sasa wenzie wakumsaidia wanagombana ye anajisikiaje wanadaiana had michango ya harusi too bad,kaka huyoo muongezee kiburi na hata kama mtayaongea na dada yako yatakwisha kwny msimamo wa matumizi ya pesa ubaki palepale usimpe nafasi akutawale
 
kama ni chuo sote tumesoma boom hiyohiyo ndo tulikua tunaripa kodi ya nyumba nauli pamoja na chakula lakini tulimaliza

Mtoto hana Adabu kabisa...BUT,,,Ukipiga fare go and return,lets approximate 1000

Chakula cha bei rahisi 1500 times 2= 3000

Maji ukijibana sana 2ltrs= 1200,

Hapo breakfast uliskip

Printing 100,lets say una assignment siku hiyo,,,vyuo vingine ka nlichosoma mimi hakuna hostel so wapanga mtaani,

Unajikuta kwenye cost kama,umeme,maji , mara oh,mtu wa kumwaga uchafu,lol!!
 
Nimesoma story ila kiukweli wewe ndo una makosa maana kama angekuwa mwanao ungemuacha kwa miezi bila kuongea nae au kumjulia hali?huyo mwanao bado ni mtoto anatakiwa aelekezwe hata kama ni mkorofi au whatever maana naamini mtoto akijisaidia kiganjani kwako huwezi kujikata but unajisafisha so ulitakiwa umfundishe hadi arudi kwenye mstari kama wababa wengine wanavyofanya kwa watoto wao

mimi wakati nasoma chuo, mawasiliano na wazazi wangu hayakuwa ya kira mara. especially wazazi wa kiume huwa haiwasumbui.
kama nimepatwa na shida basi ndo tunawasiliana. ama kwa salamu ni mata moja moja sana. ukiona kimya maranyingi huwa tuna assume upo salama.
 
Kama uliamua kubeba jukumu kama mzazi, hukutakiwa kumuacha mtoto peke yake kwa kipindi chote hicho bila kumjulia hali mtoto No matter how stubborn he is, ebu jiulize angekuwa mtoto wako wa kumzaa ungemfanyia hivyo?, watoto yatima ni ngumu sana kuishi nao, wana uchungu sana. Ushaur wangu kaeni kama familia ombaneni msamaha muyamalize full stop. Usichoke kutenda wema

Kama angetuma the very same msg?I xud have done the same
Anapaswa kujitambua sio sababu MTU anafanya kazi basi hela IPO tu ni upumbaav na wala usimtetee huyo kid
Alishindwa nn kufuatilia hyo medical feee?
na dada aka shangaz MTU anajua kabisa in charge Wa masuala ya mtoto wao ni kaka yake aka mjomba MTU sasa kwann ajiingize bila kumuuliza jamaa chochote?ts obvious either anajua kila kitu na yeye ndo source au ametumia kama advantage kumuumiza jamaa sababu ana ajenda ya siri kuhusu Mke Wa jamaaa
 
Kwa kuwa wote ni watoto sio jambo kubwa ila nitajaribu kukuelekeza kama ningalikuwa ni mimi. Upendo haufundishwi na mtu lakini kila mtu anaujua. Ndugu yako akikuambia shida yake ana maana anakupenda, anakutegemea na kukuthamini. Hakuna mtu anayependa kumweleza mtu mwingine shida yake kama hamtegemei wala hana mahusiano naye. Kijana alikutegemea kwa sababu ni baba yake mdogo na kubwa zaidi umekuwa msaada wake mkubwa kwa muda mrefu. Mazoea hujenga tabia.
Kama ungalikuwa huna uwezo ungalieleza tu kuwa hali yako kifedha kwa wakati ule ilikuwa sio nzuri kifedha , nina hakika angalikuelewa. Sio kumsimanga kama vile anakupiga mabomu nk nk. Mtoto mkiwa ingawaje wana sema hadeki, lakini ukweli ni kuwa ni mwepesi sana kujisikia vibaya (fragile) kuliko mtoto mwenye wazazi wote wawili ukimtendea kinyume cha matarajio yake.
Unasema ulimpa kadi yako ya bima ya Afya. Kadi haitoi pole, haijadili wala haionyeshi upendo wa aina yoyote. Kadi haimpi mgonjwa soda wala chungwa, kadi ni kwa dawa tu. Mgonjwa anahitaji faraja na faraja ni tunda la upendo. Kwa kukataa kwako kwenda kumuona hata kumpigia simu, unadai mgonjwa ndiye akupigie umepungukiwa upendo. Huenda kiasi cha upendo moyoni mwako ni kidogo sana kinaishia kwa mkeo hivyo unakuwa huna salio lililobakia ili utoe pia kwa ndugu zako.
Inawezekana, kabla ya kuoa ulikuwa unawapenda na kuwajali ndugu zako sasa baada ya kuoa umeishiwa upendo. Hii inaweza kuwa ndiyo sababu dada yako anaona unamjali tu mkeo na ndugu zake. Anachosema dada yako ana uhakika nacho kwa sababu anakujua, na mimi naungana naye kwa kuwa hata mtoto wa kaka yako ulimpenda na kumsomesha kabla ya kuoa. Inawezekana majukumu yameongezeka lakini hata kupiga simu kumtakia kheri mtoto wako? Umesema ni mwanafunzi unataka yeye ndiye akupigie simu, anapata wapi salio wakati hata pesa za matumizi humpi? Jipange kijana jipange. Udugu kufaana sio kufanana
Habari za usiku huu wanajamvi? Poleni sana kwa mihangaiko ya siku nzima ya leo pia kwa wale wakazi wa Dar poleni sana kwa foleni ya siku ya leo. Hope baada ya kufika now tupo kwenye jukwaa letu pendwa.

Now back to the topic, hapa nilipo nina kisirani na kero ambayo hata imechangia kuharibu siku yangu tangu usiku wa jana, kisa mtoto wa ,marehemu kaka yetu. Ipo hivi; kaka yetu mkubwa alibahatika kuzaa akiwa shuleni miaka hiyo.

Huyo mtoto nimepishana naye kama miaka mitano so kwa kiasi Fulani nimekua naye kabisa kama mdogo wangu wa kunifuata maana mie die kitinda mimba katika familia yetu. Huyu mtoto amekuwa na tabia za ajabu sana tangu akiwa mdogo kama vile ubinafsi, matumizi mabaya ya fedha, uchonganishi, kiburi na mengineyo mengi ambayo hata kwa sasa ndio yamenipelekea naandika uzi huu.

Tumeanza kumlea tangu tangu akiwa na umri wa miaka mitatu baada ya wazazi wa mama yake kutuzilia hapo ndio ikawa hadi wazazi wake wanafariki katikati na mwishoni mwa miaka ya tisini. So hadi wazazi wetu nao pia wanafariki alikuwa ni mdogo sana ndio kwanza yupo form one wakati mie nipo form six. In short baada ya mie kumaliza chuo na kuanza kazi ikawa ni jukumu letu na dada yangu kumsomesha huyo mtoto ili nae apate msingi bora wa maisha ingawa alikuwa na usumbufu ila darasani hakuwa haba kwa kweli.

Nakumbuka mwaka juzi alichaguliwa kujiunga na chuo kikuu kimoja hivi cha binafsi hapa nchini, kweli tulijipinda na kumpeleka. Akiwa huko vibweka havikuisha kabisa kwa kupiga vibomu vikubwa vikubwa huku na huku (kwangu na sister). Baada ya kushitukia hila zake dada alipendekeza mie kuwa ndie in charge bila ya kujua kuwa naingia kwenye shimo la moto nikakubali.

Akiwa chuo alipiga bomu moja kubwa sana akijumlishia na gharama za medical capitation, wakati huo bima anatumia kadi ya bima ya afya ya kwangu niliomkatia. Nijuavyo ni kuwa chuoni kama mtu una bima ya afya ya shirika Fulani unaweza usichangie hiyo medical capitation given kuwa umeweka taarifa zako bayana kuwa una bima gani na ni mwanachama hai
So baada ya hiko kibomu nikiwa pamoja dada yangu nilimpa taratibu za kufuata ili kuweza kuweka mambo yake sawa ili kupunguza gharama zisizokuwa za lazima kwangu na dada. Alionekana dhahiri kutoridhika na ile proposal yangu ila nikakomaa nae nikamwambia kuwa nampa siku tatu afanye follow up then when he is done anambie alipofikia kama kaweza au la. Basi ile kumwambia vile ndio ikawa kama nimekata undugu maana sikupata hata missed call kutoka kwake hadi wiki inaisha. Nikaona sasa isiwe taabu maana shida zake yeye anataka tena alete kiburi, so na mie nikawa jeuri nikakaa kimya.

Amini msiamini ilikuwa ni mwezi wa 9 mwaka jana alikaa kimyaaaa hadi mwezi wa 12 tarehe 31 aliponitumia message inasema “hello papaa! Happy new year. Yo ma dad and am ya son. I always love you ila kama ni shida zangu nitajitahidi kutokukushirikisha…” Hiyo text nimecopy na kupaste kama alivyotuma nothing added or removed. Kwa kweli ilinikera na nikaona kama anajiona tayari kajipanga kimaisha, let him be. Niliendelea na ukimya wangu ili kuepusha shari na wala sikutaka kumwambia mtu.

Jana usiku wa saa nne nilimpigia dada simu kumjulia hali ndio hapo ikawa balaa sasa. Dada aliuliza “mara ya mwisho ni lini ilikuwa kuongea na mwanao?”

Nilimwambia kila kitu juu ya misbehavior za mtoto. Alichonambia ni kuwa mie nakuwa mjinga na katili. Akaendelea kuwa kama hapo ukiambiwa mwanao anaumwa je? Nikajibu kuwa kwa kuwa ana bima ya afya basi mie wala sitokuwa na wasi na kama akihitaji msaada kama kweli nitatoa msaada wangu kwa kadiri niwezavyo.

Basi hapo dada yangu aliwaka vibaya mno kuwa mie katili, mtoto wiki ya tatu hii anaumwa halafu mie natoa majibu mepesi… what I told her ni kuwa je ningeota au ningejuaje kama yeye aliamua kukaa kimya.
Dada aliendelea kuwaka na kunivisha kila aina ya ubaya akimtetea mtoto. (sijui wana ajenda gani ya siri maana it seems wao wana mawasiliano ya karibu ambayo mie siyajui na sijui wanaongea nini).

Baada ya kuona vile dada anakuja juu nilikata simu kwa hasira. Hakuishia hapo, alituma message ikisema “Ahsante umekuwa nashukuru, nakuacha kama ulivyosema ndugu zako ni hao wa mkeo ila…”

Hapo pia nilishindwa kuelewa mke wangu anaingilia wapi jamani? Yaani usiku wa jana ulikuwa mchungu, kazi hazikwenda leo na hata sasa nipo mood less.

Hapa nashindwa kuelewa kosa langu lipo wapi? Je mwisho wa haya yote ni nini? Huyu mtoto nimfanyaje? Naombeni ushauri na maoni yenu wadau na pia samahani kwa posti ndefu namna hii but I was trying to explain the situation exhaustively.

Karibuni.
 
Kwa kuwa wote ni watoto sio jambo kubwa ila nitajaribu kukuelekeza kama ningalikuwa ni mimi. Upendo haufundishwi na mtu lakini kila mtu anaujua. Ndugu yako akikuambia shida yake ana maana anakupenda, anakutegemea na kukuthamini. Hakuna mtu anayependa kumweleza mtu mwingine shida yake kama hamtegemei wala hana mahusiano naye. Kijana alikutegemea kwa sababu ni baba yake mdogo na kubwa zaidi umekuwa msaada wake mkubwa kwa muda mrefu. Mazoea hujenga tabia.
Kama ungalikuwa huna uwezo ungalieleza tu kuwa hali yako kifedha kwa wakati ule ilikuwa sio nzuri kifedha , nina hakika angalikuelewa. Sio kumsimanga kama vile anakupiga mabomu nk nk. Mtoto mkiwa ingawaje wana sema hadeki, lakini ukweli ni kuwa ni mwepesi sana kujisikia vibaya (fragile) kuliko mtoto mwenye wazazi wote wawili ukimtendea kinyume cha matarajio yake.
Unasema ulimpa kadi yako ya bima ya Afya. Kadi haitoi pole, haijadili wala haionyeshi upendo wa aina yoyote. Kadi haimpi mgonjwa soda wala chungwa, kadi ni kwa dawa tu. Mgonjwa anahitaji faraja na faraja ni tunda la upendo. Kwa kukataa kwako kwenda kumuona hata kumpigia simu, unadai mgonjwa ndiye akupigie umepungukiwa upendo. Huenda kiasi cha upendo moyoni mwako ni kidogo sana kinaishia kwa mkeo hivyo unakuwa huna salio lililobakia ili utoe pia kwa ndugu zako.
Inawezekana, kabla ya kuoa ulikuwa unawapenda na kuwajali ndugu zako sasa baada ya kuoa umeishiwa upendo. Hii inaweza kuwa ndiyo sababu dada yako anaona unamjali tu mkeo na ndugu zake. Anachosema dada yako ana uhakika nacho kwa sababu anakujua, na mimi naungana naye kwa kuwa hata mtoto wa kaka yako ulimpenda na kumsomesha kabla ya kuoa. Inawezekana majukumu yameongezeka lakini hata kupiga simu kumtakia kheri mtoto wako? Umesema ni mwanafunzi unataka yeye ndiye akupigie simu, anapata wapi salio wakati hata pesa za matumizi humpi? Jipange kijana jipange. Udugu kufaana sio kufanana

Hapo kwenye red mkuu umesahau kuwa I am 5 years older than him and that does not take away my respect as a father though not biologically. Unaposema kuwa bima haitoi pole na blah blah zingine kumbuka ya kuwa tupo mikoa miwili tofauti na miles apart. Sasa kama mtu anapewa task na anaamua kukata mawasiliano tafsiri yake ni nini? simply ni kiburi
The thing ni kuwa kama yeye baada ya kufuatilia na kuona kama kashindwa si angepiga simu au hata kubip kama salio hana? Ila kwa kuwa yeye alijiona ya kuwa labda kapata nguvu ya kusimama yeye and I let him be maana nina vitu vingine pia vya kuhofia na kujali zaidi ya yeye mtu mzima na akili zake mwenye nywele kila kona.
kuhusu dada yeye amegombana na karibia ndugu wengine wote and I was the only one left and so now am in the list.
 
Nimerudi kwa mara nyingine wadau nikiwa nimefikia maamuzi baada ya kukaa na kuangalia hoja za wadau mbali mbali kupitia michango ya kwenye hii thread na pia pm.
Msimamo niliochukua ni kuwa kwa sasa naendelea kukaa kimya kwa wote n matter what. niw eke focus yangu kwa mke familia yangu na shule nayotegemea kuanza september this year.
Ahsanteni kwa michango yenu wadau na pia nakaribisha mingine zaidi ambayo ni jengefu.
 
uyo Mtoto analengo la kuwafalakanisha we achana nao me kuna mdogo Wangu alikuwa anasoma kwa asilimia kubwa me nilikuwa namgharamia Mtoto akaanza mambo ya ajabu nikawaambia wazazi wake Baba akaelewa issue ila mama akawa anaongea kwa siri na mdogo wang mwisho nikageukiwa mimi wakanitolea maneno mabaya sana nikakaa kimya dogo kamaliza form four mwaka jana matokeo kafeli na wao wananipigia kuomba msaada ili uyu Mtoto arudie shule wewe piga kimya watakutafuta tu
 
Kaongee na dada yako physically. Mwambieni asome aachane na tamaa ya maisha, aishi kama dent na si kama mfanyakazi.
 
Mkuu kusema ukweli sijaona kosa la mtoto na pia dada yako yuko sahihi. Yaani kuanzia mwezi wa 9 mwaka jana mpaka leo hujui mtoto anaishije kisa alikuomba hela unayosema ni nyingi.

Unadiriki kusema eti "shida zake akuletee kibri" which means you don't care. Kwanini kama unaona anamapungufu usimwambie ili ayarekebishe. Mwanafunzi wa chuo siyo mtoto mdogo ni mtu mzima bana.

Nadhani sms aliyokutumia mwezi dec ni kaa la moto moyoni kwako ila jitahidi ubadirike.

Hata wewe hukuzaliwa na pesa mkuu, Mtafute muongee mmalize tofauti zenu pia uendelee kumhudumia kama mwanafamilia.

Kumbuka hata yeye hakupenda kupoteza wazazi wake na pia wewe siyo jiwe wala mlima kwamba utaishi milele. Just imagine umepass away then wanao wakawa wanahitaji msaada wa namna hiyo.

Anyway naomba nikuulize. If that was your own son, would you have abandoned him like that just because of begging you money?
Sidhani huu ushauri ni wa maana kwani ukitaka cha uvunguni sharti uiname. Siamini hata akiwa mtoto wako unampa fedha yeye hakuheshimu.
 
Hapo kwenye red mkuu umesahau kuwa I am 5 years older than him and that does not take away my respect as a father though not biologically. Unaposema kuwa bima haitoi pole na blah blah zingine kumbuka ya kuwa tupo mikoa miwili tofauti na miles apart. Sasa kama mtu anapewa task na anaamua kukata mawasiliano tafsiri yake ni nini? simply ni kiburi
The thing ni kuwa kama yeye baada ya kufuatilia na kuona kama kashindwa si angepiga simu au hata kubip kama salio hana? Ila kwa kuwa yeye alijiona ya kuwa labda kapata nguvu ya kusimama yeye and I let him be maana nina vitu vingine pia vya kuhofia na kujali zaidi ya yeye mtu mzima na akili zake mwenye nywele kila kona.
kuhusu dada yeye amegombana na karibia ndugu wengine wote and I was the only one left and so now am in the list.
Acha kupoteza wakati na watu wanafiki. Mtu akitaka msaada wako lazima akupe heshima yako. Akijifanya kujua achana naye mpaka aone umuhimu wako. Usitoe senti ati kwa vile ni yatima au ndugu, achana na huo ujinga, kama unataka changu niheshimu period. Pesa inatafutwa kwa jasho baba
 
Nimerudi kwa mara nyingine wadau nikiwa nimefikia maamuzi baada ya kukaa na kuangalia hoja za wadau mbali mbali kupitia michango ya kwenye hii thread na pia pm.
Msimamo niliochukua ni kuwa kwa sasa naendelea kukaa kimya kwa wote n matter what. niw eke focus yangu kwa mke familia yangu na shule nayotegemea kuanza september this year.
Ahsanteni kwa michango yenu wadau na pia nakaribisha mingine zaidi ambayo ni jengefu.

Good decision
 
baeleze baelewe
 
Acha kudandia koki, utarowa bure.

Mzazi gani anamnunia mtoto? Ptuuuu
Mtoto gani hana heshima kwa mzazi????? Nani anatakiwa kwanza amnyenyekee mwenzie? Mtoaji au mpokeaji? Ingawa mimi ni kijana lakini nasikitika sana na sisi vijana ambao hatuna adabu kwa wanaotufadhili. Halafu watu wazima mnatudekeza ati mzazi hamnunii mtoto. Nini maana ya sanctions kama zinazotumika sasa kwa Russia. Kunyamaza au kama unavyodai kususia ni sanction ili ajirekebishe. Afterall nani mwenye shida na mwenzake? Mnatulea vibaya jaribu kutuongoza si kutudekeza
 
Nimerudi kwa mara nyingine wadau nikiwa nimefikia maamuzi baada ya kukaa na kuangalia hoja za wadau mbali mbali kupitia michango ya kwenye hii thread na pia pm.
Msimamo niliochukua ni kuwa kwa sasa naendelea kukaa kimya kwa wote n matter what. niw eke focus yangu kwa mke familia yangu na shule nayotegemea kuanza september this year.
Ahsanteni kwa michango yenu wadau na pia nakaribisha mingine zaidi ambayo ni jengefu.

Mkuu Nyaupindo uamuzi.mzuri..ila nilitaka pia kukushauri umuulize dada yako na vingine anavokudai ujue kabisa maana hiyo laki nne hukujua kama amekukopesha...ili kama vipi umtumie tu halafu upige issue zako...concentrate na afya ya mkeo....baas.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom