Pia kaongeza kushuka kwa thamani ya shilingi from 1/1000 to 1/1850. Kwa hili Mungu ambariki sana. Tofauti ya 850 ni kwamba amefanya juhudi kubwa kutufikisha hapo.
Niyeye alitupandisha kielimu mpaka division 5. Huu ni uzalendo uliotukuka.
Hakuishia hapo. Sukari sasa tunanua 2000-2500 p/kg. Huu ubunifu wake binafsi.
Akakuza harufu Kali kati ya waislamu na wakristu lakini pia baina ya madhehebu mbalimbali ndani ya dini moja. Kwa hili kamfunika Nyerere.
Kwa huruma zake sasa tunaweza kuvuta bangi kituo cha polisi tusikamatwe, ikuku unaweza unaweza kupiga bongo fleva, rushwa tunagawa hadharani usiulizwe, wakoloni wamerudi kwa kasi ya ajabu na wanatuibia rasilimali chini ya mwamvuli wa uwekezaji, ukiuliza utaambiwa tunavutia mazingira yakiuwekezaji. Awamu ya 4 tumeshuhudia umafia kwa waandishi ya habari, polisi kuua raia na waandishi wa habari, tumeshuhudia serikali yake ikiunda Chama Cha siasa cha polisi ambacho kazi yake kuua upinzani nchini japo amefeli kwa hila zake chafu wacheni ni msifu kwakuwa sili kwao.
Ikafika wakati, wanafunzi 20,000 wenye sifa yakujiunga chuo kikuu kukosa mikopo, bila aibu akajisifu hadharani.Bila abu, Ni yeye pekee ananunua suti Kariakoo anaenda kujaribisha ulaya ilimradi kuvunja rekodi ya safari.
Huku tukijisifu Uhuru wa Vyombo vya habari, kule anafungia Vyombo vya habari eti kisa vimefichua maovu ya Vyombo vyake vya usalama(-----------), huu ni udikiteta.
Tukashuhudia chama chake kinateka nyara mchakato wa katiba mpya bila maridhiano. Huu ni uhuni. Akaizindua kwa mbwembwe bila kupima upepo wa kisiasa pande mbili zinaunda muungano. Akajipa madaraka yakutunga katiba bila ridhaa ya wananchi as if anapanga bajeti ya familia yake.
Hakika anastahili pongezi.
Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.