Jakaya Mrisho Kikwete, Mungu atakulipa!

Jakaya Mrisho Kikwete, Mungu atakulipa!

Sifa za kijinga,utawala wake umeua reli ya kati,tazara hoi,ukiwa na lipasport la kijani nchi za watu tayari wewe ni mtuhumiwa wa madawa ya kulevya maana maana anawajua mapapa wa biashara hiyo ila anauchuna,tembo wameisha,sifa pekee ya utawala wake kuifanya tanzania kuonekana taifa la uchawi na ukatili kupita kiasi maana serikali yake haichukui hatua stahiki kukomesha mauwaji ya walemavu wa ngozi,deni la taifa kuongezeka kwa kasi kunbwa sana bila tija yeyote,mifuko ya hifadhi ya jamii iko icu,sifa anazo kibao hajui kwanini tanzania masikini sasa sijui anaongoza nini?
 
-ni kipindi cha kikwete ambapo ajira imekuwa ngumu kuliko awamu zote
-Ufisadi umekuwa up to the maximum kuliko kuwahi kutokea
-ni kipindi chake JK AMBACHO FISADI NA WEZI wanatambaa mtaani na wanasema hawawezi kufungwa
-Ni kipindi cha Jk Ambacho inflation rate iko juu sana kuwahi tokea na mwenye jukumu la kuhakikisha anasema hela zenu za madafu,
-ni kipindi cha JK ambacho wanaharakati wanatekwa hadharani,wauwaji wanapandishwa vyeo
-Ni kipind hiki cha JK ambacho ikulu inaendeshwa toka makongo juu,yaani fisadi anamuandikia barua rais ikulu kuwa usiwasikilize Watanzania
-Ni kipindi hiki cha JK ambacho kila rafiki wa mwana mfalme ni mkuu wa WILAYA
-Ni kipindi hiki ambacho baba,mama na mtoto wote viongozi wa chama
TUSIPENDE KUSIFIA UJINGA,KUMLINGANISHA BEN NA HUYU NI KUTOITENDEA HAKI TANZANIA
 
Ndugu zangu watanzania wenzangu, kupitia jamvi hili, kwa heshima na taadhima nichukue fursa hii kumwandikia Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete, kwanza kumpa pole kwa majukumu mazito aliyonayo katika kulitumikia taifa lake. Ninampa pole kutokana na kutambua ugumu wa majukumu aliyonayo.

Kwa nafasi yake, yeye ndiye wa kutupiwa lawama zote pale mambo yanapokwenda si sawa. Pia ni mtu wa kupongezwa pale mambo yanaponyooka. Hii ni kawaida kwani wahenga walikwushasema kuwa mkubwa ni jalala.

Ndugu zangu watanzania wenzangu, mimi leo ningependa kuzungumzia kazi nzuri ambayo Rais Kukwete ameifanya ambapo hata kama baadhi yetu tutaibeza, ukweli utajidhihirisha.

Kikwete, katika kipindi cha miaka 9 amefanya yafuatayo mazuri;
1. Uchumi; amefanya mabadiliko kwenye kilimo ambapo wakulima wengi kwasasa wanalima kisasa na kwa msaada wa pembejeo za ruzuku.

Walau imesaidia taifa kuwa na akiba ya chakula cha kutosha hivyo kutokuwa na hofu ya wananchi kufa njaa. Kilimo cha umwagiliaji kimeongezeka, kilimo cha biashara kimekua. Mabadiliko ya sheria ya uwekezaji angalau yamewezesha nchi kuanza kunufaika na kodi ya uzalishaji ingawa bado si kwa kiasi kikubwa. Uboreshaji wa huduma za kibenki, mikopo ya saccos, uboreshaji wa njia za uchukuzi kama barabara, vivuko, reli kwa kununua vichwa na mabehewa, ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege e.g. Rungwe, Katavi, Gombe, DSM. n.k.

2. Kisiasa; Ni katika kipindi cha Kikwete ambapo uhuru wa shughuli za kisiasa umetolewa. Watanzania sote ni mashahidi kwamba vyama vya siasa vimekuwa huru kiasi kwamba baadhi vimeshindwa kuutumia uhuru huo ambapo baadhi vimeishia kuitisha maandamano, kukitisha chama cha mapinduzi na kutishia uvunjifu wa amani kama mbinu ya kutaka kutimiza adhma zao za kisiasa.

Ni wakati huu ambapo majukwaa ya siasa yametumika kuvitukana na kuvidhalilisha vyombo vya dola kwamba havina lolote. Ni wakati huu ambapo wanasiasa wa vyama pinzani wameachwa kuichambua serikali kwa kadiri ya hazina ya maneno iliyoko vinywani mwao.

Ni wakati huu ambao hakuna mwanasiasa aliwekwa kizuizini kwa kutoa kauli zenye kuhatarisha usalama wa nchi. Wanasiasa baadhi yao walifikia hatua ya kutisha kuwa wanao uwezo wa kuifanya nchi isitaealike, hakuna aliyeshughulika nao.

Aidha ni wakati huu ambao siku moja watu walikuwa wakishuhudia chama fulani kimeitisha maandamano nchi nzima kisha muitisha maandamano akakimbilia South Africa! Kiukweli ni wakati unaelekea mwishonu lkn kwa wanasiasa hasa wa upinzani mtaukumbuka!!!

3. Kijamii; Rais Kikwete amejitahidu kuimarisha huduma za kijamii kama usambazaji wa umeme vijijini kupitia REA, Ujenzi wa mradi mkubwa wa umeme wa gesi asilia huko Mtwara ambapo sote tunajua jinsi wanasiasa walivyoupinga na kufanya kila aina ya uchochezi ili usifanikiwe, leo tunashuhudia mradi unelekea kujamilika.

Miradi ya maji vijijini imetekelezwa kwa kasi awamu hii. Upande wa elimu mafanikio yako wazi ambapo ongezeko la ajira za walimu, ongezeko la shule za msingi na sekondari na pia ujenzi wa vyuo vikuu kwa ujumla vimetokea wakati wako.

Maboresho ya mishahara kwa wafanyakazi yamefanyika wakati wako. Kwa upande wa afya, siyo siri ununuzi wa vifaa vya kisasa mahospitalini walau umefanyika wakati huu kwa kiwango cha kuridhisha, ujenzi wa zahanati na vituo vya afya kupitia TASSAF, hospitali za mikoa kuwa za rufaa, mapambano dhidi ya malaria na UKIMWI, uzuiaji wa vifo vya mama wajawazito, juduma bure za matibabu kwa wazee (bado changomoto katika utekelezaji), maboresho ya Hospitali ya taifa ya Muhimbili ambapo sasa ina uwezo wa kutibu magonjwa ambayo awali matibabu yake yalipatikana nje yanchi n.k.

4. Kimataifa; Kwanza amejitahidi kukwepa mitego ya maadui zetu waliotaka kuliingiza taifa vitani kwasababu za chuki binafsi na wivu kutokana na nchi yetu kuanza kukua kiuchumi kwa kasi. Mfano wa nchi hizo sote tunao. Kikwete alijua kwamba vita kwasasa siyo kipaumbele cha nchi ingawa uwezo wa kuwachapa hao maadui zetu tunao.

Alifanya uamuzi mzuri na wa kizalendo. Isingekuwa rahisi kwa Rais asiye busara kuacha kuiingiza nchi vitani dhidi ya Rwanda, Malawi na Kenya wakati ambao nchi hizo zilionesha wazi kuichokoza Tanzania. Ni busara ya kiwango cha juu aliyonayo Kikwete hata kufanikiwa kuukwepa mtego huo.

Pia amejitahidi kusuluhisha migogoro katika nchi mbalimbali kama vile ule wa Kenya mwaka 2008, wa Sudan ya Kusini, Congo DR, Comoro, Afrika ya kusini (wa ndani ya ANC). Amekuwa na ushawishi mkubwa kwa mataifa makubwa kwa kuifuata sawasawa sera mama ya taifa ya kutofungamana na upande wowote kwa lengo la kuiepusha nchi kuwa na uadui unaotokana na mivutano baina ya mataifa makubwa.

Katiba mpya; Jambo hili halijaisha, tumwombe Mungu liishe salama!. Sote ni mashahidi juu ya umahiri alionao Kikwete katika namna anavyolihandle swala hili muhomu kwa mstakabali mwema wa taifa letu. Siyo siri swala hili limegubikwa na mambo mengi lkn mbaya na hatari inayoonekana ni kuibuka kwa kundi la watu linaloipinga katiba iliyopendekezwa.

Sina tatizo na kupingwa huko ola nina tatizo na sababu za kuipinga. Mfano wengi wanadai kuwa katiba pendekezwa imekiondoa kipengele cha uadilifu, si kweli kwani kipengele hicho kipo isipokuwa kiliondolewa kwenye Ibara inayohusu tunu za taifa na kuwekwa kwenye ibara ya maadili ya mtumishi wa umma. Kiukweli uadilifu siyo tunu kwa tafsiri yake bali ni swala la uadilifu.

Tunu ni kama vile Lugha ya kiswahili,amani, muungano n.k. Swala la katiba limeingiliwa na siasa kiasi kwamba watu hawajadili tena kwa uchungu wa kulinda misingi ya utaifa wetu bali kwa maslahi na kupata upenyo wa kisiasa.

Ninaamini kwa umakini wa Rais wetu atasimamia na hatimaye tutapata katiba yenye maslahi mapana ya historia ya taifa letu hasa Muungano, udugu na amani.

My take; Pamoja na mafanikio hayo wapo baadhi ya watanzania ambao wameendelea kubeza kwa namna yoyote ile. Baadhi yao wamediriki kukashifu kwa matusi na kumdhihaki Kikwete kwa lugha mbaya kabisa. Ni kweli hakuna binadamu aliyetimilika kwa kufanya bila kukosea.

Inawezekana katika utendaji wake kuna mahali amekosea hata hivyo sidhani kama anastahili kulaumiwa kiasi hicho. Ninawaambia ndugu zangu watanzania wenzangu, tutamkumbuka Kikwete siku moja!. Wanasiasa hasa wa vyama pinzani iko siku mtamkumbuka Kikwete!.

Waropokaji msio na staha katika kauli zenu mtamkumbuka Kikwete!. Na kwako Mheshimiwa Rais, nikusihi usokate tamaa, endelea kuchapa kazi kwani kama ni ng'ombe umebakiza kipande cha mkia tu!. Ulishawashinda tayari mbona!. Up to this moment, you are the winner Sir!.

Cha muhimu malizia kazi zako na Mungu Baba Mwenyezi atakulipa kwa kazi nzuri uliyowafanyia watanzania. Jifunze kwa Prof. Muhongo, aliyekuwa waziri wako ambaye pamoja na mazuri yote aliyoyafanya mwisho wa siku watanzania wasio shukurani walimwandalia manila na kumnyonga kisiasa hadharani!.

As you signing off Sir keepon praying for your nation ili kikombe cha siasa chafu ya wasaka madaraka hali mikono yao ikinuka rushwa, kiliepushe taifa kuingia kwenye machafuko.

Huna Kazi ya kufanya we we mpuuzi, Somo kubwa CCM ni unafiki. Kikwete atalaaniwa na vizazi vyote kwa kuifisi nchi na kutoa roho za watu
 
Kimeongezeka.

FaizaFoxy my love embu niunganishe na mimi huko lumumba maana buku saba sijui 8 kwa siku is worthy than nothing......

naapa kuwa nitaipinga na kuitukana chadema kama nyinyi au zaidi......

Na pia nitapinga kila kitu ata kama ni cha maslahi ya nchi....as long as chadema ndo wame initiate

Nitatetea uovu wa sisiemu kwa nguvu zangu zote ilimradi chadema wakose pa kuhemea....

Ata kama rais wangu akifanya maamuzi ya kijinga (kama ilivyokua kawaida yake)....naahidi kumtetea kwa kadri ya akili zangu zote kama ambavyo umekua ukifanya malkia wangu bibie FaizaFoxy

Kama hiyo haitoshi nitazusha tuhuma za uongo na kashfa zisizo za kweli kama ambavyo mmekua mkifanya na nitafanya zaidi ya ninyi.....

Nitatenga masaa matano kila siku kwa ajili ya kuichafua chadema na ukawa at large.....

Nina uhakika mta-appreciate mawazo yangu na michango yangu niwapo kazini.....

Cha msingi apa ni hiyo buku saba au 8.....

Nipo njiani naelekea kariakoo ila nikimaliza shughuli zangu huko nitapitia lumumba street kuweka wipers kwenye kioo cha nyuma ya gari langu....na pia nitaingia apo ofisini kwenu kwa ajili ya kuzungumzia hili jambo kwa kina...

Niue ndege wawili kwa jiwe moja...
 
Sitegemei punguani kama wewe kunielewa.

Kikwete ndiye Rais pekee na wa kwanza Tanzania aliyepata tuzo ya utawala bora, kumbuka hilo.

Kikwet endiye wa kwanza kualikwa rasmi na Obama kutokea Afrika alipochukuwa madaraka USA.

Kikwete ndiye Rais wa kwanza dunia aliyeweza kuwakutanisha Marais wanne kwa pamoja Afrika kwa wakati mmoja, Obama, Bush, Clinton na Jimmy Carter. Haijwahi kutokea kwingine.

Na mengine mengi ya kwanza ya Kikwete nikianza kuyaweka hapa tutakesha.

Hovyoooo!!
 
Mimi huwa nnawaambia siku zote, kama ni wapinzani wa kweli na mnaitakia mema Tanzania, mtaonesha aliyoyafanya Kikwete kisha mtasema sisi tutafanya zaidi hiki na hiki na hiki, hivi na hivi na hivi. Hapo tutawaelewa. Lakini huu upinzani usio na la kufanya mimi nauona ni ujinga tu na si upinzani.

Hivi upinzani hauna cha kufanya ukichukua nchi? Mbona yapo mengi tu? Kwanza ni kushughulikia sera ya elimu kwa sababu tunakokwenda siko! Pili ni kuweka sawa mambo ya katiba kwani hii nchi ni yetu sote si ya waheshimiwa mafisadi. Tatu kupangua sera ya afya mwananchi aweze kupata huduma bila rushwa vilevile kampeni ya kutokomeza mbu itaanzishwa. Nne kuiunda upya wizara ya ardhi wananchi waweze kupata hati katika muda muafakana bila kutoa rushwa. Mipango miji yote irekebishwe kwa sababu sasa hivi majengo yanachipuka hata sehemu ambazo hazistahili. Mikataba yote ya madini na gesi itawekwa sawa. Kulinda uoto wa asili n.k.
 
JK atakumbukwa na kila mpenda amani, maendeleo na mshikamanao wa Tanzania
 
MJENyGA Na kweli Mungu atamlipa yeye na Pinda kwa Mauaji ya watoto wetu wenye ulemavu wa ngozi!

Hivi haya mauaji yameanza kipindi yeye ndio ameingia madarakani?

R.I.P Albino wote waliouwawa jaman! kwa kweli inasikitisha sana! haswa hii ya juzi mama amejeruhiwa sana kisa anamli da mwanaye jaman wanamnyang'anya kama vile mwewe arukiae kifaranga cha kuku aibu ya milele kwa Watanzania wote duuuu
 
Hunipeleki huko.

Hapa ni Kikwete tu na mafanikio yake.:

Vyuo vikuu zaidi ya 40 wakati wake tu, nani aliyefanya hivyo wa kabla yake?

Faiza
Je kuna tofauti yoyote kati ya quality(thamani) na quantity(wingi).
Kujaza utitili wa vyuo visivyo na hadhi nadhani si bora ni afadhali kuwa na vyuo vichache viwe na hadhi.
Leo hii angalia wahitimu wetu walivyo.
 
Hivi haya mauaji yameanza kipindi yeye ndio ameingia madarakani?

R.I.P Albino wote waliouwawa jaman! kwa kweli inasikitisha sana! haswa hii ya juzi mama amejeruhiwa sana kisa anamli da mwanaye jaman wanamnyang'anya kama vile mwewe arukiae kifaranga cha kuku aibu ya milele kwa Watanzania wote duuuu

Kikwete na Pinda ndio wauwaji wa hawa watoto kwa maana wana kila uwezo wa kuyazuia tena mara moja ni swala la kuongea tu na kutoa Amri kama Amiri Jeshi Mkuu na Mkuu wa vyombo vyote vya Usalama TZ mpaka Sungusungu, Yeye ni Bosi wa kila Mtu hapa Tanzania kama Kikwete na Pinda wakiamua leo kutumia madaraka na nguvu zao kuwalinda hawa watoto wetu nina uhakika kwa 100% hakuna hata Mtoto mmoja atakayeuliwa tena, lakini hawafanyi hivyo sasa ni kwa nini?
Na jibu ni rahisi tu wao ndio.

WAUWAJI WAKUBWA wa HAWA VIUMBE wa MUNGU!
 
Ni mwehu tu ndiye anaweza kupinga ukweli huu.
ni kweli mkuu, mwehu tu ndio atataka kuonyesha maendeleo against rasilimali, mzigo wa madeni uliongezeka na fedha zilizoibiwa (atataka viwe na uwiano), lakini wenye akili timamu wataonyesha maendeleo bila kujali rasilimali tulizonazo, mzigo wa madeni uliongezeka, fedha zilizoibiwa na muda uliotumika kuleta hayo maendeleo.
 
Sawa sawa tunahitaji gt kama wewe
 
Wewe hata unachokibishia hukielewi ni nini.

Development ya Tanzania wakati wa Kikwete inaongelewa Kimataifa ni kati ya nchi 20 zinazo develop kwa haraka duniani:

Fastest-Growing Economies Through 2015 - Business Insider

Hivi hizo shule huwa mnaenda kusomea ujinga?
hii ni shida tosha ya kutojua na kutafsiri uchumi madhubuti, na kwa kweli naona Dalili Zote ambazo TANZANIA inaelekea kwenye arab spring syndrome, ya wana nchi kwenda na ku revolt against its leaders, utaringaje na university 40, wakati absorption rate ya wahitimu kwenda kazini ni only 2% , unatangaza kazi ya vacancy 70 wanakuja 14000 kwa interview, just because wanaenda kwenye interview kupita Barabara ya lami basi Nchi imesonga mbele , huu ni uaji, leo tumekopa na Deni hili watamaliza watoto wa chekechea leo, kwanini hatuoni hayo, mbona mimi nasikia uchungu na kadi yangu ya ccm Mfukoni? Indication ya takwimu ya kuwa Nchi ni fastest growing economy ni machungu ambayo hayana maana bila kuwa na Chembe za good leadership, moreover 90% ya fastest growing economies ziko Afrika na wote wanauza non renewable resources kama sisi dhahabu , nasikitika kuona Nchi hii tumepotea kiasi cha kupitiliza, na huku tunangalia Tofauti kubwa Kati ya tajiri na Masikini ikiongezeka na uchumi wa matajiri wachache ukitumiwa kama statistics za kujivunia, this is madness
 
Sitegemei punguani kama wewe kunielewa.

Kikwete ndiye Rais pekee na wa kwanza Tanzania aliyepata tuzo ya utawala bora, kumbuka hilo.

Kikwet endiye wa kwanza kualikwa rasmi na Obama kutokea Afrika alipochukuwa madaraka USA.

Kikwete ndiye Rais wa kwanza dunia aliyeweza kuwakutanisha Marais wanne kwa pamoja Afrika kwa wakati mmoja, Obama, Bush, Clinton na Jimmy Carter. Haijwahi kutokea kwingine.

Na mengine mengi ya kwanza ya Kikwete nikianza kuyaweka hapa tutakesha.
Philosophy ya geo politics wewe huielewi, kwanza wamarekani wana permanent interests na hawana permanent friends, nia ya obama kuja tanzania, ni ku send message kwa Kenya, kwani hawakutaka Kenyatta ashinde (ICC factor), pili Wao wanashida kubwa sana ya mahali pa kufungua an African theatre, mahali wanapoweza kuweka sphere ya influence yao na majeshi yao, na Nina wasi wasi walitaka eneo la Rufiji, hii na wasi wasi imekubwa kitendawili , tatu, ni kuhakikisha Islamic distabilisation iliyopo Kenya na South Sudan inadhibitiwa, kwa hiyo wana weka plug tanzania na uganda. Hii wewe hujui, na kwa taarifa yako, influence ya tanzania kwa Kenya kwa mtazamo ya Marekani Nina wasi wasi inabadilika . Kwa hiyo usiwaone wanakuja hapa meno nje , ujio Wao haina tofauti na ujio wa Carl peters wa miaka iliyopita.
 
Sodoliki wasalimie Kenya uliyochangia tumeyapokea.
 
Hizo zoooote porojo.

Ukweli ni kwamba walikuwepo wote wanne kwa wakati mmoja Tanzania hii, mwenyeji wao akiwa Kikwete. Obama, Bush, Clinton na Jimmy Carter. Hata kwenye maziko ya Mandela haijatokea hiyo Huyo ndiyo Kikwete. Kumbuka hilo.

Record.
 
hii ni shida tosha ya kutojua na kutafsiri uchumi madhubuti, na kwa kweli naona Dalili Zote ambazo TANZANIA inaelekea kwenye arab spring syndrome, ya wana nchi kwenda na ku revolt against its leaders, utaringaje na university 40, wakati absorption rate ya wahitimu kwenda kazini ni only 2% , unatangaza kazi ya vacancy 70 wanakuja 14000 kwa interview, just because wanaenda kwenye interview kupita Barabara ya lami basi Nchi imesonga mbele , huu ni uaji, leo tumekopa na Deni hili watamaliza watoto wa chekechea leo, kwanini hatuoni hayo, mbona mimi nasikia uchungu na kadi yangu ya ccm Mfukoni? Indication ya takwimu ya kuwa Nchi ni fastest growing economy ni machungu ambayo hayana maana bila kuwa na Chembe za good leadership, moreover 90% ya fastest growing economies ziko Afrika na wote wanauza non renewable resources kama sisi dhahabu , nasikitika kuona Nchi hii tumepotea kiasi cha kupitiliza, na huku tunangalia Tofauti kubwa Kati ya tajiri na Masikini ikiongezeka na uchumi wa matajiri wachache ukitumiwa kama statistics za kujivunia, this is madness

Hizo statistics zako ziko wapi? naona unakuja na porojo tu.
 
Back
Top Bottom