Jamani hivi wenzangu huwa mnatongozaje?

Jamani hivi wenzangu huwa mnatongozaje?

Aise!! unajua naweza nikawa nimeplan kabisa kwamba namwanzia hivi na vile, lakini nikishamfikia tu plani zote zinapote.

Angalia "The Gods Must be Crazy" umfuatilie yule jamaa mtafiti wa wanyamapori alivyokuwa anafanya rehearsal ya kumtokea "teacher"...

"...it's an interesting psychological phenomenon..., a-ya ya ya ya yaaaah!"
 
kinachomshinda dogo ni pick up lines jinsi ya kudraw attention ya demu at the first sight

Ingekuwa enzi za ujana wetu wakati watu bado wana huruma na matapeli/majambazi hayajawa mengi alitakiwa akipita tu mbele yake ajiangushe. Lazima dada angempapole na kumwuliza kama ameumia au vp...Lakini sasa hivi, thubutu! Hakuna mwenye time na wewe hata ukizama kwenye chemba ya maji machafu pale Kariakoo!
 
Ukitaka ujue kutongoza kubali kufungua mdomo mbele yake kwa maana ya kuongea chochote tu kumhusu yy eg. kumuuliza au kumsifia, then anzia hapo.
 
Ila kutongoza hakuna formula maalum wakuu so mwana ajipange tu na awe na confidence za kutosha tu
Hakuna mtu atakufundisha kutongoza zaidi ya kukuhadithia yeye alitongozaje na wenfine huwa hawakumbuki alimzingua vipi girl wake for the first time
 
Kama mwanamme hauna hela hata upangilie mashairi yako vyema kuliko hata Mzee Sudi Amir Andanenga"Sauti ya Kiiza"bado kwa wasichana utaonekana mwehu tu!

Mambo ni pesa tu haya ya kutongoza ni makelele tu!!

Hao wanaokula kwa pesa hawana tofauti na wanaonunua machangu kwa kuwa hawawezi kutongoza.
CONFIDENCE tu inaweza kumfanya mwanaume choka mbaya akawala warembo ambao wanaonekana wanaogopwa hata kwa fedha.
 
Kuna msichama mrembo wa bure siku hizi kaka?Mm nikiwa sina kitu wala sijihangaishi kuwafuata warembo maana ni kudharirika tu

Kama hautaki kutumia pesa kila mwanadada mrembo utaishia kumuita shemeji tu!
 
Tatizo lako unaishi kwa kukariri mambo! unajua nini kuhusu female psychology? unadhani hata hao wenye pesa huwa wanatoa kiasi kikubwa kama inavyotegemewa?
 
Wewe shida yako kubwa unaogopa mavazi,mtu asikudanganye wanawake wote hawajapishana katika tabia za msingi. Wanawake wanapenda kusifiwa,kuheshimiwa na kuwajali,ukizingatia hivo vitu unaweza ukamuingia mwanamke yeyoye. Lakini ukiwa na dharau na maneno ya kashfa hata sumu utawekewa ufe kabisa.

Wewe umemaliza kabisa.

Rafiki yangu mmoja amepata katoto kazuri kirahisi.

Siku moja wakati anakuja kazini, nyuma yake alikuwa anakuja binit mmoja mzuri anafanya kazi jengo moja na jamaa ila ofisi tofauti. Alipofika getini jamaa akamwambia mlinzi "Mwambie huyo dada anayekuja amependeza"

Mlinzi akafikisha salamu....

Baada ya siku kama mbili ikatokea incident kama hiyo hiyo, mlinzi akamwambia tena nimeambiwa nikwambie umependeza, binti akamwambia yule mlinzi me naona unanichezea akili, next time akipita aache namba yake nitamtafuta...

Jamaa kesho yake kaacha namba, usiku binti kampigia and the rest is history... Kapata chombo kiulaini.
 
Tatizo lako unaishi kwa kukariri mambo! unajua nini kuhusu female psychology? unadhani hata hao wenye pesa huwa wanatoa kiasi kikubwa kama inavyotegemewa?

Mhhh naishi kwa kukariri wkt tunayaona haya mitaani?Toka zako Mbagala huko na ndala zako mkute Sitti Mtemvu hapo Mliman City mtokee uone jibu lake

Hehehehehehe mapenzi" nakupenda toka rohoni" waliondoka nayo wazazi wetu kaka
 
kitu kidogo mpge teke adondoke akiumia ataenda kuchukua rb au ataomba wewe umuhudumie apone hapo ndo sehemu ya kuchukua namba simple way.
 
ImageUploadedByJamiiForums1413611308.002055.jpg
Mwenzake huyu hapa
 
Mhhh naishi kwa kukariri wkt tunayaona haya mitaani?Toka zako Mbagala huko na ndala zako mkute Sitti Mtemvu hapo Mliman City mtokee uone jibu lake

Hehehehehehe mapenzi" nakupenda toka rohoni" waliondoka nayo wazazi wetu kaka

Mkuu hata huyo sitti anavaa ndala, ila ni kutegemeana na wapi alipo. Hata wewe ukivaa kuendana nae unamnyaka tu, pesa za nini wakati babake anazo? usidhani kila mrembo anapenda kununuliwa kama unavyodhani.
 
Kama mwanamme hauna hela hata upangilie mashairi yako vyema kuliko hata Mzee Sudi Amir Andanenga"Sauti ya Kiiza"bado kwa wasichana utaonekana mwehu tu!

Mambo ni pesa tu haya ya kutongoza ni makelele tu!!

Sio mara zote mkuu kuna watu hawana chochote lakini wanapiga mademu wa ukweli,unafikiri kwanini wenye mguu wa kuku wengi wanawafumua wapenzi wao? Pesa huwa inakuwa imeshindwa kuwadhibiti.Makapuku kibao wana mademu wakali.
 
Confidence tu hakuna cha zaidi na kila dada ana formula zake,pia kubali kutukana au kudhalilishwa ikibidi
 
Confidence tu hakuna cha zaidi na kila dada ana formula zake,pia kubali kutukana au kudhalilishwa ikibidi

Mkuu naungana na wewe kwamba, confidence ndio kila kitu, hata kama pesa unayo, kama huna confidence utamsogelea vipi mrembo na kupata ujasiri wa kumshawishi achukue pesa zako halafu akupe penzi? vipi akikataa utamshawishi na nini?
Hapo kwenye kutukanwa kupo ila kunategemea na maandalizi, kama ulianza kumzoea, hataweza kukutukana, labda umkute wa barabarani.
 
Sio mara zote mkuu kuna watu hawana chochote lakini wanapiga mademu wa ukweli,unafikiri kwanini wenye mguu wa kuku wengi wanawafumua wapenzi wao? Pesa huwa inakuwa imeshindwa kuwadhibiti.Makapuku kibao wana mademu wakali.

Mkuu mm yameisha nikuta haya hapa mtaani kwetu!Kuna demu mkali sana akahamia then demu akaulizia kwa wenyeji akaonyeshwa nani yupo saafi nani majalala!

Nilipakwa kweupe mkuu!Kama hauna kitu hupigi demu wa ukweli nakataa
 
Back
Top Bottom