Hivi wasichana huwa mnamaanisha nini mnaposema mna njaa lakini mkipewa chakula hamli?

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Sep 6, 2014
6,170
7,662
Habarini,

Yaanii daaa sijui nianzie wapi maanaaa ila ngoja nianzie hapa wanaume wenzangu mtakazia Mbele ya Safari

Sijuagi hawa ndugu zetu wasichana a.k.a mademu zetu kwa lugha nyepesi huwa wana maanisha nini? anakuja anakung'ang'ania kuwa ana njaa na angependa twende kula sehemu nzuri mwanaume huna hela lakini unajikaza unaamua kwenda naye kula unafika hotelini anaagiza chipsi kuku nusu pengine mzima na juice na makorombwezo kibao chakula kikifika anakula mikono miwili tuuu utasikia baby nimeshiba sana halafu hapa sio pazuri mimi sipapendi tuondokeee, yaaani unamwangilia huyo demu hummalizi unamwambia wambie wakufungie basi hicho chakula hataki ooh mimi sibebi

Yaani nimeshuhudia mara nyingi sana Hotelini wanaume wenzangu wakifanyiwa hivyo inaniuma sanaa kuona mwanaume mwenzangu anapoteza hela kizembe vile no matter anapesa au hana huwa napandwa na hasira hadi naamua kuhamia pale kwenye meza yenye chakula nile tuu kile chakula ili kupunguza hasira maana demu mwenye chakula kadokoa tuu kama kuku kamtoa ngozi kidogo na tuchips tuwilii tuu, juice ndo hajagusa kabisa ashachukua tishu anajipukuta

Yaani kwenye kutongozwa mnaleta pozi mashauzi mengi hadi kwenye mambo ya msingi kama chakula tena nilicho tumia hela kununua nako mnaleta poziii mnazingua sanaaaa!

Acheni mikwara ya nanasi nyie wakimama......Juzi hapa nipo sehemu nakula akaja jamaa na demu wake demu akagiza msosi wa maana jamaa akatoa pesa chakula kimefika demu akala kidogo sana kama vijiko viwili eti nimeshiba baby nilimuangalia kwa hasira nikashindwa kuvumilia nikasimama nikaenda mpaka kwenye meza yao kwa hasira nikasema wewe dada acha upumbavu huku nachukua zile sahani za chakula nikahamishia kwenye meza yangu nikafumua msosi wote na maji walikuwa amenunua na juice dada akacheka wakaondoka....yeye aliona kama sifa kumbe ujinga tuu haujui hata mpenzi wake hela kahangaikia vipi sembuse amekopa tuuu

Pia kuna siku Movie theater nimeshuhudia jamaa kaja na demu wake wakanunua tiketi elfu 12 kila mmoja jumla elfu 24 jamaa akatoa wakanunua na miwani klsababu ilikuwa ni 3D movie jamaa akatoa elfu 10 jumla 34 elfu wakachukua na pop corn za elf 5 na soda za kopo jamaa alitumia kama 50 ya haraka mle ndani tumeingia kwenye Movie inaanza tu matangazo demu akasema Baby huku baridi mimi siwezi kukaa tuondoke AC kali sana hiii, nilitamani nimfuate demu nimkate kelubu ya shingo! mshikaji akasema haya tuondoke

sasa demu alikuwa hajui movie theater huwa kuna kuaje? asee mnazingua kinyamaa mm kama ndo demu wangu nina kuwasha kibao kimoja cha uso
 
Kama una mpenzi na anakutibua na huwezi mwambia ukweli basi uko utumwani..

inatakiwa mpenzi wako ndo uwe nae free kwa kumueleza chochote kile
Mwingine ndo unakuka yuko kwenye process ya kutongoza so anaamua labda kutoa demu halafu ndo anamfanyia hivyo inakera sanaaa tena sanaaa
 
Kama na wewe ulimtongoza kwa kujifanya UNAZO PESA lazima AKUKOMOE. Ni vema mwanaume anapotongoza asijipe sifa ambazo hana! Akikujua hela yako ni ya kawaida hawezi kukuendesha hivyo!
 
Siku nyingine ukienda mahali kula au movie acha kufuatilia watu...

Pia acha kuhesabu hela za watu sijui soda popocorn viingilio utavunjika shingo
Hahahahahaha alinishangaza sana huyu mleta uzi, sijui ni mpelelezi
 
heheheheheheheh umenikumbusha siku niliyoumbuka, sitaisahau hiyo siku na kuanzia siku hiyo niliacha kuwa kama wewe.

Ilikuwa jioni maeneo flan ya watu wastaarab., niko na dogo rasi mmoja hivi tunapata cha jioni, mshikaji kaja na demu wake wakakaa meza moja nasi wakaagiza misosi demu akaagiza soda ya pepsi kdg jamaa akaagiza tangawizi demu akasema em nami leo niionje hii akaletewa akawa soda zote kaonja kdg kdg tu.. kuna mshkaj mwingine akakaa meza ya jirani jamaa akawa anaongea sana na yule mshkaji wa meza ya jiran... demu ili kurudisha attention kwake ilibidi amwambie msela eti anataka maji akaagiziwa maji lita moja nayo... hapo ndipo sisi tulipoanza kumjadili kwa kilugha kumbe demu alikuwa anatusikia...

Wacha tusalimiwe tu kilugha bila kuulizwa wakati wanasepa....

Lahaulaaaaaaaa
 
Hahahahahaha mkuu unamsema mtu unahisi hakuelewi kumbe anakuelewaaaa kabisaaa hahaahaha noma sanaaa
 
Back
Top Bottom